Mungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?
Aya za Biblia za Kurejelea:
"Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu" (LAW. 11:45).
"Na utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana" (EBR. 12:14).
"Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho" (YN. 12:47-48).