Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu.
Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Ubora wenu wa tabia ni duni sana. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile kinachosemwa. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika. Mambo mengi hayawezi kusemwa kwenu moja kwa moja na athari ya awali haiwezi kutimizwa. Kwa hiyo, kazi za ziada zinapaswa kuongezwa kwa kazi Yangu. Ni muhimu kuzindua kazi hii ya "kuinua ubora wa tabia ya watu" miongoni mwenu kwa sababu uwezo wenu wa kupokea, uwezo wa kuona mambo, na viwango vya maisha yenu ni maskini sana. Huu ndio mwelekeo unaohitajika; hakuna uchaguzi badili, na ni lazima ufanyike kwa namna hii ili sehemu ya matokeo iweze kutimizwa. Vinginevyo, maneno yote Ninayosema hayatafanikiwa, na hamngekumbukwa kama wenye dhambi? Je! Hamngekuwa wapotovu? Je, kazi hii inafanywa kwenu ni nini? Nini kinachohitajika kwenu? Je, hamjui? Mnapaswa kujua ubora wenu wenyewe wa tabia; hauwezi kufikia kile Ninachohitaji kamwe. Je, hii haicheleweshi kazi? Kwa ubora wa tabia na hulka yenu ya sasa, hakuna hata mmoja wenu ambaye anafaa kushuhudia kwa ajili Yangu, na hakuna mtu anayewezana na kazi ya kulichukua jukumu kubwa la kazi Yangu ya baadaye. Je, hamhisi aibu sana kuhusu hili? Itawezekanaje kuyakidhi matakwa Yangu yote kama hili linaendelea kutendeka? Unapaswa kufanya maisha yako yawe kamili na yenye thawabu. Usiruhusu muda upite bure. Hakuna thamani katika kufanya hivyo. Unapaswa kujua mambo ambayo inabidi kujiandaa nayo. Usijione kuwa mjuaji wa kila kitu. Hukaribii hata kidogo! Je! Kuna nini cha kuzungumzia ikiwa huna hata ufahamu wa kimsingi wa ubinadamu? Je, si vyote havingekuwa na maana? Hakuna hata mmoja kati yenu aliye na sifa zinazostahili kabisa kwa mintarafu ya kile Ninachohitaji kwa ubora wa tabia ya kibinadamu. Ni vigumu kupata mtu ambaye anafaa kutumiwa. Mnaamini ninyi ni watu ambao wanaweza kufanya kazi kubwa zaidi kwa ajili Yangu na kujitwika ukabidhi mkubwa kutoka Kwangu. Kwa kweli, hamjui jinsi hata ya kuingia katika masomo mengi mbele yenu, hivyo ingewezekanaje kuingia katika kweli za kina? Lazima kuingia kwenu kuwe kwenye utaratibu. Msifanye hivyo bila mpango. Hili si jambo la manufaa. Ingieni kutoka mwisho wenye kina kifupi—yasome maneno haya mstari kwa mstari hadi mfikie ufahamu na ubayana. Kila ndugu angalau anapaswa aweze kusoma. Usilitazame mara moja tu kwa haraka, na usilifanye kwa namna isiyo ya dhati. Kwa kawaida, unaweza pia kusoma baadhi ya kazi za kumbukumbu (kama vile sarufi au vitabu vya balagha). Hakuna haja ya kusoma vitabu vinavyoichochea akili yako sana (riwaya za mapenzi, ponografia, magazeti, au wasifu za watu mashuhuri), ambavyo husababisha madhara zaidi kuliko mema. Lazima uwe mweledi wa yote unayopaswa kuingia na unapaswa kufahamu. Madhumuni ya kuendeleza ubora wa tabia sio mengine ila kuwasaidia watu kujua asili yao wenyewe, utambulisho, hadhi au thamani. Nini jambo kuu ambalo makanisa hapa chini yanapaswa kuingia? Je, watu hawaongezi ubora wa tabia yao sasa? Ni muhimu kushikilia kuingia huku kwa kugeuka kuwa msomi; hakuwezi kuachiliwa huru! Kipengele kimoja ni kwamba lazima ninyi muelewe kwa nini ubora wa tabia ya watu unapaswa kuendelezwa, jinsi ubora wa tabia unaweza kuendelezwa, na vipengele vipi vya kuingia. Lazima muelewe maana ya ubinadamu wa kawaida, kwa nini kazi hii inapaswa kufanywa, na jinsi inapaswa kuratibiwa. Katika kuelimika, ni vipengele vipi vinayopaswa kufunzwa, na jinsi