Swahili Christian Video "Kuzinduka" | Ni nini Maana ya Uzima?
Jina lake ni Chen Xi, na tangu akiwa mtoto elimu na ushawishi wa wazazi wake na shule yake zilimfanya yeye mara zote kutaka kwa tofauti na wengine na kutafuta kuwa juu ya wengine,kwa hivyo alikuwa na bidii katika masomo yake na kutia juhudi zote. Baada ya kumwamini Mungu Chen Xi alisoma maneno ya Mungu kwa wingi na akaja kuelewa kiasi fulani cha ukweli. Aliona kuwa njia pekee inayofaa katika maisha ni kumwamini na kumfuata Mungu na kuwa mtafutaji mwenye shauku, na alijitolea kwa dhati katika kutekeleza wajibu wake. Chen Xi alienda ughaibuni mwaka 2016 ili kutoroka harakati na mateso ya serikali ya Kikomunisti ya Kichina, na alihitaji kutumia Kiingereza wakati akifanya kazi yake ya kueneza injili na kutoa ushuhuda kwa kazi ya Mungu katika zile siku za mwisho. Alihisi kuheshimiwa, na kwamba alikuwa na talanta nadra. Kama vile alivyojazwa na kujiamini na alikuwa anafikiria kujitengenezea nafasi kanisani, aligundua kwamba ndugu na dada zake walishiriki ushirika kwa maneno ya Mungu kwa nuru na kwamba walikuwa na ufahamu zaidi wa Kiingereza kumliko. Yeye hakutaka kubaki nyuma, kwa hivyo ili kuwapita wengine na kutambuliwa na kupongezwa nao, alirudufu tena jitihada zake za kujifunza. Kipindi kidogo kilipita lakini bado hakuwafikia wengine. Chen Xi hakukubali ukweli huu na alijikuta akiishi kila siku kwa maumivu ya kujitahidi kwa ajili ya jina lake na faida yake binafsi. Yeye hakuwa na moyo wa kufuata ukweli au kuzingatia kuingia katika uzima, na alikuwa hasa hawezi kutekeleza wajibu wake vizuri. Alianguka kwa maono mabaya na kuvunjika moyo.... Ni wakati huo ndipo alikuja mbele za Mungu kwa sala na kusoma maneno Yake - hukumu na adhabu ya maneno Yake iliamsha nafsi yake na kumruhusu kuona wazi kiini cha sifa na hadhi pamoja na matokeo ya kufungwa na kuteswa na mambo haya. Alikuja kuelewa umuhimu wa kutekeleza wajibu wake, thamani ya kweli ya maisha, na maisha ya aina gani ndiyo ya furaha ya kweli. Kuanzia wakati huo alianza kuwa na malengo sahihi ya kufuata na kutokuwa chini ya fikira za uso au hadhi. Pia alianza kuzingatia kufuata ukweli na kutimiza wajibu wa kiumbe wa kulipa upendo wa Mungu …
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni