5.06.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Tatu Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu VyoteI



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote(I)

Kwa mara nyingine tena Nitatumia njia ya kusimulia hadithi, ambayo ninyi nyote mnaweza kusikiliza mkiwa kimya na kutafakari juu ya kile Ninachokizungumzia. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi, nitawauliza maswali kuona mmeelewa kiasi gani. Wahusika wakuu katika hadithi ni mlima mkubwa, kijito kidogo, upepo mkali, na wimbi kubwa.

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa

Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa.

5.05.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Sehemu ya Nne Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu VyoteI


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote(I)

Kusudi la mjadala wetu wa haya mambo ni nini? Je, ni ili kwamba watu waweze kutafiti kanuni zilizopo kwenye uumbaji wa Mungu wa ulimwengu? Je, ni ili kwamba watu wavutiwe na falaki na jiografia? (Hapana.) Sasa ni nini? Ni ili kwamba watu wataelewa matendo ya Mungu. Katika matendo ya Mungu, watu wanaweza kukubali na kuthibitisha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kama unaweza kuielewa hoja hii, basi utaweza kuthibitisha kweli nafasi ya moyoni mwako na utaweza kuthibitisha kwamba Mungu ni Mungu Mwenyewe wa kipekee, Muumbaji wa mbingu na nchi na vitu vyote. Hivyo, je, inasaidia katika uelewa wako juu ya Mungu kujua kanuni za vitu vyote na kujua matendo ya Mungu? (Ndiyo.) Inasaidiaje?

5.04.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Kwanza



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Kwanza

Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Je, “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Je, una ufahamu wowote wa juujuu kuhusu jambo hilo? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu.

5.03.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Pili



   Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Pili

Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu

3. Sauti

Kitu cha tatu ni nini? Ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Ni kitu ambacho Mungu alishughulikia alipoumba vitu vyote. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kila mtu. Kama Mungu hakushughulikia suala hilo, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Pia inaweza kusemwa kwamba viumbe vyote vyenye uhai haviwezi kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Hivyo hiki ni kitu gani? Ni sauti.

5.02.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Tatu



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Nne

Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu

Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia. Watu wengi huuliza: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? (Kuku.) Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hilo ni hakika! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingetangulia? Je, kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Mayai huangua kuku, kuku huatamiza mayai. Baada ya kuatamiza mayai kwa siku 21, kuku huangua. Kisha kuku huyo hutaga mayai, na kuku huanguliwa tena kutoka kwa mayai. Hivyo kuku alitangulia au yai lilitangulia? Mnajibu "kuku" kwa uhakika.

5.01.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote II Sehemu ya Nne



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Sehemu ya Nne

Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu

Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia. Watu wengi huuliza: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? (Kuku.) Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hilo ni hakika! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingetangulia? Je, kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Mayai huangua kuku, kuku huatamiza mayai.

4.30.2019

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Kwanza



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Kwanza
     Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya hii. Ni mada gani? (Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Inaonekana yale mambo na mada niliyoyazungumzia yaliwachia kila mtu wazo dhahiri. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao.

4.29.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote III Sehemu ya Pili




Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Pili


       Ikiwa viumbe vyote vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za viumbe vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa viumbe vyote visingeweza kuendelea. Binadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wamepoteza hiyo yote, wasingeweza kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya binadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia binadamu viumbe vyote kuwalea, kuwalea binadamu kwa namna tofauti. Ni kwa sababu tu Mungu anawalea binadamu kwa namna tofauti ndio maana wameendelea kuishi mpaka sasa, kwamba wameendelea kuishi hadi siku ya leo.

4.28.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote III Sehemu ya Tatu




Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Tatu

Mungu anaweka Uwiano Kati ya Vitu Vyote ili Kumpatia Binadamu Mazingira Imara kwa ajili ya Kuendelea Kuishi
       Mungu anadhihirisha matendo Yake miongoni mwa vitu vyote na miongoni mwa vitu vyote Anavyovitawala na Anashikilia sheria za vitu vyote. Tumemaliza kusema juu ya jinsi ambavyo Mungu anatawala sheria za vitu vyote vilevile jinsi ambavyo Anawakimu na kuwalea binadamu wote ndani ya sheria hizo. Hiki ni kipengele kimoja. Kinachofuata, tutazungumza juu ya kipengele kingine, ambacho ni njia moja ambayo Mungu ana udhibiti wa kila kitu. Hivi ndivyo, baada ya kuumba vitu vyote, Akaweka uwiano wa uhusiano kati yao.

4.27.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Kwanza



         Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Kwanza


Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe? Na kwa nini Ninawapa uchaguzi huu? Kwa sababu leo Ninafikiria kufanya ushirika nanyi juu ya mambo mapya kuhusu kumjua Mungu. Lakini, hata hivyo, kwanza nitawaacha mchague kimoja kati ya vitu viwili ambavyo Nimezungumzia hivi punde.

4.26.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Pili



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Pili

Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho



1. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini

       Kwa roho yoyote, kupata kwake mwili mpya na nafasi anayochukua—nafasi yake ni ipi katika haya maisha—atazaliwa katika familia gani, na maisha yake yatakuwaje vinahusiana kwa karibu na maisha yake ya zamani. Kila aina ya watu huja katika dunia ya wanadamu, na nafasi zao ni tofauti, kama zilivyo kazi wazifanyazo. Na hizi ni kazi gani? Watu wengine wanakuja kulipa deni: Ikiwa walikuwa na pesa nyingi za watu katika maisha yao ya awali, wanakuja kulipa deni.

4.25.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Tatu


     

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Tatu
Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho


3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu

Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache.