6.07.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III Sehemu ya Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

Sasa hebu tusome dondoo za maandiko zilizo hapa chini.

12. Maneno ya Bwana Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake


Yohana 20:26-29 Na kufuatia siku nane tena wanafunzi wake walikuwa ndani, naye Tomaso alikuwa nao: kisha Yesu akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati, na kuema, Amani iwe nanyi. Kisha akasema kwa Tomaso, nyoosha kidole chako hapa, na uitazame mikono yangu, nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani. Naye Tomaso akajibu na kumwambia, BWANA Wangu na Mungu wangu. Yesu akasema kwake, Tomaso, kwa sababu umeniona, umeamini, wamebarikiwa wale ambao hawajaona, lakini wameamini.

Yohana 21:16-17 Akasema kwake tena mara ya pili, Simioni, mwana wa Yona, unanipenda mimi? Akasema kwake, Ndiyo, Bwana, unajua kwamba mimi nakupenda. Akasema kwake, Walishe kondoo wangu. Akasema kwake mara ya tatu, Simioni, mwana wa YONA, Unanipenda Mimi? Petro alisikitika kwa sababu alimwambia mara ya tatu, Unanipenda Mimi? Na akamwambia, Bwana, wewe unajua vitu vyote, unajua kwamba mimi nakupenda. Yesu akamwambia, Walishe kondoo wangu.

Kile ambacho dondoo hizi zinasimulia ni baadhi ya mambo ambayo Bwana Yesu alifanya na kusema kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka Kwake. Kwanza, hebu tuangalie tofauti zozote kati ya Bwana Yesu kabla na baada ya kufufuka Kwake. Alikuwa bado ni yule yule Bwana Yesu wa siku za kale? Maandiko yanao mstari ufuatao unaomfafanua Bwana Yesu baada ya kufufuka kwake: "kisha Yesu akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati, na kuema, Amani iwe nanyi." Ni wazi sana kwamba Bwana Yesu wakati huo hakuwa tena mwili, lakini alikuwa katika umbo la kiroho. Hii ni kwa sababu Alikuwa amepita ile mipaka ya mwili, na wakati ambapo mlango ulifungwa Aliweza bado kuja katikati ya watu na kuwaruhusu wao kumwona Yeye. Hii ndiyo tofauti kubwa zaidi kati ya Bwana Yesu baada ya kufufuka na Bwana Yesu aliyeishi kwa mwili kabla ya kufufuka. Hata ingawa hakukuwa na tofauti yoyote kati ya kutokea kwa ule mwili wa kiroho wa wakati huo na dhihirisho la Bwana Yesu kutoka awali, Yesu katika muda huo alikuwa amekuwa Yesu aliyehisi na kujioa mgeni kwa watu, kwa sababu Alikuwa amekuwa mwili wa kiroho baada ya kufufuka kutoka kwa wafu, na Akilinganishwa na mwili Wake wa awali, mwili huu wa kiroho ulikuwa wa kushangaza na kuchanganya kwa watu zaidi. Hali hii iliunda nafasi kubwa zaidi kati ya Bwana Yesu na watu, nao watu wakahisi katika mioyo yao kwamba Bwana Yesu wa wakati huo alikuwa haeleweki kabisa. Ufahamu na hisia hizi kwa upande wa watu ghafla uliwarudisha katika enzi ya kuamini kwa Mungu ambaye hakuweza kuonekana wala kugusika. Hivyo basi, kitu cha kwanza ambacho Bwana Yesu alifanya baada ya kufufuka Kwake kilikuwa kuruhusu kila mmoja kuweza kumwona, kuthibitisha kuwa yupo, kuthibitisha hoja ya kufufuka Kwake. Kuongezea hayo, hali hiyo ilirejesha uhusiano Wake na watu hadi ule uhusiano Aliokuwa nao Alipokuwa akifanya kazi kupitia kwa mwili, na Alikuwa Kristo ambaye wangeweza kuona na kugusa. Kwa njia hii, mojawapo ya matokeo ni kwamba watu hawakuwa na shaka kwamba Bwana Yesu alikuwa amefufuka kutoka kwa kifo baada ya kusulubishwa msalabani, na hakukuwa na shaka katika kazi ya Bwana Yesu ya kuwakomboa wanadamu. Na matokeo mengine ni kwamba hoja ya Bwana Yesu kujitokeza kwa watu baada ya kufufuka Kwake na kuwaruhusu watu kuweza kumwona na kumgusa Yeye kwa udhabiti kuliweza kuwasalimisha wanadamu katika Enzi ya Neema. Kuanzia wakati huu, watu hawakuweza kurudi katika enzi ya awali, Enzi ya Sheria, kwa sababu ya "kutoweka" au "kuacha na kuondoka" kwa Bwana Yesu lakini wangeendelea mbele, kufuata mafundisho ya Bwana Yesu na kazi Aliyokuwa amefanya. Hivyo basi, awamu mpya katika kazi ya Enzi ya Neema iliweza kufunguliwa rasmi na watu waliokuwa katika sheria walikuja rasmi kutoka katika sheria kuanzia hapo kuenda mbele, na kuingia katika enzi mpya, katika mwanzo mpya. Hizi ndizo maana nyingi za kujitokeza kwa Bwana Yesu kwa wanadamu baada ya kufufuka Kwake.

Kwa sababu Alikuwa mwili wa kiroho, watu waliwezaje kumgusa Yeye na kumwona Yeye? Hii inahusu umuhimu wa kujitokeza kwa Bwana Yesu kwa wanadamu. Je, mlitambua chochote katika dondoo hizi za maandiko? Kwa ujumla miili ya kiroho haiwezi kuonekana wala kuguswa, na baada ya kufufuka, kazi ambayo Bwana Yesu alikuwa amechukua tayari ilikuwa imekamilika. Hivyo basi, kinadharia Hakuwa na haja kabisa ya kurudi katikati ya watu akiwa katika taswira Yake ya asili ili kukutana na wao, lakini kujitokeza kwa mwili wa kiroho wa Bwana Yesu kwa watu kama vile Tomaso kulifanya umuhimu wake kuwa thabiti zaidi, na hali hii iliweza kupenyeza zaidi kwa kina katika mioyo ya watu. Alipomjia Tomaso, alimwacha Tomaso aliyekuwa akishuku kumgusa mkono Wake na kumwambia maneno haya: "nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani." Maneno haya, vitendo hivi vyote havikuwa vitu ambavyo Bwana Yesu alitaka kusema na kufanya tu baada ya Yeye kufufuka, lakini yalikuwa mambo Aliyotaka kuyafanya kabla ya kusulubishwa msalabani. Ni wazi kwamba Bwana Yesu ambaye alikuwa hajasulubishwa katika msalaba tayari alikuwa na ufahamu wa watu kama Tomaso. Hivyo basi, tunaweza kuona nini kutokana na haya? Alikuwa angali Bwana Yesu yule yule hata baada ya kufufuka Kwake. Kiini chake kilikuwa hakijabadilika. Kushuku kwa Tomaso hakukuwa kumeanza tu lakini kulikuwa ndani yake muda wote aliokuwa akimfuata Bwana Yesu, lakini Alikuwa Bwana Yesu aliyekuwa amefufuka kutoka kwa kifo na alikuwa amerudi kutoka katika ulimwengu wa kiroho akiwa na taswira Yake asilia, na tabia Yake binafsi, na kwa ufahamu huu wa wanadamu kutoka kwa wakati Wake akiwa mwili, kwa hivyo basi Alienda kumfuta Tomaso kwanza, ili kumfanya Tomaso kugusa mbavu Zake, kumfanya kutoona tu mwili Wake wa kiroho baada ya kufufuka, lakini pia kumruhusu auguse na kuuhisi uwepo wa mwili Wake wa kiroho, na kutupilia mbali kabisa shaka zake. Kabla ya Bwana Yesu kusulubishwa msalabani, Tomaso siku zote alishuku kwamba Yeye ni Kristo, na hakuweza kuamini. Imani yake katika Mungu ilianzishwa tu kwa msingi wa kile ambacho angeweza kuona kwa macho yake, kile ambacho angeweza kugusa kwa mikono yake. Bwana Yesu alikuwa na ufahamu mzuri wa imani ya mtu wa aina hii. Waliamini tu katika Mungu wa mbinguni, na hawakuamini kamwe, na wasingekubali Yule Aliyetumwa na Mungu, au Kristo katika mwili. Ili kufanya yeye kuweza kutambuliwa na kuaminiwa katika uwepo wa Bwana Yesu na kwamba kweli Alikuwa Mungu mwenye mwili, Alimruhusu Tomaso kuunyosha mkono wake na kugusa ubavu Wake. Je, Tomaso alikuwa akishuku kwa njia tofauti kabla na baada ya kufufuka kwa Bwana Yesu? Alikuwa daima akishuku, na mbali na mwili wa kiroho wa Bwana Yesu kujitokeza binafsi kwake na kumruhusu Tomaso kugusa alama za misumari katika mwili Wake, hakuna aliyeweza kutatua shaka zake, na hakuna mtu ambaye angemfanya kuziachilia. Hivyo basi, kuanzia muda ambao Bwana Yesu alimruhusu kuugusa ubavu Wake na kumwacha akihisi uwepo wa alama za misumari, shaka ya Tomaso ikatoweka na akajua kwa kweli kwamba Bwana Yesu alikuwa amefufuka na akatambua na kuamini kwamba Bwana Yesu ndiye aliyekuwa Kristo wa kweli, na kuamini kwamba alikuwa Mungu mwenye mwili. Ingawa wakati huu Tomaso hakushuku tena, alikuwa amepoteza milele fursa ya kukutana na Kristo. Alikuwa amepoteza milele fursa ya kuwa pamoja na Yeye, kumfuata Yeye, na kumjua Yeye. Alikuwa amepoteza fursa ya Kristo kumfanya yeye kuwa mtimilifu. Kuonekana kwa Bwana Yesu na maneno Yake yalitoa hitimisho, na hukumu kuhusiana na imani ya wale ambao walijawa na kutoamini kwingi. Alitumia maneno na vitendo Vyake halisi kuwaambia wale waliokuwa wakishuku, kuwaambia wale ambao waliamini tu katika Mungu aliye juu mbinguni lakini amini hawakumwamini Kristo: Mungu hakuitukuza imani yao, wala Hakuupongeza ufuasi wao uliojawa na shaka. Ile siku waliamini kikamilifu Mungu naye Kristo angeweza tu kufanya hivyo siku ile ambayo Mungu alikuwa akamilishe kazi Yake kuu. Bila shaka, siku hiyo ndiyo iliyokuwa siku ambayo kushuku kwao kulipokea uamuzi. Mwelekeo wao katika Kristo uliamua majaliwa yao, na kushuku kwao katika usumbufu kulimaanisha imani yao haikuwapatia matokeo yoyote, na ugumu wao kulimaanisha matumaini yao yaliambukia patupu. Kwa sababu imani yao katika Mungu aliye mbinguni ilisababishwa na njozi, na kushuku kwao katika Kristo kulikuwa kwa kweli mwelekeo wao wa kweli kwa Mungu, hata ingawa walizigusa alama za msumari kwenye mwili wa Bwana Yesu, imani yao ilikuwa bado bure bilashi na matokeo yao yangeweza tu kufafanuliwa kama kuufukuza upepo—ya bure bilashi. Kile Bwana Yesu Alichomwambia Tomaso kilikuwa kikisema hivyo waziwazi kwa kila mtu: Yule Bwana Yesu aliyefufuka ndiye Bwana Yesu ambaye mwanzo alikuwa ametumia miaka thelathini na mitatu na nusu akifanya kazi miongoni mwa wanadamu. Ingawa alikuwa amesulubishwa msalabani na kupitia bonde la kivuli cha mauti, alikuwa amepitia kitendo cha kufufuka, kila dhana Yake haikuwa imepitia mabadiliko. Ingawa kwa sasa alikuwa na alama za misumari kwenye mwili Wake, na ingawa Alikuwa amefufuka na kutoka kaburini akitembea, tabia Yake, ufahamu Wake wa wanadamu na nia Zake kwa wanadamu bado zilikuwa hazijabadilika hata kidogo. Pia, Alikuwa akiwaambia watu kwamba Alikuwa ameshuka kutoka kwenye msalaba, ameshinda dhambi, amepata ushindi juu ya ugumu, na akupata ushindi dhidi ya kifo. Alama zile za misumari zilikuwa tu ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani, ithibati ya kuwa sadaka ya dhambi ili kuweza kuwakomboa kwa ufanisi wanadamu wote. Alikuwa akiwaambia watu kwamba tayari Alikuwa ameanza kushughulikia dhambi za wanadamu na Alikuwa amekamilisha kazi Yake ya ukombozi. Aliporudi ili kuwaona wanafunzi Wake, Aliwaambia kwa kuonekana Kwake: "Mimi niko hai, bado Nipo; leo kwa kweli nasimama mbele yenu ili mweze kuniona na kunigusa Mimi. Siku zote nitakuwa na wewe." Bwana Yesu alitaka pia kutumia mfano huo wa Tomaso kama onyo kwa watu wa siku za usoni: Ingawa unaamini Bwana Yesu, huwezi kumwona wala kumgusa Yeye, na bado, unaweza kubarikiwa kutokana na imani yako ya kweli, na unaweza kumwona Bwana Yesu kupitia kwa imani yako ya kweli; mtu aina hii amebarikiwa.

Maneno haya yaliyorekodiwa katika Biblia ambayo Bwana Yesu aliongea Alipojitokeza kwa Tomaso ni msaada mkubwa kwa watu wote katika Enzi ya Neema. Kuonekana Kwake na maneno Yake kwa Tomaso yamekuwa na athari kubwa kwa vizazi vijavyo, na yatakuwa na umuhimu wa kudumu daima dawamu. Tomaso anawakilisha mtu wa aina ya kuamini Mungu ilhali anamshuku Mungu. Wao wanayo maumbile ya kushuku, wana mioyo isiyoeleweka, wao wenyewe ni wadanganyifu, na hawaamini mambo ambayo Mungu anaweza kukamilisha. Hawaamini katika kudura ya Mungu na utawala Wake, na hawaamini katika Mungu kuwa mwili. Hata hivyo, kufufuka kwa Bwana Yesu kulikuwa ni sawa na kuzabwa kofi katika nyuso zao, na pia kuliwapa fursa ya kugundua ni shaka yao wenyewe, kutambua kushuku kwao binafsi, na kuukubali udanganyifu wao binafsi na hivyo basi kuamini katika kuwepo na kufufuka kwa Bwana Yesu. Kile kilichomfanyikia Tomaso kilikuwa onyo na tahadhari kwa vizazi vijavyo ili watu wengi zaidi waweze kujitahadharisha na ili wasiwe wa kushuku kama Tomaso, na kama wangekuwa hivyo, wangezama katika giza. Ukimfuata Mungu, lakini kama Tomaso, siku zote unataka kuugusa ubavu wa Bwana na kuhisi alama Zake za msumari ili kuthibitisha, ili kuhakikisha, ili kuchambua kama Mungu yupo, basi Mungu atakuacha. Hivyo basi, Bwana Yesu anawahitaji watu wasiwe kama Tomaso, kuamini tu kile wanachoweza kuona kwa macho yao, lakini kuwa bila kasoro, mtu mwaminifu, kutouwa na shaka yoyote dhidi ya Mungu, lakini kumamini tu na kumfuata Yeye. Mtu wa aina hii amebarikiwa. Hili ni hitaji dogo sana la Bwana Yesu kwa watu, na onyo kwa wafuasi Wake.

Huu ndio mwelekeo wa Bwana Yesu kwa wale waliojaa shaka. Hivyo basi ni nini ambacho Bwana Yesu alimwambia, na ni nini Alichofanya kwa wale ambao wanaweza kuamini kwa uaminifu na kumfuata Yeye? Maswali hayo ndiyo tutakayoyaangalia katika kipindi kifuatacho, kuhusiana na kitu ambacho Bwana Yesu alimwambia Petro.

Katika mazungumzo haya, Bwana Yesu alimwuliza Petro mara kadhaa kuhusu jambo moja: "Petro, je, unanipenda?" Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi ambacho Bwana Yesu alihitaji kutoka kwa watu kama vile Petro baada ya kufufuka Kwake, wanaoamini Kristo kwa kweli na kulenga kumpenda Bwana. Swali hili lilikuwa aina fulani ya uchunguzi, na aina fulani ya kuhoji, lakini hata zaidi lilikuwa hitaji na tarajio la watu kama Petro. Aliitumia mbinu hii ya kuuliza maswali ili watu waweze kuwaza na kuwazua kujihusu na kuangalia katika maisha yao wenyewe: Mahitaji ya Bwana Yesu kwa watu ni yapi? Je, nampenda Bwana? Mimi ni mtu anayempenda Mungu? Nafaa vipi kumpenda Mungu? Hata ingawa Bwana Yesu aliuliza tu swali hili kwa Petro, ukweli ni kwamba katika moyo Wake, Alitaka kutumia fursa hii ya kumwuliza Petro ili kuuliza swali la aina hii kwa watu wengi zaidi wanaoutafuta kumpenda Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa Petro alibarikiwa kuwa mwakilishi wa mtu wa aina hii, ili kupokea swali hilo kutoka kwa kinywa cha Bwana Yesu mwenyewe.

Likilinganishwa na "nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani," ambalo Bwana Yesu alimwambia Tomaso baada ya kufufuka Kwake, Yeye kumwuliza Petro swali mara tatu: "Simioni, mwana wa Yona, unanipenda mimi?" waruhusu watu kuweza kuhisi kwa njia bora zaidi ule ukali wa mwelekeo wa Bwana Yesu na umuhimu Aliouhisi wakati huu wa kuuliza maswali hayo. Kuhusiana naye Tomaso wa kushuku pamoja na asili yake ya udanganyifu, Bwana Yesu alimruhusu yeye kufikisha mkono wake na kuzigusa zile alama Zake za msumari, jambo ambalo lilimfanya yeye kuamini kwamba Bwana Yesu ndiye aliyekuwa Mwana wa Adamu aliyefufuka na akatambua utambulisho wa Bwana Yesu kama Kristo. Na ingawa Bwana Yesu hakumkemea kwa ukali Tomaso, wala hakuonyesha kwa matamshi hukumu yoyote ilio wazi kwake, Alimjuza kwamba Alimwelewa kupitia kwa hatua za kimatendo, huku pia akionyesha mtazamo Wake na uamuzi wa aina hiyo ya mtu. Mahitaji na matarajio ya Bwana Yesu ya mtu wa aina hiyo hayawezi kuonekana kutokana na kile Alichosema. Kwa sababu watu kama Tomaso hawana katu imani ya ukweli. Mahitaji ya Bwana Yesu kwao yanapatikana tu katika, lakini mwelekeo Alioufichua kwa watu kama Petro ni tofauti kabisa. Hakuhitaji kwamba Petro aunyoshe mkono wake na kuzigusa hizo alama Zake za misumari, wala hakumwambia Petro: "usiwe bila imani, ila mwenye imani." Badala yake, Alimwuliza Petro kwa kurudia swali lilo hilo. Hili lilikuwa swali la kuchokonoa fikira, na lenye maana ambalo halina budi kumfanya kila mfuasi wa Kristo kuhisi majuto, na woga, lakini pia kuhisi ile hali ya moyo wa wasiwasi, na huzuni ya Bwana Yesu. Na wakati wakiwa katika maumivu na mateso makali, wanaweza kuelewa zaidi wasiwasi wa Bwana Yesu Kristo na utunzaji Wake; wanatambua mafundisho Yake ya dhati na mahitaji makali kuhusu watu wasio na kasoro, waaminifu. Swali la Bwana Yesu linawaruhusu watu kuhisi kwamba matarajio ya Bwana kwa watu yaliofichuliwa kupitia kwa maneno haya mepesi si ya kuamini tu na kumfuata Yeye, lakini kutimiza yote kwa kuwa na upendo, kumpenda Bwana wako, kumpenda Mungu wako. Upendo wa aina hii ni wa utunzaji na utiifu. Ni wanadamu kuishi kwa ajili ya Mungu, kufa kwa ajili ya Mungu, kujitolea kila kitu chao kwa ajili ya Mungu, na kutumia na kutoa kila kitu chao kwa ajili ya Mungu. Upendo wa aina hii pia ni kumpa Mungu tulizo, kumruhusu Yeye kufurahia ushuhuda, na kumruhusu Yeye kupumzika. Ni fidia ya wanadamu kwa Mungu, uwajibikaji wao, na wajibu wao, na ni njia ambayo wanadamu lazima wafuate kwa maisha yao yote. Haya maswali matatu yalikuwa mahitaji na ushawishi ambao Bwana Yesu alitoa kwa Petro na watu wote ambao wangefanywa kuwa watimilifu. Ni maswali haya matatu ndiyo yaliyomwongoza na kumpa motisha Petro kukamilisha njia yake ya maisha, na yalikuwa maswali haya wakati ule wa Bwana Yesu kuondoka ambayo yalimfanya Petro kuanza njia yake ya kufanywa mtimilifu, na yaliyomwongoza, kwa sababu ya upendo wake kwa Bwana, kuutunza moyo wa Bwana, kumtii Bwana, kumpa tulizo Bwana, na kuyatoa maisha yake yote na kila kitu chake chote kwa sababu ya upendo wake.

Katika Enzi ya Neema, kazi ya Mungu ilikuwa kimsingi ya aina mbili ya watu. Wa kwanza alikuwa aina ya aliyeamini Kwake na kumfuata, ambaye angetii amri Zake, ambaye angeweza kuuvumilia msalaba na kuushikilia hadi katika njia ya Enzi ya Neema. Mtu wa aina hii angepata baraka za Mungu na kufurahia neema ya Mungu. Aina ya pili ya mtu alikuwa kama Petro, mtu ambaye angefanywa kuwa mtimilifu. Hivyo basi, baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alifanya kwanza mambo haya mawili yenye maana sana. Kwanza lilikuwa ni kwa Tomaso, na jingine lilikuwa kwa Petro. Mambo haya mawili yanawakilisha nini? Yanawakilisha nia za kweli za Mungu katika kuwaokoa binadamu? Yanawakilisha uaminifu wa Mungu kwa binadamu? Kazi Aliyoifanya na Tomaso ilikuwa ni kuwapa onyo watu wasiwe wanashuku, lakini kuamini tu. Kazi Aliyofanya na Petro ilikuwa ni kuipatia nguvu imani ya watu kama vile Petro, na kuweka wazi mahitaji ya aina hii ya watu, ili kuonyesha ni shabaha zipi wanafaa kuwa wakifuatilia.

Baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alijitokeza kwa watu aliofikiria walifaa, Akaongea na wao, na kuwapa wao mahitaji, huku akiacha nyuma nia Zake, na matarajio Yake kwa watu. Hivi ni kusema, kama Mungu mwenye mwili, haijalishi kama ulikuwa katika wakati Wake akiwa mwili, au katika mwili wa kiroho baada ya kusulubishwa msalabani na kufufuliwa—haja Yake kwa wanadamu na mahitaji kwa wanadamu hayakubadilika. Alijali kuwahusu wanafunzi hawa kabla ya kufika msalabani; ndani ya moyo Wake, Alikuwa wazi katika hali ya kila mmoja, Alielewa upungufu wa kila mmoja, na bila shaka ufahamu Wake wa kila mtu ulikuwa namna ile ile baada ya Yeye kuaga dunia, kufufuka, na kuwa mwili wa kiroho kama hali ilivyokuwa Alipokuwa katika mwili. Alijua kwamba watu hawakuwa kwa kikamilifu na uhakika kuuhusu utambulisho Wake kama Kristo, lakini katika kipindi Chake akiwa mwili Hakuwa anatoa amri kali kuhusu watu. Lakini baada ya kufufuliwa Alijitokeza kwao, na Akawafanya wawe na hakika kabisa kwamba Bwana Yesu alikuwa amekuja kutoka kwa Mungu, kwamba Alikuwa Mungu mwenye mwili, na Alitumia hoja hiyo ya uwepo Wake na kufufuka Kwake kama maono na motisha kubwa zaidi kwa muda mrefu katika ufuatiliaji wa wanadamu. Kufufuka kwake kutoka kifo hakukuwapa nguvu tu wale wote Waliomfuata, lakini pia kuliweka katika taathira kazi Yake ya Enzi ya Neema miongoni mwa wanadamu, na hivyo basi wokovu wa injili ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema kwa utaratibu ukaenea katika kila pembe ya binadamu. Unaweza kusema kwamba kutokea kwa Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake kulikuwa na umuhimu wowote? Kama ungekuwa Tomaso au Petro wakati huo, na ukumbane na kitu hiki kimoja katika maisha yako ambacho kilikuwa na maana sana, ni athari ya aina gani ambayo kitu hicho kingekuwa nayo kwako? Je, ungeona huu kama msukumo wako katika kumfuata Mungu? Ungeona hali hii kama nguvu endeshi zako wewe kumfuata Mungu, kujaribu kumridhisha Yeye, na kufuatilia upendo wa Mungu katika maisha yako? Ungeweza kutumia jitihada za maisha yako yote ili kueneza maono haya makubwa zaidi? Ungefanya kueneza wokovu wa Bwana Yesu kuwa kazi unayokubali kutoka kwa Mungu? Hata ingawa hamjapitia haya, zile hali mbili za Tomaso na Petro tayari zinatosha kwa watu wa kisasa kuwa na ufahamu wazi kuhusu mapenzi ya Mungu na kumhusu Mungu. Inaweza kusemekana kwamba baada ya Mungu kuwa mwili, baada ya Yeye binafsi kupitia maisha miongoni mwa wanadamu na kuwa na maisha ya binadamu, na baada ya Yeye kuona uharibifu wa tabia wa wanadamu na hali ya maisha ya binadamu, Mungu katika mwili alihisi kwa kina ile hali ya kutojiweza, huzuni, na ukatili wa wanadamu. Mungu alipata huruma zaidi kwa hali ya binadamu kwa sababu ya ubinadamu Wake wakati akiishi katika mwili, kwa sababu ya silika Zake katika mwili. Hili lilimsababisha kuwa na wasiwasi mkubwa zaidi juu ya wafuasi Wake. Haya pengine ni mambo ambayo huwezi kuelewa, lakini Naweza kufafanua wasiwasi na utunzaji wa Mungu katika damu kwa kila mmojawapo wa wafuasi Wake kwa kauli hii: kujali kwingi. Hata ingawa kauli hii inatokana na lugha ya binadamu, na hata ingawa ni kauli yenye ubinadamu sana, inaonyesha kwa kweli na kufafanua hisia za Mungu kwa wafuasi Wake. Na kwa kujali kwingi kwa Mungu kwa ajili ya binadamu, kwa mkondo wa yale yote ambayo wewe umeyapitia utaanza kuhisi kwa utaratibu yote haya na kuyaonja. Hata hivyo, hali hii inaweza kutimizwa tu kwa kuelewa kwa utaratibu tabia ya Mungu kwa msingi wa kufuatilia mabadiliko katika tabia yako wewe binafsi. Kuonekana kwa Bwana Yesu kulifanikisha kujali Kwake kwingi kwa minajili ya wafuasi Wake katika ubinadamu na akakupokeza kwa mwili Wake wa kiroho, au unaweza kusema uungu Wake. Kuonekana Kwake kuliwaruhusu watu kuwa na hali nyingine waliyopitia na hisia walizopitia zinazohusu kujali na utunzaji wa Mungu huku kukithibitisha kwa uthabiti kwamba Mungu Ndiye anayefungua enzi, anayeiendeleza enzi, na Yeye ndiye anayetamatisha enzi. Kupitia kwa Kuonekana Kwake Aliipatia nguvu imani ya watu wote, na kupitia kwa Kuonekana Kwake alithibitishia ulimwengu hoja kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hali hii iliwapa wafuasi Wake uthibitisho wa milele, na kupitia kwa Kuonekana Kwake pia Aliweza kufungua awamu ya kazi Yake katika enzi mpya.

13. Bwana Yesu Ala Mkate na Kuonyesha Maandiko Baada ya Kufufuka Kwake

Luka 24:30-32 Na ikatimia, alipokuwa akikaa na wao ili wale, aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaupasua, na kuwapa. Na macho yao yakafunguka, na wakamjua, na akatoweka wasimwone. Na wakaambiana, je, Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu sisi, wakati alipokuwa akituzungumzia njiani, na wakati alipotufungulia maandiko?

14. Wanafunzi Wampa Bwana Yesu Kipande cha Samaki wa Kuokwa Ale

Luka 24:36-43 Na wakati walipokuwa wakinena hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akasema kwao, Amani iwe kwenu ninyi. Lakini walikuwa na woga na hofu sana, na wakafikiri kwamba walikuwa wameona roho. Naye akawaambia, Mbona mnasumbuka? na mbona mashaka yanaibuka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe: Niguseni, na kuona; kwa sababu roho haina mwili na mifupa, jinsi mnavyoniona mimi nikiwa nayo. Na baada ya yeye kunena hayo, akawaonyesha mikono yake na miguu yake. Na wakati walikuwa bado hawajaamini kwa furaha, na wakishangaa, akawaambia, Mnacho chakula chochote huku? Na wakampa kipande cha samaki wa kuokwa kwa asali. Na akakichukua, na kukila mbele yao.

Halafu tutaangalia dondoo zilizo hapo juu. Dondoo ya kwanza inamulika upya ulaji wa mkate na Bwana Yesu na unaeleza maandiko baada ya kufufuka Kwake na dondoo ya pili inaonyesha upya Bwana Yesu akila kipande cha samaki aliyekaushwa. Ni aina gani ya msaada ambao dondoo hii mara mbili inatupa kwa kuijua tabia ya Mungu? Unaweza kuwaza ni picha ya aina gani unayopata kutoka katika ufafanuzi huu wa Bwana Yesu akila mkate na kisha kipande cha samaki aliyekaushwa? Unaweza kufikiria, kama Bwana Yesu alikuwa Amesimama mbele yako wewe ukila mkate, unaweza kuhisi vipi? Au kama Angekuwa Akila pamoja nawe kwenye meza moja, huku Akila samaki kwa mkate na watu, ni hisia aina gani ambayo ungekuwa nayo wakati huo? Kama unahisi ungekuwa karibu sana na Bwana, kwamba yuko karibu sana na wewe, basi hisia yako i sahihi. Hivi ndivyo hasa tunda ambalo Bwana Yesu alitaka lizaliwe kutokana na kula Kwa mkate na samaki mbele ya umati wa watu baada ya kusulubishwa Kwake. Kama Bwana Yesu angekuwa ameongea tu na watu baada ya kufufuka Kwake, kama wasingeweza kuhisi mwili na mifupa Yake, lakini walihisi Alikuwa roho isiyoweza kufikika, wangehisi vipi? Hawangesikitishwa? Wakati watu wangesikitishwa, hawangehisi kwamba wameachwa? Hawangehisi ule umbali wa Bwana Yesu Kristo? Ni athari hasi ya aina gani ambayo umbali huu ungeweza kujenga katika uhusiano wa watu na Mungu? Watu wangehisi woga bila shaka, kwamba wasingethubutu kusonga karibu na Yeye, na wangekuwa na mwelekeo wa kumweka kwa mbali kiasi. Kuanzia hapo mpaka leo, wangekatiza uhusiano wao wa karibu na Bwana Yesu Kristo, na kurudi katika uhusiano kati ya wanadamu na Mungu aliye juu mbinguni, kama ilivyokuwa kabla ya Enzi ya Neema. Mwili wa kiroho ambao watu wasingeweza kuugusa au kuuhisi ungesababisha ukomeshaji wa ukaribu wao na Mungu, na ungefanya ule uhusiano wa karibu—ulioanzishwa wakati Bwana Yesu Kristo akiwa mwili bila ya umbali wowote kati Yake yeye na binadamu—ukose kuwepo. Hisia za watu kwa mwili wa kiroho ni za woga tu, kuepuka, na mtazamo usioeleweka. Hawathubutu kukaribia zaidi au kuwa na mazungumzo na Yeye, sikuambii hata kufuata, kuwa na imani, au kuwa na matumaini Kwake. Mungu hakupenda kuiona hisia ya aina hii ambayo wanadamu walikuwa nayo kwake Yeye. Hakutaka kuwaona watu wakimwepuka Yeye au wakijiondoa Kwake yeye; Aliwataka tu watu kumwelewa Yeye, kumkaribia na kuwa familia Yake. Kama familia yako binafsi, watoto wako wangekuona lakini wasingekutambua wewe, na hawakuthubutu kukukaribia lakini siku zote walikuepuka wewe, kama usingeweza kupata ufahamu wao kwa kila kitu ulichokuwa umewafanyia, ungehisi vipi? Halingekuwa jambo la uchungu? Je, hungevunjika moyo? Hivyo hasa ndivyo Mungu anavyohisi wakati watu wanamwepuka. Hivyo basi, baada ya kufufuka Kwake, Bwana Yesu bado alijitokeza kwa watu katika umbo Lake la mwili na damu, na kula na kunywa pamoja nao. Mungu huwaona watu kama familia na pia anataka wanadamu kumwona Yeye kwa njia hiyo; ni kwa njia hii tu ndivyo Mungu anavyoweza kuwapata watu kwa kweli, na ndio watu wanavyoweza kumpenda na kumwabudu Mungu kwa kweli. Sasa mnaweza kuelewa nia Yangu katika kudondoa dondoo hizi mbili kutoka katika maandiko pale ambapo Bwana Yesu anaula mkate na kuonyesha maandiko, na wanafunzi wanampa kipande cha samaki aliyechomwa ale baada ya kufufuka Kwake?

Inaweza kusemekana kwamba misururu ya mambo ambayo Bwana Yesu alisema na kufanya baada ya kufufuka Kwake yalikuwa ya fikira njema, na kufanywa kwa nia njema. Ilijaa huruma na huba ambayo Mungu anashikilia kwa binadamu, na akiwa amejaa shukrani na utunzaji wa makini Aliokuwa nao kwa minajili ya uhusiano wa karibu aliokuwa Ameanzisha na wanadamu wakati Akiwa katika mwili. Hata zaidi walijaa kumbukumbu za kitambo na tumaini Alilokuwa nalo kutokana na maisha ya kula na kuishi pamoja na wafuasi Wake wakati akiwa katika mwili. Hivyo basi, Mungu hakuwataka watu kuhisi umbali kati ya Mungu na binadamu, wala Hakutaka wanadamu kuwa mbali na Mungu. Hata zaidi, Hakutaka wanadamu wahisi kwamba Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake hakuwa tena Bwana ambaye alikuwa wa karibu na watu, kwamba Hakuwa pamoja tena na wanadamu kwa sababu Alirudi katika ulimwengu wa kiroho, alirudi kwa Baba ambaye watu wengi wasingeweza kumwona wala kumsikia. Hakutaka watu kuhisi kwamba kulikuwa na tofauti yoyote katika cheo kati Yake na wanadamu. Mungu anapowaona watu wanaotaka kumfuata lakini wanamweka katika umbali fulani, moyo Wake unapata maumivu kwa sababu hiyo inamaanisha kwamba mioyo yao iko mbali sana na Yeye, inamaanisha kwamba itakuwa vigumu sana Kwake yeye kuweza kuipata mioyo yao. Hivyo basi kama angekuwa amejitokeza kwa watu kupitia kwa mwili wa kiroho ambao wasingeweza kuuona ama kuugusa, hali hii kwa mara nyingine tena ingeweza kumweka binadamu mbali na Mungu, na ingewasababisha wanadamu kumwona Kristo kimakosa baada ya kufufuka Kwake kuonekana kuwa Amegeuka kuwa na majivuno, wa aina tofauti na wanadamu, na mtu ambaye asingeweza tena kushiriki meza na kula pamoja na binadamu kwa sababu wanadamu ni wenye dhambi, wananuka, na hawawezi kumkaribia Mungu hata kidogo. Ili kuondoa kutoelewana huku kwa wanadamu, Bwana Yesu alifanya mambo kadha wa kadha ambayo mara kwa mara Alifanya katika mwili, kama ilivyorekodiwa katika Biblia, "aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaupasua, na kuwapa." Pia Aliwachambulia maandiko, kama Alivyokuwa amezoea kufanya. Yote haya ambayo Bwana Yesu alifanya yalimfanya kila mmoja aliyemwona Yeye kuhisi kwamba Bwana hakuwa amebadililika, kwamba alikuwa bado Bwana Yesu. Hata ingawa Alikuwa amesulubishwa msalabani na kupitia kifo, Alikuwa amefufuliwa, na hakuwa amemwacha binadamu. Alikuwa amerudi kuwa miongoni mwa wanadamu, na kila kitu Chake hakikuwa kimebadilika. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele ya watu alikuwa bado Bwana Yesu. Mwenendo Wake na mazungumzo Yake na watu yalikuwa ya kawaida sana. Alikuwa angali bado na huruma na upendo, neema, na uvumilivu—Alikuwa bado Bwana Yesu aliyewapenda wengine kama Alivyojipenda Mwenyewe, ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu mara sabini mara saba. Kama kawaida, Alikula na watu, kuzungumza maandiko na wao, na hata muhimu zaidi, sawa tu na kama alivyofanya awali, Alifanywa kuwa mwili na damu na aliweza kuguswa na kuonekana. Mwana wa Adamu katika njia hii aliwaruhusu watu kuhisi upendo huo, kuhisi kuwa watulivu, na kuhisi furaha ya kupata tena kitu ambacho kilikuwa kimepotea, na wao pia walihisi watulivu kwa njia tosha ya kuanza kumtegemea na kumtumainia Mwana huyu wa Adamu kwa ujasiri na kwa imani ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao. Walianza pia kuomba kwa jina la Bwana Yesu bila ya kusita, kuomba ili kupokea neema Yake, baraka Zake, na kupokea amani na furaha kutoka Kwake, kupata utunzaji na ulinzi kutoka Kwake na kuanza kutenda uponyaji na kupunga mapepo kwa jina la Bwana Yesu.

Katika muda huu ambao Bwana Yesu alifanya kazi katika mwili, wengi wa wafuasi Wake wasingeweza kuthibitisha kikamilifu utambulisho Wake na mambo Aliyoyasema. Wakati aliposulubishwa msalabani, mwelekeo wa wafuasi Wake ulikuwa ule wa matarajio; aliposulubiwa msalabani na kupitishiwa yale yote aliyopitishiwa hadi alipowekwa katika kaburi, mwelekeo wa watu Kwake yeye ulikuwa wa kutoridhika. Wakati huu, watu walikuwa tayari wameanza kusonga katika mioyo yao kutoka katika kushuku hadi kukataa mambo ambayo Bwana Yesu alikuwa amesema wakati Akiwa mwili. Na Alipotembea nje ya kaburi na kujitokeza kwa watu mmoja baada ya mwengine, wengi wa watu ambao walikuwa wamemwona Yeye kwa macho yao au kusikia habari za kufufuka Kwake, walibadilika kwa utaratibu kutoka katika hali ya kumkataa hadi ile ya nadharia ya kushuku. Kufikia muda ule ambao Bwana Yesu alimfanya Tomaso kuuweka mkono wake katika upande Wake, kufikia wakati ambao Bwana Yesu aliuvunja mkate na kuula mbele ya umati wa watu baada ya kufufuka Kwake na baada yake kula kipade cha samaki aliyechemshwa mbele yao, hapo tu ndipo walipokubali kwa kweli Bwana Yesu ni Kristo katika mwili. Mnaweza kusema kwamba ni kana kwamba mwili huu wa kiroho ulio na nyama na damu uliosimama mbele ya hao watu ulikuwa ukizindua kila mmoja wao kutoka katika ndoto. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele yao Ndiye aliyekuwepo tangu miaka hiyo ya nyuma. Alikuwa na umbo, na mwili, na mifupa, na Alikuwa tayari ameishi na kula na wanadamu kwa muda mrefu.... Wakati huu, watu walihisi kwamba uwepo Wake ulikuwa halisi, wa ajabu sana; wote walichangamka na kufurahi mno, na wakati uo huo walijawa na hisia. Na kuonekana Kwake tena kuliwaruhusu watu waweze kuona kwa kweli unyenyekevu Wake, kuhisi ukaribu Wake na tamanio Lake, uhusiano Wake wa karibu na wanadamu. Kupatana huku kwa kufupi kuliwafanya watu waliomwona Bwana Yesu kuhisi kana kwamba muda mrefu umepita. Mioyo yao iliyopotea, kuchanganyikiwa, yenye woga, yenye wasiwasi, inayotarajia na isiyosikia hisia zozote vyote vilipata utulivu. Hawakuwa na shaka tena au kutoridhika tena kwa sababu walihisi kwamba sasa kulikuwa na tumaini na kitu cha kutegemea. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele yao Angekuwa nao milele, Angekuwa mnara wao dhabiti, kimbilio lao la kila wakati.

Ingawa Bwana Yesu alifufuliwa, moyo Wake na kazi Yake vyote havikuwa vimeondoka kwa wanadamu. Aliwaambia watu Alipoonekana ya kwamba haijalishi ni umbo gani Alilokuwemo ndani, Angeandamana na watu, kutembea na wao, na kuwa na wao siku zote na katika sehemu zote. Na nyakati zote na mahali popote, Angewatosheleza wanadamu na kuwachunga, kuwaruhusu kumgusa na kumwona Yeye, na kuhakikisha kwamba hawatawahi kuhisi tena kama wasio na msaada. Bwana Yesu alitaka pia watu wajue yafuatayo: Maisha yao ulimwenguni hawapo pekee. Mwanadamu ana utunzaji wa Mungu, Mungu yuko pamoja nao; watu siku zote wanaweza kumwegemea Mungu; Yeye ndiye familia ya kila mmoja wa wafuasi Wake. Akiwa na Mungu wa kumwegemea, mwanadamu hatawahi tena kuwa mpweke au bila usaidizi, na wale wanaomkubali kama sadaka yao ya dhambi hawataishia katika dhambi tena. Katika macho ya binadamu, sehemu hizi za kazi Zake ambazo Bwana Yesu alitekeleza baada ya kufufuka Kwake zilikuwa chache mno lakini Ninavyoona Mimi, kila kitu kilikuwa na maana yenye thamani sana na zote zilikuwa zenye umuhimu na uzito.

Ingawa muda wa Bwana Yesu kufanya kazi katika mwili ulijaa ugumu na mateso, kupitia katika kuonekana Kwake katika mwili Wake wa kiroho wa mwili na damu, Alikamilisha vyema na kwa njia timilifu kazi Yake ya wakati huo akiwa kwa mwili ili kuwakomboa wanadamu. Aliianza huduma Yake kwa kugeuka mwili na Alihitimisha huduma Yake kwa kujitokeza kwa wanadamu Akiwa katika umbo Lake la mwili. Alikuwa mjumbe wa Enzi ya Neema, Aliianzisha Enzi ya Neema kupitia kwa utambulisho Wake kama Kristo. Kupitia utambulisho Wake kama Kristo, Alitekeleza kazi katika Enzi ya Neema na Akaipatia nguvu na kuwaongoza wafuasi katika Enzi ya Neema. Inaweza kusemwa kuhusu kazi ya Mungu kwamba kwa kweli Yeye humaliza kazi Anayoianza. Kunazo hatua na mpango, na umejaa hekima ya Mungu, kudura Yake, na matendo Yake ya ajabu. Umejaa pia upendo na rehema za Mungu. Bila shaka, uzi mkuu unaotiririka katika kazi yote ya Mungu ni utunzaji Wake kwa binadamu; umejawa na hisia Zake za kujali ambazo Hawezi kuweka pembeni. Katika aya hizi za Biblia, katika kila kitu ambacho Bwana Yesu alifanya baada ya kufufuka Kwake, kile kilichofichuliwa kilikuwa ni matumaini yasiyobadilika ya Mungu na kujali Kwake kwa wanadamu, pamoja na utunzaji wa Mungu wenye umakinifu na kuwathamini wanadamu. Mpaka sasa hakuna chochote kati ya hivi vyote ambacho kimebadilika—unaweza kukiona? Unapoviona hivi, moyo wako haugeuki bila kusukumwa na kuwa karibu na Mungu? Kama uliishi katika enzi hiyo na Bwana Yesu Akakuonekania baada ya kufufuka Kwake, kwa njia ya kushikika ili wewe uweze kuona, na kama Aliketi mbele yako, Akala mkate na samaki na kukuchambulia wewe maandiko, Akaongea na wewe, basi ungehisi vipi? Ungehisi furaha? Je, ungehisi kuwa mwenye hatia? Kutoelewana kwa awali na kuepuka Mungu kwa awali, migogoro na shaka dhidi ya Mungu—hivi vyote havingetoweka tu? Je, unadhani kwamba uhusiano kati ya binadamu na Mungu ungekuwa bora zaidi?

Kupitia kwa ufasiri wa sura hizi finyu za Biblia, uligundua makosa yoyote katika tabia ya Mungu? Uligundua uchafuzi wowote katika upendo wa Mungu? Uliuona udanganyifu au uovu wowote katika kudura ya Mungu au hekima? Bila shaka la! Sasa unaweza kusema kwa uhakika kwamba Mungu ni mtakatifu? Unaweza kusema kwa uhakika kwamba hisia za Mungu zinafichua kiini Chake na tabia kwa ujumla? Natumai kwamba baada ya kuyasoma maneno haya, kile ambacho umeelewa kutoka katika maneno haya kitakusaidia na kukufaidi katika ufuatiliaji wako wa mabadiliko katika tabia na hali ya kumcha Mungu. Natumai pia kwamba maneno haya yataweza kukuzalia matunda ambayo yatakua kila siku, hivyo basi katika mchakato wa ufuatiliaji huu kukuleta karibu na Mungu zaidi na zaidi, wa kukuleta karibu na karibu zaidi na kiwango ambacho Mungu anahitaji, ili usichoke tena na ufuatiliaji wa ukweli na usihisi tena kwamba ufuataji wa ukweli na ule wa mabadiliko katika tabia ni usumbufu au jambo duni. Ni, kwa kweli, udhihirisho wa tabia ya kweli ya Mungu na kiini kitakatifu cha Mungu ambayo yanakupa motisha kutamani mwangaza, kutamani haki, na kuazimia kufuatilia ukweli, kufuatilia ridhaa ya mapenzi ya Mungu, na kuwa binadamu anayepatwa na Mungu, na kuwa mtu halisi.

Leo tumezungumzia baadhi ya mambo ambayo Mungu alifanya katika Enzi ya Neema wakati ambapo Alikuwa mwili kwa mara ya kwanza. Kutoka kwa mambo haya, tumeona tabia ambayo Alionyesha na kuifichua katika mwili, pamoja na kila kipengele cha kile Alicho nacho na kile Alicho. Vipengele hivi vyote vya kile Alicho nacho na kile Alicho vinaonekana kuhisishwa mno, lakini uhalisi ni kwamba kiini cha kila Alichofichua na kuonyesha hakiwezi kutenganishwa na tabia Yake mwenyewe. Kila mbinu na kila dhana ya Mungu mwenye mwili inaonyesha tabia Yake katika ubinadamu na imeunganishwa bila kutenganishwa katika kiini Chake Mwenyewe. Hivyo, ni muhimu sana kwamba Mungu alikuja kwa wanadamu kwa njia ya kuwa mwili na kazi aliyofanya katika mwili ni muhimu sana pia. Na, tabia Aliyoifichua na mapenzi Alionyesha ni muhimu hata sana kwa kila mtu anayeishi katika mwili, kwa kila mtu anayeishi katika upotovu. Je, hili ni jambo ambalo unaweza kuelewa? Baada ya kuelewa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, umefanya hitimisho lolote kuhusiana na namna unavyofaa kumtunza Mungu? Katika kulijibu swali hili, kwa hitimisho Ningependa kukupa onyo tatu: Kwanza, usimjaribu Mungu. Haijalishi ni kiasi kipi unachoelewa kuhusu Mungu, haijalishi ni kiwango kipi unachojua kuhusu tabia Yake, kwa vyovyote vile usimjaribu Yeye. Pili, usishindane na Mungu kuhusiana na hadhi. Haijalishi ni aina gani ya hadhi ambayo Mungu anakupa au ni kazi ya aina gani Anayokuaminia kuifanya, haijalishi ni wajibu wa aina gani ambao Atakuinua ili utende, na haijalishi ni kiasi kipi ambacho umegharimika au kujitolea kwa ajili Mungu, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu kwa hadhi. Tatu, usishindane na Mungu. Haijalishi kama unaelewa au kama unaweza kutii kile ambacho Mungu anafanya na wewe, kile Anachopanga na wewe, na mambo Anayokuletea wewe, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu. Kama unaweza kutekeleza onyo hizi tatu, basi utakuwa salama kwa kiasi fulani, na hutamghadhabisha Mungu kwa urahisi. Hayo ndiyo yote ya kushiriki kwa siku ya leo.

November 23, 2013

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni