12.19.2018

Viumbe Wote Lazima Waje Chini ya Utawala wa Mungu

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,nyimbo za injili

Viumbe Wote Lazima Waje Chini ya Utawala wa Mungu

I
Mungu aliumba vitu vyote, na hivyo Yeye hufanya viumbe wote
kuja chini ya utawala Wake, na kutii utawala Wake.
Anaamuru vitu vyote, akividhibiti katika mikono Yake. 
II
Vitu hai, milima, mito na mwanadamu lazima vyote viwe chini ya utawala Wake.
Vitu katika anga na duniani lazima vyote vije chini ya utawala Wake.
Vyote lazima vitii, bila uchaguzi wowote.
Hii ni amri ya Mungu na mamlaka Yake.
III
Mungu aliumba vitu vyote, na hivyo Yeye hufanya viumbe wote
kuja chini ya utawala Wake, na kutii utawala Wake.
Kila kitu kinaamuriwa na Mungu. Anaamuru na kuvipanga vitu vyote,
kila kuainishwa kulingana na aina na kwa mapenzi ya Mungu kupewa nafasi yake.
Vitu katika anga na duniani lazima vyote vije chini ya utawala Wake.
Vyote lazima vitii, bila uchaguzi wowote. Hii ni amri ya Mungu na mamlaka Yake.
IV
Haijalishi kitu ni kikubwa vipi, hakitaweza kamwe kumpita Mungu.
Mambo yote humtumikia Mungu-binadamu walioumbwa, hakuna anayethubutu kukataa au kutoa madai kwa Mungu.
Mwanadamu, kiumbe wa Mungu, lazima pia aendeleze wajibu wake.
Awe bwana au mtawala wa vitu vyote, hata hadhi yake iwe ya juu vipi,
yeye bado ni mtu mdogo chini ya utawala wa Mungu.
Mwanadamu asiye na maana, kiumbe wa Mungu, kamwe hatakuwa juu ya Mungu.
kutoka kwa "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

      Soma zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni