9.12.2018

Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu


  •  
  • Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu"
  • ni ya kugusa na yenye kutia moyo.
  • Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu,
  • uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana
  • tunaanza kuhisi mshangao, mshangao na uvutiwaji.
  • I
  • Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure,
  • upendo wa Mungu umemzunguka.
  • Mwanadamu, maasumu na safi, bila ya wajibu wa kumnyima uhuru,
  • huishi kwa furaha kamili machoni mwa Mungu.
  • Mungu humtunza mtu, na mtu huishi chini ya mabawa Yake.
  • Yote ambayo mtu hufanya, maneno yake yote na matendo,
  • yamefungwa pamoja na Mungu, hayawezi kujitenga.
  • II
  • Kutoka wakati wa kwanza Mungu alipowaumba wanadamu,
  • Mungu aliwaweka chini ya uangalizi Wake.
  • Ni uangalizi wa aina gani huo?
  • Ni jukumu Lake kumlinda mtu na kumchunga mtu.
  • Anamtumainia mtu kuamini katika,
  • kuamini katika na kuyatii maneno Yake.
  • Hiki ndicho kitu cha kwanza ambacho Mungu alikitarajia kwa wanadamu.
  • III
  • Akiwa na tumaini hili la kwanza, Mungu aliyasema maneno yafuatayo:
  • "Matunda ya kila mti wa bustani mwaweza kuyala:
  • Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, mema na mabaya,
  • msiyale:
  • kwa maana siku mtakapoyala matunda ya mti huo hakika mtakufa."
  • Maneno haya rahisi, yakisimamia mapenzi ya Mungu,
  • yaonyesha kuwa kumjali mtu kulikuwa tayari katika moyo Wake.
  • IV
  • Hivyo, kwa maneno haya rahisi, tunaona kilicho moyoni mwa Mungu.
  • Je, kuna upendo katika moyo Wake? Si kuna utunzaji na dhima?
  • Upendo na utunzaji wa Mungu ni jambo ambalo linaweza kuonekana na kuhisiwa.
  • Kama wewe ni mtu wa dhamiri na una ubinadamu,
  • utajihisi vuguvugu, ukitunzwa na kupendwa,
  • utajihisi mwenye heri na furaha.
  • V
  • Unapoyahisi mambo haya, utatenda vipi mintarafu ya Mungu?
  • Utakuwa mwaminifu Kwake?
  • Upendo wa staha, upendo wa staha hutakua katika moyo wako?
  • Moyo wako utasogea karibu na Yeye?
  • Kutokana na haya tunaona,
  • jinsi upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa mtu.
  • Lakini hata muhimu zaidi kuliko hili ni kwamba
  • mtu anaweza kuuhisi na kuuelewa upendo wa Mungu.
  •  
  • kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili


kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

                 Soma zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni