6.05.2018

Sura ya 62. Ili Kuwa Mwaminifu, Unapaswa Kujiweka Wazi kwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Sura ya 62. Ili Kuwa Mwaminifu, Unapaswa Kujiweka Wazi kwa

Mwenyezi Mungu alisema, Wengine Je, mna uzoefu wowote wa kuwa waaminifu? (Ni vigumu kuwa mwaminifu). Na mbona ni vigumu? (Ninapotafakari juu yangu kila siku, nagundua kuwa najua vyema kujifanya, na kwamba nimesema mengi ambayo si sahihi. Wakati mwingine, maneneo yangu yatakuwa na hisia na motisha, wakati mwingine, nitaunda ujanja fulani ili kutimiza malengo yangu, nikisema ukweli nusu ambao haulingani na mambo ya hakika; maneno mengine, pia, yatakuwa hayapasi kabisa, na ya kubuniwa.) Mambo haya ni upande mdanganyifu wa tabia potovu ya watu. Mbona watu hujihusisha na udanganyifu kama huu? Ili kutimiza malengo yao binafsi, na kutimiza shabaha wanazotamani. Na hivyo wanachukua na kutumia mbinu fulani, ambazo zinaonyesha kwamba wao si waadilifu, na kwamba si watu waaminifu. Wakati kama huo, kudhuru kwa watu kwa siri na ujanja unafichuliwa, au sivyo uovu na aibu yao. Na mambo haya, unahisi kwamba ni vigumu hasa kuwa mwaminifu; bila mambo haya, ungehisi kwamba kuwa mwaminifu ni rahisi. Kikwazo kikubwa zaidi kwa kuwa mwaminifu ni kudhuru kwa siri kwa watu, udanganyifu wao, uovu wao, na motisha zao za aibu. Je, mshawahi kujifunza kuwa waaminifu? Na hali yenu wakati mlikuwa mkijifunza ilikuwa ipi? (Kila jioni ningeandika upuzi, uongo, yasiyopasa, na ubunifu wote ambao nilikuwa nimesema wakati wa mchana. Kisha ningejichunguza na kujichambua, na ningegundua kwamba maneno haya yalikuwa na motisha, kwamba yalikuwa uongo uliosemwa kukiwa na vichocheo, na hayalingani na ukweli. Ingawa nilijua yalikuwa hayalingani na ukweli, wakati uliofuata singejizuia kudanganya tena, kubuni mambo, na kujifanya. Wakati mwingine, sikujua kwamba nilikuwa najifanya ama kudanganya wakati huo, nilijua tu baadaye. Wakati mwingine, nilijua wakati huo, lakini singeasi dhidi yangu mara moja. Wakati mwingine, sikuwa na hisia ya niliyokuwa nafanya wakati huo.) Ndiyo! Wakati huo hungehisi hilo—ulidhani kwamba ulikuwa hasa na sababu nzuri za kufanya hivyo, na kwamba ilifaa kufanya hivyo. Kukiwa na muktadha fulani ama katika mazingira fulani, ulihisi kwamba ilikuwa busara, ama kwamba kulikuwa na sababu nzuri kufanya hivyo, ama kwamba ulikuwa na sababu za kutosha kufanya hivyo, na hatimaye ukachukua hatua, na baadaye ukahisi ulikuwa na haki kabisa kufanya hivyo, na hukuwa na chochote cha kujutia. Jioni ilipofika na ukawaza juu ya ulichofanya, au sivyo siku moja ulipopata nuru ama ulishutumiwa, basi ulihisi kwamba sababu ya kusema maneno hayo wakati huo haikuwa sababu, na kwamba ungepaswa kutenda kwa njia nyingine. Unapaswa kutenda vipi wakati kama huo? Kwa mfano, ulimfanyia mtu kitu, ulimdanganya, ama ulisema maneno ambayo hayakuwa sahihi ama yalikuwa na motisha yako mwenyewe, na hivyo unapaswa kuenda na kumtafuta mtu huyo kuchambua kile ulichofanya, na kusema: “Maneno niliyoyasema wakati huo yalikuwa na motisha zangu binafsi. Iwapo unaweza kukubali kuomba radhi kwangu, tafadhali nisamehe.” Hivyo basi unajichambua na kujiweka wazi. Inahitaji ujasiri unapojichambua na kujiweka wazi. Angalia, wakati hakuna mwingine yeyote karibu, bila kujali iwapo unamwomba Mungu, ama kukubali makosa yako, kutubu au kuchambua tabia yako potovu kwa Mungu, unaweza kusema chochote unachotaka, kwa kuwa macho yako yakiwa yamefumbwa, huwezi kuona chochote, ni kama kuzungumzishaa hewa, na hivyo unaweza kujiweka wazi; chochote ulichofikiri, au chochote ulichosema wakati huo, na motisha zako, na udanganyifu wako unaweza kuyazungumzia. Lakini iwapo lazima ujiweke wazi kwa mtu mwingine, unaweza kupoteza ujasiri wako, na unaweza kupoteza uamuzi wako kufanya hivyo, kwa sababu huwezi kuondoa uso wako, huwezi kuondoa sura ya kinafiki, na hivyo ni vigumu sana kuweka vitu hivi katika vitendo. Ona jinsi, ukiambiwa uzungumze kwa ujumla, unaweza kusema kuwa wakati mwingine kuna motisha katika mambo unayoyafanya ama kusema, kwamba maneno yako na matendo yana ujanja, uchafu, uongo na udanganyifu na pia malengo yako mwenyewe. Lakini kitu kinapokufanyikia, iwapo lazima ujichambue, na kufichua jinsi kilichofanyika kwako kilitendeka kutoka mwanzo hadi mwisho, ni yapi katika maneno uliyoyasema yalikuwa madanganyifu, yalikuwa na motisha ya aina gani, kile ulichofikiri katika moyo wako, jinsi kilivyokuwa kiovu na cha kudhuru kwa siri, basi unaweza hata kuogopa, na hivyo hutakuwa na hiari ya kufichua kiwango hicho cha kila kitu, kuwa mahususi sana kwa kile unachosema. Kutakuwa hata na watu wanaoisitiri, na kusema: “Haya, ilikuwa tu mojawapo ya mambo hayo. Inatosha kusema kwamba mwanadamu ni mdanganyifu mkubwa, mwenye kudhuru kwa siri na asiyetegemewa.” Huku ni kutoweza kukabili kiini chako potovu, udanganyifu na kudhuru kwa siri vizuri; hali yako daima ni ile ya kuepuka, hali yako daima ni ya kuepuka, daima unajisamehe, na huna uwezo wa kuteseka ama kulipa gharama katika suala hili. Na hivyo kuna watu wengi ambao wamelia kwa miaka mingi kwamba “Mimi ni mdanganyifu sana, mwenye kudhuru kwa siri sana, mara nyingi mimi ni mnafiki katika matendo yangu, na mimi si wa kweli hata kidogo kwa wengine.” Wanaendelea na kuendelea, lakini baada ya kusema maneno haya kwa miaka mingi, leo wamebaki wadanganyifu kikamilifu na kabisa, kwa kuwa hujawahi wasikia wakionyesha majuto kwa sababu ya, ama kuchambua udanganyifu na kudhuru kwa siri kulikofichuliwa katika maneno ama vitendo vyao. Hakuna njia ya sisi kuwa na uhakika kwamba hawajakiri dhambi zao na kutubu mbele ya Mungu, lakini mbele ya watu wengine hawajawahi kuomba msamaha, kujichambua, ama kujijua, wakisema kitu kuhusu kile wamekuja kujua katika suala hili, baada ya wao kumaliza kudanganya, kulaghai, na kuwatawala wengine. Kwamba hawafanyi hivyo inadhibitisha kitu: Katika masuala haya, hawajawahi kuasi dhidi yao wenyewe; wanaongea tu misimu na mafundisho. Wanaweza kuongea misimu na mafundisho ili kufuata mwenendo wa karibuni ama mtindo wa muda, ama wanaweza kuwa wamelazimika kufanya hivyo na mazingira yao, ambayo hayatawahi kuwafanya wabadilike. Wakati Mungu anauliza kwamba watu waweke kila ukweli katika vitendo, wanatakiwa kulipa gharama, na kutenda, kufanya mazoezi na kupitia kwa kweli na neno kwa neno, kuuunganisha na maisha yao ya kweli. Mungu haulizi kwamba watu wazungumze misimu ama kukaa siku nzima wakirudia kwamba wao ni wadanganifu, na waongo, na watawala, na kwamba hakuna motisha katika kila kitu wanachofanya, wakati bado, kitu kinapowafanyikia, wakitumia mbinu na njia sawa kama awali; njia na mbinu zao hazijawahi kubadilika, vile wanavyotendea wengine haijawahi kubadilika, na njia ambayo wanatenda haijawahi kubadilika. Unasemaje, mtu kama huyu anaweza kubadilika? La, hawezi kubadilika kamwe! (Hivyo hii ni kusema kwamba, kando na kukubali makosa yetu mbele ya Mungu, lazima pia tujiweke wazi mbele ya ndugu zetu?) Bila shaka ni lazima ufanye hivyo. Usipojiweka wazi na kujichambua, unawezaje kudhibitisha kwamba unakiri kwamba wewe kweli ni mdanganyifu? Usipojiweka wazi, Nisipojiweka wazi, iwapo hakuna kati yetu atakayejiweka wazi, kama tuna mipango na fikira zetu ndani ya mioyo yetu, iwapo nafasi binafsi inadumishwa ndani ya mioyo yetu, basi tunaweza kusahau mazungumzo ya kweli kupitia—ingekuwaje yeyote kati yetu awe na uzoefu wa kweli kuwasiliana na mwengine? Hatungeweza. Katika “kushiriki na kuwasiliana kuhusu uzoefu,” kushiriki kunamaanisha kuzungumza kuhusu kila wazo katika moyo wako, hali yako, uzoefu wako na maarifa ya maneno ya Mungu, na pia tabia potovu ndani yako—na baada ya hayo, wengine wanatofautisha, na kukubali mazuri na kutambua kile kilicho hasi. Huku tu ndiko kushiriki, na huku tu ndiko kuwasiliana kwa kweli. Hakumaanishi tu kuwa na umaizi katika maneno ya Mungu ama sehemu ya wimbo wa kidini, na kuwasiliana upendavyo, na kutosema chochote kuhusu maisha yako halisi. Kila mtu huongea kuhusu maarifa ya mafundisho na ya nadharia, na hawasemi chochote kuhusu maarifa yaliyotoka kwa uzoefu halisi. Wote wanaepuka kuzungumza kuhusu vitu kama hivyo, kuhusu maisha yao binafsi, kuhusu maisha yao katika kanisa pamoja na ndugu zao, na kuhusu dunia yao ya ndani. Kwa njia hii, kunawezaje kuwa na kuwasiliana kwa kweli kati ya watu, kunawezaje kuwa na imani ya kweli? Hakuwezi kuwa na mambo haya! Unasemaje, iwapo mke hazungumzi kamwe kuhusu maneno ndani ya moyo wake kwa mume wake, wao ni wasiri? Je, wanaambiana siri? Hawaambiani siri. Tuseme kwamba siku nzima mume husema, “Ah, mke wangu, nakupenda!” na siku nzima mke husema, “Mume wangu, nakupenda, nitakupenda milele, sitawahi kukuacha.” Wanasema tu haya, lakini mke hajawahi yafichua kuweka wazi anayoyafikiri katika moyo wake, kile anachotaka kutoka kwa mume wake, ama shida alizo nazo. Hajawahi kuzungumza na mume wake kuhusu mambo kama hayo, hajawahi kumwambia siri—na iwapo hao wawili hawajawahi kuambiana siri, je wao ni wachumba wanaopendana? Iwapo hawana lolote isipokuwa maneno yenye kuvutia kwa mwingine wakiwa pamoja, kweli wao ni mke na mume? Bila shaka sio! Ili kaka na dada waweze kuambiana siri, kusaidiana, na kuruzukiana wakiwa pamoja, basi kila mtu lazima azungumze kuhusu uzoefu wake binafsi wa kweli. Usipozungumza kuhusu uzoefu wako binafsi wa ukweli, na unazungumza tu maneno yenye kuvutia, na maneno ambayo ni ya mafundisho na ya juu juu, basi wewe si mwaminifu, na huna uwezo wa kuwa mwaminifu. Angalia, mwanzoni, inawezekana kwamba mume na mke pengine hawaelewani vizuri sana, kwa sababu hawajawahi kuishi pamoja na hawakukua katika familia sawa. Baada ya kuishi pamoja kwa miaka kadhaa, watakuwa wamezoeana, na kugombana mara chache. Lakini iwapo nyote wawili ni wa ubinadamu wa kawaida, daima utawasiliana maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwake, na yeye kwako. Bila kujali ugumu ulio nao katika maisha, shida katika kazi yako, kile unachofikiri katika moyo wako, jinsi unavyopanga kutatua mambo, mawazo na mipango uliyo nayo kuhusu kazi yako ama watoto wako—utamwambia kila kitu. Katika hali hiyo, nyinyi wawili ni hasa wandani, na hasa wasiri? Iwapo kamwe hakuambii maneno yaliyo ndani ya moyo wake, na hafanyi chochote ila kuleta mshahara nyumbani, na iwapo kamwe humwambii maneno yaliyo ndani ya moyo wako, na kamwe humwambii siri, basi hakuna umbali kati ya nyinyi wawili katika mioyo yenu? Bila shaka kunao. Ako mbali na wewe, na wewe kwake, kwa sababu huyaelewi mawazo ama nia katika moyo wake. Hatimaye, huwezi kujua yeye ni mtu wa aina gani, wala hawezi kujua wewe ni mtu wa aina gani; huelewi mahitaji yake, wala haelewi matakwa yako. Iwapo watu hawana mazungumzo ya maneno ama ya kiroho, hakuna uwezekano wa urafiki wa karibu sana kati yao, na hawawezi kuruzukiana ama kusaidiana. Je, mna hisia kama hiyo? Iwapo rafiki yako anakuambia kila kitu, akisema yote anayofikiri ndani ya moyo wake, na mateso ama furaha aliyo nayo moyoni, basi huhisi hasa msiri wake? Kwamba ana hiari ya kukuambia mambo haya ni kwa sababu pia wewe umezungumza kuhusu maneno yaliyo katika moyo wako kwake—nyinyi hasa ni wandani, na ni kwa sababu ya haya kwamba unaweza kuelewana na yeye na kusaidiana. Bila hili miongoni mwa ndugu katika kanisa, hakungewahi kuwa na upatanifu miongoni mwa ndugu, ambao ni mojawapo ya mahitaji ya kuwa mwaminifu. Watu wengine husema: “Ah, ni vigumu kuwa mwaminifu, ni lazima niseme vyote ninavyofikiri katika moyo wangu kwa wengine? Je, haitoshi kuwasiliana kuhusu mambo mazuri—sitawaambia wengine kuhusu upande wangu mwovu ama mpotovu, siyo?” Iwapo huzungumzi mambo haya, na hujichambui, basi hutawahi kujijua, na hutawahi kujua wewe ni kitu cha aina gani, na hakutakuwa na uwezekano wa wengine kukuamini. Huu ni ukweli. Iwapo unawataka wengine wakuamini, kwanza lazima uwe mwaminifu. Kuwa mwaminifu, lazima kwanza uuweke wazi moyo wako, ili kila mtu aweze kuuona, na vyote unavyofikiri, na wanaweza kuona uso wako wa kweli; hupaswi kujifanya ama kujionyesha usivyo. Hapo tu ndipo watu watakuamini na kukuchukua kuwa mwaminifu. Hili ndilo tendo la msingi kabisa la kuwa mwaminifu, na ni sharti la mwanzo. Daima unajifanya, daima unasingizia utakatifu, uadilifu, ukubwa na ubora, na huwaruhusu watu kuona upotovu na kushindwa kwako. Unaonyesha taswira ya uongo kwa watu, ili waamini kwamba wewe ni mwadilifu, mkuu, anayejinyima, asiyependelea na asiye na ubinafsi. Usijifanye, usijionyeshe usivyo; badala yake, jiweke wazi, uweke wazi moyo wako ili wengine waone. Iwapo unaweza kuweka wazi moyo wako ili wengine waone, na kuweka wazi yote unayofikiri na kupanga kufanya ndani ya moyo wako—bila kujali iwapo ni nzuri ama mbaya—basi wewe huwi mwaminifu? Iwapo unaweza kujiweka wazi kwa wengine waone, Mungu pia atakuona na kusema: “Umejiweka wazi kwa wengine wakuone, na hivyo mbele Yangu bila shaka wewe ni mwaminifu pia.” Iwapo unajiweka wazi kwa Mungu wakati wengine hawaoni pekee, na daima unajifanya kuwa mkuu na mwadilifu ama mwenye haki na asiye na ubinafsi mbele yao, basi Mungu atafikiri nini? Na Mungu atasema nini? Mungu atasema: “Kwa kweli wewe ni mjanja na mnafiki, wewe ni mwenye kujishughulisha na mambo madogo madogo , na wewe si mwaminifu.” Mungu atakuhukumu hivi. Iwapo unataka kuwa mwaminifu, basi bila kujali kile unachofanya mbele ya Mungu ama watu, unaweza kuufichua moyo wako kwa wengine. Je, hili ni rahisi kutimiza? Linahitaji muda, ili kuwe na mapigano ndani ya mioyo yetu, na ili sisi tuendelee kutenda . Hatua kwa hatua, mioyo yetu itafunguliwa, na tutaweza kujiweka wazi.
Watu wanaishi katika tabia potovu ya kishetani. Haijalishi wanachofanya, wanajifanya, na kujionyesha wasivyo, na kuunda ujanja; ni wadanganyifu katika kila kitu, wakiamini hakuna chochote kisichostahili udanganyifu na utawala wao. Kuna watu ambao wanaweza kuwa wanafiki hata wakati wananunua kitu, ambayo kwa kweli ni hali ya kawaida. Tuseme kwamba mtu amenunua viatu. Anafikiria: “Viatu hivi ni vya mtindo sana wakati huu. Ndugu zangu wakiniona nikivivaa bila shaka watakuwa na kitu cha kusema kunihusu. Watasema, “Tazama, una pesa lakini huitumii kwa njia sahihi, ungewezaje kuitumia kununua hivyo? Kitu cha mtindo kama hicho lazima kilikuwa cha gharama kubwa!” Bila shaka watasema hayo kunihusu. Kwa hivyo sitavaa viatu hivi mbele yao, nitavivaa wakati hatuna mkutano na wakati tuna mkutano sitavivaa. Nitavivaa wakati vimetoka katika mtindo, wakati hawatafikiri vina thamani yoyote watakapoviona.” Bila kujali matendo yako, kwa ujumla, kwa kupiga hesabu na kufikiri kwa njia hii, wewe huwi mdanganyifu? Wewe ni mdanganyifu, siyo? Tayari unaishi katika udanganyifu, tayari umejiandaa kutenda kwa njia hii, na utakapotenda, tayari hakuna usaliti katika moyo wako? Kunao, siyo? Wewe unakuwa mdanganyifu, siyo? Na mbona unakuwa mdanganyifu? Kwa sababu una motisha zako mwenyewe na malengo yako mwenyewe. Na haya malengo yako ni halali? Kiini cha malengo haya ni kipi? Je hali si kwamba hutaki kuwa mwaminifu, na wewe unakuwa mdanganyifu? Unatenda kwa njia moja mbele ya watu, na kwa njia tofauti nyuma yao; matendo yako si sawa, kuna tofauti, unapanga njama kwa siri, uko mwangalifu sana katika kupanga na kupiga hesabu kwako, ambako tayari kumetiwa dowa na motisha zako. Kwa kufanya mazoezi na kutenda kwa njia hii, wewe unakuwa mdanganyifu. Unasemaje, je, watu ambao ni wadanganyifu ni wapumbavu? Ona jinsi njama ndongo ndogo za watu wadanganyifu haziwezi kufichuliwa. Mbona, punde tu watu wengine wanaulizwa kujichunguza, wanakuwa na wasiwasi? Njama zao ndogo ndogo zinaonekana kuwa pumbavu, jinga na za aibu na ni wa fedheha; hizi ni shughuli chafu za watu waovu. Wale ambao ni wadanganyifu hawawezi kamwe kuweka wazi matendo yao kwa wengine. Mbona hivyo? Punde wanapojiweka wazi, ghafla wanagundua: “Eh, nilikuwaje mpumbavu sana hivyo nilipofanya hiyo? Nilikuwaje wa kuchukiza sana hivyo?” Hata ni wa kujichukiza wenyewe, lakini walifanyapo hawawezi kujizuia; daima wanataka kutenda hivyo, kwani kwa asili wao ni wadanganyifu, na katika kila kitu wanafanya, asili yao janja inafichuliwa kiasili. Hata vitu vidogo vitafichua asili yao ya udanganyifu, hakuna kitu ambacho wanaweza kujizuia, na huu ndio udhaifu wao. Wakati mmoja kulikuwa na kaka ambaye familia ya mama mkwe wake hasa ilikuwa danganyifu, kama vile familia ya shemeji yake. Familia yake yote ilikuwa imejazwa na watu wadanganifu—hakuna hata mmoja wao alikuwa mwaminifu na wa kutegemewa. Maneno ya mtoto katika familia hiyo hayakuaminika. Wakati mtoto huyo alikuwa na umri wa miaka sita ama saba, kulikuwa na wakati mmoja ambapo, baada ya familia yake kuwa na mlo maalum, mtu mzima alimuuliza: “Sasa, familia zenu zilikula nini leo? “ Alipepesa, na hakutoa sauti. Mtu mzima alimuuliza tena: “Ulikula nini leo? Bila ridhaa ya kuongea, alisema: “Nimesahau.” Alikuwa amekula chini ya nusu saa iliyopita, lakini alisema kuwa alikuwa amesahau. Mtoto huyu wa miaka sita ama saba alikuwa tayari anaweza kubuni mambo, kudanganya—na alikuwa amefunzwa kufanya hivyo na watu wazima? Je, alishawishiwa na mazingira yake? Si kati ya haya. Hii kiasili ilikuwa asili yake; alikuwa mdanganyifu kiasili. Wacha tuchambue asili yake. Bila kujali kile unachokula—hata kama unakula mlima wa dhahabu ama fedha—hakuna haja ya kudanganya. Hata kama umekula kitu kitamu, hakuna anayeweza kukunyang’anya, wala hatakuonea wivu ama kijicho. Hakuna haja ya kusema uongo huu. Mnasemaje, kuna haja ya kudanganya? Hakuna haja! Kwa sababu hakukuwa na haja, je, hili linaonyesha kwamba kile alichofanya hasa kilikuwa pumbavu? Linaonyesha. Wacha tuchambue, mbona alikuwa mpumbavu: Kwanza, hakuna haja ya wewe kudanganya. Bila kujali kile umekula, watu wengine hawatakuonea kijicho, na hawatajaribu kukunyang’anya. Pili, kumbukumbu yako kweli ni mbaya hivyo? Kusahau kile ulikuwa umekula chini ya nusu saa baada ya kukila? Watoto wana kumbukumbu nzuri, hakuna uwezekano angesahau, na hivyo watu wanaweza kujua wazi kwamba anadanganya, kwamba anakuwa mdanganyifu. Aliposema, “Nimesahau,” alikwa anachelewa ili ungewacha kuuliza. Maana yake ilikuwa: “Nilisema nimesahau,’ lakini bado unauliza; je, kuuliza tena si kuharibu wakati? Sitakuambia, nitasema tu nimesahau.” Hakusema moja kwa moja, “sikuambii,” lakini “nimesahau.’” Je, huyu si mtu ambaye ni mdanganyifu? Mtoto huyu tayari amekomaa, ana miaka zaidi ya ishirini, na ukweli unadhibitisha kwamba bila shaka yeye ni mdanganyifu. Udanganyifu wake ulikuwa unaonekana kuanzia alipokuwa mdogo. Watu ambao ni wadanganyifu hawawezi kujidhibiti katika matendo yao, na udanganyifu wao unaweza kuonekana wakati wowote ama mahali popote. Hiki si kitu wanacholazimika kujifunza, ama kinachohitaji kufunzwa ama kuongozwa na wengine; katika kitu rahisi sana, kitu ambacho hakihitaji udanganyifu ama kuepukwa, yeye ni wa kukwepa, anadanganya, anawapotosha watu na anabuni uwongo na yasiyo kweli. Mshawahi kuwa katika hali kama hiyo? Nyote mshawahi, sivyo? Na kwa hivyo, hili linadhibitisha nini? Kwamba hakuna kati yenu aliye mwaminifu! Ni nini kiwango cha Mungu kwa watu ambao Anahitaji? Hili limetajwa katika maneno ya Mungu. Je, mna vitabu vyenu vya nyimbo za kidini? Kunamaanisha nini kuwa “mwaminifu”? “Kuwa mwaminifu’ kunamaanisha kumpa Mungu moyo wako, kuwa mkweli Kwake katika vitu vyote, kujiweka wazi Kwake katika vitu vyote, kutoficha ukweli, kutofanya lolote kudanganya wale walio juu ama chini yako, kutofanya vitu ili kujipendekeza kwa Mungu pekee, na kutofanya ama kusema chochote cha hila. Iwapo maneno yako yana udhuru mwingi ama kukiri kusiko na manufaa, basi Mungu husema wewe ni mtu ambaye anachukia kuweka ukweli katika vitendo. Iwapo una siri nyingi ambazo hutaki kuzisema, na iwapo huna ridhaa ya kuwaambia wengine kuhusu siri zako—ugumu wako—na kutafuta njia ya mwanga, basi Mungu anasema wewe ni mtu ambaye ni mgumu kuokoa, mtu ambaye hawezi kuibuka kutoka gizani kwa urahisi.” Kuna baadhi ya maneno muhimu sana hapa, je, unaona ni yapi? Mungu alisema, “Iwapo una siri nyingi ambazo hutaki kuzisema” “Nyingi” inarejelea jinsi umefanya vitu vingi ambavyo hudhubutu kuzungumza kuvihusu, na una pande nyingi sana ovu; hakuna matendo yako ya siku kwa siku yanayolingana na maneno ya Mungu, huasi dhidi ya mwili, unafanya kile unachotaka kufanya, na baada ya kumwamini Mungu kwa miaka hii yote huna uhalisi hata kidogo, na hujaingia katika uhalisi. “Iwapo huko tayari kuwaambia wengine kuhusu siri zako—ugumu wako—na kutafuta njia ya mwanga”ni njia ya kutenda; kwa hili kuna njia kutenda. “Basi Nasema wewe ni mtu ambaye ni mgumu kuokoa, mtu ambaye hawezi kuibuka kutoka kwa giza kwa urahisi” ni njia ambayo Mungu humpa mwanadamu, na iwapo hutendi kwa njia hii, na unaongea tu misimu na mafundisho, basi wewe ni mtu ambaye ni mgumu sana kuokoa. Ndiyo, Hili linahusiana na wokovu. Kwa kila mtu, wokovu ni muhimu sana. Lifikirie, je Mungu ametaja hili kwingine? Mara chache tu Yeye hutaja ugumu wa kuokolewa, lakini Alilizungumzia wakati Aliongea kuhusu kuwa mwaminifu. Usipotenda kwa njia hii, basi wewe ni mtu ambaye ni mgumu sana kuokoa; kuwa mgumu kuokoa kunamaanisha si rahisi kwa wewe kuokolewa, huna uwezo wa kuchukua njia sahihi ya wokovu, na hivyo haiwezekani kukuokoa. Mungu husema hili ili kutoa nafasi. Yaani, wewe si rahisi kuokoa, lakini kwa upande mwingine, ukiweka maneno ya Mungu katika vitendo, kuna matumaini kwako na unaweza kuokolewa. Usipoweka maneno ya Mungu katika vitendo, na iwapo kamwe huchambui siri ama ugumu wako mwenyewe, ama kamwe humwambii yeyote haya mambo binafsi ama kuwaambia watu kuyahusu, kuwasiliana na watu kuyahusu, ama kuyachambua na watu ili kujiweka wazi, basi hakuna uwezekano wa wewe kuokolewa. Na mbona hivyo? Iwapo hujiweki wazi ama kujichambua kwa njia hii, tabia yako potovu haiwezi kubadilika kamwe. Hii ndiyo maana ya maneno haya. Na iwapo hubadiliki, unaweza kusahau kuhusu kuokolewa. Haya ni mapenzi ya Mungu, na hii ndiyo nia ya Mungu katika kusema maneno haya. Kwa nini daima Mungu amesisitiza kuwa mwaminifu? Kwa sababu ni muhimu sana; kunahusiana moja kwa moja na iwapo unaweza kuokolewa au la. Watu wengine husema: Mimi ni mwenye kiburi sana, mwenye haki binafsi sana, mimi ni mwenye hasira fupi, mara nyingi naweka wazi uasili wangu, mara nyingi mimi ni wa juu juu na mwenye kujisifu, daima nataka kibali cha wengine….lakini haya yote ni mambo madogo tu. Na kwa nini nasema kwamba ni mambo madogo tu? Kwa sababu hayana umuhimu. Usizidi kuyazungumzia daima, ukisema: Natamani taswira sana, daima mimi ni wa mzaha, napenda kufanya masihara na mzaha …. Je, hizi ni dosari zangu? Ni mambo madogo tu. Bila kujali tabia ama nafsi yako, ili mradi unaweza kuwa mwaminifu kulingana na njia ya Mungu unaweza kuokolewa. Kwa hivyo mnasemaje, ni muhimu kuwa mwaminifu? Hiki ni kitu muhimu zaidi, na hivyo katika Maonyo Matatu Mungu huongea kuhusu kuwa mwaminifu. Ona vile, licha ya ukweli kwamba Mungu alizungumza kuhusu kuishi katika roho, kuwa na uwezo wa maisha ya kawaida ya kiroho, ama kuwa na maisha sahihi ya kanisa, ama ubinadamu wa kawaida katika maandiko mengine, hakuna mahali Alikuambia wazi uwe mtu wa aina gani, ama jinsi ya kutenda—lakini kwa kuongea kuhusu kuwa mwaminifu, Anakuonyesha njia, na kukuambia jinsi ya kuiweka katika vitendo; hii ni dhahiri kabisa. Mungu alisema, “Basi Nasema wewe ni mtu ambaye ni mgumu kuokoa.” Mshawahi kuzingatia maneno haya? Iwapo hamjawahi, ni kwa sababu bado hamjui jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu, na bado hamjui maneno gani ya Mungu hasa ni muhimu; bado hayajakuamsha, ama kuvuta nadhari yako. Ona vile kuwa mwaminifu kunahusiana na wokovu. Unasemaje, kuwa mwaminifu ni muhimu? Mungu anataka watu ambao ni waaminifu. Iwapo wewe si mwaminifu—iwapo wewe ni msaliti, mhalifu, na mwenye kudhuru kwa siri—basi wewe si mtu mwaminifu, na iwapo wewe si mtu mwaminifu, hakuna uwezekano kwamba Mungu atakuokoa; haiwezekani wewe kuokolewa. Hujabadilika kuwa mtu ambaye ni mwaminifu, na unasema, “Tayari mimi ni mwenye kumcha Mungu sana, lakini mimi si mwaminifu,” ama “Mimi sina haki binafsi, lakini pia mimi si mwaminifu,” ama “Ninaweza kabisa kulipa gharama, lakini mimi si mwaminifu,” ama “Mimi bado ni msaliti, sijabadilika hata kidogo, lakini ninaweza kueneza injili na kuleta watu wengi kwa Mungu.” Unasemaje, je watu wanaotenda hivi wanaweza kuokolewa? Hawawezi. Na hivyo haya maneno ya Mungu yanakumbusha kila mmoja wetu kwamba ili kuokolewa, lazima kwanza kabisa tuwe waaminifu kulingana na maneno na mahitaji ya Mungu, lazima tujiweke wazi, tuzifunue tabia zetu potovu, na kuweza kuweka wazi siri zetu ili kutafuta njia ya mwanga. Kunamaanisha nini “kutafuta njia ya mwanga”? Kunamaanisha kutafuta ukweli ili kutatua tabia yako potovu, ambayo ni kusema, unapojiweka wazi, pia unajichambua , na baada ya hapo unapaswa kutafuta: “Mbona ni lazima nifanye hili? Ninapata nini nifanyapo hili? Kwa kufanya hili, je, nafanya dhambi dhidi ya Mungu? Kwa kufanya hili, je, namdanganya Mungu? Iwapo linamdanganya Mungu, basi sipaswi kufanya hili; napaswa kutenda kwa namna nyingine—na namna hii inapaswa kuwa ipi? Napaswa kuangalia kile Mungu huhitaji, kile Mungu husema, kile ukweli husema,” Hii ni kutafuta njia ya mwanga.
Kwamba Mungu huuliza watu wawe waaminifu inadhibitisha kwamba kweli Anachukia wale ambao ni wadanganyifu. Mungu hapendi watu wadanganyifu, ambayo inamaanisha kwamba Anachukia matendo, tabia na hata motisha zao; yaani, Mungu hapendi vile wanavyofanya vitu, na hivyo, ili kumfurahisha Mungu, lazima kwanza tubadili matendo yetu na njia ya kuwepo. Awali, tulitegemea uongo, kujifanya, na mambo yasiyo ya kweli kuishi miongoni mwa watu. Huu ulikuwa mtaji wetu, na msingi wenye kuhusu maisha, maisha, na kanuni ambayo tulitumia kuishi. Na yote yalichukiwa na Mungu. Haijalishi uko katika kundi lipi, inaweza kuwa vigumu kwako kusimama imara ila kama unajua jinsi ya kuwa mtawala ama mdanganyifu. Nje katika dunia pana, kadri ulivyo mdanganyifu zaidi, ndivyo unaweza zaidi kutumia udanganyifu na kudhuru kwa siri kujilinda na kujifanya, na ndivyo unavyosimama imara zaidi; katika nyumba ya Mungu, ni kinyume kabisa: Kadri ulivyo mdanganyifu zaidi, ndivyo unavyotumia zaidi utawala wa kisasa kujifanya na kujionyesha usivyo, basi ndivyo una uwezo chini zaidi wa kusimama imara, na ndivyo zaidi Mungu anaweza kukataa watu kama hao. Mungu anachukia watu kama hao. Na hivyo, leo uamuzi umekwishafanywa: Iwapo sisi si waaminifu, na iwapo, katika maisha yetu, matendo yetu hayaelekezwi katika kuwa waaminifu na hatufichui nyuso zetu binafsi za kweli, basi hatutakuwa na nafasi yoyote ya kupata kazi ya Mungu ama kupata sifa ya Mungu. Haijalishi kile unachotiwa motisha kufanya. Chukua, kwa mfano, wakati unatekeleza wajibu—je wajibu huu unahitaji kwamba tuwe na mwelekeo mwaminifu? Unahitaji. Iwapo, wakati tunatekeleza wajibu wetu, kuna mambo mengine ambayo hatujafanya vizuri, basi lazima tjiweke wazi na kujichambua, na kujaribu kabisa kuyafanya vizuri wakati ujao; tunapaswa kujitahidi kufanya vyema zaidi wakati ujao, na hatufai kuzembea, ama kucheza cheza. Usipojaribu na kuridhisha Mungu na moyo ambao ni mwaminifu, na daima kutafuta kuuridhisha mwili wako mwenyewe, ama heshima yako, basi utaweza kufanya kazi nzuri wakati unafanya kazi kwa njia hii? Unaweza kutekeleza wajibu wako vyema? Bila shaka la. Wale ambao ni wadanganyifu ni wazembe, na wanacheza cheza, wakati wanatekeleza wajibu wao, hawaufanyi vizuri, na watu kama hao si rahisi kuokoa. Unasemaje, wakati watu wadanganyifu wanaweka ukweli katika vitendo, wanajishughulisha na udanganyifu? Kuweka ukweli katika vitendo kunahitaji wao kulipa gharama, kuacha maslahi yao wenyewe, kujiweka wazi kwa wengine. Lakini wanaficha kitu; wanapoongea, wanasema nusu yake, na wanashikilia nyingine. Daima lazima ukisie kile wanachoamini, daima lazima uunganishe mambo kujua maana yake. Wanajipatia baadhi ya nafasi, wanajipa nafasi ya kufanya mabadiliko. Kwa hivyo, punde tu watu wanapoona kwamba wao ni wadanganyifu, hawataki kuhusiana na wao tena, hawataki kuathiriana na wao, na daima wanajihadhari wakati wanashughulika na wao. Hakuna mbadala—watu hawa ni wadanganyifu, kwa hivyo ni lazima daima kujilinda dhidi yao, na watu hawaamini chochote wanachosema: “Je, kile alichosema ni ukweli ama uwongo? Kiwango kipi cha hicho ni sahihi?” Na hivyo, katika mioyo yao, watu mara nyingi wanapoteza imani nao, hawawaheshimu, ama kuwadhamini kabisa. Hivi ndivyo hali yako iko katika mioyo ya watu, hivyo ndivyo kiwango chako. Na hivyo utaangaliwaje na Mungu wakati uko mbele Yake? Akilinganishwa na mwanadamu, Mungu huona watu sahihi zaidi, kwa ukali zaidi, na kwa uhakika zaidi. Na hivyo, bila kujali muda ambao umemwamini Mungu, wajibu unaotekeleza, kazi unayofanya, familia unayotoka, ama jinsi ulivyo mwenye sifa zinazostahili, ili mradi unajaribu kuwa mwaminifu, basi una uhakika wa kupata kitu. Ukisema, “Sitajaribu kuwa mwaminifu, nitafanya tu wajibu wangu vizuri,” basi kamwe hutafanya wajibu wako vizuri. Wewe husema: “Sitatafuta kuwa mwaminifu. Kwanza nitaweka hiyo kwa upande mmoja, sidhani ni jambo muhimu. Kwanza nitamhudumia Mungu; iwapo ninaweza kuhudumia mapenzi Yake, basi nitakuwa nimemridhisha Mungu, na hiyo tu ndiyo inahitajika.” “Haya basi, jaribu, ona iwapo unaweza kuhudumia mapenzi ya Mungu. Watu wengine husema: “Sitatafuta kuwa mwaminifu. Kwa vyovyote, wakati utakapofika nitaenda kwa mkutano, wakati kuna mkutano nitashiriki, kila siku nitaomba na kula na kunywa maneno ya Mungu wakati unaofaa, sitafanya mambo yoyote ambayo wasioamini hufanya, na sitafanya uhalifu wowote, ama kufanya chochote ambacho ni dhambi dhidi kwa Mungu. Nitalenga tu kumridhisha Mungu.” Nitaona jinsi unavyomridhisha Mungu—iwapo wewe si mwaminifu, unawezaje kumridhisha Mungu? Yote haya yanamaanisha kwamba, ukitoka kwa kuwa mwaminifu, basi kwa mambo mengi hutaweza kuridhisha mapenzi ya Mungu. Kwa kitu kipi utaweza kumridhisha Mungu bila mwelekeo mwaminfu? Unawezaje kumridhisha Mungu ukitekeleza wajibu wako bila mwelekeo mwaminifu? Unaweza kuufanya vyema? Daima unafikiri kuhusu mwili wako na matarajio yako mwenyewe, daima unataka kupunguza mateso ya mwili, kufanya juhudi ndogo zaidi, kutoa kidogo zaidi, kulipa gharama kidogo zaidi, na daima unajipa nafasi ya kuluteka—na huu ndio mwelekeo wako mdanganyifu. Unapotumia rasilmali kwa ajili ya Mungu unafikiria mara mbili pia, ukisema: “Ah! Nijitoe kwa Mungu? Bado lazima nipate riziki nzuri; nitafanya nini iwapo kazi ya Mungu haiishi? Kwa hivyo sitajitolea kabisa kwa hiyo. Hatujui wakati maneno ya Mungu yatatimizwa, kwa hivyo napaswa kuwa mwangalifu, lazima nifikirie mara mbili. Baada ya mimi kupanga maisha yangu ya familia, na baada ya mimi kupanga matarajio yangu ya siku za mbeleni na nimeyatatua, nitajitoa kwa Mungu.” Ukimya kama huo pia ni udanganyifu, na kutenda ndani ya udanganyifu, na si mwelekeo mwaminifu. Wakati wanazungumza na ndugu zao, watu wengine wanahofia sana wao kugundua ugumu ndani ya mioyo yao. Wanaogopa kwamba ndugu watakuwa na kitu cha kusema kuwahusu ama kuwadharau. Wanapoongea, watu daima wanaweza kuhisi uchu wao, kwamba kwa kweli wanamtaka Mungu, na kweli wako makini kuweka ukweli katika vitendo lakini kwa kweli, katika mioyo yao wako dhaifu sana, na baridi kabisa. Wanajifanya kuwa wenye nguvu, na hakuna anayeweza kugundua. Huu pia ni udanganyifu. Kwa ujumla, bila kujali kile unachofanya—iwe katika maisha, kumtumikia Mungu, ama kutekeleza wajibu wako—ukionyesha uso usio wa kweli kwa watu na kuutumia kuwadanganya, kuwafanya kukuheshimu ama kutokudharau, basi unakuwa mdanganyifu! Katika moyo wake, mtu kweli anampenda mume wake wakati, kwa kweli, mume wake ni shetani, asiyeamini. Akihofia kuwa ndugu zake watakuwa na kitu cha kusema kumhusu, anafika hapo kwanza na kusema, “Mume wangu ni shetani.” Katika moyo wake, kwa kweli anasema, “Heh, mume wangu ni mtu mzuri”—lakini mdomo wake unasema, “Mume wangu ni shetani.” Kwa kweli anasema hili tu kwa manufaa ya ndugu zake, ili wafikirie: “Ona vile anamtendea mume wake, alisema kwamba yeye alikuwa shetani.” Kwa kweli, maana yake ni: “Msiseme kwanza; si lazima mliseme, nitazungumza kwanza, nitalisema ili msiseme. Wakati mnalisema, linaniumiza, kwa hivyo nitalisema mwenyewe, moja kwa moja—na hivyo hakuna kati yenu atalisema, na msipolisema lakini mimi niliseme, basi itaonyesha kwamba nina uwezo wa kuweka kando hisia zangu, kwamba sina hisia. Nimesema mume wangu ni shetani, kwa hivyo hakuna kati yenu anaweza kusema lolote!” Je, huu si udanganyifu? Huku si kujifanya? Ni kujifanya, ni kutumia kujifanya kuwadanganya watu. Unatumia hila na kutawala watu katika kila kitu unachofanya, ukionyesha uso wako mwongo kwa watu na kutowaruhusu kuuona uso wako wa kweli. Huku ni kudhuru kwa siri, na ni udanganyifu wa mwanadamu. Jaribuni kujichambua dhidi ya maneno haya. Kujifanya huku kuko kwa kila mtu, kwa kiasi kikubwa zaidi au kidogo zaidi, kwa kiwango cha kina zaidi ama cha juu zaidi, na nyote mtaweza kufikiria tukio au tendo ambalo mmejifanya kwa wengine ama kuwa wadanganyifu kwao. Iwapo wengine wenu husema: “Nisingelihisi hili aje? Mimi ni mkweli sana. Daima nasumbuliwa na kudanganywa katika dunia ya nje. Sijawahi kuwa mdanganyifu, sijawahi kuficha kitu,” hili halidhibitishi kwamba wewe ni mwaminifu; unaweza kuwa mjinga pakubwa, ama aliyefunzwa vibaya, ama unaweza kuwa huelewi vizuri teknolojia ya sasa, ustaarabu, ama sayansi. Unaweza kuwa huna hadhi ya juu katika dunia hii, unaweza kuwa wa viwango vya chini zaidi vya jamii—lakini hilo halimaanishi kwamba wewe ni mwaminifu. Inaweza kuwa kwamba unalaghaiwa na wale karibu nawe, kwamba wewe ni mnyonge, kwamba wewe ni mpumbavu katika matendo yako katika dunia ya nje, kwamba huwa uwezo mkubwa, na ni wa hadhi ya chini ya jamii—lakini hili pia halimaanishi kwamba wewe ni mwaminifu. Watu ambao ni waaminifu wanamiliki ukweli, wao si watu wa kuhuzunisha, wanyonge, wajinga, ama wenye mioyo mikunjufu. Je, mnaweza kutofautisha hili? Mara nyingi mimi husikia watu wakisema: “Ah, mimi kamwe sidanganyi, na daima nadanganywa na wengine, watu katika dunia ya nje daima wananisumbua. Mbona inasemwa kwamba Mungu unawainua maskini kutoka kwa lundo la samadi? Mimi ni maskini, hii ni neema ya Mungu. Mungu anatuonea huruma—Yeye hutuonea huruma sisi watu wa adabu ambao hatuwezani katika jamii, kwa kweli Anatuonea huruma.” Kuna uhalisi katika maneno haya, lakini kuyajua hakumaanishi kwamba wewe ni mwaminifu. Wewe ni mkweli, wewe ni mjinga, wewe ni mpumbavu, wewe ni zuzu, na huna kitu sawa na watu waaminifu waliozungumziwa na Mungu. Kutajwa kwokwote kwa maneno haya kunanichukiza, na Nasema: “Hizi hali zako ni gani? Wewe ni mjinga kiasili, wewe ni wa ubora wa tabia duni, wewe ni mwoga halisi, na kwa kuzaliwa katika familia maskini kama hii hii tu ndiyo njia unaweza kuwa. Katika jamii, hili linakufanya uwe wa hadhi ya tabaka la chini zaidi—lakini kuwa wa tabaka la chini zaidi hakumaanishi kwamba wewe ni mwaminifu; hii haiko katika “kuwa mwaminifu” iliyozungumziwa na Mungu.” Na hivyo, usiliweke taji hili juu ya kichwa chako, ukifikiri kwamba wewe ni mwaminifu kwa sababu unateseka katika jamii, unabaguliwa na kusumbuliwa na kudanganywa na kila mtu unayekutana naye. Hii si sahihi hata kidogo. Katika mioyo yao, je watu hawana uelewa wenye kosa, wa uwongo wa “kuwa mwaminifu”? Je, mawasiliano yetu yamewapa hisia ya hili? Kuwa mwaminifu si wanavyofikiria watu—watu ni waaminifu tu kwa sababu wao ni wazi na wanashughulika kwa udhahiri—sivyo hivyo. Watu wengine kiasili wanaweza kuwa wazi na kweli katika njia wanayozungumza, lakini kuwa kweli hakumaanishi wako bila udanganyifu. Udanganyifu ni motisha ya watu, na tabia yao. Kuishi katika dunia hii, kuishi chini cha ushawishi wa Shetani, haiwezekani watu kuwa waaminifu, lakini tunaweza, baada ya kuwa waaminifu, kuishi katika jamii hii na dunia hii? Je, tunaweza kutenganishwa na wao? La—tutaishi kama awali, kwa sababu hatutegemei usaliti kula chakula, ama kupumua hewa. Badala yake, tunategemea pumzi na maisha yaliyopewa na Mungu kuishi; ni tu kwamba, leo, kanuni za kuwepo kwetu, mwelekeo na malengo ya kuwepo kwetu, na msingi wa maisha yetu yote lazima yabadilike. Ni tu kwamba tunabadili mbinu zaetu na njia tunaishi ili kumridhisha Mungu na kutafuta wokovu, na hili halihusiani kabisa na chakula, nguo,na nyumba ya mwili. Haya ni mahitaji yetu ya kiroho. Sivyo?
Mnahisi kwamba kuwa waaminifu ni vigumu? Mmewahi jaribu kuwa waaminifu? Mmeona ni vipengele vingapi vya matendo viko katika “kuwa waaminifu” kulikozungumziwa na Mungu? Matendo yako yanatokana na kanuni gani? Kutenda kwa mujibu wa vipengele hivyo nne si rahisi, sivyo? Tunaona nini kutoka kwa maneno ya Mungu? Mungu hutaka kutuokoa, na kutubadilisha. Si kesi kwamba Yeye tu hufanya kazi ya utangilizi au unabii, na ni hayo tu, na Habadilishi tabia yetu ya nje. Badala yake, Anabadilisha kila mmoja wetu kuanzia vina vya mioyo yetu, na kuanzia kwa tabia yetu na dutu, Anabadilisha kila mmoja wetu kwanzia katika chanzo. Kwa kuzungumza bila kuficha, Atafanya kwa umakini. Na kwa kuwa Mungu hufanya kazi hivyo, tunapaswa kujitendeaje? Tunapaswa kuchukua jukumu la tabia zetu na kwa ajili ya harakati zetu, tunapaswa kuchukua jukumu kwa kila moja ya matendo yetu, na tunapaswa kuchukua tunayofanya kwa umakini, kuwa makini na si kuzembea, katika mambo yote na kuwa na uwezo wa kuchangua kila kitu. Kila wakati unapofanya jambo, vitu ambavyo ulidhani ulifanya vizuri lazima vichanguliwe—na, zaidi ya hayo, vitu ambavyo unafikiri ulifanya vibaya lazima vichanguliwe. Hii inahitaji kwamba ndugu watumie muda zaidi kuwasiliana, kutafuta, na kusaidiana. Tukiwasiliana zaidi, Mungu atatupa nuru katika mambo yote. Kama hakuna mmoja wetu atakayeongea, na tunajifanya tusivyo na kujisetiri, kutaka kuacha picha nzuri katika akili ya wengine, kutaka wengine kutuheshimu na si kutudharau, basi hakuna mmoja wetu atakayekua, hatutakuwa na njia za kua, haitakuwa rahisi kwetu kukua. Usipokua, na daima unajifanya usivyo na kujisetiri, basi daima utaishi katika giza na hutakuwa na uwezo wa kubadilika. Ukitaka kubadilika, basi lazima ulipe gharama, na uweke wazi yote unayofanya. Mtu anaposema, “Ah, mbona usiongee kuhusu uzoefu wako wa hivi haribuni?” hakuna anayeongea kuhusu masuala ya maana, hakuna anayejichambua, hakuna anayejiweka wazi. Akiulizwa kuongea kuhusu maneno na mafunzo hakuna mtu ana tatizo, lakini akiulizwa kujijua mwenyewe, hakuna anayesema kitu. Watu ambao wana maarifa madogo kujihusu hawadhubutu kuyaweka wazi, ama—hawana ujasiri wa kufanya hivyo. Na hivyo nini hufanyika mwishoni? Wakati kila mtu ako pamoja, wanajisifusifu wenyewe na kubembelezana: “Umekuwa ukifanya vyema karibuni, kumekuwa na mabadiliko ndani yako,” “Umekuwa mwaminifu sana karibuni,” “Umekuwa na shauku sana,” “Umetaumia hata zaidi kuniliko,” “Umejitolea hata zaidi kuniliko.” Hiyo ndiyo hali inayoundwa; kujisifusifu wenyewe, kubembelezana, na, kwa vina vya mioyo yao, hakuna mtu aliye tayari kuonyesha uso wake wa kweli kuchanguliwa na kila mtu na kujulikana na wao. Kama hivi, kunaweza kuwa na maisha ya kweli ya kanisa? Hakuwezi. Baadhi ya watu husema: “Nimeishi maisha ya kanisa kwa miaka kadhaa, na kila siku nahisi nimeridhika, kila siku naona raha.” Ukiwauliza jinsi wanavyotumia maisha yao ya kanisa wanasema, “Ninapoenda hapo namwomba Mungu, na ninapoomba nalia machozi machungu. Ndugu wote huomba, wote wako makini kufungua midomo yao kuongea na Mungu na kumwomba Mungu, baada ya hapo tunaimba nyimbo za sifa, na tunapoimba tunahamasishwa sana hadi sote tuna machozi yanayotiririka nyusoni mwetu. Wakati mwingine, napata msisimko hadi naanza kutokwa na jasho, natokwa na jasho jingi hadi naweza kukamua jasho hilo kutoka shati langu, nadondokwa. Na ndugu wanacheza ngoma pia, kuna watu wanaoimba na kucheza ngoma. Maisha ya kanisa ni ajabu! Kisha tunakula na kunywa maneno ya Mungu, na tunapokula na kunywa maneno ya Mungu, tunahisi kuwa yanaongoea hadi ndani kabisa ya mioyo yetu. Tunapowasiliana, kila mtu anahisi kuchangamka.” Na baada ya kuishi maisha ya kanisa hivi kwa miaka kumi au zaidi, matokeo ni yapi? Hakuna anayelenga kuwa mwaminifu, hakuna anayejichangua, hakuna anayeshiriki hali yao ya kweli na ndugu zao, na hakuna anayeshiriki au kuweka wazi dutu yake ya kweli nao. Miaka kumi au zaidi ya maisha ya kanisa imekuwa ya bure, iliyotumika kucheza cheza, na kati ya hisia za watu na starehe. Unasemaje, starehe za watu na furaha hutoka wapi? Nadhubutu kusema si matakwa ya Mungu, wala hayamkidhi, kwa vile Mungu anataka kuona mabadiliko katika watu, na Anataka kuona watu kweli wakiishi kwa kudhihirisha maneno Yake. Hili ndilo Analotaka kuona; Hataki kukuona ukishikila vitabu vyako vya nyimbo na kuimba wakati wa mikutano au unapohisi hamasa hasa, wala Hataki kukuona hapo ukimwabudu na kucheza ngoma. Hataki kuona hili. Kinyume kabisa, Mungu anapoona hili Anaomboleza na kuvunjwa moyo, kwa sababu Ameongea mamilioni kwa mamilioni ya maneno, lakini maneno Yake hayajatekelezwa au kuishi kwa kudhihirishwa na yeyote kati yenu. Mungu huhisi huzuni na wasiwasi: Mungu anahangaika kwa sababu ya hii. Mara nyingi, tunahisi tumeridhika baada ya kuishi kiasi kidogo cha maisha ya kanisa; mara nyingi, tunahisi kwa kiasi fulani furaha, kwa kiasi fulani amani, kwa kiasi fulani kupendezwa sana, tunapomsifu Mungu kuna hisia ya furaha na faraja ndani ya mioyo yetu, la sivyo tunahisi kutimizwa kiroho, na hivyo tunafikiri kwamba tumefanya vyema katika imani yetu kwa Mungu. Na tunaendelea kushikilia taswira hizi za uongo, tukizizingatia kuwa vitu tunavyotarajia zaidi katika imani kwa Mungu na vitu ambavyo tumeshapata, na tunazitumia kubadilisha mabaliko ya tabia na kuingia njia ya wokovu; basi hatuhitaji kufuata, wala hatuhitaji kutafuta kuwa waaminifu, hatujaribu na kujiweka wazi, au kuweka maneno ya Mungu katika vitendo. Na kwa hivyo Mungu anahisi wasiwasi sana. Wakati watu wametoka kushiriki katika hali halisi, na wametoka kushiriki katika dutu ya kweli tu, wao ni wenye shauku sana, na wanafikiri wenyewe; Ah! Sasa nimeelewa ukweli na kupata njia ya ukweli—nimefurahi sana! Kila siku ni kama mwaka mpya wa Kichina, kila siku huhisi kama kitu kizuri kitafanyika, kila siku unatamani mtu wa kuwasiliana naye, kila siku unatamani mkutano, na baada ya kutamani kwa miaka kadhaa, watu wengine wamekuwa wasiojali kuhusu maisha ya kanisa na imani ya Mungu. Mbona hivyo? Kwa sababu wako na maarifa ya juujuu na ya kinadharia kuhusu maneno ya Mungu na ukweli. Hawajaingia katika maneno ya Mungu kwa kweli au kupitia uhalisi wa maneno Yake. Kama ilivyosemwa katika maneno ya Mungu, watu wengi wameona vyakula vizuri au vyakula katika karamu, lakini wengi wao huja kuangalia tu; hawachukui chochote kujaribu, kuonja, au kujijaza tena nacho. Hii ndiyo Mungu anachukia, na pia ndiyo inayompa Mungu wasiwasi. Uko katika aina hii ya hali wakati huu? Hivyo, tunapokuwa mara nyingi na mawasiliano nanyi, tukiwasaidia na kuwasiliana nanyi, kinachotutia wasiwasi zaidi ni kwamba, baada ya kusikia ujumbe, na baada ya kuridhisha mahitaji yenu ya kiroho, na hamtendi, na kabisa hamchukulii haya mambo kama muhimu. Katika hali hiyo, maneno yetu yangekuwa yamesemwa bure. Katika iwapo mtu kweli anatafuta ukweli, miaka mitatu ya kusikiza ujumbe—au, kama ubora wao wa tabia ni nzuri zaidi kiasi, miaka miwili—huamua kama atakuwa na uwezo wa kubadilika katika siku zijazo, na huonyesha kama yeye ni mtu ambaye hutafuta ukweli. Kwa hivyo, sasa mwanzoni ninapowasiliana kuhusu hii, nina baadhi ya matarajio ya nyinyi. Lakini mtakuwa namna gani wakati ukiendelea? Mnapenda ukweli? Mko tayari kuwa waaminifu? Mtakuwa aje katika siku zijazo? Baada ya kuwasiliana maneno haya, mangapi kati yao yatafanyika ndani yenu? Kati ya maneno haya, ni mangapi yatadhibithisha ufanisi? Haijulikani. Haijalishi jinsi ulivyokuwa na hamasa ulipoanza kwanza kusikiza ujumbe, kiasi gani ungeweza kuvumilia magumu kwa ajili yake, au muda kiasi gani ungepata kushiriki katika mikutano—mambo haya hayajalishi. Bila shaka, hayo pia ni kipengele kimoja kinachoamua kama unaweza kukubali ukweli katika siku zijazo, lakini utafanya nini baada ya kusikia ujumbe huo? Unapanga vipi kuenda na kuweka ujumbe huu katika matumizi? Utauweka vipi katika vitendo? Hii inategemea mtazamo gani unao, jinsi unapanga kuuweka katika vitendo, na yaliyo malengo yako. Watu wengine husema: “Baada ya kujiandaa na ujumbe huu, nitaenda kusaidia wengine, kumtumikia Mungu, na kuongoza walio kanisani vyema.” Mtazamo huu ni sahihi? Sio. Na kwa nini sio? Bila kujali ni jumbe ngapi ambazo umesikia, au mipango yako ni ipi, wacha Nikuambie kilicho muhimu zaidi, na mtazamo upi ni sahihi zaidi: Bila kujali wajibu unaotekeleza, na kama wewe ni kiongozi au la, lazima kwanza uyatumie maneno haya kama kigezo. Usiyachukulie kama chombo katika kazi yako, au mkusanyiko wa kazi yako. Kwanza lazima uyalinganishe na wewe mwenyewe, kwanza lazima uyaweke katika vitendo ndani yako. Ukifanya haya yote, basi kwa hakika utakuwa na uwezo wa kufanya kazi yako vyema. Iwapo siku zote unajaribu na kutia alama maneno haya kuonyesha usawa dhidi ya huyu na yule, au kuyafanya kwa huyu-na-huyu, au yakiwa mtaji wa kazi yako, basi uko katika shida, unatembea njia ya Paulo. Hiyo ni kweli kabisa. Hii ni kwa sababu ukiwa na mtazamo huu, bila shaka unachukulia maneno haya kama mafunzo na nadharia, na unatamani kuyasambaza, na kufanya kazi—ambayo ni hatari sana. ukiyatumia maneno haya kama kigezo, na kwanza uyaweke katika vitendo ndani yako, basi wa kwanza kubadilika na kuingia ni wewe mwenyewe. Iwapo tu wewe mwenyewe utapata kitu ndipo utakuwa na kimo, sifa, na uwezo wa kufanya vyema katika kazi ambayo lazima ufanye; kama huna kimo, kama hujapitia, na hujaingia, basi unafanya kazi kipofu, na unakimbia kimbia kipofu, hakuna matokeo yoyote halisi, na huwezi kutimiza matokeo yoyote. Bila kujali ukweli na uhalisi gani umesikia, mradi uutumie kama kigezo kwa hakika utakua. Ukiyatekeleza haya maneno katika maisha yako mwenyewe, na kuyashirikisha katika matendo yako mwenyewe, kwa hakika utapata kitu, na kwa hakika utabadilika; ukiingiza maneno haya ndani ya tumbo lako, na kuyakariri katika ubongo wako, basi hutawahi badilika. Tunaposikiza mawasiliano, lazima utafakari hivi: “Maneno haya yanarejela hali ya aina gani? Yanarejea kipengele kipi cha dutu? Ni kwa mambo yapi napaswa kutumia kipengele hiki cha ukweli? Kila wakati ninapofanya kitu kinachohusiana na kipengele hiki cha ukweli, ninaweka kipengele hiki cha ukweli katika vitendo? Na ninapokiweka katika vitendo, hali yangu inalingana na hayo maneno? Kama hali yao hailingani, napaswa kuwasiliana, au kutafuta, au kusubiri?” Mnatenda kwa njia hii katika maisha yenu? Iwapo hamtendi, basi maisha yenu yako bila Mungu, na bila ukweli. Mnaishi kulingana na barua na mafundisho, la sivyo kulingana na maslahi yenu binafsi, ujasiri, na shauku. Wale wasio na ukweli kama uhalisi ni watu wasio na uhalisi, na mtu asiye na maneno ya Mungu kama uhalisi wake ni mtu ambaye hajaingia katika maneno ya Mungu. Mnaelewa maneno haya? Ni bora kama mna uwezo wa kuelewa maneno haya—lakini bila kujali jinsi unavyoyaelewa, bila ya kujali kiasi ambacho umeelewa kwa yale uliyoyasikia, kilicho muhimu ni kuwa una uwezo wa kuingiza ulichoelewa katika maisha yako. Hapo tu ndipo kimo chako kitaweza kukua, na hapo tu ndipo utakuwa na mabadiliko katika tabia yako.
Tazama, kwa kila kifungu cha maneno yaliyosemwa na Mungu, au kila tukio ambalo Mungu anatoa mahitaji kwa watu, Mungu ataonyesha njia ya kutenda na kanuni za kutendea. Kwa mfano, tulipozungumza kuhusu kuwa waaminifu hivi karibuni, Mungu aliwaonyesha watu njia, Aliwaambia jinsi ya kuwa waaminifu, na jinsi ya kutenda wanapokuwa waaminifu ili kuchukua njia sahihi kwa kuwa waaminifu, Akisema: “Kama huko tayari kabisa kuwaambia wengine kuhusu siri zako—matatizo yako—na kutafuta njia ya mwanga, basi Ninasema kuwa wewe ni mtu ambaye ni mgumu kuokoa, mtu ambaye hawezi kuibuka kutoka kwa giza kwa urahisi.” Matokeo ya maneno haya ni kuwa tunahitajika kuweka wazi mambo tunayoamini kuwa siri au binafsi, na lazima tuweze kuyachambua. Hili halikutokea kwenu; hamkuelewa au kujua kwamba haya maneno ya Mungu yalikuwa ili kuwafanya mtende kwa hii njia. Wakati mwingine, jinsi unavyotenda ni aina ya udanganyifu, na hivyo inapaswa kubadilika, na motisha zako pia zinapaswa kubadilika, Inawezekana kwamba hakuna anayetambua kwamba maneno yako ni danganyifu, lakini kuna motisha katika njia unavyotenda, na motisha hizi ni danganyifu, na kwa hivyo zinapaswa kubadilika—na kama zinafaa kubadilika, lazima uzichambue: Je, Mungu anachukia motisha hizi? Je, njia unavyotenda na motisha zako zinamchukiza Mungu? Je, huwezi kuziweka wazi? Ni vigumu kuongea kuzihusu? Zinapingana na ukweli? Kama, unapozichambua na kuzichunguza, unasema, “Eh, inaonekana kuwa hizi zinapingana na ukweli, inaonakena kuwa ninapotenda kwa njia hii, si rahisi kuweka mambo wazi, na kutenda hivi kunachukiwa na Mungu,” basi unafaa kubadilisha jinsi unatenda—hakuna haja ya kutenda kusivyohitajika sana. Mnahisi huzuni Ninawasilisha hili kwenu, mkifikiri: “Iwapo nafaa kumwamini Mungu kwa njia hii, basi inaonekana lazima nianze kutoka mwanzo. Imekuwa vigumu vya kutosha kufika mahali niko leo, kwa nini lazima nianze kutoka mwanzo tena”? Kwa kweli, wakati huu ndio mwanzo, na unapoanza, lazima uanze vizuri. Tangu mwanzo kabisa lazima ufahamu umuhimu wa kuingia katika uhalilisi—lazima uweke msingi mzuri; kama, kule mwanzoni kabisa, uliweka msingi wa barua na mafundisho, basi utakuwa katika shida. Ni kama wakati watu hujenga nyumba ufuoni nyumba hiyo itakuwa hatarini bila kujali umeijenga kwa urefu gani, na haitadumu sana. Bado, leo, mna faida—mna uwezo wa kukubali kile tunachowasiliana nanyi, na mko tayari kusikiza. Ni vyema! Unapaswa kufahamu kilicho muhimu, kilicho cha umuhimu wa kufuatia, and jinsi unavyopaswa kuingia. Na kuhusu makosa, dhambi, na dosari unazo ambazo zinayopaswa kurekebishwa, lazima uharakishe na uzirekebishe. Usisubiri; muda haumgoji yeyote! Ukipoteza miaka hii, na kuitumia bure, basi hivi karibuni utagutuka na kusema: Jamani! Sina kimo. Mambo yakinifanyikia, bado sina uwezo wa kushughulika nayo, na kwa kila kitu nimechanganyikiwa na sionyeshi hisia; kwa kila kitu nategemea tabia yangu potovu na falsafa yangu ya maisha kuishi, au mawazo yangu mwenyewe, au maarifa na mafundisho. Ya kusikitisha mno! Siku ikifika utakapoulizwa kufanya baadhi ya kazi kwa kanisa, au kutimiza wajibu fulani, utajipata mkono mtupu, na kuwa na wasiwasi. Zaidi ya hayo, kazi ya Roho Mtakatifu haisubiri watu. Katika miaka michache ya kwanza Alikupa baadhi ya neema, huruma, usaidizi, na utoaji. Lakini kama, baada ya Yeye kukusubiri kwa muda mrefu, bado hujabadilika au kuingia katika uhalilisi, na unaelewa tu barua na mafundisho, basi umekwisha—umeshakosa nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu. Mwanzoni unapoweka msingi, unapaswa kukaza miguu yako katika njia ya uhalilisi, na si kwa njia ya barua na mafundisho. Unapaswa kuchagua kuingia katika uhalisi, na kwa kila kitu unapaswa kuingia katika uhalisi, na kuukubali uhalisi uathiri wazo lako, na kujiuliza: “Napaswa kutenda vipi katika suala hili? Napaswa kutenda vipi katika suala hilo? Na kanuni ya kutenda katika suala hili ni ipi? Kanuni ya kutenda katika suala hilo ni ipi? Ni nini kinapaswa kufanywa ili kumridhisha Mungu? Napaswa kufanya nini ili kutimiza mahitaji ya Mungu na viwango Vyake? Haya ndiyo unayopaswa kuuliza. Lakini kimo cha watu ni kidogo sana, na kila wakati wanauliza kuhusu mambo yasiyohusika na kuweka ukweli katika vitendo, au yasiyokuwa na uhusiano na kujijua na kuwa waaminifu. Unasemaje, hiyo si ovyo? Kimo chao si kidogo? Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wafuasi tangu Mungu alipoanza hatua hii ya kazi; hata kuna wale walioanza na kuanza kufuata wakati Roho Mtakatifu alikuwa anafanya kazi katika mkondo huu—lakini kuwa wamefuata hadi leo, bado hawaelewi maana ya “uhalisi”, na kuwa wamefuata hadi leo, hawajawahi kuingia katika uhalisi wowote. Watu wengine husema: “Si sahihi kusema kwamba, kwa kuwa wamefuata hadi leo, hawajaingia katika uhalisi. Angalau wamejitumia na kujitolea; watu wengine hata wameacha matarajio yao, kazi, na familia, na hata kuna wale walioacha ndoa. Huku si kutenda? Kwa nje unaweza kuwa umeonyesha baadhi ya moyo wa ibada na kujitolea, na kutenda kwa njia fulani, lakini kufanya mambo haya hakumanishi kuwa wewe ni mwaminifu, wala kumaanisha kuwa umepata ukweli kutokana na imani yako kwa Mungu. Matendo haya hudokeza tu ushirikiano wa watu ili kuokolewa kupitia kwa imani kwa Mungu; matendo yao si onyesho la kuingia katika uhalisi wa ukweli. Na hivyo, watu wengi ambao wamemfuata Mungu kwa miaka ishirini bado wanaweza kumwacha Yeye, na kuwa wamemfuata kwa miaka ishirini bado wanaweza kufukuzwa kutoka kwa nyumba ya Mungu. Kuna hata wale ambao, ingawa wamefuata hadi leo, hawajawahi kuwa waaminifu, hawajawahi weka kuwa mwaminifu katika vitendo, kwa vile hawaoni kuwa waaminifu au kuweka ukweli katika vitendo na kuingia katika uhalisi kuwa muhimu. Na wanaona imani kwa Mungu kama nini? Wanafikiri: “Mradi nikimbie hapa na pale, nijitolee mwenyewe, lipa gharama, na kuacha kazi yangu, basi Mungu anapaswa kufanya ukumbusho wa tabia yangu,” au, “Nastahili kuwa mmoja wa wale waliookolewa.” Hii ni ruya, na ndoto za mchana. Ikiwa tunafaa kuokolewa, na kwa kweli kuja mbele ya Mungu, basi lazima tuulize kwanza: “Eh Mungu! Napaswa kuweka nini katika vitendo? Viwango Vyako ni vipi? Viwango Vyako vya kuokoa watu ni vipi? Unaokoa watu wa aina gani?” Haya yanaashiria urazini wa kweli, hii ndiyo tunapaswa kuulizwa juu ya yote, na ile tunapaswa kutafuta na kujua juu ya yote. Ukiweka mizizi yako katika uhalisi na ukweli, ukifanya kazi kwa bidii katika vipengele vyote vya ukweli na uhalisi, basi wewe ni mtu aliye na mizizi, na kumiliki uhai. Ukiweka mizizi yako katika barua na mafundisho, na hivyo usiwahi kuweka ukweli wowote katika vitendo au kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya ukweli wowote, basi utakuwa mtu ambaye kamwe hawi na uhai. Ona, kuwa mwaminifu kunapendwa na Mungu. Tunapoweka kuwa waaminifu katika vitendo, tunakuwa pia na maisha ya kuwa waaminifu, na uhalisi na dutu ya kuwa waaminifu—na hivyo tunao utendaji wa kuwa waaminifu, na onyesho la kuwa waaminifu. Angalau, upande wetu ulio mwaminifu unapendwa na Mungu na kukubaliwa na Mungu. Lakini bado tunazo sehemu nyingi ambazo hatuko waaminifu, na tunahitaji kuendelea kubadilika na kufuata—Mungu anatungoja, na kutupa nafasi. Kama kamwe hatupangi kuwa waaminifu, na kamwe hatutafuti jinsi ya kuwa waaminifu, au kutafuta matendo na maneno yapi ni onyesho la kuwa waaminifu, basi hatutawahi kuwa na dutu ya kuwa waaminifu, na hakungekuwa na uwezekano wa sisi kuwa na maisha ya kuwa waaminifu. Aina yoyote ya uhalisi ulio nao ni kimo unacho, na kipengele cha ukweli ambao umejiandaa nao. Kama huna uhalisi wa aina hii, basi huna maisha hayo ama kimo kama hicho. Na basi, wakati unakutana na majaribu au mitihani, au agizo, kama huna uhalisi, wakati mambo haya yatakufanyikia itakuwa rahisi kwako kuanguka, kufanya makosa, kufanya dhambi dhidi ya Mungu, na kuasi dhidi ya Mungu—yote ambayo yatakuwa nje ya udhibiti wako. Hatimaye, watu wengine wataondolewa, Roho Mtakatifu atawaacha na kukoma kufanya kazi ndani yao, na hata kutakuwa na wale ambao, kwa kusababisha uharibifu kwa nyumba ya Mungu, wataishia kufukuzwa. Hili ni tokeo lisiloweza kuepukwa. Lakini kama, leo, utaweka ukweli katika vitendo na kuwa mwaminifu, nani anaweza kuchukua sehemu yako ambayo ni aminifu? Hakuna anayeweza, hakuna anayeweza kukuvua kipengele hiki cha uhalisi na maisha haya. Na kama, wakati fulani katika siku zijazo, unasema: “Nimekuwa mwaminifu kwa muda mrefu sana, naweza kurudi kuwa mtu ambaye ni mdanganyifu?” kuna uwezekano haitafanyika kwa urahisi, kwa vile tayari unaishi katika mwanga wa Mungu, na kuishi katika njia ya mwanga. Si rahisi kubadilika kutoka kuwa mtu ambaye ni mdanganyifu hadi mtu ambaye ni mwaminifu. Kubadilika tena kutoka kuwa mtu mwaminifu kwa kweli anayependwa na Mungu—huko hakuwezekani wala si rahisi. Watu wengine husema, “Nimekuwa nikiweka kuwa mwaminifu katika vitendo kwa muda fulani. Mara nyingi ninaweza kuongea maneno ya kweli, na mimi ni mwaminifu kiasi, lakini wakati mwingine nafichua tabia yangu ya danganyifu, naonyesha dutu yangu ya danganyifu.” Hii inafaa kutatuliwa baadaye hatua kwa hatua. Mradi ufuate, na kufanya kazi kwa bidii na kufikia kuingia kuhusu suala hili, basi hufai kuwa na wasiwasi kuhusu jinsi utakuwa katika siku zijazo. Unapopanda miche ardhini, kama unainyunyizia maji na kuipa mwangaza kila siku, hufai kuwa na wasiwasi kama itazaa matunda; majira ya kupukutika kwa majani yanapokuja, lazima kutakuwa na kitu cha kuvuna. Leo, kinachotuhusisha zaidi kinapaswa kuwa kama tayari tunaweka kuwa waaminifu katika vitendo, na kama tunashiriki katika uhalisi huu. Ukisema, “Najua kuwa mimi ni mdanganyifu, lakini sitawahi kuweka kuwa mwaminifu katika vitendo,” basi huna uhalisi wowote wa kuwa mwaminifu, na lazima bado ufanye kazi kwa bidii: Kila utondoti wa maisha yako, kila njia unavyotenda katika maisha yako, njia ambayo daima umetenda, namna yako ya mara kwa mara ya kutenda, na jinsi unavyowatendea watu—lazima yote yachambuliwe. Usipoyachambua, bado utakuwa mwenye majivuno, na bado utaridhika na jinsi unavyofanya vitu—lakini unapoyachambua, utashtuka: Jamani, inaonekana kwamba mimi katika mawazo yangu ni wa chini sana, mbaya sana, mwenye kudhuru kwa siri sana! Utashangaa; utagundua nafsi yako ya kweli, na utajua kwa kweli shida zako mwenyewe na makosa, na udanganyifu wako mwenyewe. Na kama huchambui? Daima utajiamini kuwa mwaminifu, na mtu asiye na udanganyifu. Mdomo wako utasema wewe ni mdanganyifu, lakini ndani ya moyo wako bado utajiamini kuwa mwaminifu. Hapo basi, hutawahi kubadilika. Usipojichambua, ungewezaje kujijua? Usipojichambua, unawezaje kujiweka wazi? Unawezaje kuchimbua mambo na motisha katika kina cha moyo wako? Na usipoyachimbua, unawezaje kubadilika? Usipoyachimbua, utakuwa mjinga kuhusu mwelekeo wa kutendea, na cha kulenga katika matendo yako. Hii hasa ndiyo maana ya kweli ya maneno “Usipoingia katika uhalisi, utakuwa bila uhalisi wa ukweli milele.”
Maneno yote ya Mungu yana maana ya kweli, na ni ya watu kuyatumia kama kigezo. Si ya kukupa kitu cha kusoma, au kuridhisha mahitaji yako kadhaa ya kiroho, au ya wewe kunung’unikia kutoka mdomo wako, ukikitimiza hitaji lako la maneno na mafunzo. Maneno yote ya Mungu yana dutu yao yenyewe, na hali yao halisi, na kama usipojaribu na kuweka kipengele hiki cha uhalisi katika vitendo au kujaribu kukiingia, basi milele utakuwa mtu aliyeachana na uhalisi. Ukiweka kuwa mwaminifu katika vitendo, basi utakuwa na uhusiano na uhalisi wa kuwa mwaminifu na utaingia hali ya kweli ya kuwa mwaminifu. Pia utaelewa watu wa aina gani ni waaminifu, aina gani sio, na kwa nini Mungu anachukia wale ambao ni wadanganyifu; kwa kweli utaelewa maana ya mambo haya, na kufahamu nia za Mungu katika kuomba watu wawe waaminifu, na kwa nini Anatoa mahitaji haya. Baada ya kugundua jinsi ulivyo mdanganyifu, utataka sana kubadilika, utachukizwa na udanganyifu wako mwenyewe na uhalifu, utatiwa kinyaa na tegemeo lako lisilo la aibu la udanganyifu na uhalifu ili kuishi, na hivyo utahisi zaidi jinsi ilivyo muhimu kuwa mwaminifu, na jinsi mahitaji ya Mungu kuwa watu wawe waaminifu ni ya wakati wa kufaa, na nzuri, na jinsi maneno Yake ni sahihi. Unasemaje, si muhimu kuwa Mungu atoe mahitaji haya? Ndiyo. Na hivyo, kuanzia leo, tunapaswa kuchambua sehemu yetu ambayo ni danganyifu na halifu. Baada ya kuichambua, utagundua kuwa nyuma ya kila kipande cha udanganyifu kuna motisha, malengo fulani, aibu yako, na kuwa pia vinaonyesha ujinga wako, na hali yako ya chini. Baada ya kugundua hili, utautazama uso wako wa kweli, na baada ya kugundua uso wako wa kweli utajichukia. Unapojichukia na kujua wewe kwa kweli ni kitu cha aina gani, bado utaringa wakati huo? Bado utajigamba katika kila kitu? Bado utajaribu na kupata kibali cha watu wengine kwa kila kitu? Na bado utasema kuwa Mungu anauliza mengi sana? Kwamba hakuna haja ya mahitaji ya Mungu? Utaacha kutenda kwa njia hii na kusema mambo haya, utasema amina kwa, na kukubaliana na maneno yaliyotamkwa na Mungu, na kuaminishwa kwa kweli na kabisa nayo. Hii ndiyo fanisi zaidi kuhusu kuweka kila moja ya maneno ya Mungu katika vitendo, na kuingia katika uhalisi, na ukizidi kuweka maneno ya Mungu katika vitendo, utazidi kuhisi jinsi yalivyo sahihi na muhimu. Tuseme hutendi, na daima unasema, “Eh, mimi si mwaminifu, mimi ni mdanganyifu!” Unapokuwa mdanganyifu, unafikiri mwenyewe, “Nitatenda tu namna hii; si danganyifu sana, bado inahesabika kama kuwa mwaminifu. Mimi niko wazi kabisa, usaliti huu kidogo hauwezi kuchukuliwa kama udanganyifu,” na ni hayo tu. Jambo sawa linapokufanyikia tena, wewe ni mtawala na mhalifu mara nyingine tena; punde unapofungua mdomo wako, maneno yanayotoka ni madanganyifu, baada ya hapo unafikiri kwa muda, na kusema: “Nilikuwa mhalifu leo?” Unakuwa na wazo, na kujisemea kuwa haionekani kama umekuwa, na hakuna zaidi; unasema, “Hakuna shida, sikuwa mhalifu.” Wakati unaofuata, unadanganya tena, na baada ya kudanganya unafikiri kwa muda, na kujisemea: “Eh, nilikuwa mhalifu na mdanganyifu tena? Nilidanganya tena? Haionekani kama nilidanganya.” Ukiuomba mbele ya Mungu, unasema: “E Mungu! Ona jinsi mimi daima ni mtawala , jinsi daima mimi ni mhalifu na mdanganyifu. Nakuomba unisamehe, na kunikomesha kuwa mhalifu na mdanganyifu wakati ujao—na kama mimi ni hayo, tafadhali nifundishe nidhamu, Mungu.” Unafuta kwa kawaida mambo kama haya. Huyu ni mtu wa aina gani? Huyu ni mtu asiyependa ukweli, na asiye tayari kuweka ukweli katika vitendo. Unaweza kuwa umelipa gharama ndogo na kutumia wakati mdogo kwa ajili ya kutekeleza jukumu lako, kumhudumu Mungu, na kusikiza ujumbe, na unaweza kuwa umetumia muda ambao ungetumia vinginevyo kufanya kazi na kupata pesa kidogo, lakini kwa kweli, hujaweka ukweli katika vitendo hata. Ikujapo kuweka ukweli katika vitendo, wewe kweli ni mtu juu juu, na aliyekosa uwajibikaji, na asiyejali; hivyo, pia, wewe ni mzembe kuhusu kuweka ukweli katika vitendo. Hii inathibitisha kuwa mtazamo wako kwa ukweli ni wa chuki, kuwa wewe ni mtu asiye tayari kuweka ukweli katika vitendo, aliyepotea kutoka kwa ukweli, asiyemwacha Mungu kwa sababu tu unatamani kupata baraka na kuogopa adhabu. Kwa ajili ya kuwa sawa na mtindo, unaiga kile ndugu zako wote wanasema, unajifunza maneno fulani ya kitaaluma ya kiroho, baadhi ya nyimbo zinazojulikana, na baadhi ya maneno ambayo kila mtu husema mara nyingi, na unafikiri unafuata mwenendo, na kwamba unakuwa mroho. Hatimaye, matukio haya ya juujuu yatakuchezea hadi kifo chako, utakapomalizwa, mwisho wako utatangazwa, na utaenda jahanamu. Katika hili, kuna haja ya kumwamini Mungu? Hakuna uhalisi katika “imani” yako, hujaingia katika uhalisi wowote, na hivyo, vivyo hivyo, mwisho wako utakuwa jahanamu, na hutazaa tunda. Mungu husema nini? Mungu anataka tunda, si maua; bila kujali hadi kiasi gani utachanua, jinsi ulivyo mrembo, Mungu hakutaki. Ambayo ni kusema, bila kujali jinsi mambo unayosema ni mazuri, bila kujali jinsi kujitolea na kutoa kwako sadaka kwa nje ni kukubwa, au mambo mangapi wewe huacha, hakuna kati ya haya yanayopendwa na Mungu. Mungu anaangalia kiasi gani umebadilika kwa kweli, kiasi gani umeingia katika uhalisi, kiasi gani umeingia katika ukweli, na mambo mangapi umefanya yanayoridhisha moyo wa Mungu, na yaliyolingana na mahitaji Yake. Hii ndiyo Mungu huangalia. Wakati watu hawamfahamu Mungu, wakati hawauelewi moyo Wake, wao daima wanauelewa vibaya moyo Wake, na daima wanaleta baadhi ya mambo ya juujuu mbele Yake kutoa maelezo, wakisema: “E Mungu! Ona kwa muda gani nimejitolea Kwako, ona kwa muda gani nimekuamini, ona jinsi nimezunguka zunguka kwa ajili Yako, ona watu wangapi nimekushindia, ona ni vifungu na sentensi ngapi za maneno Yako ambayo nimekariri, ona idadi ya nyimbo hizi za kidini ninaweza kuimba—je mimi sijalipa gharama kubwa? Kila siku narauka saa kumi asubuhi kuomba, kusema maombi yangu ya asubuhi. Hata jambo kubwa linapotendeka, au niko katika ugumu, au nimefanya makosa, nafunga na kuomba. Na natumia muda mwingi kusoma maneno ya Mungu kila siku....”Lakini bado matokeo ni kwamba Mungu anasema: “Wewe ni mwaminifu sasa? Kumekuwa na mabadiliko katika ujanja wako? Umewahi kulipa gharama yoyote kwa kuwa mwaminifu? Umewahi kuleta mambo ya hila ambayo umefanya na ufunuo wa ujanja wako mbele Yangu kuuweka wazi? Udanganyifu wako Kwangu umepunguka kwa kiasi gani? Wewe mwenyewe unajua udanganyifu wako Kwangu, na uongo ambao umeniambia? Umeweka mambo haya kando? Hebu wewe fikiria kuhusu mambo haya—inaonekana hujafikiria, hata kidogo. Umeshtuka, na kushangaa kuhisi kuwa huna namna ya kutoa maelezo mbele ya Mungu. Nia Yangu katika kusema haya yote ni kwamba mnapaswa kuwa makini katika kuweka ukweli katika vitendo. Kila neno, mawasiliano, na ukweli haupaswi kupitishwa tu kwa wengine, lakini pia kuwekwa katika vitendo. Kwa nini Mungu husema kuwa ukweli ni maisha yako, kuwa unaweza kutenda kama maisha yako? Kwa sababu ukweli unaweza kukubadilisha, na katika hili, unakuwa maisha yako. Kama ukweli haujakubadilisha, hiyo si kwa sababu haujatenda kazi yake, lakini kwa sababu hujauweka katika vitendo, au kuuingia; hujaukubali ukweli ulio ndani yako ili kutoa na kubadilisha mambo yale yako yaliyo potovu, kubadilisha mambo yale ndani yako yanayoasi na kupingana na mapenzi ya Mungu. Hatimaye, kama ukweli haujatekeleza kazi yoyote ndani yako, kama haujabadilisha tabia yako yoyote potovu, basi siku moja, wakati maisha yako ya imani kwa Mungu yako karibu kuisha, majaliwa yako yataamuliwa pia. Tunapowasiliana kuhusu hili leo, hamhisi umuhimu wa kuweka ukweli katika vitendo? Usikuwe kama watu wa zamani, kusubiri miaka mitatu au mitano, mitano au sita kabla ya kuanza kuweka ukweli katika vitendo. Hakuna wakati umewekwa wa kuweka ukweli katika vitendo: Ukiweka ukweli katika vitendo mapema, utabadilika mapema. Ukiuweka katika vitendo baadaye, utabadilika baadaye—lakini kama umekawia sana na ukose nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu, na kukosa mkondo wa kazi ya Roho Mtakatifu, basi wewe umekwisha kabisa. Ukingoja hadi mpango wa usimamizi wa Mungu umefika kikomo na mkondo wa wokovu wa Mungu umepita, basi utakuwa umekosa nafasi yako kabisa, na wakati umekosa nafasi yako utasema: “Eh! Siku hizo za nyuma sikuweka bidii yoyote. Nitaanza kuweka ukweli katika vitendo leo.” Wakati huo utakuwa umekawia sana, na si rahisi kufanya, kwani Roho Mtakatifu anapoacha kufanya kazi, maarifa yako ya jambo lolote au ukweli yatakuwa ya juujuu, na kukosa mazingira, na bila nguvu—na wakati huo, kutakuwa na haja gani ya kujipiga kifua chako na kuomboleza kwa huzuni?
Unasemaje, kuishi na watu walio wadanganyifu kunakufanya uhisi mchovu? Ndio. Na wao huchoka? Wanachoka, pia, kwa sababu kuwa mdanganyifu si nzuri kama vile kuwa mwaminifu. Kuwa mwaminifu ni rahisi, mawazo na akili yako si ngumu—lakini ukiwa mdanganyifu, lazima uwe wa kukwepa daima. Gani huchukua muda mrefu zaidi: njia ya mzunguko, au ile ya moja kwa moja? Ile ya mzunguko, kwa hakika. Na mabomba ya maji, ikiwa bomba ni laini maji hutatoka moja kwa moja, ni rahisi, si vigumu kupata maji. Lakini ukipitisha maji kupitia katika bomba lililo na kona kadhaa ndani lake, je si maji hutoka polepole zaidi? Kuenda polepole huchukua nguvu zaidi. Nguvu zaidi hufanya watu wahisi kama ni ya ziada, na uziada hufanya watu wahisi karaha. Na hivyo watu wadanganyifu wenyewe pia huhisi uchovu; kuwa mdanganyifu daima kunachosha. Unajua umbali gani watu wengine hata huenda wanapokuwa wadanganyifu? Wanazozana na kila mtu. Na kwa kiasi kipi? Inakuwa hadi hawawezi kulala usiku, na ni kwa sababu kugombana siku nzima kunachosha, na kunawachosha kiakili. Unasemaje, wakati mambo yamefika kiwango hicho, mtu huyu ni mdanganyifu kiasi kipi? Iwapo angekuwa mwaminifu, hakuna vile angekuwa amechoshwa kiakili na kukosa uwezo wa kulala usiku. Kuishi maisha kama mtu mwaminifu hakuchoshi: Anasema chochote kilicho kwa akili yake, anafichua anachofikiria, na anatenda chochote anachofikiri katika akili yake, akitafuta mapenzi ya Mungu katika kila kitu anachofanya na kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu. Kunaweza kuwa na mambo kumhusu yaliyo majinga, kwa hivyo katika siku zijazo lazima awe mwenye busara zaidi, na lazima daima akue. Lakini watu wadanganyifu hutegemea falsafa yao wenyewe, mambo, na dutu kuishi. Wao si kama wale walio waaminifu; lazima wawe na tahadhari katika kila kitu wanachofanya isiwe wengine wawe na kitu dhidi yao, lazima watumie njia zao, utawala wao wenyewe wa udanganyifu na uhalifu ili kulinda na kuficha nyuso zao za kweli katika kila kitu wanachofanya. Karibuni au baadaye wataonyesha tabia zao za kweli, na wakifanya hivi watajaribu kugeuza mambo. Wanapojaribu kusema kitu ili kugeuza mambo, kuna nyakati ambazo si rahisi sana, na wasipoweza, wanaanza kuwa na wasiwasi. Wanaogopa kuwa wengine wataweza kuona ndani yao; hiyo inapofanyika, wanahisi wamejiaibisha wenyewe, na wanapoaibika lazima wafikirie njia za kusema kitu cha kuokoa hali. Si kuenda mbele na nyuma hivi kunachosha? Lazima wafikiri yote tena katika akili zao: kama hawangefanya hivi, maneno haya yangetoka wapi? Kama wewe ni mwaminifu, na uko bila motisha au nia, basi utatenda kwa njia wazi na kukosa kitu kisichoweza kuletwa kwa mwanga. Lakini watu walio wadanganyifu daima huficha nia katika maneno wanayoyasema na mambo wanayoyafanya, na mara tu wanapowekwa wazi, wanafikiri njia za kubadili mambo, watakapokupa fikra nyingine ya uongo, na kukufanya kutoelewa suala hilo tena, itakayowafanya wachovu. Kuishi nao unahisi jinsi ni ujinga kwao kutenda kwa njia hii, na ni bure kusema hivyo. Kwa kweli hakuna haja wao kujieleza kwako, hudhani ni muhimu, lakini wanendelea kueleza na kueleza, wakijaribu kuokoa hali. Unachoka kuwasikiza, kwa hivyo ili kuvumilia nao, kwa hivyo ili kuwavumilia, ili kuwaheshimu kidogo na kuwasamehe, unalazimika kuwa mvumilivu na mstahamilivu kwao, na wanafikiri kwa wenyewe: Ona jinsi daima lazima niseme mambo ambayo ni ya kweli; kama singelazimika kueleza mambo haya kwako haingekuwa ya kuchosha sana. Katika akili zao, daima lazima wafikiri kuhusu jinsi ya kukuzuia kutowaelewa, jinsi ya kukufanya usikize kile wanachosema na kutazama wanachofanya kwa njia inayofikia malengo na motisha zao. Na hivyo wanaipitia tena na tena katika akili yao: Wanapokosa uwezo wa kulala usiku wanafikiri kuihusu; wakati wa mchana, kama hawana uwezo wa kula wanafikiri kuihusu; wakati wa majadiliano na wengine wanaifikiri sana. Daima wanavalia sura ya kujifanya, ili usifikiri wako hivyo, ili usifikiri wano ni wazuri, au kuwa hivyo sivyo walivyomaanisha. Wakati wewe, mtu mdanganyifu, uko na mtu mwaminifu, anaweza kukuona jinsi ulivyo. Hawakukosoi, lakini: Wanakuvumilia, na ni hayo tu. Lakini ikiwa wote wawili ni wadanganyifu, basi kutoelewana kati yao kutakuwa wa kina zaidi na hawatakuwa na uwezo wa kuelewana. Lakini kama wewe ni mwaminifu, na wao ni wadanganyifu, basi bila shaka utachukizwa na jinsi wanavyotenda. Wanapoendelea kutenda kwa njia hii utawaona kuwa hasa wa kuchukiza. Wanapofanya hivyo mara kwa mara, utasema: “Watu wote wana tabia potovu, hakuna kitu cha kufanywa,” lakini wakiendelea kuifanya, utawaona kuwa hasa wa kuchukiza, utachukia jinsi wanavyotenda, utachukia nyuso zao, utachukia nia zao—na kuwachukia kwa kiasi hicho, bado ungetaka kuwa na mawasiliano nao bado? Bado ungetaka kuadhiriana nao? Ila wakibadilika, sivyo?
Je, haichoshi sana kuwa mdanganyifu? Kwa vile inachosha sana, kwa nini watu bado wako tayari kuwa wadanganyifu badala ya waaminifu? Mmewahi kufikiri kuhusu hiyo? Hili ndilo tokeo la jinsi asili ya kishetani inacheza na watu, ikiwaacha bila uwezo wa kutoroka maisha haya na tabia hii. Pia wako tayari kukubali kuchezewa kwa njia hii; wako tayari kuishi ndani ya hii, na hawako tayari kuweka njia ya mwanga katika vitendo. Unahisi kuwa kwao kuishi hivi kunachosha, kuwa hakuna sababu ya kutenda kwa njia hii—lakini wanahisi kuwa inahitajika sana, wanafikiri kuwa wana mengi ya kupoteza wasipotenda kwa njia hio, kuwa maslahi yao wenyewe yatadhuruiwa, kuwa watapata aibu nyingi na sifa yao itaharibika. Wanahisi watapoteza mengi sana, na wanayathamini mambo haya; wanathamini heshima yao na motisha zao. Hii ndiyo sura ya kweli ya chuki ya watu ya ukweli. Hata hivyo, watu hawaweki ukweli katika vitendo na hawako tayari kuwa waaminifu kwa sababa hawapendi ukweli. Na mbona hiyo? Daima unathamini mambo hayo. Umeamini katika Mungu kwa siku moja au mbili tu, wewe si mtu ambaye ameanza tu kuamini katika Mungu, mtu asiyeelewa ukweli na hana ufahamu wa aina gani ya watu wanapendwa na Mungu, na nani hivyo anategemea mambo yale ya wasioamini ili kuishi, anayetegemea mambo ya Shetani ili kuishi. Leo, kuna watu ambao wanajua ukweli. Tayari wameskia mengi, na wamefichua mengi, la sivyo wamesikiza kwa muda na wanafahamu kuamini katika Mungu kunahusu—lakini kwa nini bado hakujakuwa na mabadiliko ndani yao? Kwa sababu hawapendi ukweli. Na wale wasiopenda ukweli wanafaa kufanya nini? Hakuna njia ya mkato katika hili! Wao wenyewe lazima walipe gharama, wateseke, na kuomba na kujiweka wazi mbele ya Mungu, na baadaye wanahitaji kujiweka wazi hatua kwa hatua na kujichambua mbele ya watu wengine. Hii inahitaji ujasiri, inahitaji uasi dhidi yako mwenyewe, na inahitaji kujinyima. Usipojinyima na kuasi dhidi yako mwenyewe, kama unatamani kuweka ukweli katika vitendo bila kuvumilia mateso yoyote au kulipa gharama yoyote, basi hakutakuwa na matokeo. Watu wengine huuliza maswali kama, “Nifanye nini kama sipendi ukweli?” Kama hupendi ukweli, basi fanya mambo yale yanayoenda dhidi ya ukweli, na uone kama Mungu atafundisha nidhamu! Watu wengine husema: “Nifanye nini kama sitaki kishiriki katika mikutano?” Basi nenda na uishi na wale wasioamini, nenda na uchezecheze nao, uone ni nini hatimaye kitafanyika! Watu wengine husema: “Nataka kuwa mdanganyifu, sitaki kuwa mwaminifu. Kuwa mwaminifu, nitapoteza mengi sana, siwezi kufanya hivi. Kuwa mwaminifu, maslahi yangu mwenyewe yatateseka sana, na siri zangu nyingi sana zitajulikana na wengine. Sitaki kuwaruhusu watu wengine kujua mambo yangu ya binafsi, sitaki kuwaacha wanijue au kunielewa, napaswa kuwa na udhabiti wa majaliwa yangu.” Hivyo jaribu—uone nini kitakachofanyika kwako mwishowe, uone ni nani ataenda jahanamu na kuteseka adhabu!
Mko tayari kuwa waaminifu? Mnapanga kufanya nini baada ya kusikiza mawasiliano haya? Mtaanza na nini kwanza? (Kwanza nitamakinikia kutodanganya.) Sahihi. Kutodanganya si rahisi. Je, uwongo huwa na motisha? Hivyo kwanza, usiseme uongo wenye motisha. Hiyo ni rahisi kufikia? Kwa mfano, unahisi maneno haya yana motisha, kwamba yana madoa, kwamba ni uwongo—na unajua unapodanganya, sivyo? Hivyo kwanza usiseme uwongo huu. Upeleke mbele ya Mungu kuweka katika maombi yako na kuweka wazi; kwanza weka hii katika vitendo. Baada ya kufanya hivyo kwa muda, unapaswa kuomba kwa Mungu na kuuliza kwamba Akufundishe nidhamu na kukushutumu kama utawahi kudanganya tena, baada ya hapo unapaswa kuleta uwongo wako hatua kwa hatua mbele ya ndugu zako ili uchambuliwe.... Kwa njia hii, hatua kwa hatua, uwongo wako utakuwa daima chache, daima pungufu. Leo utasema uwongo kumi, kesho unaweza kusema tisa, siku baada ya hiyo utasema nane, baada ya hapo utasema mbili au tatu pekee. Utasema ukweli zaidi na zaidi. Kuwa mwaminifu, utakuja karibu na mapenzi ya Mungu, mahitaji Yake, na viwango Vyake daima zaidi—na hiyo itakuwa vyema iliyoje! Lazima uwe na lengo, lazima ukuwe na njia. Kwanza usiseme uongo huo, kisha chambua motisha zilizo ndani wake: Kwa nini umemiliki motisha kama hizi? Na dutu yao ni nini? Hii pia lazima uichambue hatua kwa hatua, na kama ukiendelea kuweka hii katika vitendo, basi kwa hakika kutakuwa na tokeo. Siku moja utasema: “Haya, ni rahisi kuwa mwaminifu. Kuwa mdanganyifu kunachosha sana! Sitaki kuwa mdanganyifu tena daima, kunachosha! Kuna mengi sana yanayofanyika ndani ya moyo wangu, kila kitu kimechanganyika ndani ya ubongo wangu, akili yangu daima lazima ifikiri mambo na kujadili: ‘Nitasemaje hili? Maneno yanaweza kutumiwa vipi kudanganya watu na kuwalaghai? Daima lazima nifikiri sana na kupima mambo hivi; maneno yangu hayawezi kuwa machangamfu sana, lakini pia hayawezi kuwa mazito zana—na ndani ya moyo wangu sina uwezo wa kubeba shinikizo hili, sitaki kuishi namna hii tena, kuishi namna hii kunachosha sana!” Wakati huu, utakuwa na matumaini ya kuwa kweli mwaminifu, na inathibitisha kuwa umeanza kuchukua hatua kuelekea kuwa mwaminifu. Haya ni mafanikio mapya. Bila shaka, kunaweza kuwa na baadhi yenu ambao, mwanzoni, baada ya kuongea maneno maaminifu, watahisi: Nilipojiweka wazi leo ilikuwa inadhalilisha, uso wangu ulikuwa mwekundu, ilikuwa aibu sana!” Unapokutana na wengine, utajisemea: “Kila mtu anajua ni nini nilimfanyia, ni nini nilisema nyuma yake, na uwongo mdanganyifu niliosema! Mimi nimeisha. Kila mtu anajua jinsi nisivyo na thamani. Walikuwa wanafikiri nilikuwa sawa, watu wengine walikuwa na wazo nzuri kunihusu; leo, kwa kuwa nimejiweka wazi, hakuna anayefikiri mimi ni wa maana. Nifanye nini?” Lazima uombe kuhusu hii mbele ya Mungu, ukisema: “Mungu, nataka kuwa mwaminifu. Leo naweka kuwa mwaminifu katika vitendo. Nakuomba uniruhusu kuingia kwa kina zaidi, nakuomba uniruhusu kuweka kando kiburi changu, na kuniruhusu kutoongozwa na kuzuiwa na maneno haya madanganyifu na motisha danganyifu. Nataka kuisha katika mwanga, sitaki kuishi katika miliki ya Shetani na kuzuiwa na Shetani, sitaki kutawaliwa, kudhibitiwa, kuzuiwa na tabia potovu ya kishetani, au hata kuumizwa nayo.” Unapoomba kwa njia hii, kutakuwa na mwangaza zaidi ndani ya moyo wako, na utajisemea: “Ni vyema kuweka hili katika vitendo. Leo nimeweka ukweli katika vitendo—vyema! Nahisi kwamba wakati huu tu ndio naishi kama mtu halisi.” Na unapoomba hivi, je Mungu hajakupa nuru? Mungu ameanza kufanya kazi ndani ya moyo wako, Amekugusa, na kukuruhusu kuthamini jinsi inavyohisi kuwa mtu halisi. Hivi ndivyo ukweli unapaswa kuwekwa katika vitendo. Kutoka kutojua njia mwanzoni, hadi kujua njia; baada ya hapo, utalipa gharama na kuteseka, kisha upitie ugumu wa kiakili hadi utakapopata raha ya kiroho, ukihisi kuwa kumridhisha Mungu kuna umuhimu sana, kuwa faraja ya kiroho na hisia ya kutimiza unayopata baada ya kumridhisha Mungu ni muhimu sana. Wakati huo, utaelewa inamaanisha nini kuweka ukweli katika vitendo kwa kweli, utaelewa inamaanisha nini kumridhisha Mungu, na inamaanisha nini kuwa mtu halisi—na katika hii, utakuwa umechukua njia sahihi katika imani kwa Mungu.

kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni