1.31.2019

Neno la Mungu | "Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu"


Neno la Mungu | "Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu"


Ili uwe na ushuhuda kwa Mungu na kuliaibisha joka jekundu ni sharti uwe na kanuni, na sharti: Katika moyo wako ni lazima umpende Mungu na uingie katika maneno ya Mungu. Kama huingii katika maneno ya Mungu, basi hutakuwa na njia ya kumuaibisha Shetani. Katika ukuaji wa maisha yako, unalikataa joka kuu jekundu na kuliletea aibu kamili, na ni hapo tu ndipo hili joka jekundu kweli linaaibika. Kadiri unavyohiyari kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo, ndivyo unavyothibitisha kwamba unampenda Mungu na kulichukia joka kuu jekundu; kadiri unavyotii maneno ya Mungu, ndivyo unavyothibitisha kwamba unautamani ukweli. Watu ambao hawayatamani maneno ya Mungu ni watu wasio na uzima. Watu kama hao ni wale walio nje ya maneno ya Mungu, walio ndani ya dini. Wanaomwamini kweli Mungu huwa na ufahamu wa kina wa maneno ya Mungu kupitia kula na kunywa maneno ya Mungu. Ikiwa huyatamani maneno ya Mungu, basi huwezi kweli kula na kunywa haya maneno ya Mungu, na kama huna ufahamu wa maneno ya Mungu, basi huna njia ya kumshuhudia Mungu au kumtosheleza Mungu.
Katika imani yako kwa Mungu, utamjuaje Mungu? Unapaswa kumjua Mungu kupitia maneno na kazi ya leo ya Mungu, bila upotovu au uwongo, na hata kabla jambo lolote lile ni sharti uijue kazi ya Mungu. Huu ndio msingi wa kumjua Mungu. Huo uwongo wa aina mbalimbali unaokosa ukubalifu wa maneno ya Mungu ni dhana za kidini, ni ukubalifu ambao ni potovu na wenye makosa. Ujuzi mkubwa zaidi wa watu mashuhuri wa kidini ni kuyachukua maneno ya Mungu yaliyokuwa yakikubalika zamani na kuyalinganisha na maneno ya Mungu ya leo. Unapomhudumia Mungu wa leo, ikiwa unashikilia vitu vilivyoangaziwa nuru na Roho Mtakatifu hapo zamani, basi huduma yako itasababisha hitilafu na vitendo vyako vitakuwa vimepitwa na wakati na havitakuwa tofauti na ibada ya kidini. Ikiwa unaamini kuwa wanaomhudumia Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wavumilivu…, na ukiweka ufahamu wa aina hii katika vitendo leo hii, basi vitendo kama hivi ni dhana ya kidini, na vitendo kama hivyo ni maigizo ya kinafiki. “Dhana za kidini” inarejelea vitu vilivyopitwa na wakati (kutia ndani ukubalifu wa maneno yaliyonenwa na Mungu zamani na kufichuliwa na Roho Mtakatifu), na vikiwekwa katika vitendo leo, basi vitahitilafiana na kazi ya Mungu na havitamfaidi mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kuyatakasa dhana za kidini yaliyomo ndani yake, basi yatakuwa kizuizi kizito katika kumuhudumia Mungu. Walio na dhana za kidini hawana njia ya kuendelea sawia na hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, watakuwa nyuma hatua moja, halafu mbili—kwani hizi dhana za kidini humfanya mwanadamu kuwa mtu wa kujitukuza na mwenye kiburi. Mungu hahisi kumbukumbu kwa ajili ya Alichokinena na kukifanya hapo zamani; kama kimepitwa na wakati, basi Anakiondoa. Hakika unaweza kuziacha dhana zako? Ukiyakatalia maneno aliyoyanena Mungu hapo zamani, je hili linadhihirisha kuwa unaijua kazi ya Mungu? Kama huwezi kukubali mwangaza wa Roho Mtakatifu leo na badala yake unashikilia mwangaza wa zamani, hili laweza kuthibitisha kuwa unafuata nyayo za Mungu? Je, bado huwezi kuziacha dhana za kidini? Ikiwa ndivyo ilivyo, basi utakuwa mpinga Mungu.


 Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni