5.30.2018

Umeme wa Mashariki | 45. Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu, Umeme wa Mashariki

45. Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika
Changkai Mji wa Benxi, mkoa wa Liaoning
Maneno ya kawaida "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho" ni ambayo mimi binafsi ninayafahamu sana. Mimi na mume wangu sote tulikuwa hasa watu wasio na hatia: Wakati wa masuala yaliyohusisha faida au hasara yetu binafsi, hatukuwa aina ya watu wa kubishana na kusumbuana na wengine. Pale ambapo tuliweza kuwa wavumilivu tulikuwa wavumilivu, pale ambapo tungeweza kuwa na fadhila tulifanya tulivyoweza kuwa na fadhila. Kama matokeo yake, mara nyingi tulijipata tukiwa tumedanganywa na kudhulumiwa na wengine. Kwa hakika ilionekana kuwa katika maisha, "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho"—iwapo una huruma nyingi sana katika moyo wako, iwapo una fadhila nyingi sana na mwenye staha katika mambo yako, uko katika hatari kuu ya kudanganywa. Nikiwa na mawazo haya katika akili yangu, niliamua kutojiingiza katika unyanyasaji huu wote na kuishi katika matatizo tena: Katika masuala ya siku zijazo na katika kujishughulisha na watu wengine, ninaapa ya kwamba sitakuwa mwenye fadhila nyingi. Hata baada ya kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu, bado nilitumia kanuni hii katika kuendesha tabia yangu na kutangamana kwangu na wengine.
Wakati mmoja, nilikuwa ninafanya kazi na dada katika kutimiza wajibu wetu. Dada huyu mara kwa mara alionyesha upungufu na dosari zangu; nilikuwa na hisia kuwa alikuwa akinivuta chini kwa kila njia. Hapo mwanzo nilifikiri kuwa: Si rahisi kuwa peke yako mbali na nyumbani, jaribu kutumia uvumilivu fulani. Baadaye, hata hivyo, baada ya dada huyu kudhibitisha kutochoka katika ukosoaji wake, mwishowe nilifikiri nyuma kuhusu maneno "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho." Ilitokea kwangu kuwa huyu dada lazima awe alitambua kuwa nilikuwa mwenye huruma sana na hivyo rahisi kuonewa na akaamua kufanya mambo kuwa magumu kwangu kwa kuyachukua masuala madogo na yasiyofaa na kuyafanya kuwa makubwa. Niliamua kuwa singekubali au kuvumilia tabia zake tena, hivyo nikakusanya nguvu zote za aina ya mwanamke aliyekasirika zilizo ndani mwangu na nikamkaripia kwa kughadhibika, nikiacha tu wakati ambapo huyu dada hakujaribu kunena neno lingine. Baadaye, dada huyu akaniambia niwasiliane naye kwa karibu na kuniambia kwa siri kuwa alikuwa ametambua kwamba jinsi alivyozungumza na kutenda ilikuwa kwa njia ya kinyama sana na alitarajia kwamba ningemsamehe. Pia alisema kwamba Mungu alikuwa amepanga hali hii na kunitumia mimi kama njia ya kumshughulikia. Niliposikia hivi, nilifurahi sana ungedhani mimi ni jenerali wa nyota nne anayetoka kwa ushindi kwa uwanja wa vita. Nini zaidi, nilishawishika hata zaidi kuwa kulikuwa na ustahili mwingi kwa maneno "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho."
Hivi karibuni tu, nilipokuwa nikisoma “Semi 100 za Shetani ambazo Watu Wapotovu Hutegemea ili Kuishi” nilichopewa na kanisa, ndio niliona kifungu kilichosema: “‘Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho.’ … Wanadamu wameharibiwa na Shetani kwa maelfu ya miaka na kuna uongo usioweza kuhesabika ambao shetani hutumia kuwatia kasumba watu. Hapa tunapeana muhtasari wa uongo 100 ambao wanadamu huchukulia kuwa wa thamani kuwaongoza maishani. Uongo huu tayari umekita mizizi katika vilindi vya mioyo ya wanadamu, wasipojihami na ukweli, kwa kiwango kikubwa wanadamu hawawezi kufichua hali ya kweli ya uongo huu. Iwapo wanadamu wataendelea kushika uongo wa Shetani kama semi na kanuni zakuishi, wanadamu wapotovu kamwe hawatawahi kupata wokovu." Baada ya kusoma kifungu hiki kutoka kwa ushirika nilipata utambuzi wa ghafla kama kwamba nimeamka kutoka kwa ndoto ndefu: Maneno "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho" yalikuwa uongo uliokuwa umetengenezwa na Shetani ili kutia kasumba na kuwaharibu wanadamu. Mungu husema kwamba katika kutangamana kwetu na wengine tunapaswa kuwa wa kukubali, kuwa na subira, wa kuvumilia, na wa kusamehe. Tunapaswa kuwa watu wa kufikiria, kuheshimu na kuwapenda wengine. Kinyume chake, kanuni ya maisha ya Shetani, "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho," kwa njia iliyo ngumu kutambua hutuelekeza mbali na uzuri na kutupeleka kwa uovu, hutufunza kutokuwa na huruma sana au wapatanishi katika kushughulika na wengine. Ili kujilinda sisi wenyewe, ni lazima tuchukue "jicho kwa jicho, jino kwa jino," ni lazima tujifunze kuwa wakorofi, wakatili na waovu. Nilitambua kwamba "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho" huonyesha uongo, ambao ni kinyume kabisa na ukweli—ni mantiki ya Shetani, ni ya uhasi wa Shetani, sumu ya joka kuu jekundu Shetani hufanya kazi kupitia "nadharia" hizi zilizo na nafasi ili kuwatia kasumba wanadamu ili kufanyiana njama, kuuana, kujihusisha katika ushindani mkali na usio na mwisho, kutotii yeyote hadi wakati hakuna ubinadamu uliobaki ndani mwao. Kwa njia hii wanadamu wanakuwa wapotovu kama shetani mwenyewe, vyombo vya kutolea dhabihu vya kuzikwa naye, na shetani hutimiza lengo lake la kupotosha na kuteketezawanadamu wote. Sikuweza kubaini uongo na nilichukulia "Wanadamu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho" kuwa ukweli wa kukubaliwa na kuheshimiwa. Nilifikiri kuwa singeweza kuwa mwenye huruma na mwenye fadhila sana, na kwamba kuwa mvumilivu au mwenye subira katika kushughulikia wengine ilikuwa njia ya wajinga na wasiojua na ingeniacha tu nikiwa katika hatari ya kudanganywa na kudhulumiwa. Kwa kuwa kila wakati nilikuwa nimechukulia uongo huu kama kanuni ya kufuatwa maishani, wakati ambapo dada alionyesha upungufu wangu ili kunisaidia kuutambua na nibadilike kuwa mzuri, sikukataa tu kukubali maoni yake, bali kwa hakika nilidhani alikuwa akinidhulumu na kuyachukua mambo madogo na kuyafanya kuwa makubwa. Matokeo yake, niliachilia unyama uliokuwa ndani yangu, nikitenda kama pepo mbaya. Hata dada aliponyenyekea kupita kiasi na kuniomba msamaha, bado sikupata kujifahamu au kuona haya, badala yake nilikaa pale nikiwa nimeridhika sana, nikifikiri kuwa dada mwishowe alikuwa "amekubali kushindwa" kwa kuwa nilikuwa nimeshikilia kanuni yangu "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho." Huku nikiwa "nimepata ushindi huu," nilihisi kuwa nimeguswa hata zaidi kushikilia na kusifu usemi huu wa Shetani. Nilikuwa mpumbavu, nilikuwa mpuzi kiasi gani! Nilikuwa nimeelewa mambo kinyume kabisa, nikichukulia uovu kuwa uzuri; kwa ufupi mtu hangeweza kuwaza na mimi! Kazi ya Mungu ya mwisho ni kutakasa binadamu kutokana na sumu ya Shetani, na kutumia ukweli kubadilisha tabia zao mbaya. Katika kisa changu mimi mwenyewe, hata hivyo, sikuwa nimeutafuta ukweli, au kutia bidii kuitambua sumu ya Shetani iliyokuwa ndani yangu, wala kufanya mazoezi ya ukweli ili kujibadilisha mwenyewe. Badala yake, nilishikia uongo wa shetani na kukataa ukweli. Iwapo ningeendelea hivyo, kamwe singewahi kuanza kujielewa mwenyewe. Kamwe singewahi kupata ukweli na kupata mabadiliko katika tabia yangu. Mwishowe, ningelazimika kuharibiwa na Mungu, kama vile hatima ya Shetani.
Asante Mungu kwa nuru na mwangaza Wako, ambao uliniruhusu kutambua kuwa usemi wa Shetani "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho" sio kitu kingine bali ni uongo ambao Shetani hutumia ili kuwatia kasumba na kuharibu wanadamu. Maneno haya hutumiwa kama kisingizio na kifaa na wanadamu wapotovu ili kuendelea kupambana mtu dhidi ya mwingine. Maneno haya ni kinyume cha ukweli, na yanaweza tu kumpotosha na kumharibu mwanadamu. Iwapo mwanadamu atapata riziki yake kutoka kwa sumu ya Shetani, iwapo atatenda kulingana na semi za Shetani, atakuwa tu maovu na mbaya zaidi. Ataendelea kupungukiwa na utu na kuzidi kumpinga Mungu, kutolewa kutoka kwa Mungu. Kamwe hatawahi kupokea wokovu wa Mungu. Mwenyezi Mungu, ninaapa kutia bidii yangu yote katika maneno Yako na katika utafutaji wangu wa ukweli, ili niweze kutambua aina nyingi za sumu ya Shetani ndani yangu, kutelekezakikamilifu uongo wa Shetani, na kamwe kutotenda tena kulingana na semi za Shetani. Ninaapa kutafuta mapenzi Yako katika masuala yote, na kulifuata neno Lako, ili neno Lako liweze kukita mizizi ndani ya moyo wangu na kuwa semi ambazo ninafuata katika kufanya mambo, viwango ambavyo ninatumia kujipima. Wacha niishi kikamilifu kulingana na neno Lako.  Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!


kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni