10.04.2018

Tamko la Arubaini na Tano

Tamko la Arubaini na Tano

Wakati mmoja Nilichagua bidhaa nzuri kubaki ndani ya nyumba Yangu, ili ndani yake kungekuwa na utajiri usio na kifani, na ingepambwa hivyo, Nilipata raha kutokana na hilo. Lakini kwa sababu ya mtazamo wa mwanadamu Kwangu, na kwa sababu ya motisha za watu, Sikuwa na budi ila kuiweka kazi hii kando na kufanya kazi nyingine. Nitatumia motisha za mwanadamu kufanikisha kazi Yangu, Nitashawishi vitu vyote vinihudumie, na kusababisha nyumba Yangu kutokuwa ya kusononeka na ya ukiwa tena kama matokeo. Wakati mmoja Nilitazama miongoni mwa wanadamu: Chote kilichokuwa cha mwili na damu kilikuwa katika mzubao, hakuna hata kitu kimoja kilipitia baraka ya kuweko Kwangu. Watu huishi katikati ya baraka lakini hawajui jinsi walivyobarikiwa. Kama baraka Zangu kwa wanadamu hazingekuweko mpaka leo, nani miongoni mwa wanadamu angeishi mpaka wakati huu na kukosa kuangamia? Kwamba mwanadamu anaishia ni baraka Yangu, na linamaanisha anaishi katikati ya baraka Zangu, kwa sababu hapo mwanzo hakuwa na chochote, kwa kuwa hapo mwanzo hakuwa na rasilimali ya kuishi katikati ya mbingu na dunia; leo Naendelea kumsaidia mwanadamu, na ni kwa sababu ya hili tu ndio mwanadamu anasimama mbele Yangu, akibahatika ya kutosha kuepuka kifo. Watu wamejumuisha siri za kuweko kwa mwanadamu, lakini hakuna mtu ambaye ametambua kwamba hii ni baraka Yangu. Kutokana na hili, watu wote wanalaani udhalimu ulio ulimwenguni, wote wanalalamika kunihusu kwa sababu ya kutokuwa na furaha ndani ya maisha yao. Kama si baraka Zangu, nani angeona leo? Watu wote hulalamika kunihusu kwa sababu hawawezi kuishi katikati mwa faraja. Kama maisha ya mwanadamu yangekuwa yenye kung'aa na machangamfu, kama "dharuba ya vuguvugu ya ghafula ya majira ya kuchipua" ingeingizwa ndani ya moyo wa mwanadamu, isababishe furaha isiyo na kifani ndani ya mwili wake wote, ikimwacha bila maumivu hata kidogo, basi nani miongoni mwa wanadamu angekufa akilalamika? Nina tatizo kubwa kupata uaminifu kamili wa mwanadamu, kwani watu wana hila nyingi sana za ujanja—za kutosha, kweli kabisa, kukanganya mtu. Lakini Niletapo upinzani kwao, wao hunidharau, hawanisikilizi, kwani upinzani Wangu umegusa nafsi zao, ukiwawacha bila uwezo wa kuadilishwa kutoka utosini hadi wayoni, na hivyo watu huchukia sana kuweko Kwangu, kwani kila mara Mimi hupenda "kuwatesa." Kwa sababu ya maneno Yangu, watu huimba na kucheza, kwa sababu ya maneno Yangu, wao hushusha vichwa vyao kwa ukimya, na kwa sababu ya maneno Yangu, wao huangua kilio. Katika maneno Yangu, watu hukata tamaa, katika maneno Yangu, wao hupata nuru ya kuendelea kuishi, kwa sababu ya maneno Yangu, wao hugaagaa na kugeuka, bila usingizi mchana na usiku, na kwa sababu ya maneno Yangu, wao huenda kasi kila mahali. Maneno Yangu huwatumbukiza watu ndani ya Kuzimu, kisha huwatumbukiza katika kuadibu—lakini, bila kulitambua, watu hufurahia baraka Zangu pia. Je, hili laweza kutimizwa na mwanadamu? Lingeweza kupatikana kama malipo ya juhudi za kutochoka za watu? Ni nani anaweza kuepuka mipango ya maneno Yangu? Hivyo, kwa sababu ya udhaifu wa mwanadamu, Natoa maneno Yangu kwa wanadamu, kusababisha kasoro za mwanadamu kusitawishwa kwa sababu ya maneno Yangu, kuleta utajiri usio na kifani katika maisha ya wanadamu.
Mimi mara kwa mara Huchunguza maneno na vitendo vya watu. Katika mienendo yao na sura zao, Nimegundua 'siri" nyingi. Katika kuingiliana kwa watu na wengine, "mbinu za siri" kwa utendaji huchukua nafasi muhimu sana—na hivyo, Ninaposhirikiana na mwanadamu, Nipatacho ni "mbinu za siri za kuingiliana kwa mwanadamu," ambalo huonyesha kwamba mwanadamu hanipendi. Mimi mara kwa mara humkemea mwanadamu kwa sababu ya kasoro zake, lakini Siwezi kupata uaminifu wake. Mwanadamu hayuko radhi kuniacha Nimchinje, kwani katika "mbinu za siri za kuingiliana kwa mwanadamu" za mwanadamu, haijawahi kamwe kugunduliwa kwamba mwanadamu amepatwa na msiba wa mauti—yeye amepitia tu vipingamizi vichache katika nyakati za taabu. Watu hulia kwa sababu ya maneno Yangu, na maombi yao kila mara huwa na manung'uniko kuhusu ukatili Wangu. Ni kana kwamba wote wanatafuta "upendo" Wangu wa kweli kwa mwanadamu—lakini wangewezaje kupata upendo Wangu katika maneno Yangu makali? Kutokana na hilo, wao kila mara hukata tamaa kwa sababu ya maneno Yangu. Ni kana kwamba, punde tu wasomapo maneno Yangu, wao huona “mvunaji wa roho za wafu,” na hivyo hutetemeka kwa hofu. Hili hunifanya Nikose raha: Kwa nini watu wa mwili, ambao wanaishi katikati ya kifo, kila mara huogopa kifo? Je, mwanadamu na kifo ni maadui wakali? Mbona hofu ya kifo kila mara husababisha huzuni ndani ya watu? Kotekote katika matukio "yasiyo ya kawaida" ya maisha yao, wao hupitia tu kiasi kidogo cha kifo? Mbona, katika kile wasemacho, watu daima hulalamika kunihusu? Hivyo, Nafanya muhtasari wa methali ya nne ya maisha ya mwanadamu: Watu hunitii kiasi kidogo tu, na hivyo wao kila mara hunichukia. Kwa sababu ya chuki ya mwanadamu, Mimi huondoka mara kwa mara. Kwa nini lazima Nipitie hili? Kwa nini lazima Nichochee chuki ndani ya watu kila mara? Kwa vile watu hawafurahii kuweko Kwangu, kwa nini lazima Niwe na ujasiri wa kukabiliana na hilo jambo na kuishi katika nyumba ya mwanadamu? Sina budi ila kuchukua "mzigo" Wangu na kumwacha mwanadamu. Lakini watu hawawezi kuvumilia kuniacha Niende, hawataki kamwe kuniacha Niondoke, wao huomboleza na kumamia, wakiwa na woga mwingi kwamba Nitaondoka, na hivyo watapoteza wanachotegemea ili kuishi. Nionapo kukaza macho kwao kwa kusihi, moyo Wangu huwa wenye huruma . Katikati ya bahari za ulimwengu, nani anaweza kunipenda? Mwanadamu amefunikwa kwa maji machafu, amemezwa na nguvu za bahari. Nachukia sana ukaidi wa mwanadamu, lakini pia Naona huruma kwa ajili ya taabu zote za wanadamu—kwani mwanadamu, hata hivyo, bado ni mwathiriwa. Nawezaje kumtupa mwanadamu ndani ya maji wakati ambapo yeye ni mnyonge na mdhaifu? Je, Mimi ni mkatili hivyo kiasi cha kumpiga teke akiwa chini? Je, moyo Wangu ni katili sana? Ni kwa sababu ya mtazamo Wangu kwa wanadamu ndio mwanadamu huingia katika enzi hii ubavuni Mwangu, ni kwa sababu ya hili ndio amepitia mchana na usiku huu usio wa kawaida pamoja na Mimi. Leo, watu wako katika maumivu makubwa ya furaha, wana ufahamu mkuu wa upendo Wangu, na wananipenda kwa nguvu nyingi, kwa sababu kuna uhai katika maisha yao, nao hukoma kuwa wana wapotevu wanaozurura mpaka kwa miisho ya dunia.
Katika siku Zangu za kuishi na mwanadamu, watu hunitegemea, na kwa sababu Namjali mwanadamu katika mambo yote, na ni mwangalifu sana katika kumtunza, watu kila mara huishi katika kumbatio Langu kunjufu, wakikosa kustahimili upepo wowote uvumao, mvua inyeshayo, au jua lichomalo; watu huishi kati ya furaha, na kunichukulia kama mama mwenye upendo. Watu ni kama maua yaliyo ndani ya nyumba ya kioo ya kuhifadhi mimea, wasioweza kabisa kuhimili mvamio wa "maafa ya asilia," wasiweze daima kusimama imara. Hivyo Nawaweka katikati ya majaribio ya bahari zivumazo, na hawana budi ila "kuyumbayumba" bila kukoma, hawana kabisa nguvu za kupinga—na kwa vile kimo chao ni dhaifu sana na miili yao ni minyonge sana, Nahisi mzigo. Hivyo, bila kutambua hilo, watu hupitia majaribio Yangu, kwa sababu wao ni wadhaifu sana, na hawawezi kuhimili upepo unaovuma na jua lichomalo. Je, hii si kazi Yangu ya wakati huu? Kwa nini, wakati ambapo wanakabiliwa na majaribio Yangu, watu daima hububujika machozi. Je, Nawatendea udhalimu? Je, Nawachinja kwa makusudi? Kwa nini hali ya mwanadamu ambayo ni ya kupendeka hufa, isiweze kufufuliwa kamwe? Watu daima huninyakua na hawaachilii; kwa sababu hawajawahi kuweza kuishi wenyewe, kila mara wamejiruhusu kuongozwa na mkono Wangu, wakiogopa sana kuchukuliwa na mtu mwingine. Je, maisha yao yote hayaongozwi na Mimi? Wakati wa maisha yao yenye ghasia, wanapovuka milima na mabonde, wamepitia misukosuko mingi sana—je, hili halikutoka mkononi Mwangu? Kwa nini watu hawawezi kamwe kuuelewa moyo Wangu? Kwa nini nia Zangu nzuri kila mara hueleweka vibaya na wao? Kwa nini kazi Yangu haiwezi kuanzishwa kwa ufanisi duniani? Kwa sababu ya unyonge wa mwanadamu, Nimejitenga na mwanadamu kila mara, ambalo hunijaza huzuni: Kwa nini hatua Yangu inayofuata ya kazi isiweze kutekelezwa na mwanadamu? Hivyo, Nanyamaza, Nikimhakiki kwa makini: Mbona kila mara Mimi huzuiwa na kasoro za mwanadamu? Kwa nini huwa kuna vizuizi kwa kazi Yangu kila mara? Leo, bado Sijapata jibu kamili katika mwanadamu, kwani mwanadamu kila mara hughairighairi, yeye si wa kawaida kamwe, ama ananichukia kabisa, au ana upendo mkubwa sana Kwangu. Mimi, Mungu Mwenyewe wa kawaida, Siwezi kustahimili mateso kama hayo kutoka kwa mwanadamu. Kwa sababu watu kila mara huwa si wa kawaida kiakili, Mimi inavyoonekana Namwogopa mwanadamu kidogo, na kwa hiyo kutazama kila mwendo wake hunifanya Nifikirie kuhusu kutokuwa kawaida kwake. Nimegundua bila kusudi siri iliyo ndani ya mwanadamu: Inadhihirika kwamba kuna mwanzilishi nyuma yake: kutokana na hilo, watu kila mara ni wakakamavu na wenye kujiamini, kana kwamba wamefanya kitu fulani kinachostahiki. Hivyo, watu kila mara hujifanya kuwa mtu mzima na humbembeleza "mtoto mdogo." Nitazamapo kitendo cha uongo cha mwanadamu, Sina budi ila kughadhibishwa: Kwa nini watu hawajipendi na hukosa kujiheshimu hivyo? Kwa nini wasijijue? Je, maneno Yangu yamekufa? Je, maneno Yangu ni adui wa mwanadamu? Kwa nini, wanaposoma maneno Yangu, watu hukuza chuki Kwangu? Kwa nini watu huongeza mawazo yao kwa maneno Yangu kila mara? Je, Mimi ni asiye na huruma sana kwa mwanadamu? Watu wote wanapaswa kufikiri sana kuhusu hili, kuhusu kilicho ndani ya maneno Yangu.

Mei 24, 1992

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni