6.29.2019

1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?


1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?


Aya za Biblia za Kurejelea:

“Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17).

“Na kwamba toba na msamaha wa dhambi vinapaswa kuhubiriwa katika jina lake miongoni mwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu” (Luka 24:47).

“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).

“Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya Yesu ilikuwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu na kusulubiwa tu. Kwa hivyo, hakukuwa na haja Kwake kusema maneno zaidi ili kumshinda mtu yeyote. Mengi ya yale Aliyomfundisha mwanadamu yalitolewa kutoka kwa Maandiko, na hata kama kazi yake haikuzidi Maandiko, bado Aliweza kutimiza kazi ya kusulubiwa. Yake haikuwa kazi ya neno, wala kwa ajili ya kumshinda mwanadamu, lakini kwa minajili ya kumkomboa mwanadamu. Yeye Alihusika kama dhabihu ya dhambi tu kwa mwanadamu, na hakuhusika kama chanzo cha Neno kwa mwanadamu.

kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wakati huo, Yesu alizungumza tu na wanafunzi Wake mfululizo wa mahubiri kwa Enzi ya Neema, kama jinsi ya kuweka vitendoni, jinsi ya kukusanyika pamoja, jinsi ya kuuliza kwa maombi, jinsi ya kuwatendea wengine, na mengineyo. Kazi Aliyoifanya ilikuwa hiyo ya Enzi ya Neema, na alielezea tu juu ya jinsi wanafunzi na waliomfuata wanapaswa kuweka vitendoni. Alifanya tu kazi ya Enzi ya Neema na hakuna hata moja ya siku za mwisho. Wakati Yehova aliandika sheria ya Agano la Kale kwa Enzi ya Sheria, mbona basi hakufanya kazi ya Enzi ya Neema? Mbona hakueleza wazi mapema kazi ya Enzi ya Neema? Hii haingekuwa ya manufaa kwa kukubali kwa mwanadamu? Alitabiri tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa na kuja mamlakani, lakini Hakutekeleza mapema kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu jinsi mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani, ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu.

kutoka katika “Ni Jinsi Gani Mwanadamu Ambaye Amemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hebu kwanza tuangalie katika kila sehemu ya “Ibada Mlimani.” Haya yote yanahusiana na nini? Yaweza kusemekana kwa uhakika kwamba haya yote yameinuliwa zaidi, yana uthabiti zaidi na karibu zaidi katika maisha ya watu kuliko taratibu zile za Enzi ya Sheria. Kuzungumza katika muktadha wa kisasa, yanahusiana zaidi na matendo halisi ya watu.

Hebu tusome maudhui mahususi ya yafuatayo: Mnafaa kuzielewa vipi hali hizi za heri? Ni nini mnachofaa kujua kuhusu sheria? Ghadhabu inafaa kufasiliwa vipi? Wazinzi wanafaa kushughulikiwa vipi? Ni nini kinachosemwa, na ni sheria aina gani zipo kuhusu talaka, na ni nani anayeweza kutalikiwa na ni nani asiyeweza kutalikiwa? Na je, viapo, jicho kwa jicho, kuwapenda adui zako, maagizo kuhusu sadaka, n.k? Mambo haya yote yanahusu kila kipengele cha matendo ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, na ufuataji wao wa Mungu. Baadhi ya desturi hizi zinatumika leo, lakini bado yapo katika hali ya kimsingi kuliko mahitaji ya sasa ya watu. Kwa kiasi kikubwa uko katika hali ya kimsingi ambao watu wanakumbana nao katika kuamini kwao katika Mungu. Tangu wakati Bwana Yesu alianza kufanya kazi, Alikuwa tayari anaanza kufanya kazi kwa tabia ya maisha ya binadamu, lakini yalitokana na msingi wa sheria. Je, sheria na misemo kuhusu mada hizi ilikuwa na uhusiano wowote na ukweli? Bila shaka zilikuwa nao! Taratibu, kanuni na ibada zote zingine za awali katika Enzi ya Neema zilikuwa na uhusiano, na tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho na bila shaka kwa ukweli. Haijalishi ni nini ambacho Mungu anaonyesha, kwa njia gani Anaonyesha, au Akitumia lugha gani, asili yake, na mwanzo wake, vyote vinatokana na kanuni za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hili halina kosa. Kwa hivyo ingawa haya mambo Aliyoyasema yanaonekana kuwa ya juujuu, bado hamwezi kusema kwamba mambo haya si ukweli, kwa sababu yalikuwa mambo ambayo yalikuwa ya lazima kwa watu katika Enzi ya Neema ili kuridhisha mapenzi ya Mungu na kutimiza mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Unaweza kusema kwamba mambo yoyote yale katika ibada hayaambatani na ukweli? Huwezi! Kila mojawapo ya mambo haya ni ukweli kwa sababu yote yalikuwa mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu; yote yalikuwa kanuni na mawanda yaliyotolewa na Mungu kuhusu namna ambavyo unaweza kuwa na mwenendo, na yanawakilisha tabia ya Mungu. Hata hivyo, kutokana na kiwango cha ukuaji wao katika maisha wakati huo, waliweza tu kukubali na kuyafahamu mambo haya. Kwa sababu dhambi ya mwanadamu ilikuwa bado haijatatuliwa, Bwana Yesu angeweza tu kuyatoa maneno haya, na Angeweza kutumia mafundisho mepesi kama hayo miongoni mwa aina hii ya upana ili kuwaambia watu wa wakati huo namna ambavyo walifaa kutenda, kile walichofaa kufanya, ndani ya kanuni na upana gani walifaa kufanya mambo, na vipi walivyofaa kuamini katika Mungu na kutimiza mahitaji Yake. Haya yote yaliamuliwa kulingana na kimo cha mwanadamu wakati huo. Haikuwa rahisi kwa watu wanaoishi katika sheria kuyakubali mafundisho haya, hivyo basi kile Alichofunza Bwana Yesu lazima kingebaki ndani ya mawanda haya.

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ambayo Mungu Alizungumza katika enzi hii ni tofauti na yale yaliyozungumzwa katika Enzi ya Sheria, na kwa hivyo, pia yako tofauti na maneno yaliyonenwa katika Enzi ya Neema. Katika Enzi ya Neema, Mungu hakufanya kazi ya neno, lakini Alieleza tu usulubisho ili kuwakomboa binadamu wote. Biblia inaelezea tu ni kwa nini Yesu alikuwa Asulubiwe, na mateso ambayo Alipitia kwenye msalaba, na jinsi mwanadamu anapaswa kusulubiwa kwa ajili ya Mungu. Katika enzi hiyo, kazi yote iliyofanywa na Mungu ilikuwa kuhusu usulubisho. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, “Neno kuonekana katika mwili”; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili.” Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapumziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaufanyikia Misri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili.

kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kile ambacho Nasema leo ni kuhukumu dhambi za watu na maovu yao; ni kulaani uasi wa watu. Udanganyifu na upotovu wao, na maneno na matendo yao, mambo yote ambayo hayako sambamba na mapenzi Yake yatapitia hukumu, na uasi wa watu unaamuliwa kuwa wenye dhambi. Ananena kulingana na kanuni za hukumu, naye anadhihirisha tabia Yake yenye haki kwa kuhukumu maovu yao, kulaani uasi wao, na kufichua nyuso zao zote mbaya.

kutoka katika “Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika, uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu.

kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.

kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ingawa neno “neno” ni rahisi na la kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu mwenye mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Kuanzia wakati huu kuendelea, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, wakichungwa na kuruzukiwa na neno. Binadamu wote wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata kuna binadamu zaidi wanaoishi chini ya hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kwa minajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa minajili ya kubadilisha sura asilia ya ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, na pia hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa.

kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wakati huo, Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haikueleweka kwa wanafunzi Wake, na kusema mengi kwamba watu hawakuelewa. Hii ni kwa sababu, wakati huo, Hakutoa maelezo. … Yesu hakuja kumkamilisha na kumpata mwanadamu, lakini kufanya awamu moja ya kazi: kuleta injili ya ufalme wa mbinguni na kukamilisha kazi ya kusulubiwa—na punde tu Yesu Aliposulubishwa, kazi Yake ilifika mwisho kamili. Lakini kwa awamu iliyoko sasa—kazi ya ushindi—maneno mengi zaidi lazima yasemwe, kazi nyingi zaidi lazima ifanywe, na lazima kuwe na hatua nyingi. Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kujua. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kumaliza kazi ya Mungu? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kumalizia. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno Yake pia yalifika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimyakimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko yake ingine na makosa yake yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo.

kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili


Tazama zaidi: Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haitabadilika kamwe


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni