Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Nne
Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu
Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia. Watu wengi huuliza: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? (Kuku.) Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hilo ni hakika! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingetangulia? Je, kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Mayai huangua kuku, kuku huatamiza mayai. Baada ya kuatamiza mayai kwa siku 21, kuku huangua. Kisha kuku huyo hutaga mayai, na kuku huanguliwa tena kutoka kwa mayai. Hivyo kuku alitangulia au yai lilitangulia? Mnajibu "kuku" kwa uhakika.