10.25.2018

Mungu Katika Mwili Hufanya Kazi Kimya ili Kuwaokoa Wanadamu

Mungu Katika Mwili Hufanya Kazi Kimya ili Kuwaokoa Wanadamu

I
Mungu alipata mwili, akabaki kujificha miongoni mwa wanadamu
ili kufanya kazi mpya, kutuokoa kutoka katika upotovu.
Anahifadhi maelezo.
Kwa mipango Aliyoifanya, Yeye hufanya kazi Yake hatua kwa hatua.
Maneno Yake yanaongezeka kila siku,
yakifariji, kukumbusha, kushutumu, na kuonya.
Kutoka mapole na yenye huruma hadi makalina maadhimu,
maneno Yake yanaingiza huruma na hofu.
Kila kitu Anachosema kinafichua siri zetu za kina zaidi.
Maneno Yake yanaweza kutuchoma na tukaona haya.
Kuna ugavi usio na mwisho wa maji Yake ya uzima.
Na kwa sababu Yake, tunaishi na Mungu uso kwa uso.
Mungu alipata mwili, akabaki kujificha miongoni mwa wanadamu
ili kufanya kazi mpya, kutuokoa kutoka katika upotovu.
Anahifadhi maelezo.
Kwa mipango Aliyoifanya, Yeye hufanya kazi Yake hatua kwa hatua.
II
Tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu mbinguni,
na hatujawahi kuzingatia hisia
za mtu huyu wa kawaida aliye na uungu.
Bado anafanya kazi Yake kwa unyenyekevu akijificha ndani ya mwili,
Akionyesha sauti ya moyo Wake,
kama kwamba hatambui kukataliwa Kwake na binadamu,
inavyoonekana Akisamehe milele utoto na ujinga wa mwanadamu,
na Akivumilia milele mwanadamu kutomheshimu.
Mungu alipata mwili, akabaki kujificha miongoni mwa wanadamu
ili kufanya kazi mpya, kutuokoa kutoka katika upotovu.
Anahifadhi maelezo.
Kwa mipango Aliyoifanya, Yeye hufanya kazi Yake hatua kwa hatua.
III
Maneno Yake yana nguvu ya uzima,
na yanaonyesha njia ya kutembea, yanatusababisha tujue ukweli ni nini.
Tunapovutiwa na neno Lake, tunaisikiliza sauti
na sauti ya moyo wa mtu huyu asiye wa ajabu.
Yeye hufanya kila jitihada na huvuja damu ya moyo Wake.
Ni kwa ajili yetu Anaomboleza na kulia kwa maumivu,
huvumilia aibu kwa ajili ya majaliwa na wokovu wetu.
Moyo Wake unavuja damu na hulia kwa ajili ya uasi wetu.
Hakuna mtu anayeweza kupata hali na mali kama hiyo.
Hakuna mtu anayeweza kufikia uvumilivu Wake.
Hakuna kiumbe kinachoweza kuwa na upendo na uvumilivu Alio nao.
Mungu alipata mwili, akabaki kujificha miongoni mwa wanadamu
ili kufanya kazi mpya, kutuokoa kutoka katika upotovu.
Anahifadhi maelezo.
Kwa mipango Aliyoifanya, Yeye hufanya kazi Yake hatua kwa hatua,
Ndio, Yeye hufanya kazi Yake hatua kwa hatua.
kutoka kwa "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

      Sikiliza nyimbo: Kanisa la Mwenyezi Mungu Wimbo wa Maneno ya Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni