11.13.2018

Siwezi Kusema Yote Yaliyo Moyoni Mwangu

Umeme wa Mashariki,Nyimbo,hukumu
I
Leo nimekutana na Wewe, matumaini yangu yote yametimia.
Nimefurahia utajiri wote katika kumbatio Lako la upendo na ukunjufu.
Moyo Wako hakika ni mzuri sana, upendo Wako unanivutia.
Kile Ulicho nacho na kile Ulicho, ni vya thamani sana kwangu.
Siwezi kuelezea, hakuna maneno: 
Jinsi gani anavyopendeza Mwenyezi Mungu!
Unaishi hapa miongoni mwa wanadamu
na kuweka mifano kwa kila njia.
Upendo Wako ni mwenzi wangu.
Maneno Yako daima yananiruzuku.
Unasafisha na kunitakasa.
Katika kuteseka hukumu,
ninaonja utamu ulio ndani.
Katika upendo Wako wa kweli kwangu,
siwezi kusema yote yaliyo moyoni mwangu.
Nikiwa nimetakaswa, mimi ni Wako, nami nitakupenda milele!
II
Baada ya kustahimili dhoruba, nimeshikana na Wewe zaidi.
Kupitia mateso na usafishaji, moyo wangu umeamshwa.
Katika njia ya shida, nimejifunza kutii.
Sio tena baridi au mwasi, sasa ninajua mapenzi Yako.
Ingawa maneno Yako ni makali,
Una moyo wenye ukarimu zaidi.
Unafanya kazi kwa ajili ya hatima ya mwanadamu,
Unawasubiri warudi.
Upendo Wako ni mwenzi wangu.
Maneno Yako daima yananiruzuku.
Unasafisha na kunitakasa.
Katika kuteseka hukumu,
ninaonja utamu ulio ndani.
Katika upendo Wako wa kweli kwangu,
siwezi kusema yote yaliyo moyoni mwangu.
Nikiwa nimetakaswa, mimi ni Wako, nami nitakupenda milele!

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

          Tazama zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni