1.27.2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Utakatifu wa Mungu (III)

Mwenyezi Mungu alisema, Mnahisi vipi baada ya kusema sala zenu? (Tunafurahia na kuguswa sana.) Wacha tuanze ushirika wetu. Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini hasa mada inayohusiana na kiini cha Mungu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu. Ni nini ilikuwa dhamira kuu tuliyoshiriki wakati uliopita? (Kutambua uovu wa Shetani.) Na ni yapi tuliyoyashiriki wakati uliopita kuhusu uovu wa Shetani? Mnaweza kukumbuka? (Jinsi Shetani anampotosha mwanadamu.

1.26.2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Utakatifu wa Mungu (II)

Habari za jioni kila mtu! (Habari ya jioni Mwenyezi Mungu!) Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu “Upendo Safi Bila dosari.”)
Kiitikio: “Upendo” unarejelea hisia safi bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, hakuna mpango, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna chaguo na hakuna chochote kichafu.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Utakatifu wa Mungu (I)

Mwenyezi Mungu alisema, Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni, tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo.

1.25.2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Biblia

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Mamlaka ya Mungu (II)

Mwenyezi Mungu alisema, Leo tutaendelea na ushirika wetu kuhusu mada ya “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee.” Tayari tumekuwa na ushirika mara mbili katika mada hii, wa kwanza kuhusiana na mamlaka ya Mungu na wa pili kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika huu mara mbili, je, umepata ufahamu mpya wa utambulisho wa Mungu, hadhi, na hali halisi? Je, maono haya yamekusaidia kufikia maarifa mazito zaidi na uhakika wa ukweli kuuhusu uwepo wa Mungu? Leo Ninapanga kufafanua mada hii ya “Mamlaka ya Mungu.”

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tabia ya Haki ya Mungu

Kwa vile sasa mumesikiliza kikao cha ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mumejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kushika, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo-upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe kwa upekee wake, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango kuu la kujua hali halisi ya ule upekee wa Mungu Mwenyewe. Ufahamu huu ni sehemu moja ya kumjua Mungu. Sehemu ile nyingine ni nini, hivyo basi? Hii ndiyo mada ambayo Ningependa tuweze kushiriki pamoja leo—tabia ya haki ya Mungu.

1.24.2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Mungu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Mamlaka ya Mungu (I)


Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? 

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Umeme wa Mashariki, Biblia, Mungu

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III


Mwenyezi Mungu alisema, Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa kwa kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wamemwani Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa.

1.23.2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II
Kwenye mkutano wetu wa mwisho tuliweza kuzungumzia mada muhimu sana. Je, wakumbuka mada hiyo ilikuwa kuhusu nini? Hebu Niirudie. Mada ya ushirika wetu wa mwisho ilikuwa: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Je, mada hii ni muhimu kwako? Ni sehemu gani katika mada hii ni muhimu kwako? Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, au Mungu Mwenyewe? Ni sehemu ipi inakuvutia zaidi? Ni sehemu ipi unayotaka kusikiliza kuhusu zaidi? Najua ni vigumu kwako wewe kulijibu swali hilo, kwa sababu tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika kila kipengele cha kazi Yake, na tabia Yake inafichuliwa katika kazi Yake siku zote na pahali pote, na, kutokana na hayo, inawakilisha Mungu Mwenyewe; kwenye mpango wa usimamizi wa ujumla wa Mungu, kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe vyote hivi haviwezi kutenganishwa.

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila mtu. Kwa maneno mengine, hili ni suala ambalo kila mmoja atakutana nalo kwenye mchakato wote wa kusadiki kwake katika Mungu na suala ambalo lazima lizungumziwe. Ni suala muhimu, lisiloepukika ambalo mwanadamu hawezi kujitenganisha nalo.

1.22.2018

Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watii kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini.

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu


MwenyeziMungu alisema, Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa.

1.21.2018

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huifahamu kamwe kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi.