10.03.2018

Nitampenda Mungu Milele

Umeme wa Mashariki, nyimbo, mungu


  • Nitampenda Mungu Milele

  • I
  • Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kukurudia Wewe.
  • Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku.
  • Majaribu mengi na uchungu, dhiki nyingi sana.
  • Mara nyingi nilitoa machozi na kuhuzunika sana,
  • mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.
  • Lakini hujaniacha kamwe. 
  • Uliniongoza kupitia taabu nyingi,
  • Ukanilinda katika hatari nyingi.
  • Sasa najua kuwa Umenipenda.
  • II
  • Ee Mungu! Unaniongoza katika maisha mapya.
  • Nikifurahia maneno Yako,
  • nimeelewa mapenzi Yako.
  • Maneno Yako yanihukumu na kuniadhibu,
  • na kutakasa upotovu wangu.
  • Kupitia majaribu nimejifunza kukutii Wewe.
  • Ninapokua katika neno Lako,
  • nimekuja kukujua Wewe.
  • Niko tayari kufanya wajibu wangu
  • kwa ushahidi Wako na utukufu.
  • Nitakupenda Wewe wakati wote.
  • Nikibarikiwa au kulaaniwa,
  • nitafurahia kuwa chini ya rehema Yako.
  • Nitakupa upendo wa kweli,
  • na sitakufanya Ungoje.
  • Nitakupa upendo safi,
  • tafadhali furahia upendo wangu.
  • Nitakupa upendo wangu wote,
  • na kuacha Upate upendo wangu.
  • Nitakupenda wakati wote;
  • kukuridhisha ni tamanio langu.
  •  
  • kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

                         Tazama zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni