6.05.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Kwanza


Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Kwanza


Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya hali halisi nzima ya Mungu, na kila kitu Anacho na alicho?

6.04.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Pili

Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Pili

Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena

Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu zake za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu. Ulimwengu mpya kabisa ulijitokeza mbele ya macho Yake, na, kipande kwa kipande, picha nzuri na ya kupendeza ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya fikira Zake ilikuwa tayari imefichuliwa kwa matamshi ya Mungu.

6.03.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Uendelezo wa Sehemu ya Pili



Mamlaka ya Mungu (I) Uendelezo wa Sehemu ya Pili

Kwenye Siku ya Sita, Muumba Aongea, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Akilini Mwake 

Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine


Bila kuchoka, kazi ya Muumba ya kuumba viumbe vyote ilikuwa imeendelea kwa siku tano, na punde tu baada ya hapo ndipo Muumba alipokaribisha siku ya sita ya uumbaji Wake wa viumbe vyote. Siku hii ilikuwa mwanzo mwingine mpya, na siku nyingine isiyo ya kawaida. Nini, basi, kilikuwa mpango wa Muumba mkesha wa siku hii mpya? Ni viumbe vipi vipya ambavyo Angezalisha, je, Angeviumba? Sikiliza, hii ndiyo sauti ya Muumba….

6.02.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Tatu

Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Tatu


2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu.

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

6.01.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Nne



Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Nne
Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayakadiriki

       Hebu tutazame Mwanzo 22:17-18. Hili ni fungu jingine lililozungumziwa na Yehova Mungu, Alisema kwa Ibrahimu, "Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu." Yehova Mungu alimbariki Ibrahimu mara nyingi ili uzao wake uweze kuzidishwa—na kuzidishwa hadi kiwango gani?

5.31.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Tano


Mamlaka ya Mungu (I) Sehemu ya Tano

Maneno yaliyo hapa chini ni lazima katika kujua mamlaka ya Mungu, na maana yake yametolewa kwenye ushirika ulio hapa chini. Hebu tuendelee kuyasoma Maandiko.

4. Amri ya Mungu kwa Shetani

Ayubu 2:6 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.

Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio

5.30.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Kwanza


Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Kwanza

        Kwa vile sasa mmesikiliza ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mmejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kufahamu, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe kwa upekee wake, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango kuu la kujua hali halisi ya ule upekee wa Mungu Mwenyewe.

5.29.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Pili

Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Pili

Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote


Namna Mungu alivyoshughulikia binadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati binadamu anapokabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya kuvumilia na kusamehe binadamu—yaani, wakati onyesho la mwisho la Mungu la huruma na onyo Lake la mwisho linapowafikia—kama bado wangali wanatumia mbinu zile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali huruma Yake, Mungu hataweza tena kuwapatia uvumilivu na subira yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, ni katika wakati huu ambapo Mungu atafuta huruma Yake. Kufuatia hili, Atatuma tu hasira Yake. 

5.28.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Tatu



Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Tatu

Binadamu Hupata Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya Dhati


Kinachofuata ni hadithi ya biblia ya "Wokovu wa Mungu kwa Ninawi."

       Yona 1:1–2 Sasa neno la Yehova likaja kwa Yona mwana wa Amitai, likisema, Amka, nenda Ninawi, mji mkuu, na uipigie kelele, kwani uovu wao umeenda juu mbele yangu.

       Yona 3 Neno lake Yehova likakuja kwake Yona kwa mara ya pili, likisema, Inuka, nenda Ninawi, mji huo mkuu; na uuhubirie mahubiri ninayokuambia. Kwa hivyo Yona akainuka, na kuenda Ninawi, kulingana na neno la Yehova. Sasa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa safari ya siku tatu. 

5.27.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Nne


Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Nne

Kutubu kwa Kweli Ndani ya Mioyo ya Waninawi Kunawapa Rehema ya Mungu na 

Kwabadilisha Hatima Zao Wenyewe



Je, kulikuwa na kuhitilafiana kokote kati ya mabadiliko ya moyo wa Mungu na hasira Yake? Bila shaka la! Hii ni kwa sababu uvumilivu wa Mungu kwa wakati ule ulikuwa na sababu yake. Je, sababu yake yaweza kuwa nini? Ni ile iliyotajwa kwenye Biblia: "Kila mtu aligeuka kutoka kwenye njia yake ya maovu" na "kuacha udhalimu uliokuwa mikononi mwake."

5.26.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Tano



Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Tano
Aina Tano za Watu

Kwa sasa, Nitaacha ushirika wetu kuhusu tabia ya haki ya Mungu umalizikie hapo. Kinachofuata Nitaainisha wafuasi wa Mungu katika kategoria mbalimbali, kulingana na ufahamu wao wa Mungu na ufahamu wao na kile wamepitia kuhusiana na tabia ya haki Yake, ili muweze kujua awamu ambayo kwa sasa mnapatikana ndani pamoja na kimo chenu cha sasa. Kuhusiana na maarifa yao ya Mungu na ufahamu wao wa tabia Yake ya haki, awamu na kimo tofauti ambavyo watu huwa navyo vinaweza kugawanywa katika aina tano. Mada hii imeelezewa kwa msingi wa kumjua Mungu wa kipekee na tabia Yake ya haki;

5.25.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Kwanza

Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Kwanza

Leo tutaendelea na ushirika wetu kuhusu mada ya "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee." Tayari tumekuwa na ushirika mara mbili katika mada hii, wa kwanza kuhusiana na mamlaka ya Mungu na wa pili kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika huu mara mbili, je, mmepata ufahamu mpya wa utambulisho wa Mungu, hadhi, na hali halisi? Je, maono haya yamewasaidia kufikia maarifa mazito zaidi na uhakika wa ukweli kuuhusu uwepo wa Mungu? Leo Ninapanga kufafanua mada hii ya "Mamlaka ya Mungu."