9.08.2018

Nisingeokolewa na Mungu

Umeme wa Mashariki, Mungu, Roho Mtakatifu

Nisingeokolewa na Mungu

Nisingeokolewa na Mungu, ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu,
nikipambana kwa bidii na maumivu katika dhambi; kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio.
Nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani,
kama nimenaswa katika dhambi na starehe zake, bila kujua maisha yangu yangekuwaje.
Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma kwangu, maneno Yake yananiita.
Huniruhusu niisikie sauti Yake na kuniinua mbele ya kiti Chake cha enzi.
Kila siku nakula na kunywa maneno ya Mungu, nafurahia kazi ya Roho Mtakatifu.
Naona kwamba upotovu wa binadamu ni wa kina sana, kwamba tunahitaji wokovu wa Mungu.
Ukweli wa Mungu hunitakasa na kuniokoa.
Nahukumiwa na kusafishwa mara nyingi, na tabia yangu ya kishetani inatakaswa.
Kujua kwamba Mungu ni mwenye haki na mtakatifu, nakuja kuelewa uzuri Wake.
Naweza kumwogopa Mungu na kuepuka uovu, na tabia ya maisha yangu inabadilika.
Nimemwona Mungu uso kwa uso, nimeonja upendo Wake wa kweli.
Naona kwamba ukweli ni wa thamani sana, kwamba ni maisha ya milele ambayo Mungu humpa mwanadamu. 
Namtii Mungu na kutimiza wajibu wangu; moyo wangu una utulivu na unapata amani, ninaridhika.
Baada ya hukumu na kuadibu kwa Mungu, napokea wokovu Wake wa siku za mwisho.
Natembea katika njia inayong’aa ya maisha, maisha yangu yana maana.
Napokea wokovu mkuu zaidi wa Mungu, na moyo wangu umejaa shukrani isiyo na mwisho.
Mungu yuko karibu sana, mwenye kupendeza sana, niko tayari kumpa Yeye mwili na roho yangu.
Nitamtii Yeye na kumpenda katika maisha yangu yote, nitalipiza upendo Wake kwa uaminifu wangu.

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni