5.24.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Pili


Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Pili

Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu


Katika mkondo wa maisha ya mtu, kila mtu hufikia kwenye misururu ya awamu muhimu. Hizi ni hatua za kimsingi zaidi, na muhimu zaidi, zinazoamua hatima ya maisha ya mtu. Kile kinachofuata ni ufafanuzi mfupi kuhusu mafanikio haya ambayo kila mtu lazima apitie kwenye mkondo wa maisha yake.

Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza

       Mahali ambapo mtu amezaliwa, amezaliwa katika familia ya aina gani, jinsia ya mtu, umbo la mtu, na wakati wa kuzaliwa: haya ndiyo maelezo ya awamu ya kwanza ya maisha ya binadamu.

5.23.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Tatu

Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Tatu
Uhuru: Awamu ya Tatu

Baada ya mtu kupita utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye kuuaga kabisa ule ujana wake, kuwaaga wazazi wake, na kukabiliana na barabara iliyo mbele yake akiwa mtu mzima huru. Wakati huo[c] lazima wakabiliane na watu, matukio na mambo yote ambayo mtu mzima lazima apitie, na kukabiliana na viungo mbalimbali katika msururu wa hatima yake. Hii ndiyo awamu ya tatu ambayo lazima mtu apitie.

5.22.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Nne


Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Nne
Uzao: Awamu ya Tano

Baada ya kuoa, mtu anaanza kulea kizazi kijacho. Mtu hana uwezo wa kujua atakuwa na watoto wangapi na watoto hawa watakuwa aina gani; hili pia linaamuliwa na hatima ya mtu, iliyoamuliwa kabla na Muumba. Hii ndiyo awamu ya tano ambayo lazima mtu apitie.

Kama mtu amezaliwa ili kutimiza jukumu la mtoto wa mwengine, basi mtu analea kizazi kijacho ili kutimiza jukumu la mzazi wa mwengine. Mabadiliko haya ya majukumu yanamfanya mtu kupitia awamu tofauti za maisha kutoka mitazamo tofauti. Yanampa pia mtu mseto tofauti wa mambo mbalimbali ya maisha kupitia, ambapo mtu anajua ukuu ule wa Muumba, pamoja na hoja kwamba hakuna mtu anayeweza kuzidi au kubadilisha kile ambacho Muumba aliamua kabla.

5.21.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Tano


Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Tano
Kifo: Awamu ya Sita

Mwenyezi Mungu alisema, “Baada ya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya maisha, baada ya miaka mingi sana isiyosahaulika, baada ya kutazama misimu ikipita na kujirudia, mtu hupita kwenye kiungo muhimu sana cha maisha bila ya arifa, na kwa ghafla tu mtu anajipata kwenye miaka yake ya kufifia. Alama za muda zimejichora kotekote kwenye mwili wa mtu: Mtu hawezi tena kusimama wima, kichwa cha nywele nyeusi kinageuka na kuwa cha nywele nyeupe, macho maangavu na mazuri yanabadilika na kuanza kufifiliza na kuwa na wingu mbele yao, nayo ngozi laini, yenye unyumbufu inageuka na kuwa na makunyanzi na madoadoa.

5.20.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kazi ya Mungu

Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Sita
Kifo: Awamu ya Sita
4. Njoo Chini ya Utawala wa Muumba na Ukabiliane na Kifo kwa Utulivu

Wakati ule ambao mtu anazaliwa, nafsi ya mtu iliyo pweke inaanza kupitia maisha hapa duniani, inapitia mamlaka ya Muumba ambayo Muumba ameipangilia. Ni wazi kwamba, kwa mtu husika, ile nafsi, hii ni fursa nzuri kabisa ya kupata maarifa kuhusu ukuu wa Muumba, kujua mamlaka Yake na kuyapitia binafsi. Watu wanaishi maisha yao kulingana na sheria za hatima zilizowekwa wazi kwao na Muumba, na kwa mtu yeyote mwenye akili razini aliye na dhamiri, kuelewa ukuu wa Muumba na kutambua mamlaka yake kwenye mkondo wa miongo yao mbalimbali hapa nchini si jambo gumu kufanya.

5.19.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Saba


Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Saba
Hakuna Anayeweza Kubadilisha Hoja Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu

Baada ya kusikiliza kila kitu Nilichomaliza kusema, je, fikira yenu ya hatima imebadilika? Mnaelewa vipi hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Ili kuiweka kwa urahisi, katika mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi mbovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye mzingo wa hatima ambayo Muumba amempangia yeye.

5.18.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Kwanza



Utakatifu wa Mungu (I) Sehemu ya Kwanza

Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni cha tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.)

5.17.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Pili


Kwa sababu sasa tumemaliza kuzungumza kuhusu Shetani, hebu turudie kuzungumza kuhusu Mungu wetu. Wakati wa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita wa Mungu, matamshi machache sana ya moja kwa moja ya Mungu yamerekodiwa katika Biblia, na yale yaliyorekodiwa ni rahisi sana. Hivyo wacha tuanzie mwanzoni. Mungu alimuumba mwanadamu na tangu hapo kamwe Ameongoza maisha ya binadamu. Iwe kwa kuwapa wanadamu baraka, kuwapa sheria na amri Zake, ama kuweka masharti kanuni mbalimbali za maisha, mnajua lengo analonuia Mungu kwa kufanya mambo haya ni nini? Kwanza, mnaweza kusema kwa uhakika kwamba yote anayofanya Mungu ni kwa wema wa binadamu? (Ndiyo, tunaweza.)

5.16.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Tatu



Kwa sababu sasa tumemaliza kuzungumza kuhusu Shetani, hebu turudie kuzungumza kuhusu Mungu wetu. Wakati wa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita wa Mungu, matamshi machache sana ya moja kwa moja ya Mungu yamerekodiwa katika Biblia, na yale yaliyorekodiwa ni rahisi sana. Hivyo wacha tuanzie mwanzoni. Mungu alimuumba mwanadamu na tangu hapo kamwe Ameongoza maisha ya binadamu. Iwe kwa kuwapa wanadamu baraka, kuwapa sheria na amri Zake, ama kuweka masharti kanuni mbalimbali za maisha, mnajua lengo analonuia Mungu kwa kufanya mambo haya ni nini?

5.15.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II Sehemu ya Kwanza




Utakatifu wa Mungu (II) Sehemu ya Kwanza

      Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu "Upendo Safi Bila dosari.")

      1. "Upendo" unarejelea hisia ambayo ni safi na bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna umbali na hakuna chochote kichafu. Iwapo una upendo, basi hautadanganya, kulalamika, kusaliti, kuasi, kushurutisha, au kutafuta kupata kitu au kupata kiasi fulani.

5.14.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II Sehemu ya Pili



Utakatifu wa Mungu (II) Sehemu ya Pili

Kuhusu utakatifu wa kiini cha Mungu, wakati uliopita tulishiriki kidogo kuuhusu na huo ulikuwa msukumo wa maarifa ya watu ya utakatifu wa Mungu, lakini hautoshi. Hauwezi kutosha kusaidia watu kujua kikamilifu utakatifu wa Mungu, wala hautoshi kuwasaidia kuelewa kwamba utakatifu wa Mungu ni wa kipekee. Zaidi, hautoshi kuruhusu watu kuelewa kipengele cha maana ya ukweli ya utakatifu kwani imejumuishwa kabisa kwa Mungu. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba tuendelee na ushirika wetu katika mada hii. Hapo nyuma ushirika wetu ulijadili mada tatu, kwa hivyo sasa tunapaswa kujadili mada ya nne, na tutaanza kusoma maandiko.

5.13.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II Sehemu ya Nne

Utakatifu wa Mungu (II) Sehemu ya Nne
5. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu

Mienendo ya kijamii ilianza lini? Je, ni kitu kipya? (La.) Hivyo mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu? (Ndiyo.) Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi? Je, misemo maarufu ambayo watu wanapenda kusema inahesabika pia? Je, pia mitindo ya maisha ambayo watu wanataka inahesabika? Je, nyota wa muziki, watu mashuhuri, majarida, na riwaya ambazo watu hupenda zinahesabika? (Ndiyo.)