9.10.2018

Mwanadamu Anafaa Kuishi kwa Ajili Ya Nani

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Nyimbo, Mungu, maombi

Mwanadamu Anafaa Kuishi kwa Ajili Ya Nani

Sikuwa wazi kuhusu yule mwanadamu anafaa kuishi kwa ajili yake. Sasa nina jibu lake.
Nilikuwa nikiishi tu kwa ajili yangu mwenyewe, nikitafuta tu hadhi na umaarufu.
Maombi kwa Mungu yaliyojawa na maneno mazuri, ilhali nashikilia njia yangu mwenyewe katika maisha.
Imani inayotegemea siku za usoni na hatima, sina ukweli wowote au uhalisi.
Mila na masharti, vikiifungia imani yangu; niliachwa na utupu pekee.
Nikikosa kuishi kama mwanadamu, sistahili upendo wa Mungu kwangu.
Moyo wangu umeamshwa sasa, ukiniambia lazima nilipize upendo wa Mungu.
Najichukia kwani sikuwa na dhamiri, kumuasi Mungu na kuuvunja moyo Wake.
Sijawahi kujali kuhusu moyo wa Mungu; sikujali kamwe kuhusu maneno Yake.
Bila dhamiri, bila kuwa na akili, nawezaje kutajwa kama mwanadamu?
Hukumu ya Mungu inanifanya nione, nilikuwa nimepotoshwa kwa kina na Shetani.
Uovu, dunia hii, imejaa mitego; ukweli ni kile ambacho muumini anafaa kuchagua.
Ee Mungu mpendwa, Unanipenda sana, Ukifanya yote uwezayo kunifanya niokolewe.
Kile ambacho Umenifanyia, nitaweka akilini mwangu! Sitasahau kamwe.
Kuujali moyo wa Mungu, hiyo ndiyo nia yangu yote. Naazimia kufuatilia ukweli.
Nikijitumia mwenyewe kumtumikia Mungu, nikijitolea kulipa upendo Wake,
nikijitolea kulipa upendo Wake.

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

         Soma zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni