11.30.2018

Umeme wa Mashariki | Tamko la Hamsini na Moja

Ee! Mwenyezi Mungu! Amina! Ndani Yako yote yanaachiliwa, yote ni huru, yote ni wazi, yote hufichuliwa, yote hung’aa, bila sitara au maficho yoyote. Wewe ni Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Umetawala kama Mfalme. Umefichuliwa wazi, wewe tena si fumbo lakini Umefichuliwa kabisa milele na milele! Kwa kweli Nimefichuliwa kabisa, Nimefika hadharani, na Nimejitokeza kama Jua la haki kwa kuwa leo si enzi ya kuonekana kwa nyota ya asubuhi tena, si awamu ya sitara tena. Kazi Yangu ni kama mwanga wa umeme, inakamilishwa na wepesi wa ajabu. Leo kazi Yangu imeendelea hadi hatua hii na yeyote anayekawia au kuzembea anaweza tu kukabiliwa na hukumu isiyo na huruma. Ni lazima uelewe dhahiri hasa kwamba Mimi ni uadhama na hukumu na Mimi si huruma na upendo tena kama mnavyodhani. Kama bado huelewi vizuri hoja hii, kile utakachopokea basi ni hukumu, kwa kuwa wewe mwenyewe utaonja kile ambacho wewe bado hujakiri, vinginevyo bado utakuwa na mashaka na kutothubutu kuwa imara katika imani yako.
Kile ambacho Nimewaaminia, mna uwezo wa kukimaliza kwa mapenzi? Nasema kwamba inahitaji hekima kufanya kitu chochote, ilhali ni vitu vingapi mmefanya ambavyo mmechunguza kwa makini ushawishi Wangu mara kwa mara, na kuvipa fikira zaidi? Hata kama mnao ufahamu wa neno moja la ushawishi Wangu na mnafikiri ni sawa mnapolisikia, hatimaye si la muhimu kwenu. Mnapolisikia, mnajichukia wakati mnalielekeza kwa hali zenu halisi wenyewe, je, na kuhusu baadaye? Kisha mnaliamini kuwa jambo dogo[a]. Leo ni suala la kama maisha yako yanaweza kuendelea au la, na si suala la uso ambao wewe huchukua kwa nje. Hakuna kati yenu aliye na azimio lolote na hamko tayari kuwa na ushupavu, hamtamani kulipa gharama, hamtaki kuweka kando anasa zisizodumu za dunia na bado mnahofia kupoteza baraka kutoka mbinguni, huyu ni mtu wa aina gani? Huyu ni mjinga! Hampaswi kuhisi kukerwa—je, kile ambacho Nimesema si cha kweli? Je, hakijasisitiza kile ambacho umekifikiri kwako mwenyewe? Wewe huna ubinadamu! Wewe huna hata sifa ya mtu wa kawaida, na hata kama hivi ndivyo kulivyo, bado wewe hujioni mwenyewe kama maskini, wewe ni taratibu na asiyejali siku yote nzima, wa kujiridhisa! Wewe hujui jinsi upungufu wako mwenyewe ni mkubwa na kile unachokosa. Upumbavu ulioje!
Je, hamwoni kwamba kazi Yangu tayari ishakuja hadi mahali kama hapo? Mapenzi Yangu yote yako ndani yenu, mtaweza kuyafahamu lini, mtafikiri kuyahusu lini? Mzembe! Wewe huko tayari kulipa gharama, huko tayari kufanya kazi ngumu, huko tayari kuchukua wakati, na huko tayari kuweka bidii. Acha Nikwambie! Kadiri unavyohofia kupata taabu, ndivyo maisha yako yatavyokuwa na faida chache zaidi, aidha ndivyo utakavyokabiliwa na vikwazo zaidi maisha yako yanavyokua, na ndivyo uendeleaji wake unaonekana hutaendelea zaidi. Nakukumbusha mara nyingine tena (Sitalisema tena)! Yeyote asiyewajibika na maisha yake mwenyewe, Mimi sitamjali na Nitamwacha. Tayari Nimeshaanza kulitekeleza hili; hujaona hili kwa uwazi? Haya si mapatano ya kibiashara wala si ubadilishanaji na ugawaji wa bidhaa, lakini ni maisha, je hilo ni dhahiri?
Tanbihi:
a. Nakala asili inasema "Basi ni jambo dogo."

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

 Tazama zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni