XI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Uhusiano kati ya Mungu na Biblia
Ni kwa jinsi gani mtu anafaa kuisogelea na kuitumia Biblia kwa njia inayokubaliana na mapenzi ya Mungu? Thamani ya asili ya Biblia ni nini?
“Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai” (Yohana 5:39-40).
Maneno Husika ya Mungu:
Leo, Ninaichambua Biblia kwa namna hii na haimaanishi kwamba Naichukia, au kukana thamani yake kwa ajili ya marejeleo. Ninakuelezea na kukufafanulia thamani ya asili na chanzo cha Biblia ili uweze kuondoka katika giza. Maana watu wana mitazamo mingi kuhusu Biblia, na mingi yao ina makosa; kusoma Biblia kwa namna hii sio tu kunawazuia kupata kile wanachopaswa kupata, lakini, muhimu zaidi, kunazuia kazi Niliyokusudia kufanya.