11.13.2019

Ni thawabu ipi inayopewa wanawali wenye hekima? Wanawali wapumbavu wataanguka katika maafa?

Ni thawabu ipi inayopewa wanawali wenye hekima? Wanawali wapumbavu wataanguka katika maafa?
  Maneno Husika ya Mungu:
“Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu” kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao.
Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli. Wale ambao huondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu wasioweza kufuata kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na ambao huasi dhidi ya kazi ya karibuni zaidi ya Mungu. Kwamba watu hao humpinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu picha ya Mungu si sawa na ile iliyo ndani ya dhana zao—kutokana na hilo wao humpinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, kusababisha wao kuchukiwa na kukataliwa na Mungu. Kuwa na ufahamu wa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu si jambo rahisi, lakini kama watu wanaweza kutii kazi ya Mungu kwa kudhamiria na kuitafuta kazi ya Mungu, basi watakuwa na nafasi ya kumwona Mungu, na watakuwa na nafasi ya kupata uongozi mpya zaidi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao hupinga kazi ya Mungu kwa kudhamiria hawawezi kupata nuru ya Roho mtakatifu au uongozi wa Mungu; hivyo, kama watu wanaweza kupokea kazi ya karibuni zaidi ya Mungu au la hutegemea neema ya Mungu, hutegemea ukimbizaji wao, na hutegemea makusudi yao.

  Wale wote ambao huweza kutii matamshi halisi ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Haijalishi vile walikuwa, au vile Roho Mtakatifu alikuwa akifanya kazi ndani yao—wale ambao wamepata kazi ya karibuni zaidi ni waliobarikiwa zaidi, na wale ambao hawawezi kufuata kazi ya karibuni zaidi huondoshwa. Mungu anataka wale wanaoweza kukubali nuru mpya, na Anataka wale ambao hukubali na kujua kazi Yake ya karibuni zaidi. Kwa nini husemwa kwamba lazima uwe mwanamwali safi? Mwanamwali safi anaweza kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu na kuelewa mambo mapya, na zaidi ya hayo, kuweza kuweka kando dhana za zamani, na kutii kazi ya Mungu leo. Kundi hili la watu, ambao hukubali kazi mpya zaidi ya leo, walijaaliwa na Mungu kabla ya enzi, na ni ambao wamebarikiwa zaidi ya watu wote. Ninyi huisikia sauti ya Mungu moja kwa moja, na kutazama kuonekana kwa Mungu, na hivyo, kotekote mbinguni na duniani, na kotekote katika enzi, hakuna waliobarikiwa kuliko ninyi, hili kundi la watu.

  kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

  Wakati umepitia matukio yote ya kazi ya Mungu mwenye mwili katika Enzi ya Ufalme, utahisi kwamba matumaini ya miaka mingi hatimaye yametimika. Utahisi kwamba ni sasa tu ndipo umemwona Mungu uso kwa uso; ni sasa tu ndipo umeutazama uso wa Mungu, umesikia matamshi ya Mungu Mwenyewe, umeifahamu hekima ya kazi ya Mungu, na kuhisi kwa kweli jinsi Mungu ni wa kweli na mwenye nguvu. Utafahamu kuwa umepata vitu vingi ambavyo watu wa nyakati zilizopita hawajawahi kuviona wala kuwa navyo. Wakati huu, utajua kwa uhakika ni nini hasa kuamini katika Mungu, na ni nini kupendeza nafsi ya Mungu. Bila shaka, ukikwamilia maoni ya kitambo, na ukatae au ukane ukweli wa kupata mwili kwa Mungu mara ya pili, basi utabaki mkono mtupu na hutapata chochote, na mwishowe utakuwa na hatia ya kumpinga Mungu. Wale wanaotii ukweli na kunyenyekea kwa kazi ya Mungu watakuja chini ya jina la Mungu mwenye mwili wa pili—Mwenyezi. Wataweza kukubali uelekezi binafsi wa Mungu, na watapata ukweli zaidi na wa juu zaidi na watapokea maisha ya kweli ya mwanadamu. Wataona maono ambayo watu wa zamani hawajawahi kuona kamwe: “Na nikapinduka ili kuiona sauti hiyo iliyonizungumzia. Na baada ya kupinduka, nikatazama vinara saba vya taa vilivyokuwa vya dhahabu; Na hapo katikati ya hivyo vinara saba vya taa nilimwona mtu aliyefanana na Mwana wa Adamu, aliyekuwa amevalia nguo iliyofika katika miguu yake, na kifuani alikuwa amefungwa kanda ya dhahabu. Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye” (Ufunuo 1:12-16). Maono haya ni maonyesho ya tabia kamilifu ya Mungu, na maonyesho ya aina hii ya tabia Yake nzima pia ndiyo maonyesho ya kazi ya Mungu Anapopata mwili mara hii. Katika mibubujiko ya kuadibu na hukumu, Mwana wa Adamu Anaonyesha tabia Yake ya asili kupitia kuzungumza kwa maneno, Akiwaruhusu wale wote wanaokubali kuadibu Kwake na hukumu kuuona uso wa kweli wa Mwana wa Adamu, uso ulio mfano wa kuaminika wa Mwana wa Adamu Alivyooneka na Yohana. (Bila shaka, yote haya hayatawaonekania wote wasioikubali kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.) Uso wa kweli wa Mungu hauwezi kuelezwa kikamilifu na maneno ya mwanadamu, na hivyo Mungu Hutumia maonyesho ya tabia Yake asili kuuonyesha uso Wake wa kweli kwa mwanadamu. Ambayo ni kusema wote ambao wamepitia tabia asili ya Mwana wa Adamu wameuona uso wa kweli wa Mwana wa Adamu, kwa kuwa Mungu ni mkuu zaidi na Hawezi kuelezwa kikamilifu na maneno ya mwanadamu. Mara tu mwanadamu amepitia kila hatua ya kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme, basi atapata kujua maana kamili ya maneno ya Yohana alipozungumza kuhusu Mwana wa Adamu kati ya vinara vya taa: “Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye.” Wakati huo, utajua bila shaka yoyote kwamba mwili huu wa kawaida uliozungumza maneno mengi ni kwa hakika Mungu mwenye mwili mara ya pili. Na utahisi ni jinsi gani kwa kweli umebarikiwa, na kujiona mwenyewe kama mwenye bahati kubwa. Je, ungekuwa huna radhi kuikubali baraka hii?

  kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili

  Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayeidaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Utaashiria mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi, na utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu?

 kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili

  Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha.

  kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

  Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

  Katika siku za mwisho, Mungu anapata mwili na kushuka kwa siri kati ya binadamu kutamka na kuongea, Akifanya kazi ya hukumu Akianzia na nyumba ya Mungu, Akiwatakasa na kuwakamilisha wote ambao wanao sikia sauti Yake na kurudi mbele ya kiti Chake cha enzi. na kuwafanya katika kikundi cha washindi. Kisha Mungu analeta maafa makubwa, Akiwasafisha na kuwaadibu wale wote ambao hawakukubali hukumu ya Mungu ya siku za mwisho. Baadaye, Mungu atashuka na mawingu Akionekana kwa wazi mbele ya binadamu wote. Hiyo basi itatimiza kikamilifu unabii katika Ufunuo 1:7: “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye.” Wakati Bwana atashuka na mawingu, wale waliomchoma watamwona Yeye bado? Ni akina nani hasa ndio walimchoma? Wengine wanasema ni waliomsulubisha Bwana Yesu msalabani. Je, hiyo ndiyo hali? Je, si watu waliomsulubisha Bwana Yesu walilaaniwa na kuangamizwa na Mungu kitambo sana? Kwa kweli, wale ambao walimchoma Yeye ni wale ambao, katika wakati ambao Mungu mwenye mwili ameshuka kwa siri katika siku za mwisho kufanya kazi, hawatafuti sauti ya Mungu na kumshutumu na kumkataa Mwenyezi Mungu. Kwa wakati huo, watamwona Mwenyezi Mungu ambaye walimkataa na kumshutumu ni hasa Yule Mwokozi Yesu waliyekuwa wakimngoja kwa uchungu kwa miaka hii zote. Watapiga vifua vyao, watoe machozi na kusaga meno yao, na matokeo yao yanaweza tu kuwa adhabu. Kitabu cha Ufunuo hakisemi kama watu wa aina hii wataishi ama watakufa mwishowe, hivyo basi hatuwezi kujua kwa kweli. Ni Mungu pekee Ajuaye. Kila mtu anafaa kuwa wazi. Bikira wenye busara tu ambao wanasikia sauti ya Mungu ndio wanaweza kupata nafasi ya kukaribisha kurudi kwa Bwana, waletwe mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kuhudhuria chajio ya ndoa ya Mwanakondoo, na kukamilishwa na Mungu kuwa washindi. Hii inatimiza unabii katika Ufunuo 14:4, “Hao ndio wale hawakunajisiwa na wanawake; kwani wao ni bikira. Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo.” Kwa wale ambao walishikilia tu wazo kuwa Bwana atashuka na mawingu lakini hawatafuti na kuchunguza kazi ya Bwana ya siku za mwisho, wanachukuliwa kuwa bikira wajinga. Hasa wale ambao wanamkataa kwa nguvu na kumshutumu Mwenyezi Mungu, hao ni Mafarisayo na maadui wa Kristo wanaowekwa wazi na kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Ni watu wote ambao wamesulubisha Mungu tena. Hawa watu wote wataanguka kwenye maafa makubwa na kupokea adhabu.

  kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

  Leo neno la Mungu limeenezwa na kushuhudiwa, na ninyi ni kundi la kwanza la watu kutoka mataifa yote, kutoka kwa dini zote kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Ninyi ndio mliobarikiwa zaidi. … Kwanza, mmekubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa sababu mmeona kwamba Bwana Yesu amerudi, kwamba Yeye amepata mwili kama Mwana wa adamu, akionyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa hiyo kukubali kwenu kunamaanisha mmenyakuliwa, mmenyakuliwa juu mbele za Mungu. Mmeinuliwa juu hewani kukutana na Bwana. “Hewa” hii inamaanisha nini? Kueneza injili kuwapata watu na kuzungumza mtandaoni, je, hiyo si “hewani”? “Hewa” iko wapi? “Hewa” ni sitiari, na inawakilisha suala la iwapo tuko mbinguni ama duniani. Kuzungumza neno kwa neno kabisa, tuko duniani, lakini tunafurahia maisha kandokando ya Mungu na tunakula na kunywa neno la Mungu, ambalo ni maji ya mto wa uhai unaotiririka kutoka kwa kiti cha enzi, kwa hiyo tunaishi kana kwamba tuko katika mbingu ya tatu. Kulingana na umuhimu wake halisi, tuko wapi? Je, tuko mbinguni, au duniani? Ni vigumu kusema, kwa hiyo tunatumia “hewani” kulieleza. Leo, umenyakuliwa mbele ya kiti cha Mungu cha enzi ili kushiriki katika karamu na Mwanakondoo, ambayo ni kushiriki katika karamu na Mungu. Pili, umepata fursa ya kukamilishwa na Mungu katika siku za mwisho. Ikiwa umetakaswa na kukamilishwa kupitia hukumu na kuadibu mbele ya kiti cha Kristo, utastahili kupata idhini ya Mungu. Baraka kubwa kweli! Tumepata kile ambacho watakatifu katika enzi zote walitamani sana kupata lakini wengi wao walikosa kupata. Je, sisi si wenye bahati zaidi? Tatu, tunapitia kuadibu na hukumu ya Mungu, kupogolewa na kushughulikwa, na kurudiwa na kufundishwa nidhamu. Ingawa kunateseka kiasi mioyoni mwetu na linaweza kuhisi kuwa jambo la kutia aibu mwanzoni, mwishowe tutapata kitu. Yaani, tutatimiza matokeo ya kutakaswa, ya kuelewa ukweli na kumjua Mungu. Ingawa tunaporudiwa tunaweka kando heshima na hadhi yetu, tukijisujudu na kulia kwa uchungu, kukiri dhambi zetu na kutubu, lakini baada ya kupitia kipindi cha usafishaji kama hicho, tunaanza kuishi kwa kudhihirisha mfano halisi wa binadamu. Tunakuwa wa maana zaidi na zaidi, dhamiri yetu inazinduka, roho zetu zinachangamka, na tunamwona Mungu. Tunakuwa na hakika kabisa kuhusu njia hii, na njia yetu inakuwa angavu zaidi na zaidi hadi hatimaye tunajiweka katika njia ya kukamilishwa na tunakuwa washindi. Ni nini maana ya kuwa washindi? Inamaanisha kutopitia mateso ya maafa makubwa; yanapofika, “Watu elfu wataanguka kando yako, na elfu kumi katika mkono wako wa kulia; lakini haitakuja karibu na wewe” (Zaburi 91:7). Je, hii si baraka kubwa? Wasioamini na watu wa dini watajipata katika maafa, na wakati tunaweza kuonekana kuwa katikati ya maafa sisi wenyewe, Mungu yuko nasi, kwa hiyo maafa hayatatupata. Ikiwa kweli umepata ukweli, nakwambia, hutaonja kifo. Maneno haya ni ya kweli. Ahadi ya Mungu ya siku za mwisho, baraka kubwa zaidi, zitatimizwa juu yetu.

  kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha, Juzuu ya 130


Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni