10.06.2018

Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Maneno Husika ya Mungu:

Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu! Mungu ana hamu ya mwanadamu kumpenda Yeye, lakini kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo kuteseka kwa mwanadamu huwa kwingi zaidi, na kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo majaribio ya mwanadamu huwa makubwa zaidi. Ikiwa unampenda Yeye, basi kila aina ya mateso yatakufika—na ikiwa humpendi, basi labda kila kitu kitaendelea kwa urahisi kwako, na kila kitu kinachokuzunguka kitakuwa kitulivu kwako.   Unapompenda Mungu, utahisi kwamba mengi kandokando yako hayawezi kushindikana, na kwa sababu kimo chako ni kidogo sana utasafishwa; aidha, huwezi kumridhisha Mungu, na daima utahisi kwamba mapenzi ya Mungu ni ya juu sana, kwamba hayawezi kufikiwa na mwanadamu. Kwa sababu ya haya yote utasafishwa—kwa sababu kuna udhaifu mwingi ndani yako, na mengi yasiyoweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, utasafishwa ndani. Lakini lazima muone kwa dhahiri kwamba utakaso hutimizwa tu kupitia usafishaji. Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana.
kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Usivunjike moyo, usiwe dhaifu, Nitakufichulia. Njia ya kwenda kwa ufalme sio laini hivyo, hakuna kitu kilicho rahisi hivyo! Unataka baraka zije kwa urahisi rahisi, sivyo? Leo kila mtu atakuwa na majaribio machungu ya kukumbana nayo, vinginevyo moyo wa upendo ulio nao Kwangu hautakuwa wenye nguvu zaidi na hutakuwa na upendo wa kweli Kwangu. Hata kama ni hali ndogo tu, kila mtu lazima azipitie, ni kwamba tu zinatofautiana kwa kiwango fulani. Hali hiyo ni moja ya baraka Zangu, ni wangapi hupiga magoti mbele Yangu mara kwa mara kuomba baraka Yangu? Watoto wapumbavu! Wewe daima huhisi kwamba maneno machache ya bahati huhesabika kama baraka Yangu, lakini huhisi kuwa uchungu ni moja ya baraka Zangu. Wale wanaoshiriki katika uchungu Wangu bila shaka watashiriki utamu Wangu. Hiyo ni ahadi Yangu na baraka Zangu kwenu.
kutoka katika “Sura ya 41” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati Mungu anafanya kazi ili kumsafisha mwanadamu, mwanadamu huteseka. Kadiri usafishaji wake ulivyo mkubwa, ndivyo upendo wake kwa Mungu ulivyo mkubwa zaidi na ndivyo nguvu za Mungu zinafichuliwa zaidi kwake. Kadiri usafishaji wa mwanadamu ulivyo wa kiwango cha chini, ndivyo upendo wake kwa Mungu ulivyo wa kiwango cha chini, na ndivyo nguvu za Mungu zinafichuliwa kwake kwa kiwango cha chini. Kadiri usafishaji wake na uchungu wake ulivyo mkubwa na zaidi yalivyo mateso yake, ndivyo upendo wake wa kweli kwa Mungu utakavyokuwa, ndivyo imani yake kwa Mungu itakavyokuwa ya kweli, na ndivyo maarifa yake ya Mungu yatakuwa ya kina. Katika uzoefu wako utaona kwamba wale ambao wanakabiliwa na usafishaji mkubwa na uchungu, na kushughulikiwa sana na kufundishwa nidhamu, wana upendo mkubwa kwa Mungu, na maarifa ya kina na elekevu ya Mungu. Wale ambao hawajapitia kushughulikiwa wanayo maarifa ya juu juu tu, na wanaweza tu kusema: “Mungu ni mzuri sana, Yeye huwapa watu neema ili waweze kumfurahia Yeye.” Kama watu wamepitia kushughulikiwa na kufundishwa nidhamu, basi hao wanaweza kuyazungumza maarifa ya kweli ya Mungu. Hivyo kazi ya Mungu katika mwanadamu ilivyo ya ajabu zaidi, ndivyo ilivyo ya thamani zaidi na ni muhimu zaidi. Kadiri inavyokosa kupenyeza kwako zaidi na kadiri isivyolingana na mawazo yako, ndivyo kazi ya Mungu inavyoweza kukushinda, kukupata, na kukufanya mkamilifu. Umuhimu wa kazi ya Mungu ni mkubwa sana! Kama Hangemsafisha mwanadamu kwa njia hii, kama Hangefanya kazi kulingana na njia hii, basi kazi ya Mungu haingekuwa na ufanisi na ingekuwa isiyo na maana. Hii ndiyo sababu ya umuhimu wa ajabu wa uteuzi Wake wa kundi la watu katika siku za mwisho. Hapo awali ilisemwa kuwa Mungu angelichagua na kulipata kundi hili. Kadiri ilivyo kuu kazi Anayofanya ndani yenu, ndivyo ulivyo mkubwa na safi upendo wenu kwa Mungu. Kadiri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi, ndivyo mwanadamu anavyoweza kuonja hekima Yake na ndivyo maarifa ya mwanadamu Kwake yalivyo ya kina zaidi.
