Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" (Sehemu ya Pili)
Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu.
Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. name="more">Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu. Hivyo basi, mwanadamu hana uwezo wa kujitenga na Mungu. Vilevile, Mungu Hajawahi kuwa na nia ya kujitenga na mwanadamu. Kazi Aifanyayo Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote na mawazo Yake daima ni mema. Kwa mwanadamu, kwa hivyo, kazi ya Mungu na mawazo ya Mungu kwa mwanadamu (yaani mapenzi ya Mungu) ni “maono” ambayo yanafaa kutambuliwa na mwanadamu. Maono kama hayo pia ni usimamizi wa Mungu, na kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu. Mahitaji ambayo Mungu anatarajia kutoka kwa mwanadamu wakati wa kazi Yake, wakati uo huo, yanaitwa “vitendo” vya mwanadamu. Maono ni kazi ya Mungu Mwenyewe au ni mapenzi Yake kwa mwanadamu au madhumuni na umuhimu wa kazi Yake. Maono pia yanaweza kusemekana kuwa sehemu ya usimamizi, kwani usimamizi huu ni kazi ya Mungu, iliyokusudiwa kwa mwanadamu, kwa maana kwamba ni kazi ambayo Mungu anaifanya miongoni mwa wanadamu. Kazi hii ni ushahidi na njia ambayo kwayo mwanadamu anamfahamu Mungu na ni ya umuhimu wa hali ya juu kwa mwanadamu. Iwapo wanadamu hawatatilia maanani kuijua kazi ya Mungu na badala yake kutilia maanani mafundisho ya dini kuhusu imani kwa Mungu au kutilia maanani vitu vidogo visivyo na maana, hawatamjua Mungu, na, aidha, hawatakuwa wanautafuta moyo wa Mungu. Kazi ya Mungu inamsaidia sana mwanadamu kumfahamu Mungu na inaitwa maono. Maono haya ni kazi ya Mungu, mapenzi, madhumuni na umuhimu wa kazi ya Mungu na yote ni kwa manufaa ya mwanadamu. Vitendo vinamaanisha yale ambayo yanafaa kufanywa na mwanadamu, yale ambayo yanafaa yafanywe na viumbe wanaomfuata Mungu. Ni wajibu wa mwanadamu pia. Kinachotakiwa kufanywa na mwanadamu si kile alichokielewa tangu awali bali ni yale matakwa ya Mungu wakati wa kuifanya kazi Yake. Matakwa haya taratibu yanakuwa ya kina na kuinuliwa kadri Mungu anavyofanya kazi. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, mwanadamu alilazimika kuifuata sheria na katika Enzi ya Neema mwanadamu alitakiwa kuubeba msalaba. Enzi ya Ufalme ni tofauti: Matakwa kwa mwanadamu ni mazito kuliko yale ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kadiri maono yanavyoinuliwa zaidi ndivyo matakwa haya yanavyokuwa mazito, ya wazi zaidi na halisi. Vivyo hivyo, maono yanaendelea kuwa halisi. Maono haya mengi na halisi si fursa tu ya utiifu wa mwanadamu kwa Mungu, bali pia, zaidi ya hayo, yanamsaidia yeye kumfahamu Mungu.
Ikilinganishwa na enzi za awali, kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme ni ya vitendo zaidi, imekusudiwa zaidi dutu ya mwanadamu na mabadiliko katika tabia yake na uwezo zaidi wa kuwa na ushuhuda wa Mungu Mwenyewe kwa wale wote wamfuatao Mungu. Kwa maneno mengine, katika Enzi ya Ufalme, Mungu anapofanya kazi hujionyesha zaidi kwa mwanadamu, kuliko kipindi kingine chochote kile cha awali, ikiwa inamaanisha kuwa maono ambayo yanafaa kujulikana na mwanadamu ni ya juu kuliko yale ya enzi yoyote ile ya awali. Kwa kuwa kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu imeingia maeneo ambayo haikuwa imefika, maono yanayojulikana na mwanadamu katika Enzi ya Ufalme ni ya juu zaidi katika kazi nzima ya usimamizi. Kazi ya Mungu imeingia katika maeneo ambayo haikuwa imewahi kufika, na kwa hivyo maono yanayojulikana na mwanadamu yamekuwa ya juu zaidi katika maono yote, na matokeo ya vitendo vya mwanadamu ni ya juu zaidi kuliko enzi za awali kwani utendaji wa mwanadamu hubadilika kulingana na mabadiliko ya maono na ukamilifu wa maono vilevile huonyesha ukamilifu wa vitendo vya mwanadamu. Punde tu usimamizi wa Mungu usitapo, vitendo vya mwanadamu navyo husimama, na bila kazi ya Mungu mwanadamu hatakuwa na jingine ila tu kujikita katika mafundisho ya zamani, vinginevyo hatakuwa na pa kukimbilia. Bila maono mapya, hapatakuwa na utendaji mpya kutoka kwa mwanadamu; bila kuwepo na maono kamili hapatakuwa na utendaji kamili wa mwanadamu; na bila maono ya juu hapatakuwa na utendaji wa juu wa mwanadamu. Utendaji wa mwanadamu huandamana na nyayo za Mungu na vivyo hivyo ufahamu na tajriba ya mwanadamu hubadilika sawa na kazi ya Mungu. Bila kujali mwanadamu ana uwezo kiasi gani, hawezi kujitenga na Mungu, na iwapo Mungu angaliacha kufanya kazi hata kwa muda kidogo, mwanadamu angalikufa ghafla kutokana na ghadhabu ya Mungu. Mwanadamu hana lolote la kujivunia, kwani haijalishi ufahamu wa mwanadamu ulivyo wa juu leo, haijalishi jinsi uzoefu wake ulivyo wa kina, hawezi kujitenga na kazi ya Mungu—kwani vitendo vya mwanadamu na yale yote anayoyaandama katika imani yake kwa Mungu, hayatengani na maono haya. Katika kila aina ya kazi ya Mungu kuna maono yanayofahamika na mwanadamu; maono yanayofuatwa na matarajio mwafaka ya Mungu kwa mwanadamu. Bila haya maono kama msingi, mwanadamu hawezi kuwa na uwezo wa utendaji na pia hangeweza kumfuata Mungu bila kuyumbayumba. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu au hayaelewi mapenzi ya Mungu, basi yote ayafanyayo ni bure na yasiyoweza kukubalika na Mungu. Hata mwanadamu awe na vipawa vingi kiasi gani, bado hawezi kujitenga na kazi ya Mungu na uongozi wa Mungu. Bila kujali uzuri na wingi wa matendo ya mwanadamu, bado hayawezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hivyo basi, utendaji wa mwanadamu hauwezi kutenganishwa na maono katika hali yoyote ile. Wale ambao hawakubali maono mapya hawana vitendo vipya. Vitendo vyao havina uhusiano na ukweli kwani wanajifunga katika mafundisho ya dini na kufuata sheria zilizokufa; hawana maono mapya kabisa na kwa sababu hiyo hawatendi kulingana na enzi mpya. Wamepoteza maono na kwa kufanya hivyo wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, hivyo basi kupoteza ukweli pia. Wasio na ukweli ni wazawa wa upuuzi, ni mifano ya Shetani. Bila kujali mtu ni wa aina gani, hawezi kuwepo bila maono ya kazi ya Mungu, hawezi kuishi pasipo na uwepo wa Roho Mtakatifu; punde tu mtu apotezapo maono, anaingia Kuzimu na kuishi gizani. Watu wasio na maono ni wale wamfuatao Mungu kipumbavu, ni wale wasio na kazi ya Roho Mtakatifu, na wanaishi kuzimu. Watu kama hawa huwa hawafuatilii ukweli, na hulitundika jina la Mungu kama bango. Wale ambao hawafahamu kazi ya Roho Mtakatifu, ambao hawamjui Mungu katika mwili, ambao hawajui hatua tatu za kazi katika uzima wa usimamizi wa Mungu—hawajui maono na hivyo wanaishi bila ukweli. Je, si wale wote wasiokuwa na ukweli ni watenda maovu? Wale wanaotaka kuweka ukweli katika vitendo, ambao wako tayari kuutafuta ufahamu wa Mungu, na ambao kwa kweli wanashirikiana na Mungu ni watu ambao maono yanakuwa msingi wao. Wanakubaliwa na Mungu kwa sababu wanashirikiana na Mungu na ushirika huu ndio ambao unafaa kuwekwa katika vitendo na mwanadamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni