Tumeona mazungumzo mengi kwa mtandao na serikali ya Kikomunisti ya Kichina na ulimwengu wa kidini wakilisingizia, kulikashifu, kulishambulia na kulitahayarisha Kanisa la Mwenyezi Mungu (kama vile “tukio la 5.28” huko Zhaoyuan, jimbo la Shandong). Tunajua pia kuwa CCP ni bora mno kwa kudanganya na kunena uongo na kupinda ukweli ili kuwahadaa watu, na vilevile kuwa bora sana katika kuyakashifu, kuyashambulia na kuyahukumu yale mataifa ambayo ina chuki kwayo, hivyo neno lolote ambalo CCP husema ni lazima lisiaminiwe kabisa. Lakini mambo mengi yanayosemwa na wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa ni sawa na yale ambayo CCP huyasema, hivyo ni jinsi gani tunafaa kutambua maneno ya kashfa, ya kutahayarisha yanayotoka kwa CCP na ulimwengu wa kidini?
Jibu:
Kwa nini nguvu ovu za Shetani zinashambulia kazi ya Mungu sana, kuhukumu kazi ya Mungu hivyo? Kwa nini nguvu ovu za joka kubwa jekundu zinamshambulia na kumshutumu Mungu kwa mhemuko, na kukandamiza kanisa Lake? Kwa nini nguvu zote ovu za Shetani, vikiwemo vikundi vinavyompinga Kristo ndani ya jamii za dini, zinamshutumu Mwenyezi Mungu? Ni kwa sababu Shetani anajua kwamba mwisho wake unakaribia, kwamba Mungu tayari ameupata ufalme Wake na ufalme umefika duniani, na kwamba ataangamia mara moja asiposhiriki katika vita vya kuamua mshindi na mshinde dhidi ya Mungu. Je, umeelewa ukweli huu? Mara wanaposikia shutuma za mhemuko za serikali ya Kikomunisti ya China za kazi ya Mwenyezi Mungu, watu wengi waliokanganywa wanafikiri kwamba haiwezekani hii kuwa njia ya kweli. Mara wanapoona shutuma iliyosambaa kutoka kwa wachungaji na wazee wa jamii za dini, wanafikiri kwamba hii hakika si njia ya kweli.
Watu hawa wamekanganywa kwa njia zipi? Je, wanaweza kubaini asili ya giza na ovu ya dunia? Biblia inasema, “Nayo nuru hung’aa gizani, wala giza halikuielewa nuru” (Yohana 1:5). Je, kweli wanaelewa maneno haya? “Ulimwengu mzima uko ndani ya maovu” (1 Yohana 5:19). Je, wanaweza kutambua maana ya kweli ya maneno haya? Hawawezi kubaini chochote. Wanafikiri kwamba kama hii ingekuwa njia ya kweli, kama Mungu angekuwa amefika, basi serikali ya China inapaswa kukaribisha kwa furaha, jamii za dini zinapaswa kukaribisha kwa furaha, na ni hapo tu ndipo inaweza kuwa njia ya kweli. Hii ni mantiki ya aina gani? Je, hii si mantiki ya Shetani? Watu wengine wanapochunguza kazi ya Mungu, kwanza wanaangalia iwapo dunia inakaribisha na kukubali Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, na iwapo jamii za dini zinaikaribisha na kuikubali. “Dunia ikikaribisha kwa furaha tu, na hasa, serikali ya CCP ikitangaza kwamba ni njia ya kweli, ndipo tunaweza kuiamini. Wachungaji na wazee wote kutoka jamii za dini wakitangaza kwamba hii ni njia ya kweli, kwamba huku ni kurudi kwa Bwana Yesu, hapo tu ndipo tunaweza kuikubali.” Je, kuna watu wengi waliokanganywa hivi? Watu wengine, wakati tu wako karibu kujitumia kwa ajili ya Mungu, joka kubwa jekundu, Shetani, linakuja kuwajaribu: “Kanisa la Mwenyezi Mungu linawateka watu nyara. Ukimwamini Mwenyezi Mungu, basi hutaweza kuondoka, vinginevyo watatoa macho yako, kukata masikio yako, na kuvunja miguu yako.” Niambie, hali ingekuwa hivi kweli, ni watu wangapi katika dunia nzima tayari wangekuwa wametolewa macho yao na kukatwa masikio yao? Je, umewahi kuona tukio hata moja kama hilo? Kwa watu wote ambao wamejitumia kwa ajili ya Mungu, je, umemwona yeyote ambaye alilazimishwa kufanya hivyo kwa sababu alitekwa nyara na hangeweza kuondoka? Ikiwa kweli angekuwa ametekwa nyara, je, kazi na mahubiri yake yangekuwa ya kufaa? Yeyote aliye na ubongo angetafakari hili na kufikiri: “Hiyo ni sahihi. Huu ni uvumi uliobuniwa na CCP, uongo uliosemwa na CCP. Shetani ibilisi kweli ni mjuzi wa kueneza uvumi—kwa nini sikuona ukweli?” Watu wengine hawaamini maneno haya ya joka kubwa jekundu, wakati wengine wanaogopa na hawathubutu tena kujitumia kwa ajili ya Mungu wanaposikia mambo haya. “Siwezi tena kujitolea kwa hili. Ni hatari; naweza kupoteza maisha yangu!” Kisha, wanakimbia. Je, watu hawa wana uwezo wa kuelewa? Hawana; hawana utambuzi. Wengine pia wanasema: “Naona kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni maneno ya Mungu, kwamba ni sauti ya Mungu. Kimsingi nimebaini ya kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, lakini shirika hili, Kanisa la Mwenyezi Mungu, ni lipi? Sijalichunguza hili kikamilifu—sielewi kanisa hili. Kweli wanaweza kuwateka watu nyara? Wakiniteka nyara, watatoa macho yangu na kukata masikio yangu?” Kiwewe chao kipo hapa. Wanasema: “Siwezi kuungana nao. Je, wakitoa macho yangu na kukata masikio yangu? Sitakuwa mlemavu maisha yangu yote? Kanisa la Mwenyezi Mungu bado ni geni kwangu; Silielewi. Hata hivyo, kimsingi nimekuwa na hakika kuhusu maneno ya Mwenyezi Mungu. Wao ni sauti ya Mungu, na wana ukweli.” Wako makini sana katika uchunguzi wao: Kwanza wanachunguza maneno ya Mwenyezi Mungu kuona ikiwa ni maneno ya Mungu. Mara wanapokubali kwamba kweli ni maneno ya Mungu, basi wanachunguza zaidi iwapo Kanisa la Mwenyezi Mungu ni kanisa la kweli. Wanafikiri: “Si kutakuwa na shida kama Kanisa la Mwenyezi Mungu ni shirika halifu lakini maneno ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli?” Je, unaweza kusema kwamba hilo hata linawezekana? Hali ingekuwa hivyo, basi Kanisa la Mwenyezi Mungu halingekuwa kanisa la kweli. Mambo yangekuwa kama wanavyofikiri, kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu ambalo linaeneza maneno ya Mungu na kumshuhudia Mwenyezi Mungu ni shirika la binadamu, lakini halina watu ambao ni wa Mungu, basi kazi ya Mwenyezi Mungu haingekuwa bandia tu? Basi ni nani wanaohubiri na kushuhudia maneno ya Mungu? Ni nani wanaomshuhudia Mwenyezi Mungu? Mungu angewaruhusu vipi watu kutoka kwa shirika halifu, shirika la wanadamu, kumtukuza na kumshuhudia? Hilo halingekuwa kumfedhehesha Mungu? Mungu angeweza kujifedhehesha? Watu wengine hawawezi kubaini suala hili. Wamekiri maneno ya Mungu, lakini hawawezi kuona wazi Kanisa la Mwenyezi Mungu ni kanisa la aina gani kweli—hawathubutu kuliamini. Wanafikiri: “Sitaki kuwasiliana na ninyi watu. Nitafanya nini mkiniteka nyara?” Watu hawa hawawezi kukaribia kulinganishwa na wale watakatifu walioifia dini kwa ajili ya Mungu kotekote katika enzi. Bwana Yesu alipowatuma watakatifu wale nje kuhubiri, ilikuwa kama kuwarusha kondoo katika kundi la mbwa mwitu, lakini wote walithubutu kwenda. Sasa watu hawa wanajua wazi maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli na sauti ya Mungu, lakini ni wepesi wa kutishwa na waoga, wasithubutu kuwasiliana na Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa sababu ya uvumi. Je, hili halimsikitishi Mungu? Imani ovyo ya watu, watu kumsikiliza na kumwamini Shetani Ibilisi ni tanzia za wanadamu.
Adamu na Hawa walikuwa na furaha sana katika Bustani ya Edeni, wakitii na kusikiza sauti ya Mungu, lakini ni nini kiliwasababisha kutenda dhambi mwishowe? Baada ya Mungu kuwazungumzia, Shetani alisema maneno machache kuwajaribu—waliyaamini maneno hayo na kisha kutenda dhambi. Walitengwa na Mungu mara moja—Mungu hakuwazungumzia tena, na Aliwaficha uso Wake. Je, hii si tanzia ya binadamu? Baada ya kusikiza maneno ya Mwenyezi Mungu, watu wachache husema, “Oo, kweli hii ni sauti ya Mungu, kweli huu ni ukweli. Maneno haya ni ya utendaji sana, hakukuwa na maneno mengi yaliyotamkwa wakati wa kazi ya Bwana Yesu.” Ni kana kwamba wamerudi tena kwa kumbatio la Mungu kufumba kufumbua—wanahisi wenye furaha kamili na ridhaa. Ni nani angeweza kufikiri kwamba jaribio la Shetani lingekuja wakati huu hasa: “Umesikia kuhusu Umeme wa Mashariki? Ni shirika halifu. Kama huamini injili wanayohubiri, watatoa macho yako na kukata masikio yako. Wao ni wa kutisha! Ukikutana nao, lazima uwe makini. Bila kujali lolote, usinaswe na mtego wao.” Jaribio hili kutoka kwa Shetani linawalaghai na kuwadhibiti, kwa hiyo hawathubutu tena kujitumia kwa ajili ya Mungu. Huku kunaitwa “kuwa mwerevu maisha yako yote, lakini kuangamizwa na muda mfupi sana wa upumbavu.” Hawafikirii kama kuna tukio moja la mtu kutolewa macho na kukatwa masikio yake katika bara lote la China. Kama kungewahi kuwa, je, CCP kingewahi kutulia? Kingehamasisha vyombo vyote vya habari kulitangaza kwa dunia nzima, na wangetumia yote kueneza habari hiyo kwa siku kadhaa. Lakini hakuna tukio hata moja kama hilo linaweza kupatikana—ni habari ya kubuniwa tu. CCP hutumia kila fursa kufanya mambo kama hayo, lakini wale waliojaribiwa na Shetani hawatambui asili yake ya kweli. Hawawezi kubaini uovu wote ambao CCP kimetenda kwa miaka mingi sana, mambo yote mabaya ambayo kimefanya. Hakuna ukweli hata kidogo katika mambo yaliyosemwa na vyombo vya habari vya CCP, lakini watu hawa wameshindwa kubaini hili.
kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha, Juzuu ya 130
Watu wengine huuliza ni kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China kimepachika Umeme wa Mashariki jina la ibada mbovu.
Kama sote tunavyojua, CCP ni chama kikana Mungu. Kinampinga Mungu na huchukia ukweli zaidi kuliko kingine chochote. Kimeyaamu makanisa na makundi yote yanayomwamini Mungu wa kweli kama madhehebu maovu na kimetangaza wazi kwamba Biblia ni kitabu cha dhehebu ovu. Huu ni ukweli unaotambuliwa. Je, kweli bado hatuoni? Mbali na hilo, hatujapitia mateso ya kutosha kwa kumwamini Bwana Yesu kwa miaka yote hii? Je, hakujakuwa na wahubiri wa kutosha na Wakristo walioteswa hadi kufa na kufungwa na CCP? Je, tunawezaje bado kusikiliza uvumi wa serikali ya CCP? Linapokuja kutofautisha kati ya makundi na dini nzuri, haiwezi kutofautishwa na jinsi chama fulani cha siasa au mtu anataka kutofautisha, na zaidi ya hayo haiwezi kuamuliwa na nchi fulani au katiba yake ya kitaifa. Dini nzuri huchukuliwa kama kitu chanya cha faida kwa wanadamu. Makundi ya dini huchukuliwa kama mambo mabaya ambayo humpotosha binadamu. Ikiwa mtu anataka kuamua kama kanisa ni dini nzuri au dhehebu ovu, inapaswa kuzingatia kama ni jambo zuri au hasi. Makanisa ambayo yanatoka kwa Mungu na yaliyoundwa kutokana na kazi ya Mungu ni dini nzuri. Yale yote yanayotoka kwa Shetani na kazi ya roho wabaya huchukuliwa kama madhehebu maovu. Serikali ya CCP huchukuliwa kama utawala wa kishetani ambalo humpinga Mungu zaidi na huchukia ukweli. CCP ni dhehebu ovu la kweli. Haina haki ya kutoa maoni juu ya imani katika Mungu, na hata hivyo haina sifa ya kuhukumu kikundi au kanisa lolote la imani za kidini.
Baadhi ya watu hufuata CCP katika kushutumu Umeme wa Mashariki kama ibada mbovu kwa sababu mateso ya serikali ya CCP ya Umeme wa Mashariki ni makali kuliko yale ya dini nyingine yoyote. Wazo hili linapatana na ukweli? Kuchukulia hatua kali za kisheria kwa Umeme wa Mashariki na serikali ya kishetani ya CCP ni kali sana, wenye hasira zaidi. Hii inatosha kuonyesha kwamba CCP inaogopa ukweli na kumdharau Mungu zaidi. Kwa miaka hii, makanisa ya nyumbani ya China na makanisa ya siri yameendelea kuhukumiwa, kuteswa na kuwindwa kwa utawala wa CCP. Je, tunapinga kuwa Bwana Yesu ni Mungu wa kweli na njia ya kweli kwa sababu ya hili? Tumemwamini Mungu kwa miaka mingi. Je, hatuwezi kuelewa hili? CCP kimeupindua ukweli na kugeuza mema na mabaya. Hiki ni kiini cha Shetani ibilisi. Je, bado huwezi kutofautisha kati ya dini nzuri na dhehebu ovu? Makanisa yote yanayoamini katika Mungu wa kweli ni dini nzuri. Yale yote yanaoamini miungu ya uongo, pepo wabaya, au Shetani ibilisi ni madhehebu maovu. Yote ambayo yanatetea kumpinga Mungu, vikwazo vinavyopinga Mungu kama vile ukanaji Mungu na mageuzi yote ni madhehebu mabaya. Sasa, Umeme wa Mashariki ndilo linalohukumiwa kwa ukali na kuchukuliwa hatyua kali za kisheria na CCP. Dunia nzima inaweza kuona hili wazi kabisa. Ikiwa watu wanaweza kweli kutofautisha, wanapaswa kuona kile ambacho serikali hii ya Shetani inakataa na kudharau, na wanaweza kuwa na hakika ni njia gani ya kweli. CCP huchukia ukweli na kuogopa watu kukubali kweli. Hiyo ndiyo maana kinampinga Mungu kwa ukali sana. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayeonyesha ukweli ili kuwaokoa wanadamu, Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anafanya kazi ya kuokoa na kutakasa wanadamu. Je, huu si ukweli? Kwa njia hii, tunaweza kuona kwa nini CCP kinachukia zaidi Kanisa la Mwenyezi Mungu na kumoinga Mungu zaidi. Wale wote ambao wanasubiri kuonekana kwa Bwana wanapaswa kufungua macho yao na kuona ni nani ambaye anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho!
kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme
Je, ni rahisi kwa mwanadamu kupata ukweli? Ukiona kwamba mtu hawezi kuelewa maana ya kitu kinachomfanyikia, hii ni kwa sababu hamiliki ukweli. Mtu akiweza kuelewa maana ya chochote kinachomfanyikia, iwapo hakuna kitu kinamwathiri katika kumfuata na kumwabudu Mungu, basi anamiliki ukweli. Iwapo wewe ni baridi, una fikira, unamshuku Mungu, ama kumsaliti Mungu kitu kidogo kinapokufanyikia, basi humiliki ukweli. Hutaweza kuelewa maana ya chochote kinachokufanyikia, kwani wewe ni kipofu na huna maarifa ya Mungu! Wale ambao hawamjui Mungu wana shida nyingi sana, siyo? Wale ambao hawamjui Mungu ni wagumu kushughulikia, siyo? Je, watu ambao hawana maarifa ya Mungu wanaweza kumfuata Mungu hadi mwisho? Hilo si jambo rahisi! Watu ambao hawana maarifa ya Mungu wanaweza kumpinga Mungu, kumkana Mungu, ama kumsaliti Mungu wakati wowote. Wao wako katika hatari ya kumsaliti Mungu asilimia mia moja! Je, sasa uko katika hatari yoyote ya kumsaliti Mungu? Nyote mko katika hatari ya hili. Lazima mchukulie kila kitu kwa njia yenye maadili, si jambo rahisi kumwelewa Mungu na kuwa na maarifa ya Mungu. Iwapo humwelewi Mungu, iwapo huna maarifa ya Mungu, basi itakuwa rahisi kwako kuamini uongo wa Shetani. Tunawaita nini wale wanaoamini chochote anachosema joka kubwa jekundu, ama chochote ambacho wale walio katika jamii ya dini wanasema? Wapumbavu! Maneno haya yanatoka wapi? Maneno haya yanatoka kwa kinywa cha ibilisi, na bado unayaamini. Je, wewe si mpumbavu? Umeanguka katika mtego wa Shetani; Shetani amekudanganya kwa ufanisi. Huamini neno la Mungu, huamini utakatifu na haki ya Mungu, huamini kwamba Mungu ni ukweli, lakini unaamini maneno ya Shetani; hii ndiyo tunayoita kuwa kipofu! Je, si Mungu unayemwamini? Iwapo unaamini kwamba maneno ya Shetani ni ukweli, yanawezekana, na ni ya kuaminika, basi ni nani ambaye kwa kweli unamwamini, Mungu ama Shetani? Huwezi kusema kwa hakika, waweza? Je, ni sawa kusema kwamba unamwamini Mungu kwa maneno tu, lakini kwa uhalisi unachoamini zaidi moyoni mwako bado ni Shetani? Je, nyote mnaamini kwamba maneno ya ukweli yanaweza kutamkwa kutoka kwa kinywa cha Shetani? (La, hatuamini.) Kwa hivyo, tunaweza kutumia maneno gani kueleza ukweli huu? (“Mdomo mchafu hauwezi kutamka maneno ya adabu.”) Ndiyo! Msemo huu unatosha. Unapoelewa msemo huu unamaanisha nini kwa kweli, utajua kwamba maneno ya ukweli kamwe hayataweza kutamkwa kutoka kwa kinywa cha Shetani. Kuna baadhi ya watu ambao wanaelewa mafundisho tu, lakini mafundisho hayana faida hapa, kwani punde tu Shetani anasema kitu bado watakiamini: “Haya! Hicho kinaweza kuwa kweli!” Basi wataangamia! “Mdomo mchafu hauwezi kutamka maneno ya adabu.” Ni lazima uamini maneno haya. Maneno ya ukweli hayatawahi kuweza kutamkwa kutoka kinywa cha Shetani. Kila kitu ambacho Shetani hutamka daima ni uongo na uvumi; daima atalaumu, kubadili, kukashifu, na kuharibu jina ya vitu mema! Unaamini hili kuwa kweli? Watu wengi wakikashifu, kueneza uvumi kuhusu, na kulaumu kwa uongo Kanisa la Mwenyezi Mungu, utafanya nini kuhusu hili? Mnaweza kuona kwamba haya yote ni uongo kabisa, mnaweza kupuuza kila kitu wanachosema na kukikataa mioyoni mwenu? Mnapaswa kukataa vitu hivi. Bila kujali kile kinachosemwa, mnapaswa kuwa wazi kuhusu ni nani anakisema. Kama ni maneno yaliyonenwa kutoka kwa kinywa cha Mungu, ni ukweli. Kama ni maneno yaliyonenwa na mwanadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu, yanaaminika. Kama ni maneno yaliyonenwa na asiyeamini, na watu wa dini, ama na joka kubwa jekundu, basi hayaaminiki. Unapaswa kuyakataa kabisa, usiyakubali. Hata kama yanaonekana kuwa ya kweli, bado ni maneno yanayopotosha ukweli, na maneno ya kuharibu jina na lawama ya uongo. Unahisi vipi kuhusu “tukio la Zhaoyuan”? Hili lilikuwa joka kubwa jekundu likijaribu kusingizia, haribu jina na kunasa mtegoni Kanisa la Mwenyezi Mungu. Watu hao hawakumwamini Mwenyezi Mungu kabisa. Wengine kati yao walikuwa wenzi wa Kristo wa uongo, walimwamini Kristo wa uongo na waliipinga nyumba ya Mungu kwa makusudi. Watu hao walikuwa wapinzani wa nyumba ya Mungu. Walipambana na Mungu kwa ajili ya waumini na walikuwa wa mapepo wabaya. Sasa wangewezaje kuchukuliwa kuwa washirika wa Kanisa la Mwenyezi Mungu? Hao hawakuwa washirika la Kanisa la Mwenyezi Mungu kabisa, hakuna yeyote katika nyumba ya Mungu angewakubali. Unaelewa mbona nashiriki kuhusu hili hapa leo? Iwapo mtu kwa kweli ana maarifa na ufahamu wa kweli wa Mungu, hili linaamua kila kitu. Iwapo unaelewa tu mafundisho fulani ya msingi, hayo ni bure, hayawakilishi kwamba una maarifa ya kweli ya Mungu. Iwapo tu una maarifa ya kweli na ufahamu wa Mungu ndipo hutadanganywa na hila za Shetani. Hapo tu ndipo utaweza kuacha uongo wote ambao Shetani husema. Hapo tu ndipo utaweza kushinda majaribu ya Shetani. Hiyo ndiyo hasa ninayomaanisha.
kutoka katika “Mahubiri na Ushirika Kuhusu Neno la Mungu ‘Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III’ (I)” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha XI
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni