Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwokozi Yesu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwokozi Yesu. Onyesha machapisho yote

10.22.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ukweli Kuhusu Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Ukweli Kuhusu Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Mwenyezi Mungu alisemaMpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu-au, inatofautiana kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kutoa wazi hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.