Sura ya 38. Yeye Ambaye Hukosa Ukweli Hawezi Kuwaongoza Wengine
Mwenyezi Mungu alisema, Je, kweli mnaelewa kuhusu mabadiliko katika tabia ya mtu? Mabadiliko katika tabia yanamaanisha nini? Je, mnaweza kutambua mabadiliko katika tabia? Ni hali zipi zinaweza kufikiriwa kuwa mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu, na ni hali zipi ambazo ni mabadiliko tu katika tabia ya nje? Tofauti ni ipi kati ya mabadiliko katika tabia ya mtu ya nje na mabadiliko katika maisha ya mtu ya ndani? Je, mnaweza kueleza tofauti? Mnamwona mtu mwenye hamu ya kukimbia pote kwa ajili ya kanisa, na mnasema: "Yeye amebadilika!"
Mnamwona mtu akiitelekeza familia yake au kazi, na mnasema: "Yeye amebadilika!" Ikiwa amejitoa mhanga kwa namna hiyo, mnafikiri kwa hakika lazima amebadilika. Hivyo ndivyo mnavyoona mambo. Watu wengine hata wana upuuzi zaidi; wao huangalia kwa makini mtu akitelekeza familia yake au kazi, na wanasema: "Lo, huyu mtu kwa kweli anampenda Mungu" Leo, mnasema mtu huyu anampenda Mungu, kesho mnasema mtu mwingine anampenda Mungu. Mkiona mtu akihubiri bila kukoma, mnasema: "Lo, huyu mtu amemjua Mungu. Amepata ukweli. Kama hakumjua Mungu, angewezaje kuwa na mengi kiasi hicho cha kusema? "Si hivyo ndivyo mnavyoyaona mambo? Hakika, hivi ndivyo wengi wenu mnavyoona watu na vitu. Daima nyinyi huwaheshimu wengine kwa mataji na kuimba sifa zao. Leo mnampa mtu taji kwa kumpenda Mungu, kesho mnampa mtu mwingine taji kwa kumjua Mungu, kwa kuwa waaminifu kwa Mungu. Nyinyi ni wataalamu katika kuwapa wengine mataji. Kila siku, nyinyi huwaheshimu wengine kwa mataji na kuimba sifa zao, na matokeo yake ni ya kuleta hasara kwao, ilhali nyinyi hata hujivunia kufanya hivyo. Mtu ambaye nyinyi humsifu amevimba kwa kiburi siku nzima na hujisemeza mwenyewe: "Lo, nimebadilika! Nitapokea taji. Nina uhakika wa mafanikio. "Je, hamuwezi kuona jinsi mnavyowachimbia shimo? Bado hawajashika mwelekeo sawa wa kuamini katika Mungu, lakini wanahisi kana kwamba tayari wamefaulu. Je, si kwa jinsi hiyo mnaathiri uharibifu wao? Ni mara ngapi mmefanya kitu cha kuogofya kama hicho? Hamuwezi kuwakimu wengine na maisha wala kuzichangua hali zao, yote mnayojua kufanya ni kuwaheshimu na mataji. Matokeo yake ni kusababisha uharibifu wao. Wewe hujui kuwa watu wapotovu hawawezi kudumisha sifa za wengine? Hata bila ya kusifiwa, watu tayari hujihisi wazuri kuliko watu wengine, vichwa vyao vikifura kwa kiburi. Mkiwasifu, si mauti yao hata yatakuja mapema? Hamjui ni nini maana ya kumpenda Mungu, kumjua Mungu, au kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa moyo wote. Hamuelewi lolote la mambo haya. Yote mnayofanya ni kutazama mambo kulingana na kuonekana kwayo, kufanya uamuzi wa haraka, kuimba nyimbo za sifa za wengine na kuwaheshimu na mataji. Mmewadhuru watu wengi sana! Mnapowasifu wengine kwa njia hii, wataanguka. Wanakuwa kinaifu, wanaanza kupendezwa na sifa zenu, na kuzungumza kwa kiburi. Kanisani, wao daima huwakaripia wengine na kufanya jeuri. Mnapofanya kazi kwa njia hii, mnawaongoza wengine kuzimu. Si nyinyi ni kama mwuaji aliye na kisu kisichoonekana? Inamaanisha nini kwa mtu kumpenda Mungu? Wale wanaompenda Mungu lazima wawe kama Petro, lazima wawe wamekamilishwa tayari, na lazima wawe wamefikia mwisho wa njia yao. Mungu tu ndiye anayeweza kufikia uamuzi wa ni nani anayempenda Yeye, na Mungu anaweza kuona ndani ya nyoyo za watu. Watu wanaweza kukosa kuwa na ufahamu kama huo, kwa hiyo wanawezaje kuwafafanua wengine? Ni Mungu peke yake anayemjua anayempenda Yeye kwa kweli. Hata kama mtu ana moyo wa kumpenda Mungu, hathubutu kusema kwamba yeye ni mtu mpenda Mungu. Mungu alisema kwamba Petro alimpenda, lakini Petro mwenyewe hakusema kuwa alikuwa mtu mpenda Mungu. Hivyo unawezaje kuwasifu wengine kikawaida sana? Huu sio wajibu wa mwanadamu. Kufanya hivyo ni kutotambua kabisa. Ni Mungu pekee anayejua ni nani anayempenda Yeye na ni Mungu pekee anayeweza kusema ni nani anayempenda Yeye. Mtu akifanya madai kama hayo, anasimama mahali pabaya. Wakati unawasifu na kuwapongeza wengine ukiwa umesimama katika nafasi ya Mungu, ni nani unayemwakilisha? Mungu hawezi kuwasifu au kuwapongeza wengine. Baada ya kumfanya Petro mtimilifu, haikuwa mpaka kuifanya hatua hii ya kazi ambapo Mungu alimtaja kuwa mfano. Wakati huo, Mungu hakuwahi kusema maneno kama hayo kwa mtu yeyote kamwe. Ni wakati tu wa kufanya hatua hii ya kazi ndipo Yeye alipotoa maoni kama hayo. Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni cha umuhimu. Ni jinsi iliyoje ya upuuzi na mzaha kwa mtu kusema kikawaida kwamba fulani ni mtu mpenda Mungu! Kwanza, wanasimama mahali pabaya. Pili, hili si la mtu kuamua. Inamaanisha nini kuimba nyimbo za sifa za watu? Inamaanisha kuwadhuru, kuwachanganya, kuwadanganya. Tatu, kuongea bila upendeleo, athari sio tu kwamba huwaweki wengine kwenye njia sahihi, lakini hata unavuruga kuingia kwao kwa kawaida na kuwaleta kwenye shida. Ukizunguka na kusema fulani anampenda Mungu, fulani ni mwaminifu kwa Mungu, au fulani amejitoa mhanga, si kila mtu atajaribu kuiiga tabia ya nje ya mtu huyo? Sio tu kwamba hukuwaweka watu kwenye njia sahihi, lakini umewaongoza wengi wao nje. Baada ya kupotoshwa kupokea taji kwa vitendo vyao vya nje, wao bila kujua huingia kwa njia ya Paulo. Si hiyo ndiyo athari? Unaposema hivi, unayajua matatizo haya? Unasimama kwa nani? Unachukua wajibu gani? Je, matokeo ya lengo ni nini? Hatimaye, umewaongoza kwa njia gani? Ni kwa kiasi gani umewanasa? Matokeo ya kazi kama hiyo ni mabaya sana. Wafanyakazi wengine wako hivyo. Sio tu kwamba hawawezi kufanya kazi ya kuwapa wale walio chini maisha, lakini vitendo vyao ni viharibifu na vya kuvuruga, vya kuwatuma watu kwenye njia ya Paulo, lakini wanafikiri wao ni viongozi wazuri na wanajivunia wenyewe. Kwa mujibu wa njia zenu za sasa, mnaweza kuwaleta wengine kwenye njia sahihi? Ni kwa njia gani hasa mnaweza kuwapeleka wengine? Je, hamwachukui wote kwenye njia ya Paulo? Jinsi Ninavyoona Mimi, hivyo kweli ndivyo ilivyo; Silo jambo la kutia chumvi. Inaweza kusemwa kuwa ninyi nyote ni viongozi wanaofanana na Paulo, kuwaongoza wengine kwenye njia ya Paulo. Na bado mnataka kupokea taji? Mtakuwa na bahati vya kutosha ikiwa hamtahukumiwa. Kwa mazoea kama hayo, mnampinga Mungu; nyinyi humtumikia Mungu, lakini humkataa Yeye na kuwa wataalamu wa kuvuruga kazi Yake. Ikiwa mtaendelea kwa njia hii, hatimaye mtakuwa wachungaji wa uongo, wafanyakazi wa uwongo, mitume wa uongo. Hii ni enzi ya mafunzo ya ufalme. Kama hamuweki juhudi katika ukweli na kulenga tu juu ya kazi yenu, mtaingia kwenye njia ya Paulo bila kujua na kuwapata wengine wengi kama Paulo. Je, si kwa hivyo mtakuwa watu wanaompinga Mungu na huingilia kazi Yake? Kwa hiyo, kama wale ambao humtumikia Mungu hawatawaelekeza watu kwa njia sahihi na kupata idhini ya Mungu, basi wao wanampinga Mungu. Hizi ni njia mbili tu. Kuna wachache ambao hufanikiwa, na wengi ambao hushindwa. Wakati wa kufanya mambo makuu, matokeo ni mafanikio makubwa au kushindwa kukubwa. Kwa nyinyi, mkiendelea kwa njia yenu ya sasa bila kugeuka, matokeo yatakuwa kushindwa kukubwa. Mtakuwa wapinga Mungu waovu, wafanyakazi wa waongo, mitume wa uongo, wachungaji wa uongo. Mkianza kuingia kwenye njia sahihi, kwa kweli kuanza njia ya Petro, basi bado mnaweza kuwa wafanyakazi wanaosifu Mungu, mitume, viongozi wazuri na wachungaji wema. Msipotafuta ukamilifu, msipotafuta kuingia ukweli wa neno la Mungu, basi mtajikuta katika hatari. Kutokana na ujinga wenu, ukosefu wa uzoefu na ukomavu, yote ambayo yanaweza kufanywa ni kuwasiliana nanyi ukweli kwa kiasi kiwezekanacho ili muweze kuelewa. Kwa sababu leo ni tofauti sana na wakati wa Petro na Paulo. Siku hizo, Yesu alikuwa bado hajafanya kazi ya kumhukumu mtu, kumwadibu mtu, au kuibadilisha tabia ya mtu. Leo, kupata mwili kwa Mungu kumeeleza ukweli kwa uwazi sana. Lakini bado nyinyi hufuata njia ya Paulo, ambayo inaonyesha kwamba uwezo wako wa kuelewa una dosari na zaidi inaonyesha kwamba, kama Paulo, wewe ni mwovu sana, na wa kujigamba sana katika tabia yako. Enzi hiyo ilikuwa tofauti na leo, na mazingira yalikuwa tofauti. Leo, neno la Mungu ni bashashi sana na wazi sana; ni kama kwamba Yeye amenyosha mkono Wake ili kukufundisha na kukuongoza. Kama bado unachukua njia mbovu, hilo kwa kweli haliwezi kutetewa. Aidha, leo, kuna watu aina mbili wa mfano mmoja, aina moja ya kujenga na moja hasi, moja mfano mwema na nyingine onyo. Ukichukua njia mbaya, inamaanisha umefanya uchaguzi mbaya. Kama wewe ni mwovu sana, basi huna yeyote wa kulaumu ila wewe mwenyewe. Ni yule tu aliye na ukweli anayeweza kuwaongoza wengine. Yeye anayekosa ukweli anaweza kuwapotosha wengine tu.
kutoka kwa Kumbukumbu
za Maongezi ya Kristo
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni