2.07.2019

Neno la Mungu | Sura ya 29

Kati ya kazi inayofanywa na watu, baadhi yake hutekelezwa kwa maagizo ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu, lakini kwa sehemu yake Mungu hatoi maagizo ya wazi, ikionyesha vya kutosha kwamba kile kinachofanywa na Mungu, leo, bado hakijafichuliwa kabisa—ambalo ni kusema, mengi bado yamefichwa na bado hayajajulikana na watu. Lakini mambo mengine yanahitaji kujulikana na watu, na kuna mwengine yanayohitaji kuwaacha watu wakiwa wamekanganywa na kuchanganyikiwa; hiki ndicho kinachohitajika na kazi ya Mungu. Kwa mfano, ujio wa Mungu kutoka mbinguni miongoni mwa mwanadamu: jinsi Alivyofika, Alifika kwa sekunde ipi, au kama mbingu na dunia na vitu vyote vilibadilika au la—mambo haya yanahitaji watu kuchanganyikiwa. Hili pia linategemea hali halisi, kwani mwili wa binadamu wenyewe hauwezi kuingia moja kwa moja katika ulimwengu wa kiroho. Hivyo, hata kama Mungu anasema wazi jinsi Alivyokuja duniani kutoka mbinguni, au wakati Anasema, “Siku hiyo ambayo vitu vyote vilifufuliwa, Nilikuja miongoni mwa wanadamu, na Nimeshinda naye kwa siku zilizokuwa za ajabu usiku na mchana,” maneno hayo ni kama mtu akilizungumzia shina la mti—hakuna athari hata kidogo, kwa sababu watu hawazijui hatua za kazi ya Mungu. Hata wakati wanapofahamu kweli, wanaamini kwamba Mungu alipaa kutoka mbinguni hadi duniani kama kichimbakazi na akazaliwa tena miongoni mwa wanadamu. Hili ndilo linalofikiwa na mawazo ya mwanadamu. Ni kwa sababu kiini cha mwanadamu ni kwamba hawezi kuelewa dutu ya Mungu, na hawezi kuelewa ukweli wa ulimwengu wa kiroho. Kwa asili yao pekee, watu hawangeweza kutenda kama mfano kwa wengine, kwa sababu watu wako sawa kwa asili, na si tofauti. Kwa hivyo, kuwataka watu waweze kuwa mfano wa wengine kufuata au kutumika kama mfano kinakuwa kitu kisicho na ukweli wa aina yoyote, inakuwa mvuke unaoinuka kutoka kwa maji. Ilhali Mungu anaposema, “anapata ujuzi fulani kuhusu kile Nilicho nacho na Nilicho,” maneno haya yanahutubiwa tu kwa dhihirisho la kazi ambayo Mungu anafanya katika mwili; kwa maneno mengine, yanaelekezwa kwa uso halisi wa Mungu—uungu, ambao hasa unahusu tabia Yake takatifu. Hiyo ni kusema, watu wanaulizwa kuelewa mambo kama vile kwa nini Mungu anafanya kazi kwa njia hii, ni mambo gani yanayohitajika kufanikishwa kwa maneno ya Mungu, kile ambacho Mungu anataka kutimiza duniani, kile Anachopenda kupata miongoni mwa wanadamu, mbinu ambazo kwazo Mungu hunena, na mtazamo wa Mungu kwa mwanadamu ni upi. Inaweza kusemwa kwamba hakuna kitu kinachostahili kujivunia katika mwanadamu, yaani, hakuna chochote ndani yake ambacho kinaweza kuonyesha mfano wa wengine kufuata.
Ni hasa kwa sababu ya ukawaida wa Mungu katika mwili, kwa sababu ya utofauti wa Mungu aliye mbinguni na Mungu aliye katika mwili, Asiyeonekana kuzaliwa na Mungu aliye mbinguni, ndio Mungu anasema, “Nimepita kati ya wanadamu kwa miaka mingi, lakini hajawahi kufahamu hili, na hajawahi kunijua.” Mungu anasema pia, “Wakati nyayo Zangu zitaukanyaga ulimwengu mzima, mwanadamu ataanza kutafakari juu yake mwenyewe, na watu wote watakuja Kwangu na kusujudu mbele Zangu na kuniabudu. Hii itakuwa siku ya utukufu Wangu, siku ya kurudi Kwangu, na pia siku ya kuondoka Kwangu.” Hii tu ndiyo siku ambayo uso halisi wa Mungu unaonyeshwa kwa mwanadamu. Hata hivyo Mungu hacheleweshi kazi Yake kama matokeo, na Yeye hufanya tu kazi ambayo inapaswa kufanyika. Wakati Anapohukumu, Anahukumu kulingana na mtazamo wa watu kwa Mungu aliye katika mwili. Hii ni mojawapo ya milolongo muhimu ya matamko ya Mungu wakati wa kipindi hiki. Kwa mfano, Mungu anasema, “Nimeanza kirasmi, katika ulimwengu wote, ukamilishaji wa mpango Wangu wa usimamizi. Kuanzia sasa na kuendelea, wowote ambao si waangalifu wanastahili kutumbukizwa katikati ya kuadibu kusiko na huruma wakati wowote.” Haya ni maudhui ya mpango wa Mungu, na sio yasiyo ya kawaida wala ya ajabu, lakini yote ni hatua ya kazi. Watu na wana wa Mungu walio ng’ambo, wakati huo huo, wanahukumiwa na Mungu kulingana na yote wanayoyafanya katika makanisa, na hivyo Mungu asema, “Ninapofanya kazi, malaika wote wanaanzisha vita vya maamuzi na Mimi na kuamua kutimiza matakwa Yangu katika hatua ya mwisho, ili watu walio duniani wajitoe Kwangu kama malaika, na wasiwe na haja ya kunipinga Mimi, na wasifanye chochote ambacho kinaniasi. Hii ndio elimumwendo ya kazi Yangu kotekote katika ulimwengu.” Hii ni tofauti katika kazi ambayo Mungu hutekeleza kotekote duniani; Yeye hutumia hatua tofauti kulingana na wale wanaoelekezewa. Leo, watu wote wa makanisa wana mioyo yenye shauku, na wameanza kula na kunywa maneno ya Mungu—ambalo linatosha kuonyesha kwamba kazi ya Mungu inakaribia mwisho wake. Kuangalia chini kutoka angani ni sawa na kutazama kwa mara nyingine mandhari ya kuchosha ya matawi yaliyonyauka na majani yaliyoanguka, ya mashapo yaliyopeperushwa kwa upepo wa majira ya kupukutika kwa majani, inaonekana kama ufunuo unakaribia kutokea miongoni mwa wanadamu, kama kwamba yote yanakaribia kugeuzwa kuwa ukiwa. Labda ni kwa sababu ya kiwango cha hisi cha Roho, ndio daima huwa kuna hali ya kutokuwa na furaha ndani ya moyo, na kipande cha faraja tulivu, lakini hii pia imechanganywa na kaisi fulani cha huzuni. Huu unaweza kuwa ufafanuzi wa maneno ya Mungu kwamba “mwanadamu anaamka, kila kitu kilicho duniani kiko katika utaratibu, na siku za kunusurika kwa dunia hazipo tena, kwa maana Mimi Nimefika!” Watu wanaweza kuwa hasi kwa kiasi fulani baada ya kuyasikia maneno haya, au wanaweza kusikitishwa kidogo na kazi ya Mungu, au wanaweza kuzingatia sana hisia iliyo katika roho zao. Lakini kabla ya kukamilisha kazi Yake duniani, Mungu hangeweza kuwa mpumbavu kiasi hicho kuwapa watu uwongo kama huo. Ikiwa kweli una hisia kama hizo, basi inaonyesha wewe huzingatia sana hisia zako, kwamba wewe ni mtu ambaye hufanya upendavyo, na humpendi Mungu; inaonyesha kwamba watu kama hao huzingatia sana mambo ya miujiza, na hawamsikilizi Mungu kabisa. Kwa sababu ya mkono wa Mungu, haijalishi jinsi watu wanavyojaribu kuondoka, hawawezi kuiepuka hali hii. Ni nani anayeweza kuuepuka mkono wa Mungu? Ni wakati gani ambapo hadhi na hali yako havikupangwa na Mungu? Kama unateseka au umebarikiwa, ungewezaje kujikwapua kutoka kwa mkono wa Mungu? Hili si suala la kibinadamu, ni hitaji la Mungu kabisa—nani asingetii kwa sababu ya hili?
“Mimi nitatumia kuadibu ili kueneza kazi Yangu katika Mataifa, ambayo ni kusema, Nitatumia nguvu dhidi ya wale wote walio watu wa Mataifa. Kwa kawaida, kazi hii itafanyika kwa wakati mmoja na ile kazi Yangu miongoni mwa wale waliochaguliwa.” Kwa kutamka maneno haya, Mungu anaanza kazi hii kotekote ulimwenguni, nayo ni hatua ya kazi ya Mungu, ambayo tayari imeendelea kufikia kiwango hiki; hakuna mtu anayeweza kugeuza mambo kuwa bora. Msiba utatatua sehemu moja ya wanadamu, na kuwasababisha kuangamia pamoja na ulimwengu. Wakati ulimwengu unaadibiwa rasmi, Mungu huonekana rasmi kwa watu wote. Na kwa sababu ya kuonekana Kwake, watu wanaadibiwa. Zaidi ya hayo, Mungu alisema pia, “Wakati Ninafungua rasmi hati ya kukunjwa ndio wakati watu ulimwenguni kote wanaadibiwa, wakati watu wote duniani wanakabiliwa na majaribu.” Kutokana na hili inaweza kuonekana wazi kwamba maudhui ya mihuri saba ni maudhui ya kuadibu, ambako ni kusema, kuna msiba katika mihuri saba. Hivyo, leo, mihuri saba bado haijafunguliwa; “majaribio” yanayotajwa hapa ni kuadibu ambako mwanadamu anapitia, na kati ya kuadibu huku kundi la watu litapatwa ambalo litakubali rasmi “cheti” kinachotolewa na Mungu, na hivyo watakuwa watu katika ufalme wa Mungu. Hizi ni asili za wana na watu wa Mungu, na leo bado hazijaamuliwa, na zinaweka tu msingi kwa ajili ya uzoefu wa baadaye. Ikiwa mtu ana uzima wa kweli, ataweza kusimama imara wakati wa majaribio, na ikiwa hana uzima, basi hii inathibitisha kwa hakika kwamba kazi ya Mungu haijakuwa na athari kwake, kwamba yeye hujaribu kupata faida kutokana na machafuko, na hazingatii maneno ya Mungu. Kwa sababu hii ni kazi ya siku za mwisho, ambayo ni kuikamilisha enzi hii badala ya kuendelea na kazi, kwa hiyo Mungu anasema, “Kwa maneno mengine, ni maisha ambayo mwanadamu hajawahi kupitia kutoka wakati wa uumbaji mpaka siku ya leo, na hivyo Ninasema kwamba Ninafanya kazi ambayo haijawahi kufanyika mbeleni,” na pia Anasema, “Kwa sababu siku Yangu inakaribia kwa wanadamu wote, kwa sababu haionekani kuwa mbali, lakini iko mbele ya macho ya mwanadamu.” Katika nyakati zilizopita, Mungu Mwenyewe aliangamiza miji kadhaa, lakini hakuna hata mmoja kati ya miji hiyo ulioteketezwa sawa na wakati wa mwisho. Ingawa, katika siku zilizopita, Mungu aliiangamiza Sodoma, Sodoma ya leo haipaswi kutendewa kama nyakati zilizopita—haipaswi kuangamizwa moja kwa moja, bali kushindwa kwanza na kisha kuhukumiwa, na hatimaye, kupitia adhabu ya milele. Hizi ndizo hatua za kazi, na mwishowe, Sodoma ya leo itateketezwa katika mfuatano sawa na maangamizo ya ulimwengu ya wakati uliopita—ambao ni mpango wa Mungu. Siku ambayo Mungu ataonekana ndiyo siku ya shutuma rasmi, na sio kuiokoa kwa njia ya kuonekana Kwake. Hivyo, Mungu anasema, “Mimi huonekana kwa ufalme mtakatifu, na kujificha kutoka kwa nchi ya uchafu.” Kwa sababu Sodoma ya leo ni chafu, Mungu haonekani kwayo kwa hakika, lakini Anatumia njia hii kuiadibu—hujaona jambo hili wazi? Inaweza kusemwa kwamba hakuna mtu duniani anayeweza kuuona uso halisi wa Mungu. Mungu hajawahi kuonekana kwa mwanadamu, na hakuna mtu anayejua Mungu yuko katika kiwango gani cha mbinguni. Hili ndilo limewasababisha watu wa leo kuwa katika hali hii. Kama wangeuona uso wa Mungu, huo hakika ungekuwa wakati ambao mwisho wao ungefichuliwa, wakati ambapo kila mmoja anaainishwa kulingana na aina. Leo, maneno katika uungu yanaonyeshwa moja kwa moja kwa watu, ambalo linatabiri kwamba siku za mwisho za wanadamu zimewadia, na hazitakaa muda mrefu zaidi. Hii ni mojawapo ya ishara za watu kutiishwa kwa majaribio wakati ambapo Mungu anaonekana kwa watu wote. Hivyo, ingawa watu hufurahia maneno ya Mungu, daima wao huwa na hisia ya kuogofya, kama kwamba msiba mkubwa unakaribia kuwafika. Watu wa leo ni kama jurawa katika nchi zenye barafu, ambao ni kama kwamba kifo kinawalazimishia deni na kuwaacha bila njia yoyote ya kuishi. Kwa sababu ya deni la kifo ambalo mwanadamu anadaiwa, watu wote wanahisi kuwa siku zao za mwisho zimewadia. Hiki ndicho kinachofanyika katika mioyo ya watu duniani kote, na ingawa hakifichuliwi kwa nyuso zao, kile kilicho ndani ya mioyo yao hakiwezi kujificha kutoka kwa macho Yangu—huu ni uhalisi wa mwanadamu. Pengine, mengi ya maneno yanachaguliwa vibaya kwa kiasi fulani—lakini ni maneno yaya haya ambayo yanafaa kuonyesha tatizo. Kila mojawapo ya maneno yanayonenwa kutoka kinywani mwa Mungu yatatimizwa, kama ni ya zamani au ya sasa; yatafanya ukweli uonekane mbele ya watu, karamu kwa macho yao, wakati ambao watakanganywa na kuchanganyikiwa. Je, bado hujaona wazi leo ni enzi gani?

Tazama zaidi: neno la Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni