10.30.2017

Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

 
       Kufahamu kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mtu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu.

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili


 ukweli, kupata mwili

Mwenyezi Mungu alisema:Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, Mungu ni lazima Awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi. 

10.28.2017

Ni Wale Tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu

Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, ukweli

Ili uwe na ushuhuda kwa Mungu na kuliaibisha joka jekundu ni sharti uwe na kanuni, na sharti: Katika moyo wako ni lazima umpende Mungu na uingie katika maneno ya Mungu. Kama huingii katika maneno ya Mungu, basi hutakuwa na njia ya kumuaibisha Shetani. Katika ukuaji wa maisha yako, unalikataa joka kuu jekundu na kuliletea aibu kamili, na ni hapo tu ndipo hili joka jekundu kweli linaaibika.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kufanya Matendo Mema ya Kutosha Ili Uandae Mwisho Wako wa Safari



siku za mwisho, ukwli, hukumu

Mwenyezi Mungu alisema:Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, ni wazi kwamba, Nimezungumza vizuri pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele na katika mpango Wangu mpya, kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya ili wale ambao wataniona watajipiga kifuani na kuulilia uwepo Wangu bila kukoma. Kwani Ninaleta mwisho wa mwanadamu duniani, na baada ya hapo, Nitaweka wazi tabia Yangu kwa mwanadamu ili wanijuao na wasionijua “watayalisha macho yao” na kuona kwamba kweli, nimekuja kwa wanadamu, duniani mahali ambapo vitu vyote vinazidi kuongezeka. Huu ni mpango Wangu, “kukiri” Kwangu kwa pekee tangu Nimuumbe mwanadamu. Matilaba yangu ni kuona mnafuatilia kwa moyo wenu wote kila Ninachokifanya, maana kiboko Changu kinamkaribia mwanadamu tena, karibu na wale wote wanaonipinga.

10.26.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi Katika Enzi ya Sheria

Yehova , Injili, Umeme wa Mashariki

Kazi katika Enzi ya Sheria

  Mwenyezi Mungu alisema, “Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.”

10.25.2017

Je, Wewe ni Muumini wa Kweli wa Mungu?



katika Mungu, wako wa Kristo, neema

Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Mwenyezi Mungu alisema,  
Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu.

10.24.2017

Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Roho Mtakatifu,Yesu
Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake.

10.23.2017

Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

 

Mwenyezi Mungu alisema: Kila hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu ina umuhimu wake mkubwa. Yesu alipokuja zamani, Alikuwa mwanaume, lakini Mungu anapokuja wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia. Roho Wake anapowasili, Anaweza kuchukua mwili wowote kwa matakwa Yake na mwili huo unaweza kumwakilisha Yeye. 

10.22.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ukweli Kuhusu Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Ukweli Kuhusu Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Mwenyezi Mungu alisemaMpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu-au, inatofautiana kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kutoa wazi hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. 

10.21.2017

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje, kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu na dada wanaomfuata Yesu wangependa kumpa Yesu makaribisho mazuri.

10.20.2017

Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu


       Mwenyezi Mungu alisema:Ni kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu.

10.19.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Mwenyezi Mungu alisema, Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi.

10.16.2017

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo


Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa
I

Nilitaka kulia lakini hakuna mahali palihisi sawa.

Nilitaka kuimba lakini hakuna wimbo ulipatikana.

Nilitaka kuonyesha upendo wa kiumbe aliyeumbwa.

Nikitafuta juu na chini, lakini hakuna maneno yangeweza kusema,

yangeweza kusema jinsi hasa ninavyohisi.

10.15.2017

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana | "Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu"



Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu

Ha … nyimbo ni nyingi na ngoma ni za madaha;

ulimwengu na miisho ya dunia zinakuwa bahari inayosisimka.

Ha … mbingu ni mpya na dunia ni mpya.

10.14.2017

Mwenyezi Mungu Amekuwa Ameketi Kwenye Kiti Kitukufu cha Enzi


Mwenyezi Mungu Amekuwa Ameketi Kwenye Kiti Kitukufu cha Enzi


Mfalme mwenye ushindi amekuwa ameketi kwenye kiti kitukufu cha enzi.

Amekamilisha ukombozi, akiongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu.

Vitu vyote vimo mkononi Mwake. Kwa busara takatifu na nguvu,

Amejenga na kuimarisha Sayuni, kujenga na kuimarisha Sayuni.

10.13.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa


 Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninaweka migawo hii kulingana na uaminifu alionao mwanadamu Kwangu. Wanadamu wote wakitofautishwa kulingana na aina, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu.

10.12.2017

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu.

10.11.2017

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe.

10.08.2017

Kuhusu Biblia (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kuhusu Biblia (4)

Kuhusu Biblia (4)

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wanaamini kwamba kuelewa na kuwa na uwezo wa kufasiri Biblia ni sawa na kutafuta njia ya kweli—lakini, kimsingi, je, vitu ni rahisi sana? Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema.

10.06.2017

NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA: MHALIFU NI NANI?(Ukuzaji)



Utambulisho

Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Filamu hii ya habari inaelezea uzoefu halisi wa Mkristo Mchina, Zhou Haijiang, ambaye alikamatwa na serikali ya CCP, akateswa, na kufa kutokana na kuteswa kwake kwa sababu ya imani yake kwa Mungu na utendaji wake wa kazi. 

10.05.2017

Neno la Mungu Humwongoza Mtu Kuishi Maisha Mapya | Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana



Utambulisho

Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana
I
Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunaimba nyimbo za sifa kubwa Kwako.
Wewe hutuleta katika maisha ya ufalme.
Sisi watu wa ufalme tu katika karamu yako ya fahari,
tukifurahia maneno Yako, tukitakaswa upotovu wetu.
Neno Lako hutuongoza na sisi kukufuata kwa karibu.
Ni neema ya Mungu kwamba tabia yetu ya kishetani imetupiliwa mbali.
Sisi hufurahia neno la Mungu na kuishi maisha mapya mbele Zake.
Kutunza moyo wa Mungu, kumpenda Yeye kwa dhati, kumshukuru na kumsifu.
La la la la la ... la la la la la ...

10.04.2017

Kuhusu Biblia (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kuhusu Biblia (3)


Kuhusu Biblia (3)


Mwenyezi Mungu alisema, Sio kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki.

10.02.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea
 Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu.