Utakatifu wa Mungu (III) Sehemu ya Pili
Tumetoka tu kuongea kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu, basi kinachofuata wacha tushiriki kuhusu jinsi Shetani hutumia sayansi kumpotosha mwanadamu. Kwanza, Shetani hutumia jina la sayansi kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu, kuridhisha hamu ya mwanadamu[a] kutafiti sayansi na kuchunguza siri. Pia, katika jina la sayansi, Shetani huridhisha haja ya mwili na mahitaji ya mwanadamu kuendelea kuinua ubora wao wa maisha. Shetani hivyo, katika jina hili, hutumia njia ya sayansi kumpotosha mwanadamu. Je, ni kufikiria tu kwa mwanadamu ama akili za mwanadamu ambazo Shetani anapotosha kwa kutumia njia hii ya sayansi? Miongoni mwa watu, matukio na mambo katika mazingira yetu ambayo tunaweza kuona na ambayo tunakutana nayo, ni yapi mengine ambayo Shetani anatumia sayansi kupotosha? (Mazingira ya kiasili.) Mko sahihi.