gani mtu anapaswa kuingia? Nyote mnapaswa kujua lengo la kuelimika ni nini. Je, sio kuyafahamu maneno ya Mungu na kuingia katika ukweli? Hali inayosambaa makanisani sasa ni ipi? Mkimwomba mtu apate kuelimika, anasahau kuhusu furaha ya maneno ya Mungu. Mkizungumza kuhusu ubinadamu wa kawaida, anashughulikia tu kuisafisha nyumba yake, kufagia sakafu au kupika, kusafisha jikoni na kununua vyombo vya kupika. Anajali tu kuhusu mambo haya na hajui jinsi ya kuishi maisha ya kanisa kwa kawaida. Vinginevyo anatafuta tu maneno katika kamusi na kujifunza maneno mapya, lakini hafanyi jambo lingine lolote siku nzima. Umepotoka ikiwa unabaki katika hali ya sasa. Basi kwa nini unaombwa kuingia katika maisha ya kiroho? Yote unayojifunza ni mambo haya ambayo hayawezi kukusaidia kufikia kile kinachohitajika kwako. Jambo la muhimu zaidi bado ni kuingia kwa maisha. Sababu ya kufanya kazi hii ni kutatua shida ambazo watu hukumbana nazo katika uzoefu wao. Kuinua ubora wa tabia kunakuwezesha kujua ubinadamu na kiini cha mwanadamu—kusudi kuu la kuyajua mambo haya ni ili maisha ya watu ya kiroho yaweze kukua na tabia yao iweze kubadilika. Unaweza kujua jinsi ya kuvaa na kupendeza; unaweza kuwa na utambuzi na hekima, na hata hivyo hatimaye, siku inapokuja kwako kuenda kazini, unashindwa kufanya hivyo. Unapaswa kujua, kwa hiyo, kile unapaswa kufanya pia wakati unainua ubora wako wa tabia. Kukubadilisha ni lengo. Kuinua ubora wa tabia ni jambo la ziada. Haitakubalika kama ubora wako wa tabia hauendelezwi. Ni vibaya hata zaidi ikiwa tabia yako haiwezi kubadilishwa. Moja bila ya nyingine haitoshi. Kuwa na ubinadamu wa kawaida hakumaanishi kwamba umekuwa na ushuhuda mkubwa sana. Kile kinachohitajika kwako si rahisi sana.
Wakati ambapo ubora wa tabia ya mtu umeendelea kiasi kwamba ana hisia na mtindo wa maisha ya ubinadamu wa kawaida na pia kuwa na kuingia kwa maisha, ni hapo tu ndipo ataweza kubadilika na kushuhudia. Siku ya kutoa ushuhuda inapofika, pia kuna haja ya kuzungumza kuhusu mabadiliko katika maisha ya binadamu na kuhusu ufahamu wa Mungu ndani. Mchanganyiko wa vipengele hivi viwili tu ndio ushahidi wa kweli na faida yako ya kweli. Haitakubalika ikiwa una mabadiliko tu katika ubinadamu kwa nje na huna ufahamu kwa ndani. Haitakubalika pia ikiwa una ufahamu na ukweli kwa ndani lakini hutilii maanani kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida. Kazi inayofanyika kwako leo sio kuwaonyesha wengine bali kukubadilisha. Unahitaji tu kuzingatia kujibadilisha. Unaweza kuandika na kusikiliza kila siku, lakini haitawezekana ikiwa hushiriki katika maeneo mengine ya maisha yako. Unapaswa kuwa na kuingia katika kila kipengele. Unapaswa kuwa na maisha ya kawaida ya mtakatifu. Akina dada wengi huvaa kama wanawake matajiri na kaka wanavaa kama waungwana matajiri au mabwana, wakipoteza kabisa ustahifu wa watakatifu. Kipengele kimoja ni kuinua ubora wa tabia ya mtu, ambacho kinaweza kufanikishwa kwa kawaida. Kipengele kingine cha umuhimu mkubwa ni kula na kunywa maneno ya Mungu. Je, haingekuwa kupoteza elimu ikiwa ubora wako wa tabia umeinuliwa lakini haukukutumiwa kwa sababu hukula na kunywa maneno ya Mungu? Lazima vipengele vyote viwili viunganishwe. Kwa nini maarifa ya Mungu yanatajwa katika majadiliano ya kile kinachohitajika kwako? Je, hii si kwa ajili ya matokeo ya kazi ya baadaye? Baada yako kushindwa, lazima uweze kushuhudia kutokana na uzoefu wako mwenyewe. Haitakubalika kama sura yako ya nje ni moja ya ubinadamu