2.05.2018

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu


Mwenyezi Mungu alisema, Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na kinachopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako.

2.04.2018

Umeme wa Mashariki | Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia


Mwenyezi Mungu alisema, Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama watu, wanaotembea na Mimi hadi leo, hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na ningali nafanya hivyo sasa. Ingawaje kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio lake linabakia lilelile.

Ngurumo Saba Zatoa Sauti— Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Injili

Ngurumo Saba Zatoa Sauti— Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni
Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika mtawanyiko wa wanadamu, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi ambayo Nimewapa. Kuanzia wakati huu kuendelea, Nimeingia katika enzi mpya, kuwaleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Niliporudi katika “nchi Yangu,” Nilianza sehemu nyingine tena ya kazi katika mpango Wangu wa asili, ili mwanadamu aje kunijua zaidi. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba[a] ni wakati muafaka wa kazi Yangu, kwa hiyo Naharakisha mbele na nyuma kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu.

2.03.2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?


Mwenyezi Mungu alisema, Je, unaweza kuonyesha tabia ya Mungu ya nyakati kwa lugha inayofaa iliyo na umuhimu wa nyakati? Kupitia uzoefu wako wa kazi ya Mungu, unaweza kueleza kwa undani tabia ya Mungu? Utaielezaje vizuri, kikamilifu? Ili kupitia haya, watu wengine wapate kufahamu uzoefu wako. 

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu.

2.02.2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (8)

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, Mungu

Njia... (8)


Mwenyezi Mungu alisema, Wakati ambapo Mungu anakuja duniani kuchanganyika na wanadamu, kuishi nao, sio tu kwa siku moja au mbili. Labda kwa wakati huu wote watu wamemjua Mungu kwa kiwango fulani, na labda wamepata utambuzi muhimu wa kumhudumia Mungu, na wamepata uzoefu sana katika imani yao katika Mungu. Hata iweje, watu wanaelewa vizuri sana tabia ya Mungu, na maonyesha ya kila aina ya tabia za binadamu yanatofautiana kwa kweli. Jinsi Nionavyo, maonyesho tofautitofauti ya watu yanatosha kwa Mungu kuyatumia kama sampuli, na shughuli zao za fikira zinatosha kwa Yeye kurejelea.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (7)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Biblia

Njia… (7)


Mwenyezi Mungu alisema, Sote tunaweza kuona katika uzoefu wetu wa utendaji kwamba kuna nyakati nyingi ambazo Mungu binafsi ametufungulia njia ili tuwe tunakanyaga njia iliyo imara zaidi, ya kweli zaidi. Hii ni kwa sababu hii ndiyo njia ambayo Mungu alitufungulia tangu mwanzo wa wakati na imepitishwa kwa kizazi chetu baada ya makumi ya maelfu ya miaka. Kwa hiyo tunarithi watangulizi wetu ambao hawakutembea njia hii mpaka mwisho wake; sisi ndio tumechaguliwa na Mungu kutembea sehemu ya mwisho ya njia hii. Hivyo, imetayarishiwa hasa sisi, na haijalishi ikiwa tutapokea baraka au kupata taabu, hakuna mwingine anayeweza kutembea njia hii.

2.01.2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (6)

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, ukweli

Njia... (6)


Mwenyezi Mungu alisema, Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu ndio tumeletwa katika siku hii. Kwa hiyo, sisi sote ni wasaliaji katika mpango wa usimamizi wa Mungu, na kwamba tunaweza kubakizwa mpaka siku hii ni kutiwa moyo kwa hali ya juu kutoka kwa Mungu. Kulingana na mpango wa Mungu, nchi ya joka kuu jekundu inapaswa kuangamizwa, lakini Ninadhani kwamba labda Ameanzisha mpango mwingine, au Anataka kutekeleza sehemu nyingine ya kazi Yake. Kwa hiyo mpaka leo Sijaweza kuueleza kwa dhahiri—ni kama kwamba ni kitendawili kisichofumbuliwa. Lakini kwa jumla, kundi hili letu limejaaliwa na Mungu, na Ninaendelea kuamini kwamba Mungu ana kazi nyingine ndani yetu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (5)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Mungu

Njia… (5)


Mwenyezi Mungu alisema, Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mbele ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba karibu watu wote wanaoamini katika Mungu hawamjui Roho, lakini tu wana aina ya imani iliyochanganyikiwa. Ni wazi kutokana na hili kwamba watu hawamfahamu Mungu, na hata ingawa wanasema wanaamini katika Yeye, kuhusu kiini chake, kulingana na matendo yao wanaamini katika wao wenyewe, sio Mungu.

1.31.2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia

Njia… (4)


Mwenyezi Mungu alisema, Kwamba watu wanaweza kugundua kupendeza kwa Mungu, kutafuta njia ya kumpenda Mungu katika enzi hii, na kwamba wako radhi kukubali mafunzo ya ufalme wa leo—hii yote ni neema ya Mungu na hata zaidi, ni Yeye ndiye anawainua wanadamu. Kila Nifikiriapo juu ya hili Mimi huhisi kwa uthabiti kupendeza kwa Mungu. Ni kweli kwamba Mungu anatupenda. La sivyo, nani angeweza kutambua kupendeza Kwake? Ni kutoka tu kwa hili ndio Naona kwamba kazi hii yote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na watu wanaongozwa na kuelekezwa na Mungu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (3)

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, Yesu

Njia… (3)


MwenyeziMungu alisema, Katika maisha Yangu, Niko radhi kila mara kujitolea Mwenyewe kwa Mungu kabisa, mwili na fikra. Kwa njia hii, hakuna lawama kwa dhamiri Yangu na Naweza kupata kiasi kidogo cha amani. Mtu anayeandama uzima ni lazima kwanza aukabidhi moyo wake wote kwa Mungu kabisa. Hili ni sharti la mwanzo. Ningependa ndugu na dada Zangu wamwombe Mungu pamoja na Mimi: “Ee Mungu! Roho Wako aliye mbinguni awape neema watu walio duniani ili moyo Wangu uweze kukugeukia Wewe kikamilifu, kwamba Roho Yangu iweze kusisimuliwa Nawe, na kwamba Niweze kuona kupendeza Kwako ndani ya moyo Wangu na Roho Yangu, ili wale walio duniani wabarikiwe kuuona uzuri Wako.

1.30.2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (2)

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, ukweli

Njia… (2)


Mwenyezi Mungu alisema, Labda ndugu na dada zetu wana muhtasari kidogo wa utaratibu, hatua, na mbinu za kazi ya Mungu katika China bara, lakini Mimi huhisi kila mara kwamba ni heri kuwa na kumbukumbu au muhtasari kidogo wa ndugu na dada zetu. Ninatumia tu nafasi hii kusema machache ya kile kilicho moyoni Mwangu; Sizungumzi juu ya chochote nje ya kazi hii. Natarajia kwamba ndugu na dada wanaweza kuelewa hali ya moyo Wangu, na pia Naomba kwa unyenyekevu kwamba wote wanaosoma maneno Yangu wafahamu na kusamehe kimo Changu kidogo, kwamba uzoefu Wangu wa maisha kweli si wa kutosha, na kwamba kweli Siwezi kuwa na ujasiri mbele ya Mungu. Kwa hali yoyote, Mimi huhisi kila mara kwamba hizi ni sababu halisi tu.