kutoka katika “Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili
Lazima uvumilie mateso kwa ajili ya ukweli, lazima ujitoe kwa ajili ya ukweli, lazima uvumilie udhalilishaji kwa ajili ya ukweli, na kupata ukweli zaidi lazima upate mateso zaidi. Hili ndilo unalopaswa kufanya. Msitupilie mbali ukweli kwa ajili ya maisha ya amani ya familia, na lazima msiipoteze heshima na uadilifu wa maisha kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Unapaswa kufuata yote ambayo ni ya kupendeza na mema, na unapaswa kufuata njia katika maisha ambayo ni ya maana zaidi. Kama wewe unaishi maisha ya kishenzi, na wala hufuati malengo yoyote, je, si huko ni kupoteza maisha Yako? Ni nini unachoweza kupata kutoka kwa maisha ya aina hii? Unapaswa kuziacha starehe zote za mwili kwa ajili ya ukweli mmoja, na hupaswi kutupilia mbali ukweli wote kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Watu kama hawa hawana uadilifu au heshima; hakuna maana ya kuwepo kwao!
kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati ambapo tunapokea hukumu ya maneno ya Mungu, hatupaswi kuogopa mateso, wala hatupaswi kuogopa maumivu; sembuse kuogopa kwamba maneno ya Mungu yataumiza mioyo yetu. Tunapaswa kusoma matamshi Yake zaidi kuhusu jinsi Anavyotuhukumu na kutuadibu na kufichua asili zetu potovu, na tunapokuwa tukisoma maneno ya Mungu, tunapaswa kujilinganisha mara kwa mara dhidi ya maneno hayo. Tuna upotovu huu wote; sote tunaweza kulingana nao. … Kwanza lazima tujue kuwa haijalishi ikiwa maneno yoyote Yake yanavutia kuyasikia, ikiwa yanatufanya tuhisi uchungu au utamu—lazima tuyakubali yote. Tunapaswa kuwa na mtazamo huu juu ya maneno ya Mungu. Mtazamo huu ni wa aina gani? Je, ni mtazamo wa kumcha Mungu? Wa uvumilivu? Au, ni mtazamo wa kuteseka? Nitawaambia, si wowote kati ya hii. Katika imani yetu, lazima tusisitize kwa uthabiti kwamba maneno ya Mungu ndiyo ukweli. Kwa kuwa kweli ndiyo ukweli, tunapaswa kuyakubali kwa busara. Bila kujali ikiwa tunaweza kutambua au kukubali au la, mtazamo wetu wa kwanza kuelekea maneno ya Mungu unapaswa kuwa ule wa kukubali kabisa.
kutoka katika “Umuhimu na Njia ya Kufuatilia Ukweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kumpenda Mungu kunahitaji utafutaji wa mapenzi ya Mungu katika mambo yote, na kwamba ujisaili wewe mwenyewe kwa kina jambo lolote likikutokea, kujaribu kujua mapenzi ya Mungu na kujaribu kuona mapenzi ya Mungu ni yapi katika suala hili, Anataka ufanikishe nini, na ni jinsi gani utayajali mapenzi Yake? Kwa mfano: jambo fulani linafanyika linalokutaka uvumilie hali ngumu, wakati huo unapaswa ufahamu ni nini mapenzi ya Mungu, na ni jinsi gani unapaswa kuyajali mapenzi ya Mungu. Usijiridhishe mwenyewe: Jiweke kando kwanza. Hakuna kitu kilicho duni kuliko mwili. Ni lazima udhamirie kumridhisha Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako. Katika mawazo kama hayo, Mungu atakupa nuru ya kipekee katika jambo hili, na moyo wako pia utapata faraja. Jambo lolote likikutendekea, liwe dogo au kubwa, ni sharti kwanza ujiweke pembeni na kuuona mwili kama kitu duni zaidi kuliko vitu vyote. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo unavyochukua uhuru zaidi; ukiuridhisha mara hii, wakati mwingine utataka zaidi, na jinsi hili linaendelea, ndivyo unapata kuupenda mwili hata zaidi. Mwili mara zote una tamaa kupita kiasi, mara zote mwili unakutaka uuridhishe, na kwamba uutosheleze kwa ndani, iwe ni katika chakula unachokula, unachokivaa, au kuwa na hasira katika matendo yako, au kuushawishi udhaifu na uzembe wako…. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo tamaa yake inaongezeka, na jinsi mwili unavyopotoka zaidi, hadi kufikia kiwango ambacho miili ya watu inahodhi dhana nzito, na kutomtii Mungu, na kujiinua, na kuanza kuishuku kazi ya Mungu. … Hivyo unafaa kuuasi mwili na usiutosheleze: “Mume wangu(mke), watoto, matarajio, ndoa, familia—hakuna hata moja kati ya haya ambalo ni la thamani! Moyoni mwangu mna Mungu pekee na nitajaribu kumridhisha Mungu kadiri ya uwezo wangu, na si kuuridhisha mwili.” Lazima uwe na azimio hili. Daima ukiwa na azimio hili, basi ukiuweka ukweli katika vitendo, na kujiweka kando, utaweza kufanya hivyo kwa juhudi kidogo.
kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Iwapo utapata uzima mbele za Mungu, na namna hatima yako itakavyokuwa, inategemea uasi wako dhidi ya mwili utakuwa wa namna gani. Mungu amekuokoa, na kukuteua na kukuamulia kabla, bado ikiwa leo hauko radhi kumridhisha, hauko radhi kuuweka ukweli katika vitendo, hauko radhi kuuasi mwili wako kwa moyo umpendao Mungu kwa dhati, hatimaye utajiangamiza mwenyewe, na kwa hivyo utapitia mateso mengi. Ikiwa mara zote unautosheleza mwili, Shetani atakumeza hatua kwa hatua, na kukuacha bila uzima, au upako wa Roho, hadi siku itafika ambayo ndani utakuwa giza. Ukiishi katika giza, utakuwa umetekwa nyara na Shetani, hutakuwa na Mungu tena moyoni mwako, na wakati ule utaukataa uwepo wa Mungu na kumwacha. Kwa hivyo, ikiwa unataka kumpenda Mungu, ni lazima ulipe gharama ya uchungu na kupitia shida. Hakuna haja ya hamasa za nje na shida, kusoma zaidi na kuzungukazunguka zaidi; badala yake, unafaa kuweka kando vitu vilivyomo ndani yako: mawazo kupita kiasi, maslahi ya kibinafsi, na masuala yako binafsi, dhana, na motisha. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.
kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu huwagusa watu ndani ya mioyo yao, na kuwapa nuru na mwangaza. Kwa hivyo katika tukio lolote katika vita: Kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Mtu anashindwa kujua ama acheke au alie. Kwa sababu motisha nyingi ndani ya watu zina makosa, ama kwa sababu kazi kubwa ya Mungu inakinzana na dhana zao, watu wakiuweka ukweli katika vitendo vita vikali huzuka kisirisiri. Baada ya kuuweka huu ukweli katika vitendo, kisirisiri watu watakuwa wamemwaga machozi mengi sana ya huzuni kabla ya kuamua kumridhisha Mungu. Ni kwa sababu ya vita hivi watu huvumilia shida na usafishaji; huku ni kuteseka kwa kweli. Vita vikikukabili, kama unaweza kusimama kweli upande wa Mungu, utaweza kumridhisha. Kuteseka katika harakati ya kutenda ukweli hakuepukiki; ikiwa, wanapoweka ukweli katika vitendo, kila kitu ndani yao kingekuwa sawa, basi wasingehitaji kufanywa wakamilifu na Mungu, na kusingekuwa na vita, na hawangeteseka. Ni kwa sababu kuna mambo mengi ndani ya watu ndipo hawafai kutumiwa na Mungu, na tabia nyingi za uasi wa mwili, ndipo watu wanapaswa kujifunza funzo la kuasi dhidi ya mwili kwa kina zaidi. Huku ndiko Mungu anaita kuteseka ambako Alimtaka mwanadamu kushiriki Naye.
kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika imani yao kwa Mungu, kile ambacho watu hutafuta ni kupata baraka kwa ajili ya siku zijazo; hili ndilo lengo lao katika imani yao. Watu wote wana kusudi na tumaini hili, lakini upotovu ulio katika asili yao lazima uondolewe kupitia majaribu. Katika hali ambazo bado hujatakaswa, hizi ndizo hali ambamo lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili uweze kujua upotovu wako mwenyewe. Hatimaye, unafika hatua ambapo unaona heri kufa na kuziacha njama na tamaa zako, na kutii mamlaka na mipango ya Mungu. Kwa hiyo, kwa yeyote ambaye hana miaka kadhaa ya usafishaji na hajapitia kiwango fulani cha mateso, hataweza kujiondolea vifungo vya upotovu wa mwili katika mawazo na mioyo yake. Katika hali zozote zile ambazo bado ungali mtumwa wa Shetani, na katika hali zozote zile ambazo bado ungali na tamaa zako mwenyewe na matakwa yako mwenyewe, hizi ndizo hali ambamo unapaswa kuteseka. Ni kupitia mateso tu ndio watu wanaweza kupata mafunzo, kupata ukweli, na kuelewa mapenzi ya Mungu. Kwa kweli, ukweli mwingi unafahamika kwa kupitia majaribu makali. Hakuna anayeweza kufahamu mapenzi ya Mungu, kutambua uweza na busara ya Mungu, wala kuiona tabia ya haki ya Mungu anapokuwa katika mazingira ya utulivu na rahisi au wakati hali ni nzuri. Hilo halingewezekana!
kutoka katika “Namna ya Kumridhisha Mungu Katikati ya Majaribu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Mungu hufanya kazi ndani ya kila mtu, na bila kujali mbinu Yake ni ipi, Anawatumia watu, vitu na mambo ya aina gani kufanya huduma, au maneno Yake yana sauti ya aina gani, Ana lengo moja tu la mwisho: kukuokoa. Kukuokoa kunamaanisha kukugeuza, na hivyo utakosaje kuteseka kidogo? Ni lazima upate kuteseka. Kuteseka huku kunaweza kuhusisha mambo mengi. Wakati mwingine, Mungu huibua watu, mambo, na vitu ambavyo viko karibu nawe ili kukufunua, kukuwezesha kujitambua, vinginevyo Yeye hukushughulikia moja kwa moja, kukupogoa, na kukufichua. Kama vile tu mtu aliye juu ya meza ya upasuaji–lazima upitie maumivu kiasi kwa ajili ya matokeo mazuri. Kama kila wakati Mungu anapokupogoa na kukushughulikia na kila wakati Anaibua watu, mambo, na vitu, hilo huchochea hisia zako na kukuongezea nguvu, basi kupitia hayo kwa njia hii ni sahihi, na utakuwa na kimo na utaingia katika uhalisi wa ukweli. Ikiwa, kila wakati unapopogolewa na kushughulikiwa, na kila wakati Mungu anapoinua mazingira yako, wewe huhisi maumivu au usumbufu wowote, na huhisi chochote kabisa, na kama huji mbele za Mungu kuelewa mapenzi Yake, wala huombi au kutafuta ukweli, basi wewe kweli ni mtu asiyejali kabisa! Watu ambao hawajali kabisa kamwe si hawatambui kiroho; kwa hiyo, Mungu hana njia ya kufanya kazi kwao. Mungu atasema: “Mtu huyu hajali kabisa na amepotoshwa sana. Nimemfanyia mambo mengi, nimetia bidii nyingi, lakini bado Siwezi kuuita moyo wake na Siwezi kuamsha roho yake. Jambo hili ni sumbufu na gumu sana.” Mungu akipanga mazingira, watu, vitu, na mambo fulani kwa ajili yako, Akikupogoa na kukushughulikia na ukijifunza kutokana na hili, ikiwa umejifunza kuja mbele za Mungu kutafuta ukweli, na, bila kujua, umetiwa nuru na kuangaziwa na kupata ukweli, ikiwa umepitia mabadiliko katika mazingira haya, umepata thawabu, na kupiga hatua, ukianza kuwa na ufahamu mdogo kuhusu mapenzi ya Mungu na kuacha kulalamika, basi yote haya yatamaanisha kuwa umesimama imara katikati ya majaribio ya mazingira haya, na umestahimili jaribio. Kwa hiyo, utakuwa umeshinda majaribu haya.
kutoka katika “Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Kujua zaidi Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni