10.31.2018

Maana ya Ishara ya Ghadhabu ya Mungu

Maana ya Ishara ya Ghadhabu ya Mungu

I
Maonyesho ya Mungu ya ghadhabu Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za uovu zitakoma kuwepo;
yanaashiria kuwa nguvu zote za kihasama zitaharibiwa.
Huu ndio upekee wa tabia ya Mungu ya haki, na ni upekee wa ghadhabu ya Mungu.
Heshima ya Mungu na utakatifu unapopingwa,
nguvu za haki zinapozuiliwa, bila kuonekana na mwanadamu,
hapa ndipo wakati Mungu atatuma ghadhabu Yake.
Hapa ndipo wakati Mungu atatuma ghadhabu Yake.
Kwa sababu ya kiini cha Mungu,
nguvu zote duniani zinazoshindana naye, kumpinga ni ovu, zisizotenda haki.
Zote zinatoka kwa Shetani, ni za Shetani.
Kwa kuwa Mungu ni mwenye haki, mwenye mwanga, na mtakatifu,
hivyo vitu vyote viovu, vilivyopotoka, vya Shetani, vitatoweka kutoka hapa.
Hii itatokea Mungu atakapotuma ghadhabu Yake.
Hapa ndipo wakati Mungu atatuma ghadhabu Yake.
Nguvu zote za uovu zitakomeshwa Mungu atakapotuma ghadhabu Yake.
Dhambi zote zinazomdhuru mwanadamu zitakomeshwa Mungu atakapotuma ghadhabu Yake.
Nguvu zote za kihasama zitatambulika, zitatengwa na kulaaniwa,
wasaidizi wa Shetani kuadhibiwa, kuondolewa Mungu atakapotuma ghadhabu Yake.
II
Na kazi ya Mungu inaendelea bila vikwazo.
Mpango Wake wa usimamizi unaendelea hatua moja kwa wakati kwa ratiba Yake.
Hii ni baada ya Mungu kutuma ghadhabu Yake.
Wateule Wake wawe huru kutokana na usumbufu na udanganyifu wa shetani.
Wafuasi Wake wanafurahia ugavi Wake katika mahali pa amani.
Hii ni baada ya Mungu kutuma ghadhabu Yake.
Hii ni baada ya Mungu kutuma ghadhabu Yake.
III
Ghadhabu ya Mungu ni kinga
ikizuia nguvu za uovu kuzidishwa na kuenea pote.
Ghadhabu ya Mungu ni kinga
ikilinda kuwepo kwa vitu vyote vya haki na vizuri.
Ghadhabu ya Mungu ni kinga ikilinda vilivyo vya haki na vizuri
kutokana na ukandamizaji na na mapinduzi.
kutoka kwa "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni