Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Pili
Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu
3. Sauti
Kitu cha tatu ni nini? Ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Ni kitu ambacho Mungu alishughulikia alipoumba vitu vyote. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kila mtu. Kama Mungu hakushughulikia suala hilo, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Pia inaweza kusemwa kwamba viumbe vyote vyenye uhai haviwezi kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Hivyo hiki ni kitu gani? Ni sauti.