11.23.2019

Drama ya Muziki "Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19"

 

 Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki "Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19"

Chini ya mbingu ya usiku yenye nyota, tulivu na kimya, kundi la Wakristo wanasubiri kwa ari kurudi kwa Mwokozi wakiimba na kucheza kwa muziki mchangamfu.Wanaposikia habari za furaha "Mungu amerejea" na "Mungu ametamka maneno mapya", wanashangaa na kusisimka.
Wanafikiri: "Mungu ameonekana? Tayari ametokea?" Kwa udadisi na kutokuwa na uhakika, mmoja baada ya mwingine, wanaingia katika safari ya kuyatafuta maneno mapya ya Mungu. Katika kutafuta kwao kugumu, baadhi ya watu wanauliza maswali hali wengine wanalikubali tu. baadhi ya watu wanaangalia bila kutoa maoni, wakati wengine wanafanya mapendekezo na kutafuta majibu katika Biblia–wanaangalia lakini mwishowe kuangalia huku hakuzai matunda .... Wakati tu wanapokata tamaa, shahidi mmoja anawaletea nakala ya Biblia ya Enzi ya Ufalme, na wanavutiwa kwa kina na maneno yaliyomo katika kitabu. Hiki ni kitabu cha aina gani kweli? Je, kwa kweli wamepata maneno mapya ambayo Mungu ameyanena katika kitabu hiki? Je, wamekaribisha kwa furaha kuonekana kwa Mungu?

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni