9.01.2018

Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ni Kuwa na Uhalisi

Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ni Kuwa na Uhalisi

Kuwa na uwezo wa kuyaeleza maneno ya Mungu kiwazi haimaanishi kwamba wewe unaumiliki uhalisi. Mambo si rahisi kama ulivyofikiria. Ikiwa unaumiliki uhalisi au la haina msingi kwa kile unachokisema, badala yake inatokana na kile unachoishi kwa kudhihirisha. Wakati maneno ya Mungu yanakuwa maisha yako na kujionyesha kwako kwa asili, hapo ndipo unapoumiliki uhalisi, hapo ndipo umeupata uelewa na kimo cha kweli. Lazima uwe na uwezo wa kuhimili uchunguzi kwa muda mrefu, lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kuidhihirisha sura ambayo inahitajika kwako na Mungu. Isiwe mkao tu, lakini ni lazima ibubujike kwa kawaida kutoka ndani mwako; ndipo basi tu utakapokuwa na uhalisi kikweli, ndipo tu basi utakapopata maisha. Acha Nitumie mfano wa “watendaji-huduma” ambao kila mtu ana uzoefu nao. Mtu yeyote anaweza kuzungumzia nadharia zenye fahari sana kuhusu “watendaji-huduma”; nyote mnacho kiwango kinachofaa cha ufahamu kuhusu jambo hili, na kila mmoja wenu anao uhodari katika kuzungumzia jambo hili kana kwamba ni mashindano. Hata hivyo, kama mwanadamu hajakuwa na uzoefu wa jaribio kubwa, ni vigumu sana kwake kuwa na ushahidi mzuri. Kwa ufupi, kuishi kwa kudhihirisha kwa mwanadamu bado ni fukara sana, ambayo inatofautiana na uelewa wake. Kwa hiyo, bado hakijakuwa kimo halisi cha mwanadamu, bado hayajakuwa maisha ya mwanadamu. Kwa sababu uelewa wa mwanadamu haujaletwa katika uhalisi, kimo cha mwanadamu ni kama ngome katika anga, bila msingi wowote wa ukweli. Mwanadamu anao uhalisi kidogo mno, ni vigumu kuupata uhalisi wowote katika mwanadamu. Kunao uhalisi kidogo mno unaobubujika kwa asili kutoka kwa mwanadamu, uhalisi wote katika maisha yake umelazimishwa, hivyo nasema kwamba mwanadamu hamiliki uhalisi wowote. Usiweke hisa nyingi sana katika wanadamu wakisema kwamba upendo wao wa Mungu haubadiliki kamwe, hiki tu ni kile wanadamu wangesema kabla ya kukabiliwa na majaribu. Mara tu wanapokabiliwa na majaribu kwa ghafla, mambo ambayo wanadamu hunena kwa mara nyingine tena hayalingani na uhalisi, na kwa mara nyingine yatathibitisha kwamba wanadamu hawana uhalisi. Inaweza kusemwa kwamba, wakati wowote unapokumbana na mambo ambayo hayalingani na dhana zako nayo inakuhitaji kujiweka kando, haya ni majaribu yako. Kila wakati kabla mapenzi ya Mungu hayajafichuliwa ni mtihani mkali kwa kila mwanadamu, ni jaribio kubwa kwa wanadamu wote; je, waweza kuona wazi kupitia jambo hili? Wakati Mungu anataka kuwajaribu wanadamu, Mungu daima huwaacha wanadamu kufanya maamuzi yao kabla ya ukweli wa uhalisi kufichuliwa; ambayo ni kusema, wakati Mungu anakujaribu, kamwe Yeye hatakwambia ukweli, na hivyo ndivyo wanadamu wanaweza kufichuliwa. Hii ni njia mojawapo ambayo Mungu huifanya kazi yake, ili kuona kama unamwelewa Mungu wa leo, ili kuona kama unaumiliki uhalisi wowote. Je, kweli wewe huna shaka yoyote kuhusu kazi ya Mungu? Je, utabaki umesimama wakati jaribio kuu linakujia? Ni nani anayethubutu kusema maneno kama vile “Nahakikisha hakutakuwa na matatizo”? Nani anayethubutu kusema maneno kama vile “Wengine wanaweza kuwa na mashaka, lakini Mimi sitakuwa na shaka kamwe”? Kama vile wakati Petro alipokuwa akijaribiwa—anazungumza vikubwa daima kabla ukweli haujafichuliwa. Huu sio udhaifu wa kibinafsi wa kipekee kwa Petro, hii ni shida kubwa zaidi inayomkabili kila mwanadamu sasa. Kama ningetembelea maeneo kadhaa, au kama ningewatembelea ndugu na dada kadhaa, kuuangalia uelewa wenu wa kazi ya Mungu ya leo, hakika mngeweza kuzungumza kuhusu mengi ya uelewa wenu, nayo ingeonekana kwamba ninyi hamna shaka yoyote. Kama ningewauliza: “Je, kweli waweza kutabainisha kwamba kazi ya leo inatekelezwa na Mungu Mwenyewe? Bila shaka yoyote”? ungejibu bila shaka: Bila shaka yoyote, ni kazi inayotekelezwa na Roho wa Mungu. Mara tu unapojibu kwa namna hiyo, kwa hakika usingekuwa hata na chembe cha shaka, unaweza hata kuhisi starehe kubwa, unaweza kuhisi kuwa umepata uhalisi kiasi kidogo. Wale ambao huelewa mambo kwa njia hii ni wale ambao wanamiliki uhalisi kidogo zaidi; kadri mtu anavyodhani kwamba “amepata uhalisi,” ndivyo atakavyokosa uwezo wa kustahimili majaribio. Ole wao walio na kiburi na wenye maringo, ole wao wasio na maarifa ya wao wenyewe. Watu kama hawa ni hodari katika kuzungumza, lakini huendelea vibaya zaidi katika matendo yao. Wakati kuna dalili ndogo zaidi ya matatizo, watu hawa wataanza kuwa na mashaka, mawazo ya kukata tamaa yangeingia akilini mwao. Hawana umiliki wa uhalisi wowote, yote waliyo nayo ni nadharia zenye fahari zaidi kuliko zile za dini, bila ya hali halisi ambazo Mungu amewahitaji wafanye leo. Nachukizwa zaidi na wale wanaosema kuhusu nadharia tu nao hawana uhalisi. Wao kufanya kilio kikubwa zaidi wanapoitenda kazi yao, lakini wao huanguka wakati wanapokabiliwa na uhalisi. Je, si inaonyesha kwamba watu hawa hawana uhalisi? Kama unaweza kubaki umesimama licha ya ukali wa dhoruba ambayo unakabiliwa nayo, bila hata ya chembe cha shaka kuingia mawazoni mwako, kama unaweza kubaki umesimama, kama unaweza kuendelea kutoikana kazi ya Mungu, hata kama hakuna mtu mwingine aliyebaki, basi hii inaonyesha kwamba unao uelewa wa kweli, hii inaonyesha kwamba kweli unao umiliki wa uhalisi. Ikiwa unapaswa kufuata njia yoyote ambayo upepo unavuma, ikiwa unapaswa kuwafuata walio wengi na kujifunza kusema yale ambayo wengine wanasema, haijalishi jinsi gani unavyoweza kusema mambo hayo vizuri, sio thibitisho kwamba unao umiliki wa uhalisi. Kwa hiyo, napendekeza kwamba usiwe na haraka ya kupiga kelele kwa maneno matupu. Je, unaijua kazi ambayo Mungu ataitekeleza? Usitende kama Petro mwingine usije ukajiletea aibu, usije ukashindwa tena kutembea bila haya, nayo haimfaidi mtu yeyote. Wanadamu wengi hawana kimo cha kweli. Wao bado hawajatembelewa na ujio wowote wa ukweli baada ya kazi yote ambayo Mungu ameitekeleza, kwa kuwa sahihi zaidi, Mungu hajawahi kumwadibu yeyote binafsi; baadhi yao walikashifiwa na majaribio kama haya, na minyiri yao ya dhambi ikitambaa nje zaidi na zaidi, wakifikiri kwamba wanaweza kumchukulia Mungu kwa kutojali, na kufanya chochote wanachotaka. Kwa kuwa hawawezi hata kustahimili majaribu kama hayo, kadri majaribio yenye changamoto yasivyowezekana, ndivyo uhalisi pia hauwezekani. Je, si hii ni kumpumbaza Mungu? Kuwa na uhalisi sio kitu ambacho kinaweza kubuniwa, pia sio kitu ambacho unaweza kukipata kutokana na maarifa yako kwao; unalingana na kimo chako cha ukweli, unalingana na kama unao uwezo wa kuhimili majaribu yote. Je, unaelewa sasa?
Masharti ya Mungu kwa wanadamu siyo tu kuweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Je, si hiyo itakuwa rahisi sana? Kwa nini basi Mungu anazungumza kuhusu kuingia katika maisha? Kwa nini Anaongea kuhusu mabadiliko? Kama kunayo mazungumzo matupu tu kuhusu uhalisi, mabadiliko katika tabia yangeweza kupatikana? Kuwafunza jeshi la tabaka aali ya watu wenye uwezo wa ufalme sio sawa na kuwafunza wanadamu ambao wanaweza tu kuongea kuhusu uhalisi, sio sawa na kuwafunza wanadamu ambao wanajivunia tu, lakini wanadamu ambao wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu wakati wote, kuwa wagumu bila kujali vikwazo wanavyokumbana navyo, kuishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu wakati wote, bali si kuurudia ulimwengu. Huu ndio uhalisi ambao Mungu anauzungumzia, nayo ni matakwa ya Mungu kwa binadamu. Kwa hiyo, usiuzingatie uhalisi ulionenwa na Mungu kimchezo. Kupata nuru tu kwa Roho Mtakatifu sio sawa na kuumiliki uhalisi: Hiki sicho kimo cha wanadamu, lakini neema ya Mungu, nayo haihusishi mafanikio yoyote ya wanadamu. Kila mwanadamu ni lazima ayavumilie mateso ya Petro, na hata zaidi aumiliki utukufu wa Petro, ambao ndio watu huishi kwa kudhihirisha baada ya kupewa kazi ya Mungu; hii tu ndiyo inaweza kuitwa uhalisi. Usidhani kwamba atakuwa na uhalisi kwa sababu unaweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Huu ni uongo, huu haulingani na mapenzi ya Mungu, na huu hauna maana halisi. Usiseme mambo kama haya katika siku zijazo, komeshamisemo kama hii! Wale wote walio na uelewa wa uongo wa maneno ya Mungu ni makafiri. Hawana maarifa yoyote halisi, hata kwa kiasi kidogo hawana kimo chochote halisi; wao ni watu wenye kujigamba bila ya uhalisi. Hiyo ni, wale wote wanaoishi nje ya dutu ya maneno ya Mungu ni makafiri. Wale wanaoonekana kuwa makafiri na wanadamu ni wanyama mbele za Mungu, wale wanaoonekana kuwa makafiri na Mungu ni wale ambao hawana maneno ya Mungu kama maisha yao. Kwa hiyo, wale ambao hawana uhalisi wa maneno ya Mungu nao wanashindwa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ni makafiri. Nia ya Mungu ni kufanya iwe kwamba kila mmoja anaishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu, sio kwamba kila mtu anaweza tu kuzungumza kuhusu uhalisi, lakini muhimu zaidi, kwamba kila mmoja anaweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu. Uhalisi ambao mwanadamu anautambua ni wa juu juu sana, hauna thamani, unashindwa kutimiza mapenzi ya Mungu, hauna adabu kwa kiasi kikubwa, hata haustahili kutajwa, unakosa sana, uko mbali sana na kiwango cha mahitaji ya Mungu. Ukaguzi mkuu utawatembelea kila mmoja wenu, ili kuona ni nani kati yenu anayejua tu kuzungumza kuhusu uelewa wako lakini hawezi kuonyesha njia, kuona ni nani kati yenu ni taka bure. Kumbuka hili katika siku zijazo. Usizungumze kuhusu uelewa mtupu, zungumza tu kuhusu njia ya utendaji, zungumza tu kuhusu uhalisi. Ondoka kutoka maarifa halisi hadi kwenye vitendo halisi, kisha ondoka kutoka kutenda hadi kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. Usiwahutubie wengine, usizungumze kuhusu maarifa ya ukweli. Kama uelewa wako ni njia, basi unaweza kuuachilia; kama si njia, basi tafadhali nyamaza, na uache kuongea. Kile unachosema ni bure, baadhi ya maneno ya uelewa ya kumpumbaza Mungu tu, ili wengine wakuonee wivu, si hilo ni lengo lako? Je, si hii ni kuwachezea wengine kimakusudi? Je, kunayo thamani yoyote katika hili? Zungumza tu kuhusu uelewa baada ya kuwa na uzoefu, basi hutakuwa unajisifu tena, ama sivyo wewe ni mtu tu ambaye anasema maneno yenye kiburi. Huwezi hata kuyashinda mambo mengi katika uzoefu wako halisi, huwezi hata kuasi dhidi ya mwili wako wenyewe, siku zote ukifanya chochote unachoelekezwa kukifanya kwa tamaa zako, sio kwa kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, lakini bado unayo nyongo ya kuzungumzia uelewa wa kinadharia, huna haya, lakini unayo nyongo ya kuzungumza kuhusu uelewa wako wa maneno ya Mungu, u mfidhuli jinsi gani. Majivuno na majisifu ya aina hii yamekuwa asili yako, umekuwa na desturi kwavyo, viko kwenye ncha ya vidole vyako kila wakati unapotaka kuvizungumzia, nawe unajiingiza katika mapambo inapokuja wakati wa kutenda. Je, si hii ni kuwapumbaza wengine? Unaweza kuwapumbaza wengine, lakini Mungu hawezi kupumbazwa. Wanadamu hawajui, hawawezi kutambua, lakini Mungu anatilia maanani masuala hayo, naye hatakusaza. Ndugu na dada zako wanaweza kukutetea, wakiusifu uelewa wako, wakipendezwa nawe, lakini ikiwa huna uhalisi, Roho Mtakatifu hatakusaza. Labda Mungu wa matendo hatazikaripia dosari zako, lakini Roho wa Mungu hataweka makini yoyote kwako, na hiyo itatosha. Je, unaniamini? Zungumza zaidi kuhusu uhalisi wa utendaji; Je, umeshasahau tayari? Zungumza zaidi kuhusu njia za kiutendaji; Je, ushasahau tayari? “Zungumza kwa uchache kuhusu nadharia za fahari, au majivuno yasiyo na maadili, ni bora uanze kuweka hii katika matendo kuanzia sasa na kuendelea,” Je, umesahau maneno haya? Je, huelewi yoyote haya? Je, hauna uelewa wa mapenzi ya Mungu?

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

     Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni