X. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Jinsi ya Kumjua Mungu
Ni vipi Mungu huutawala na kuusimamia ulimwengu mzima?
Ni viumbe wangapi wanaoishi na kuzaana katika ulimwengu mpana, wakifuata sheria ya maisha tena na tena, wakifuata sheria isiyobadilika. Wanaokufa huenda na hadithi za walio hai, na walio hai hurudia historia hii yenye huzuni ya wale waliokufa. Na kwa hivyo wanadamu hawawezi kujizuia ila kujiuliza wenyewe; Kwa nini tunaishi? Na kwa nini inatulazimu kufa? Nani anayeitawala dunia hii? Na ni nani muumbaji wa mwanadamu?