wa kawaida lakini huwezi kuonyesha uzoefu wako kupitia kinywa chako. Unapokuwa na maisha ya kawaida ya kiroho, unapaswa kufikia ubinadamu wa kawaida, na vipengele vingi vya ubinadamu wa kawaida vitaweza kufunzwa kwa dhahiri. Je, ungesema kwamba kufagia sakafu kunahitaji mafunzo maalum? Ikiwa unahitaji kutumia saa moja kufanya mazoezi jinsi ya kushikilia vijiti kwa kula, hiyo haikubaliki hata zaidi! Ubinadamu wa kawaida unashirikisha vipengele hivi: utambuzi, hisia, dhamiri na tabia. Iwapo unaweza kufanikisha ukawaida katika kila mojawapo ya vipengele hivi, ubinadamu wako uko katika kiwango kinachostahili. Unapaswa kuwa na mfanano wa binadamu wa kawaida na utende kama anayemwamini Mungu. Sio lazima ufikie viwango vya juu zaidi au kujishughulisha na diplomasia. Unapaswa tu kuwa mwanadamu wa kawaida, na hisia za kawaida za mtu, uweze kung’amua vitu, na kwa kiwango cha chini uonekane kama mwanadamu wa kawaida. Hiyo itakuwa imetosha. Kila kitu kinachohitajika kwako leo kiko katika uwezo wako, na huku si kukulazimisha ufanye kadri ya uwezo wako hata kidogo. Hakuna maneno yasiyo na maana au kazi isiyofaa yatatekelezwa kwako. Uovu wote ulioonyeshwa au kufichuliwa katika maisha yako lazima uondolewe. Ninyi mmepotoshwa na Shetani na mna sumu nyingi sana za Shetani. Yote ambayo yanahitajika kwako ni kuiepuka tabia hii potovu ya kishetani, si wewe kuwa mtu mwenye cheo cha juu, au mtu maarufu au mkuu. Hii haina maana. Kazi ambayo imefanyika kwenu inaafikiana na kile ambacho ni cha asili kwenu. Kuna mipaka ya kile Ninachohitaji kutoka kwa watu. Ikiwa watu wa leo wote wangeulizwa kutenda kama watu wa kada za Kichina, na kujizoeza toni ya sauti ya kada za Kichina, kujifunza katika namna ya kuzungumza ya viongozi wa serikali wenye cheo cha juu, au kujifunza kwa namna na sauti ya kuzungumza ya waandishi wa insha na waandishi wa riwaya, basi hili halingekubalika pia. Halingeweza kufikiwa. Kwa mujibu wa ubora wa tabia za watu hawa, wanapaswa angalau kuweza kuzungumza kwa hekima na busara na kuelezea mambo wazi. Ni wakati huo ndipo watakapoyatosheleza mahitaji. Kwa kiwango kidogo sana, utambuzi na hisia vinapaswa kufikiwa. Kwa sasa jambo kuu ni kuitupilia mbali tabia potovu ya kishetani. Lazima uutupilie mbali uovu unaouonyesha. Ikiwa hujavitupilia mbali hivi, unawezaje kugusia hisia na utambuzi wenye mamlaka mkubwa kabisa? Watu wengi wanaona kwamba enzi imebadilika. Hivyo hawajizoezi unyenyekevu au uvumilivu wowote, na pengine pia hawana upendo wowote au mwenendo mwema wa kitakatifu pia. Watu hawa ni wajinga mno! Je, wana kiwango chochote cha ubinadamu wa kawaida? Je, wanao ushuhuda wowote wa kuzungumziwa? Hawana utambuzi na hisia zozote kamwe. Bila shaka, vipengele fulani vya utendaji wa watu vilivyopotoka na vyenye makosa vinapaswa kurekebishwa. Kama vile maisha ya watu ya kiroho yasiyopindika au mwonekano wenye ganzi na upumbavu wa zamani—vitu hivi vyote vinapaswa kubadilika. Mabadiliko hayamaanishi kukuruhusu uwe mpotovu au kujiingiza katika mwili, au kusema chochote utakacho. Kuzungumza kiholela hakuwezi kukubalika! Kutenda kama mwanadamu wa kawaida ni kuzungumza kwa kueleweka. Ndiyo inamaanisha ndiyo, na la inamaanisha la. Kuwa mwenye ukweli kwa uhakika na uzungumze inavyofaa. Usilaghai, usidanganye. Inapaswa kujulikana ni mipaka gani mtu wa kawaida anaweza kufikia kuhusu mabadiliko ya tabia. Ikiwa hiyo haijulikani, hutaweza kuingia katika uhalisi.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni