6.21.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Sehemu ya Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia



Kisha, tutazungumzia hadithi ya Nuhu na namna ambavyo inahusiana na mada ya kazi ya Mungu, tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe.

Mnaona Mungu akimfanya nini Nuhu kwenye sehemu hii ya maandiko? Pengine kila mmoja aliyeketi hapa anajua kitu kuhusu hayo baada ya kusoma maandiko: Mungu alimfanya Nuhu kujenga safina, kisha Mungu akatumia gharika kuangamiza ulimwengu. Mungu alimruhusu Nuhu kujenga safina ili kuokoa familia yake ya wanane, kuwaruhusu kuweza kuishi, ili kuwa babu wa kizazi kifuatacho cha wanadamu. Sasa hebu tuyasome maandiko.

6.20.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Uendelezo wa Sehemu ya Nne


3) Mungu Atumia Upinde wa Mvua Kama Ishara ya Agano Lake na mwanadamu.

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

6.19.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Pili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli


Katika kipindi sawa na kile cha Ibrahimu, Mungu pia aliliangamiza jiji. Jiji hili liliitwa Sodoma. Bila shaka, watu wengi wanaijua hadithi ya Sodoma, lakini hakuna yeyote aliyejua fikira za Mungu zilikuwa usuli wa kuangamiza Kwake jiji hili.

Na hivyo leo, kupitia mazungumzo yake Mungu na Ibrahimu hapa chini, tutajifunza fikira Zake wakati huo, huku pia tukijifunza kuhusu tabia Yake. Kinachofuata, hebu tusome vifungu vya maandiko.

6.18.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Uendelezo wa Sehemu ya Nne


Mungu aliwaumba wanadamu; licha ya kama wamepotoka au kama wanamfuata Yeye, Mungu hushughulikia binadamu kama wapendwa Wake—au kama vile binadamu wangesema, watu walio wapenzi Wake sana—na wala si makaragosi Yake. Ingawaje Mungu anasema Yeye ndiye muumba na kwamba binadamu ni uumbaji Wake, hali ambayo inaweza kuonekana ni kana kwamba kuna tofauti kiasi katika mpangilio wa cheo, uhalisia ni kwamba kila kitu ambacho Mungu amefanya kwa mwanadamu kinazidi kabisa uhusiano wa asili hii. Mungu anampenda mwanadamu, anamtunza mwanadamu, na anaonyesha kwamba anamjali mwanadamu, pamoja na kumkimu mwanadamu bila kuacha na bila ya kusita. Kamwe hahisi katika moyo Wake kwamba hii ni kazi ya ziada au ni kitu kinachostahili sifa nyingi.

6.17.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli

Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Wanadamu Yaanza na Ibrahimu Kumtoa Isaka

Baada ya kumpa mtoto Ibrahimu, maneno ambayo Mungu alikuwa ametamka kwa Ibrahimu yakawa yametimizwa. Hii haimaanishi kwamba mpango wa Mungu ulifikia mwisho hapa; kinyume cha mambo ni kwamba, mpango wa ajabu wa Mungu wa usimamizi na wokovu wa wanadamu ndipo ulikuwa tu umeanza, na baraka Yake ya mwana kwa Ibrahimu ilikuwa tu ni utangulizi wa mpango wa usimamizi Wake kwa ujumla. Wakati huo, ni nani aliyejua kwamba vita vya Mungu na Shetani vilikuwa vimeanza kimya kimya wakati Ibrahimu alipomtoa Isaka?

6.16.2019

"Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Tatu"


Kuanzia mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe wote walio hai na viumbe wa Mungu, hakuna yeyote isipokuwa binadamu ameweza kuzungumza na Mungu. Binadamu anayo masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona, anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika kusikia Mungu akiongea, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu anayaweka matamanio yake yote kwake binadamu, Akitaka kumfanya binadamu kuwa mwandani Wake ambaye anayo akili sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye.

6.15.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

Kuhusu Ayubu


      Baada ya kusikia namna Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe, hasa kuhusiana na siri iliyomfanya akapata sifa za Mungu. Hivyo basi leo, hebu tuzungumzie kuhusu Ayubu!


Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu Kwake


      Kama tutazungumzia Ayubu, basi lazima tuanze na namna ambavyo alitathminiwa kwa mujibu wa matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe: "hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu."

6.14.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Saba

Msiwe na Wasiwasi Wowote Kuhusu Majaribio ya Mungu


Baada ya kuupokea ushuhuda kutoka kwa Ayubu kufuatia mwisho wa majaribio yake, Mungu aliamua kwamba angepata kundi au zaidi ya kundi—la watu kama Ayubu, ilhali aliamua kutowahi tena kumruhusu Shetani kushambulia au kunyanyasa mtu yeyote mwingine kwa kutumia mbinu ambazo kwazo alimjaribu, kumshambulia na kumnyanyasa Ayubu, kwa kufanya mzaha na Mungu; Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo kwa binadamu ambaye ni mnyonge, mjinga, na asiyejua—ilikuwa tosha kwamba Shetani alikuwa amemjaribu Ayubu! Kutomruhusu Shetani kuwanyanyasa watu vyovyote anavyotaka ndiyo rehema ya Mungu. 

6.13.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III Sehemu ya Kwanza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,


Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa kwa kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wamemwani Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa.

6.12.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III Sehemu ya Pili


Tumezungumza tu kuhusu kazi yote ambayo Mungu amekamilisha, misururu ya mambo Aliyoyafanya kwa mara ya kwanza. Kila mojawapo ya mambo haya yanahusiana na mpango wa Mungu wa usimamizi na mapenzi ya Mungu. Yanahusiana pia na tabia binafsi ya Mungu na kiini Chake. Kama tunataka kuelewa bora zaidi kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho, hatuwezi kukoma katika Agano la Kale au katika Enzi ya Sheria, lakini tunahitaji kusonga mbele pamoja na hatua ambazo Mungu alichukua katika kazi Yake. Hivyo basi, Mungu alipotamatisha Enzi ya Sheria na kuanza Enzi ya Neema, hatua zetu binafsi zimefika katika Enzi ya Neema—enzi iliyojaa neema na ukombozi.

6.11.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III Sehemu ya Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Biblia


Kifuatacho tutaangalia mfano uliozungumziwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.

3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea

Mat 18:12-14 Mnafikiri vipi? Iwapo mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi hao tisini na tisa, na kuenda milimani, na amtafute huyo ambaye amepotea? Na iwapo atampata, kweli nawaambia, anafurahi zaidi kwa sababu ya huyo kondoo, kuliko wao tisini na tisa ambao hawakupotea. Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.

6.10.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III Sehemu ya Nne


  Halafu, hebu tuangalie vifungu vifuatavyo katika maandiko.

       9. Bwana Yesu Atenda Miujiza.

       1) Bwana Yesu Awalisha Watu Elfu Tano.

       Yohana 6:8-13 Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akasema kwake, Kuna mvulana hapa, aliye na mikate mitano ya shayiri nao samaki wawili wadogo: lakini ni yapi miongoni mwa watu wengi? Naye Yesu akasema, Wafanye watu waketi chini. Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo.