Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu
Tofauti Kati Ya Matendo Mazuri ya Nje na Mabadiliko Katika Tabia
Maneno Husika ya Mungu:
Mabadiliko katika tabia hasa huhusu mabadiliko katika asili ya watu. Mambo ya asili ya mtu hayawezi kuonekana kutoka kwa mienendo ya nje; yanahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuwepo kwake. Yaani, yanahusisha moja kwa moja mitazamo ya mtu kuhusu maisha na maadili yake, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi yake, na kiini chake. Mtu ambaye hawezi kukubali ukweli hatakuwa na mabadiliko katika hali hizi. Ni kwa kupitia kazi ya Mungu pekee, kuingia kikamilifu katika ukweli, kubadili maadili na mitazamo yake kuhusu kuwepo na maisha, kulinganisha msoni yake na ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zake zinaweza kusemekana zimebadilika.
Huenda ukaonekana kufanya juhudi fulani, unaweza ukawa thabiti unapokabiliwa na shida, huenda ukaweza kutekeleza utaratibu wa kazi kutoka walio juu, au huenda ukaweza kwenda popote unapoambiwa kwenda, lakini haya ni mabadiliko madogo tu katika mienendo yako, na hayatoshi kujumuisha mabadiliko katika tabia yako. Huenda ukaweza kukimbia katika njia nyingi, kuvumilia shida nyingi na kustahamili fedheha kuu; huenda ukajihisi karibu sana na Mungu, na Roho Mtakatifu anaweza kukufanyia kazi fulani. Hata hivyo, Mungu anapokuomba ufanye jambo fulani ambalo halipatani na fikira zako, huenda bado usitii, lakini utafute visababu, na kuasi na kumpinga Mungu, hata kufikia kiwango cha wewe kumhakiki Mungu na kumpinga Yeye. Hili ni tatizo kubwa! Hili linaonyesha kwamba bado una asili inayompinga Mungu na kwamba hujapitia mabadiliko yoyote kabisa.
kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Watu wanaweza kuwa na tabia nzuri, lakini hiyo haimaanishi kuwa wako na ukweli. Bidii ya watu inaweza tu kuwafanya wazingatie mafundisho na kufuata kanuni; watu wasio na ukweli hawana namna ya kutatua shida halisi, na mafundisho hayawezi kushikilia nafasi ya ukweli. Wale ambao wamepitia mabadiliko katika tabia zao ni tofauti. Wale ambao wamepitia mabadiliko katika tabia zao wameelewa ukweli, wanatambua masuala yote, wanajua jinsi ya kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, jinsi ya kutenda kulingana na kanuni za ukweli, jinsi ya kutenda ili kumridhisha Mungu, nao wanaelewa asili ya upotovu wanaoufichua. Mawazo na dhana zao wenyewe vinapofichuliwa, wanaweza kutambua na kuunyima mwili. Hivi ndivyo mabadiliko katika tabia yanavyoonyeshwa. Kitu cha muhimu kuhusu mabadiliko katika tabia ni kwamba wameelewa vyema ukweli, na wanapotekeleza mambo, wanauweka ukweli katika matendo kwa usahihi wa karibu na upotovu wao hauonekani mara nyingi. Kwa jumla, watu ambao tabia zao zimebadilika huonekana kuwa hasa wenye busara na wenye utambuzi, na kwa sababu ya kuelewa kwao ukweli, hawaonyeshi kujidai na kiburi sana. Wanaweza kubaini na kutambua upotovu mwingi unaofichuliwa, kwa hiyo hawana kiburi. Wanaweza kuwa na ufahamu wa taratibu kuhusu ni ipi nafasi ya mwanadamu, jinsi ya kutenda kwa busara, jinsi ya kuwa mtiifu, nini wanachofaa kusema na nini wasichofaa kusema, na nini cha kusema na nini cha kutenda kwa watu gani. Hii ndiyo sababu inasemwa kuwa watu wa aina hii ni wenye busara kiasi. Wale ambao wana mabadiliko katika tabia zao wanaishi kwa kudhihirisha sura ya binadamu kwa kweli, nao wanao ukweli. Daima wanaweza kuzungumza na kuona vitu kulingana na ukweli, na wana maadili katika kila kitu wanachokifanya; hawashawishiwi na mtu, kitu au jambo lolote, na wote wana maoni yao wenyewe na wanaweza kudumisha maadili ya ukweli. Tabia zao hazisitasiti, na haijalishi hali zao, wanaelewa jinsi ya kutimiza wajibu wao sawasawa na jinsi ya kufanya mambo ili kumridhisha Mungu. Wale ambao tabia zao zimebadilika hawalengi nini cha kufanya ili kujifanya waonekane wazuri katika kiwango cha juujuu—wanao uwazi wa ndani kuhusu kile cha kufanya ili kumridhisha Mungu. Kwa hivyo, kutoka nje wanaweza kukosa kuonekana wenye shauku sana ama kama wamefanya jambo lolote kubwa, lakini kila kitu wanachofanya kina maana, kina thamani, na kina matokeo ya kiutendaji. Wale ambao tabia zao zimebadilika wana uhakika kuwa na ukweli mwingi—hii inaweza kuthibitishwa kwa mitazamo yao kuhusu mambo na kanuni zao katika vitendo vyao. Wale wasio na ukweli hawajakuwa na mabadiliko katika tabia hata kidogo. Hiyo si kusema kwamba mtu aliyekomaa katika ubinadamu wake lazima atakuwa na mabadiliko katika tabia; labda hufanyika wakati baadhi ya sumu za kishetani katika asili ya mtu zinabadilika kwa sababu ya maarifa yao kuhusu Mungu na ufahamu wao wa ukweli. Hiyo ni kusema, sumu hizo za Shetani zinatakaswa na ukweli unaoonyeshwa na Mungu unaanza kustawi ndani ya mtu huyo, unakuwa maisha yake, nao unakuwa msingi wa kuwepo kwake. Hapo tu ndipo anakuwa mtu mpya, na hivyo tabia yake inabadilika. Hivi si kusema kwamba tabia yake ya nje ni ya upole kuliko hapo awali, kuwa alikuwa na kiburi lakini sasa maneno yake ni ya busara, kwamba hakuwa anamsikiza mtu yeyote lakini sasa anaweza kuwasikiza wengine—mabadiliko haya ya nje hayawezi kusemwa kuwa ni mabadiliko katika tabia. Bila shaka mabadiliko katika tabia yanajumuisha hali hizi, lakini jambo lililo muhimu zaidi ni kuwa maisha yake ya ndani yamebadilika. Ukweli unaoonyeshwa na Mungu unakuwa maisha yake hasa, baadhi ya sumu za kishetani zilizo ndani zimetolewa, mtazamo wa mtu huyo umebadilika kabisa, na hakuna chochote kati ya hali hizo kinachokubaliana yale ya dunia. Anaona waziwazi njama na sumu za joka kubwa jekundu; amefahamu kiini cha kweli cha maisha. Kwa hivyo maadili ya maisha yake yamebadilika—hili ndilo badiliko la muhimu zaidi na kiini cha mabadiliko katika tabia.
kutoka katika “Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Katika ulimwengu wa dini, watu wengi huteseka pakubwa maishani mwao mwote, kwa kuihini miili yao au kuubeba msalaba wao, au hata kuteseka na kustahimili hadi pumzi zao za mwisho! Wengine huwa wanafunga hadi siku ya kifo chao. Katika maisha yao yote wanajinyima chakula kizuri na mavazi mazuri, wakisisitiza mateso tu. Wanaweza kuihini miili yao na kuinyima miili yao. Uwezo wao wa kustahimili mateso unastahili sifa. Ila fikira zao, mawazo yao, mielekeo yao ya kiakili, na kwa hakika asili yao ya kale—hakuna kati yavyo kilichoshughulikiwa hata kidogo. Hawajifahamu. Picha ya Mungu akilini mwao ni ya kijadi na ya kidhahania, Mungu asiye yakini. Uamuzi wao wa kuteseka kwa ajili ya Mungu unaletwa na azma na asili yao chanya. Hata ikiwa wanamwamini Mungu, hawamfahamu Mungu wala kuyafahamu mapenzi Yake. Wanamfanyia Mungu kazi na kumtesekea Mungu kama vipofu. Hawawekei utambuzi thamani yoyote na hawajishughulishi na jinsi ambayo huduma yao inatimiza mapenzi ya Mungu kwa kweli. Aidha hawajui jinsi ya kutimiza ufahamu kuhusu Mungu. Mungu wanayemhudumia si Mungu katika sura Yake ya asili, ila ni Mungu waliyejifikiria, Mungu waliyemsikia, au Mungu wa kihadithi wanayemsoma katika maandiko. Kisha wanatumia mawazo yao dhahiri na mioyo yao ya kiungu kumtesekea Mungu na kuifanya kazi ambayo Mungu anapaswa kufanya. Huduma yao haiko sahihi, kiasi kwamba hakuna anayemhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi Yake. Haijalishi wako radhi kiasi gani kuteseka, mitazamo yao asilia ya huduma na picha ya Mungu akilini mwao havibadiliki kwani hawajapitia hukumu ya Mungu na kuadibu na usafishaji Wake na ukamilifu, na kwa sababu hakuna yeyote aliyewaongoza na ukweli. Japo wanasadiki kwa Yesu Mwokozi, hamna kati yao aliyewahi kumwona Mwokozi. Wamemsikia tu kwa hadithi na uvumi. Hivyo huduma yao ni sawa na kuhudumu mara mojamoja macho yao yakiwa yamefungwa kama kipofu anayemhudumia baba yake. Ni nini kinaweza kupatikana kutokana na huduma kama hiyo? Na ni nani anaweza kuikubali? Huduma yao haibadiliki kamwe toka mwanzo hadi mwisho. Wanapokea mafunzo ya kibinadamu na kukita huduma yao katika uasili wao na kile wanachokipenda wao. Hili laweza kuzalisha faida gani? Hata Petro, aliyemwona Yesu, hakujua jinsi ya kumhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi ya Mungu. Ni katika uzee wake ndipo alipopata ufahamu. Hili linaonyesha nini kuhusu wanadamu vipofu ambao hawajapitia ushughulikiaji na hawana upogoaji na ambao hawajawahi kupata yeyote wa kuwaongoza? Je, si huduma ya wengi miongoni mwenu leo ni kama ile ya vipofu? Wale wote ambao hawajapokea hukumu, hawajapokea upogoaji na ushughulikiaji, na hawana mabadiliko—je, wao si waliokosa kushindwa kabisa? Wana manufaa gani watu kama hao? Ikiwa fikira zako, ufahamu wako wa maisha, na ufahamu wako wa Mungu hauonyeshi mabadiliko mapya na hautoi faida hata kidogo, hutatimiza chochote kizuri katika huduma yako. Bila maono na bila ufahamu mpya wa kazi ya Mungu, huwezi kuwa mtu aliyeshindwa. Njia yako ya kumfuata Mungu itakuwa kama ile ya wale wanaoteseka na kufunga—itakuwa ya thamani ndogo! Hii ni kwa sababu kuna ushuhuda kidogo katika yale wayafanyayo ndipo Nasema huduma yao ni bure! Kotekote katika maisha yao, hao watu huteseka, hukaa gerezani kwa muda, na kwa kila wakati, hustahimili, husisitiza mapenzi na ukarimu, na kubeba msalaba wao. Wanatukanwa na kukataliwa na ulimwengu na hupitia kila ugumu. Wanatii hadi mwisho ila bado hawapati ushindi na hawawezi kutoa ushuhuda wa kutwaliwa. Wameteseka si haba, ila kwa ndani hawamfahamu Mungu kabisa. Hakuna fikira zao za zamani, mawazo ya zamani, vitendo vyao, uelewa wa wanadamu, na mawazo ya wanadamu yaliyoshughulikiwa. Kamwe hakuna uelewa mpya ndani yao. Hakuna hata chembe ya ufahamu wao wa Mungu ambao ni wa kweli au ni sahihi. Wamekosa kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Je, huku kwaweza kuwa kumhudumia Mungu? Japo ulimfahamu Mungu zamani, tuseme umeudumisha ufahamu huo hadi leo na kuendelea kukita ufahamu wako kuhusu Mungu kwenye fikira na mawazo yako bila kujali Mungu anafanya nini. Yaani, ikiwa huna ufahamu mpya na wa kweli kuhusu Mungu na ukose kutambua sura na tabia ya kweli ya Mungu. Ikiwa ufahamu wako wa Mungu bado unaongozwa na fikira za uhasama na ushirikina na bado una mawazo na fikira za mwanadamu. Ikiwa hii ndiyo hali, basi hujashindwa. Lengo langu la kukwambia maneno haya yote sasa ni kukupa fursa ya kufahamu na kutumia utambuzi huu kukuongoza katika ufahamu sahihi na mpya. Aidha yanalengwa kukuondolea mawazo ya zamani na utambuzi wa zamani ulio nao ili uweze kuwa na ufahamu mpya. Ikiwa unakula na kunywa matamshi Yangu kweli, basi ufahamu wako utabadilika kwa kiwango kikubwa. Bora tu udumishe moyo mtiifu kwa kula na kunywa matamshi ya Mungu, mtazamo wako utabadilika. Bora tu unaweza kukubali kuadibu kwa kila mara, fikira zako za zamani zitabadilika taratibu. Bora tu fikira zako za zamani zimebadilishwa kabisa na kuwa mpya, vitendo vyako vitabadilika ipasavyo. Kwa njia hii, huduma yako itaendelea kuwa yenye malengo zaidi, na itaweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Ukibadilisha maisha yako, ufahamu wako wa maisha, na mawazo yako mengi kuhusu Mungu, basi uasili wako utadidimia taratibu. Hili, na hakuna jingine ila hili, ndilo tokeo baada ya Mungu kumshinda mwanadamu; haya ndiyo mabadiliko yatakayoonekana ndani ya mwanadamu. Ikiwa katika kumwamini Mungu, yote ujuayo ni kuutiisha na kuuhini mwili wako na kustahimili na kuteseka, na hujui wazi ikiwa unachokifanya ni sawa au la, bila kujali unamfanyia nani kazi, basi vitendo kama hivi vitaletaje mabadiliko?
kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kila mara watu wa kidini kama hao wanapokusanyika, wanauliza, “Dada, umeshinda vipi siku hizi?” Anajibu, “Nahisi kuwa mimi ni mdeni wa Mungu na siwezi kuridhisha matakwa ya moyo Wake.” Mwingine anasema, “Mimi, pia, ni mdeni wa Mungu na nimeshindwa kumkidhi.” Sentensi na maneno haya machache pekee yanaonyesha mambo maovu yaliyo ndani ya nyoyo zao. Maneno kama hayo ni ya kuchukiza zaidi na yenye makosa sana. Asili ya watu kama hao inampinga Mungu. Wale ambao huzingatia uhalisi huwasilisha vyovyote vilivyomo katika nyoyo zao na kufungua mioyo yao katika mawasiliano. Hakuna shughuli hata moja ya uongo, hakuna heshima ama salamu na mazungumzo matupu. Wao daima huwa na uwazi na hawafuati sheria za duniani. Kuna wale ambao wako na upendeleo wa kujionyesha kwa nje, hata bila maana yoyote. Wakati mwingine anaimba, yeye anaanza kukatika, bila hata kugundua kuwa wali katika sufuria yake umeshaungua. Watu wa aina hii si wacha Mungu au waheshimiwa, bali ni watu wa kijinga kupindukia. Hizi zote ni maonyesho ya ukosefu wa ukweli! Wakati watu wengine wanawasiliana kuhusu masuala ya maisha katika roho, ingawa hawasemi kuhusu kuwa wadeni wa Mungu, wao hubaki na upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Kuwa kwako mdeni kwa Mungu hakuhusiani na watu wengine; wewe ni mdeni kwa Mungu, si kwa mwanadamu. Kwa hiyo ina maana gani wewe daima kuzungumzia haya kwa watu wengine? Lazima uweke umuhimu kwa kuingia katika uhalisi, si kwa bidii au maonyesho ya nje.
Je, matendo mazuri ya kijuujuu ya mwanadamu yanawakilisha nini? Hayo huwakilisha mwili, na hata matendo yaliyo bora zaidi ya nje hayawakilishi maisha, ila tabia yako tu mwenyewe. Matendo ya nje ya mwanadamu hayawezi kutimiza matakwa ya Mungu. Wewe daima huzungumza kuhusu udeni wako kwa Mungu, lakini huwezi kuyaruzuku maisha ya wengine au kuwafanya wengine kumpenda Mungu. Je, unaamini kwamba matendo kama hayo yatamridhisha Mungu? Unaamini kwamba hii ndiyo matakwa ya moyo wa Mungu, kwamba haya ni ya roho, lakini kwa kweli huu ni ujinga! Unaamini kwamba yale yanayokupendeza wewe na unayotaka ni yale yanayomfurahisha Mungu. Je, yanayokupendeza yanaweza kuwakilisha yanayompendeza Mungu? Je, tabia ya mwanadamu inaweza kumwakilisha Mungu? Yale yanayokupendeza wewe ndiyo hasa yale humchukiza Mungu, na mienendo yako ni ile ambayo Mungu huchukia na kukataa. Kama unahisi kuwa wewe ni mdeni, basi nenda na usali mbele za Mungu. Hakuna haja ya kuzungumzia jambo hilo kwa watu wengine. Usipoomba mbele za Mungu na badala yake mara kwa mara unajivuta nadhari kwako mbele ya wengine, jambo hili linaweza kutimiza matakwa ya moyo wa Mungu? Kama matendo yako daima yanaonekana tu, hii ina maana kuwa wewe ni mtu bure zaidi ya wote. Ni mtu wa aina gani yule aliye na matendo mazuri ya kijuujuu tu lakini hana uhalisi? Watu kama hao ni Mafarisayo wanafiki na watu wa dini! Msipoacha matendo yenu ya nje na hamuwezi kufanya mabadiliko, basi dalili za unafiki ndani yenu zitazidi kuimarika. Kadiri dalili za unafiki zinavyozidi, ndivyo upinzani kwa Mungu unavyozidi, na mwishowe, watu wa aina hii hakika watatupiliwa mbali!
kutoka katika “Kumwamini Mungu Kunapaswa Kulenge Uhalisi, Si Kaida za Kidini” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Katika ulimwengu wa kidini, kuna wacha Mungu wengi, wao husema, “Tumebadilika kwa sababu ya imani yetu katika Bwana Yesu. Tunaweza kujitahidi kwa ajili ya Bwana, kutenda kazi, kuvumilia gerezani kwa ajili ya Bwana, na hatulikatai jina Lake mbele yawengine. Tunaweza kuyatenda mambo mengi mema, kufadhili, kuchanga na kuwasaidia maskini. Haya ni mabadilikomakubwa! Tumebadilika, ndiyo sababu tunafaa kumngojea Bwana ili atulete katika ufalme wa mbinguni.” Je, mnafikiria nini juu ya maneno haya? Je, mna ufahamu wowote ijapo kwa maneno haya? Je, kutakaswa kunamaanisha nini? Je, unafikiria kwamba kama tabia yako imebadilika na unatenda matendo mema basi umetakaswa? Mtu mwingine husema, “Nimeacha kila kitu.” Hata Nimeiacha kazi yangu ulimwenguni, familia yangu na tamaa za mwili ili kujitahidi kwa ajili ya Mungu. Je, hii ni sawa na kutakaswa? Ingawa umeyatenda haya yote, huu si ushahidi thabiti kwamba umetakaswa. Hivyo, jambo muhimu ni lipi? Je, ni katika kipengele kipi unaweza kupata kutakaswa kunakoweza kuchukuliwa kama kutakaswa halisi? Kutakaswa kwa tabia ya kishetani ambayo humpinga Mungu. Sasa, udhihirisho wa tabia ya kishetani ambao humpinga Mungu ni upi? Je, udhihirisho ulio wazi zaidi ni upi? Kiburi cha mtu, majivuno, haki ya kibinafsi, na kujidai mwenyewe, pamoja na upotovu, hila, kusema uongo, udanganyifu na unafiki. Wakati mambo haya si sehemu ya mtu tena, basi kwa kweli ametakaswa. Kuna madhihirisho 12. Acheni tulitazame kila mojawapo ya haya madhihirisho 12: mtu mwenyewe kujiona kuwa mwenye kuheshimika zaidi; kuwaruhusu wale ambao hunitiiMimi kustawi na wale ambao hunipinga Mimikuangamia; kufikiria tu kuwa Mungu ndiye mkuu zaidi kukushinda, kutomnyenyekea mtuyeyote, kutowajali wengine; kufanyiza ufalme wa kibinafsi mara tu unapokuwa na uwezo; kutaka kuwa mtawala wa pekee na mjua yote na kuyaamua mambo wewe mwenyewe. Huu udhihirisho wote ni tabia za kishetani. Tabia hizi za kishetani lazima zitakaswe kabla ya mtu kuyapitia mabadiliko katika tabia ya maisha yake. Mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu ni kuzaliwa upya kwa sababu kiini chake kimebadilika. Awali, wakati alipopewa uwezo, aliweza kuunda ufalme wa kibinafsi. Sasa, wakati anapopewa uwezo, yeye humhudumia Mungu, humshuhudia Mungu na huwa mtumishi wa wateule wa Mungu. Je, haya siyo mabadiliko halisi? Awali, aliringa mwenyewe katika hali zote na aliwataka watu wengine wamheshimu na kumwabudu. Sasa, yeye humshuhudia Mungu kila mahali, hajishughulishi tena. Bila kujali wanavyonishughulikia watu, ni vyema. Bila kujali watu wanasema nini juu yangu, ni vyema. Sijali. Ninataka tu kumtukuza sana Mungu, kumshuhudia Mungu, kuwasaidia wengine wapate ufahamu wa Mungu, na kuwasaidia wengine watii mbele za uwepo wa Mungu. Je, haya si mabadiliko katika tabia ya maisha? “Nitawashughulikia ndugu kwa upendo. Nitawahurumia wengine katika hali zote. Katika mambo yote, sitajifikiria, nitawafikiria tu wengine. Nitawasaidia wengine kuyastawisha maisha yao na kuyatimiza majukumu yangu. Nitawasaidia wengine kuupata ukweli na kuufahamu ukweli.” Hii ndio maana ya kuwapenda watu, kuwapenda wengine kama mwenyewe! Kumhusu Shetani, unaweza kumtambua, kuwa na kanuni, kuwa na mipaka naye na kuyafunua maovu ya Shetani kabisa ili wateule wa Mungu wasipatwe na madhara yake. Huku ni kuwalinda wateule wa Mungu, na huku ni kuwapenda wengine zaidi kama mwenyewe. Zaidi ya hayo, unapaswa kukipenda ambacho Mungu hukipenda na kukichukia ambacho Mungu hukichukia. Je, basi, Mungu hukichukia nini? Yeye huwachukia wapinga Kristo, pepo waovu, na watu waovu. Hilo linamaanisha kuwa sisi pia tunapaswa kuwachukia wapinga Kristo, pepo waovu na watu waovu. Lazima tusimame upande wa Mungu. Hatuwezi kupatana nao. Mungu huwapenda wale ambao Yeye hutaka kuwaokoa na kuwabariki. Kuhusu watu hawa, lazima tuwajibike, tuwashughulikie kwa upendo, tuwasaidie, tuwaelekeze, tuwakimu na kuwahimili wao. Je, haya si mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu? Zaidi ya hayo, wakati umetenda dhambi au makosa fulani, au umetelekeza kanuni katika kulitenda jambo fulani, unaweza kukubali ukosoaji wa ndugu, kukaripia, kushughulikia na kupogoa; unaweza kuyapokea mambo haya yote kutoka kwa Mungu, usiwe na kinyongo, na uutafute ukweli ili kuusuluhisha upotovu wako. Je, haya si mabadiliko katika tabia yako ya maisha? Ndio, ni mabadiliko. …
Je, mabadiliko katika mwenendo ambao unazungumziwa katika ulimwengu wa kidini huwakilisha mabadiliko katika tabia ya maisha? (Hapana, hauwezi.) Kwa nini mabadiliko katika mwenendo wa mtu hayawezi kuwakilisha mabadiliko katika tabia yake ya maisha? Sababu muhimu ni kuwa bado anampinga Mungu. Unaweza kuyaona hayo kwa nje, Mafarisayo walikuwa wacha Mungu sana, waliomba, waliyaelezea maandiko na walizifuata kanuni za sheria vizuri sana. Ingeweza kusemwa kwamba kwa nje, hawakufedheheka. Watu hawakuweza kuyaona makosa. Hata hivyo, kwa nini bado waliweza kumpinga na kumshutumu Kristo? Je, hili linaonyesha nini? Hawakuwa na ukweli na hawakumjua Mungu. Kwa nje, walikuwa wazuri sana, lakini hawakuwa na ukweli, hii ndiyo sababu waliweza kumpimga Mungu. Kama walikuwa wazuri sana kwa nje, kwa nini hili halichukuliwi kama mabadiliko katika tabia ya maisha? Hii ni kwa sababu bado walikuwa wenye kiburi, wenye majivuno na hasa wenye unyoofu. Waliyaamini maarifa yao, nadharia na ufahamu wa maandiko. Waliamini kwamba walifahamu kila kitu na kwamba walikuwa bora kuliko watu wengine. Hii ndiyo sababu wakati ulimwengu wa kidini unasikia kwamba Kristo wa siku za mwisho ameuelezea ukweli wote, wanamshutumu Yeye ingawa wanajua kwamba ni ukweli.
kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha, Juzuu ya 138
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni