1.18.2019

Neno la Mungu | "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" (Sehemu ya Kwanza)


Neno la Mungu | "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" (Sehemu ya Kwanza)


Hatua tatu za kazi ni rekodi ya kazi nzima ya Mungu, ni rekodi ya wokovu wa Mungu wa mwanadamu, na si porojo tu. Kama kweli mnataka kutafuta kujua tabia nzima ya Mungu, basi sharti mfahamu hatua tatu za kazi inayofanywa na Mungu, na, zaidi, sharti msiache hatua yoyote.  Hiki ndicho kiwango cha chini kinachopaswa kufikiwa na wale wanaotafuta kumjua Mungu. Mwanadamu mwenyewe hawezi kuvumbua maarifa ya Mungu. Si kitu ambacho mwanadamu mwenyewe anaweza kufikiria, wala si matokeo ya fadhila za Roho Mtakatifu kwa mtu mmoja. Badala yake, ni maarifa yanayotokea mwanadamu anapopitia kazi ya Mungu, na ni maarifa ya Mungu yanayotokana tu na mwanadamu kupitia ukweli wa kazi ya Mungu. Maarifa kama haya hayawezi kutimizwa kwa ghafla, wala si jambo linaloweza kufundishwa. Inahusiana kabisa na uzoefu wa kibinafsi. Wokovu wa Mungu wa mwanadamu ndiyo kiini cha hatua hizi tatu za kazi, ilhali katika kazi ya wokovu kumejumuishwa mbinu kadhaa za kufanya kazi na namna ambazo tabia ya Mungu imeonyeshwa. Hili ndilo jambo gumu sana kwa mwanadamu kutambua na kwa mwanadamu kuelewa. Mgawanyiko wa enzi, mabadiliko ya kazi ya Mungu, mabadiliko katika eneo la kazi, mabadiliko ya wanaopokea kazi na kadhalika—haya yote yamejumuishwa katika hatua tatu za kazi. Hususan, tofauti katika njia ya utendakazi wa Roho Mtakatifu, na vilevile mabadiliko katika tabia ya Mungu, picha, jina, utambulisho, au mabadiliko mengine, yote ni sehemu ya hatua tatu za kazi. Sehemu moja ya kazi inaweza tu kuwakilisha sehemu moja, na imewekewa mipaka ndani ya wigo fulani. Haihusiani na mgawanyiko wa enzi, ama mabadiliko ya kazi ya Mungu, wala masuala mengine. Huu ni ukweli ulio waziwazi. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo ukamilifu wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu lazima ajue kazi ya Mungu, tabia ya Mungu katika kazi ya wokovu, na bila ukweli huu, maarifa yako kumhusu Mungu yatakuwa tu maneno matupu, ni mahubiri ya starehe tu. Maarifa kama haya hayawezi kumshawishi au kumshinda mtu, maarifa kama haya yako nje ya uhalisi, na si ukweli. Yanaweza kuwa mengi, na mazuri kwa masikio, lakini kama hayaambatani na tabia ya asili ya Mungu, basi Mungu hatakusamehe. Hatakosa kuyasifu maarifa yako tu, bali pia atakuadhibu kwa kuwa mwenye dhambi aliyemkufuru. Maneno ya kumjua Mungu hayazungumzwi kwa mzaha. Ingawa unaweza kuwa na ulimi laini wenye maneno matamu, na maneno yako yaweza kuwafufua wafu, na kuwaua walio hai, bado huna elimu ya kuzungumza kuhusu maarifa ya Mungu. Mungu si mtu ambaye unaweza kuhukumu kwa urahisi, ama kusifu bila mpango, ama kupaka tope bila kujali. Unamsifu mtu yeyote na watu wowote, ilhali unajitahidi kupata maneno sahihi ya kuelezea ukuu wa wema na neema za Mungu—hili ndilo mshindwa yeyote hujifunza. Ingawa kuna wataalam wengi wa lugha wanaoweza kumwelezea Mungu, usahihi wa kile wanachoelezea ni asilimia moja ya ukweli unaozungumzwa na watu wa Mungu na wana misamiati michache tu, ilhali wanamiliki tajriba yenye uzito. Basi inaweza kuonekana kuwa maarifa ya Mungu yapo katika usahihi na uhalisi, na wala si utumiaji mzuri wa maneno au misamiati mingi. Maarifa ya mwanadamu na maarifa ya Mungu kabisa hayahusiani. Somo la kumjua Mungu liko juu zaidi kuliko sayansi za asili za mwanadamu. Ni somo linaloweza kutimizwa tu na idadi ndogo sana ya watu wanaotafuta kumjua Mungu, na haliwezi kutimizwa na mtu yeyote tu mwenye kipaji. Na kwa hivyo lazima msione kumjua Mungu na kufuatilia ukweli kama kwamba kunaweza kupatikana na mtoto mdogo tu. Pengine umekuwa na mafanikio makuu katika maisha yako ya kifamilia, ama kazi yako, ama katika ndoa yako, lakini inapofika kwenye ukweli, na somo la kumjua Mungu, huna lolote la kujivunia, hujatimiza malengo yoyote. Kutia ukweli kwenye vitendo, inaweza kusemwa, ni jambo gumu kwenu, na kumjua Mungu ni tatizo kuu hata zaidi. Hili ni tatizo lenu, na pia ni tatizo linalokabiliwa na wanadamu wote. Kati ya wale wenye mafanikio katika kumjua Mungu, karibu wote hawajafikia kiwango. Mwanadamu hajui maana ya kumjua Mungu, ama kwa nini ni muhimu kumjua Mungu, ama kiasi gani kinahesabiwa kama kumjua Mungu. Hili ndilo linalomshangaza mwanadamu, na ni kitendawili kikubwa zaidi kinachokabiliwa na mwanadamu—na hakuna awezaye kujibu swali hili, ama aliye na hiari kujibu hili swali, kwa sababu, hadi leo, hamna katika wanadamu aliyefanikiwa katika kusomea kazi hii. Pengine, kitendawili cha hatua tatu za kazi kitakapotambulishwa kwa mwanadamu, kutakuwepo katika mfululizo kundi la watu wenye vipaji wanaomjua Mungu. Bila shaka, Natumaini kuwa hivyo ndivyo ilivyo, na, hata zaidi, Niko katika harakati ya kutekeleza kazi hii, na Ninatumaini kuona kujitokeza kwa vipaji zaidi kama hivi katika siku za hivi karibuni. Watakuwa wale wanaoshuhudia ukweli wa hatua hizi tatu za kazi, na, bila shaka, watakuwa pia wa kwanza kushuhudia hizi hatua tatu za kazi. Kama kutakuwa na aliye na vipaji hivi, siku ambayo kazi ya Mungu itafikia kikomo, ama kuwe na wawili ama watatu, na kibinafsi wamekubali kufanywa wakamilifu na Mungu mwenye mwili, basi hakuna jambo la kuhuzunisha na kujutia kama hili—ingawa ni katika hali mbaya zaidi tu. Kwa vyovyote vile, Ninatumai kuwa wale wote wanaotafuta kwa kweli wanaweza kupata baraka hii. Tangu mwanzo wa wakati, hakujawahi kuwa na kazi kama hii, hapo awali hakujawahi kuwa na kazi kama hii katika historia ya ukuaji wa mwanadamu. Kama kweli unaweza kuwa mmoja wa wale wa kwanza wanaomjua Mungu, je, si hii itakuwa heshima ya

Kazi ya Mungu Mwenyewe ni maono ambayo mwanadamu lazima afahamu, kwa kuwa kazi ya Mungu haiwezi kutekelezwa na mwanadamu, wala haimilikiwi na mwanadamu. Hatua tatu za kazi ndizo ukamilifu wa usimamizi wa Mungu, na hakuna ono kuu kuliko hili linalopaswa kufahamika kwa mwanadamu. Kama mwanadamu hafahamu maono haya makuu, basi si rahisi kumjua Mungu, na si rahisi kujua mapenzi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, njia ambayo mwanadamu anapitia inazidi kuwa ngumu. Bila maono, mwanadamu hangeweza kufika umbali huu. Ni maono ambayo yamemlinda mwanadamu hadi leo, na ambayo yamempa mwanadamu ulinzi mkuu. Katika siku za usoni, maarifa yenu lazima yawe ya kina, na sharti mfahamu mapenzi Yake yote na umuhimu wa kazi Yake yenye busara katika hatua tatu za kazi. Hiki tu ndicho kimo chenu cha kweli. Hatua ya kazi ya mwisho haisimami peke yake, ila ni sehemu ya yote iliyounganishwa pamoja na hatua mbili za awali, ambayo ni kusema kwamba haiwezekani kukamilisha kazi nzima ya wokovu kwa kufanya kazi ya hatua moja pekee. Ingawa hatua ya mwisho ya kazi inaweza kumwokoa mwanadamu kabisa, hii haimaanishi kwamba ni muhimu tu kutekeleza hatua hii pekee, na kwamba hatua mbili za hapo awali hazihitajiki kumwokoa mwanadamu kutokana na ushawishi wa Shetani. Hakuna hatua moja kati ya zote tatu inayoweza kuwekwa kama maono ya kipekee ambayo lazima yajulishwe mwanadamu, kwa kuwa ukamilifu wa kazi ya wokovu ni hatua tatu za kazi, wala si hatua moja kati ya tatu. Ilimradi kazi ya wokovu bado haijakamilishwa, usimamizi wa Mungu utashindwa kufikia kikomo. Nafsi ya Mungu, tabia, na hekima zimeonyeshwa katika ukamilifu wa kazi ya wokovu, wala hazikufichuliwa kwa mwanadamu hapo mwanzo, lakini zimeonyeshwa hatua kwa hatua katika kazi ya wokovu. Kila hatua ya kazi ya wokovu huonyesha sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya nafsi Yake: si kila hatua ya kazi inayoweza moja kwa moja kuonyesha kabisa na kwa ukamilifu nafsi ya Mungu. Kwa hivyo, kazi ya wokovu inaweza tu kuhitimishwa hatua tatu za kazi zitakapokamilika, na kwa hivyo, maarifa ya mwanadamu ya ukamilifu wa Mungu hayawezi kutenganishwa na hatua tatu za kazi ya Mungu. Kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa hatua moja ya kazi ni tabia ya Mungu inayoonyeshwa katika sehemu moja ya kazi yake tu. Haiwezi kuwakilisha tabia na nafsi inayoonyeshwa katika hatua ya awali na ijayo. Hii ni kwa sababu kazi ya kumwokoa mwanadamu haiwezi kumalizika mara moja katika kipindi kimoja, ama katika eneo moja, lakini hukuwa kwa kina hatua kwa hatua kulingana na kiwango cha kukua kwa mwanadamu katika wakati na maeneo tofauti. Ni kazi inayofanywa hatua kwa hatua, na haikamilishwi katika hatua moja. Na kwa hiyo, hekima yote ya Mungu imejumuishwa katika hatua tatu, badala ya hatua moja. Nafsi yake yote na hekima yake yote zimewekwa wazi katika hatua hizi tatu, na kila hatua ina nafsi Yake, na ni rekodi ya hekima ya kazi Yake. Mwanadamu anapasa kujua tabia yote ya Mungu iliyoonyeshwa katika hatua hizi tatu. Nafsi hii ya Mungu ndiyo ina maana zaidi kwa wanadamu wote, na ikiwa watu hawana maarifa haya wanapomwabudu Mungu, basi hawana tofauti na wale wanaoabudu Budha. Kazi ya Mungu kati ya wanadamu haijafichiwa mwanadamu, na inapaswa kujulikana na wale wote wanaomwabudu Mungu. Kwa sababu Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi ya wokovu kati ya wanadamu, mwanadamu anapaswa kujua maonyesho ya kile Anacho na alicho wakati wa hatua hizi tatu za kazi. Hili ndilo ambalo ni lazima lifanywe na mwanadamu. Kile ambacho Mungu anamfichia mwanadamu ni kile ambacho mwanadamu hawezi kutimiza, na kile ambacho mwanadamu hapaswi kujua, ilhali yale Mungu anayomfunulia mwanadamu ni yale ambayo mwanadamu anapaswa kujua na yale ambayo mwanadamu anapaswa kumiliki. Kila moja ya hatua tatu za kazi huendelea juu ya msingi wa hatua iliyopita; haitekelezwi peke yake, tofauti na kazi ya wokovu. Ingawa kuna tofauti kubwa katika enzi na aina ya kazi ambayo inafanywa, katika kiini chake bado ni wokovu wa mwanadamu, na kila hatua ya kazi ya wokovu ina kina kuliko iliyopita. Kila hatua inaendelea kutoka kwa msingi wa hatua ya mwisho ambayo haiondolewi. Kwa njia hii, katika kazi Yake ambayo daima huwa mpya na kamwe si kuukuu, Mungu mara kwa mara anaonyesha kipengele cha tabia Yake ambayo hayajawahi kuonyeshwa kwa mwanadamu hapo awali, na daima anamfichulia mwanadamu kazi Yake mpya, na nafsi Yake mpya, na hata ikiwa wazoefu wakongwe wa kidini hufanya juu chini kukinzana na hili, na kulipinga waziwazi, Mungu daima hufanya kazi mpya ambayo anakusudia kufanya. Kazi Yake daima hubadilika, na kwa sababu hili, daima inakabiliwa na upinzani wa mwanadamu. Na hivyo, pia, tabia Yake inabadilika daima, na vilevile enzi na wanaopokea kazi Yake. Zaidi ya hayo, kila mara Yeye hufanya kazi ambayo haijawahi kufanywa tena, hata kufanya kazi ambayo huonekana kwa mwanadamu kuhitilafiana na kazi iliyofanywa awali, kuwa kinyume nayo. Mwanadamu anaweza kukubali tu aina moja ya kazi, ama njia moja ya matendo. Ni vigumu kwa wanadamu kukubali kazi ama njia za matendo, ambayo yanakinzana nao, ama yaliyo juu kuwaliko—lakini Roho Mtakatifu daima anafanya kazi mpya, na kwa hivyo kunakuwepo kikundi baada ya kikundi cha wataalamu wa kidini wanaoipinga kazi mpya ya Mungu. Watu hawa wamekuwa wataalamu hasa kwa sababu mwanadamu hana maarifa ya jinsi Mungu huwa mpya wala hazeeki, na zaidi ya hayo, hana maarifa ya kanuni za kazi ya Mungu, na hata zaidi hawana maarifa ya njia nyingi ambazo Mungu humwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, mwanadamu kabisa anashindwa kueleza kama ni kazi inayotoka kwa Roho Mtakatifu, au ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Watu wengi hushikilia mtazamo ambao, kama inalingana na maneno yanayokuja kabla, basi wanaweza kuikubali, na kama kuna tofauti na kazi ya awali, basi wanaipinga na kuikataa. Leo, je, nyote hamjafuata katika kanuni hizi? Hatua tatu za kazi ya wokovu hazijakuwa na athari kubwa kwenu, na kuna wale wanaoamini kuwa hatua mbili zilizopita za kazi ni mzigo usiohitaji kufahamika. Wanafikiria kuwa hatua hizi hazifai kutangazwa kwa umati na zinafaa kufutwa haraka iwezekanavyo, ili watu wasihisi kwamba wamezidiwa na hatua mbili za awali za zile hatua tatu za kazi. Wengi wanaamini kuwa kupeana ufahamu kuhusu hatua mbili zilizopita ni hatua ya mbali sana, wala haina faida katika kumjua Mungu—hivyo ndivyo mnavyofikiria. Leo, nyote mnaamini kuwa ni haki kutenda vile, lakini siku itawadia ambapo mtagundua umuhimu wa kazi Yangu: Mjue kuwa Sifanyi kazi yoyote ambayo haina umuhimu. Kwa sababu Ninawatangazia hatua tatu za kazi, kwa hivyo lazima ziwe na faida kwenu; kwa sababu hatua hizi tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, kwa hivyo lazima ziwe lengo la kila mmoja duniani. Siku moja, nyote mtagundua umuhimu wa kazi hii. Fahamuni kuwa mnapinga kazi ya Mungu, ama mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa makini kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, ubinadamu wako ya zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotevu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.


  Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni