1.21.2019

Maonyesho ya Mungu | "Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo" (sehemu ya kwanza)


      Mwenyezi Mungu alisema, Je, watu hawaamini kwamba ilipangwa awali kabla ya uumbaji kwamba Yuda angeweza kumwuza Yesu? Kwa hakika, Roho Mtakatifu alikuwa amepanga haya kulingana na uhalisia wakati huo. Ilifanyika tu kwamba kulikuwepo mtu kwa jina la Yuda ambaye siku zote angebadhiri fedha. Hivyo basi alichaguliwa kutekeleza wajibu huu na kuwa mwenye huduma katika njia hii. Huu ni mfano halisi wa kutumia rasilimali za mahali palepale. Yesu hakujua hili kwanza; Alilijua hili tu Yuda alipolifichuliwa baadaye. Kama mtu mwingine angeweza kutekeleza wajibu huu, basi mtu mwingine angeweza kufanya hivi badala ya Yuda. Kile ambacho kiliamuliwa awali kiliweza hasa kufanywa wakati mmoja na Roho Mtakatifu. Kazi ya Roho Mtakatifu siku zote inafanywa kwa hiari; wakati wowote Anapopanga kazi Yake, Roho Mtakatifu ataitekeleza. Kwa nini sikuzote Nasema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni ya uhalisi? Kwamba siku zote ni mpya na haijawahi kuwa zee, na siku zote inakuwa na uhai zaidi? Kazi ya Mungu ilikuwa bado haijawahi kupangwa wakati ulimwengu ulipoumbwa; hivi sivyo kamwe ilivyofanyika! Kila hatua ya kazi hufikia athari yake bora kwa wakati wake mwafaka, nazo haziingiliani kati. Kunao wakati mwingi ambapo mipango katika akili zako hazilingani kamwe na kazi ya hivi punde ya Roho Mtakatifu. Kazi Yake si rahisi kama wanavyofikiria watu, wala si ngumu kama watu wengi wanavyofikiria; inajumuisha kuwaruzuku watu wakati wowote na mahali popote kulingana na mahitaji yao ya sasa. Hakuna aliye wazi zaidi kuhusu kiini halisi cha watu kama Yeye, na ni kwa sababu hii mahususi ndiposa hakuna kinachoweza kufaa mahitaji ya kihalisi ya watu kama vile ambavyo kazi Yake inavyofanya. Hivyo basi, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kazi Yake ilipangiwa milenia kadha mbele. Anavyofanya kazi miongoni mwenu sasa, kulingana na hali yenu, Yeye pia Anafanya kazi na kuongea wakati wowote na mahali popote. Wakati watu wako katika hali fulani, Yeye huongea maneno hayo ambayo hasa ndiyo wanayohitaji ndani yao. Ni kama hatua ya kwanza ya kazi Yake ya nyakati za kuadibu. Baada ya nyakati za kuadibu, watu walionyesha tabia fulani, walikuwa na mienendo ya kuasi katika njia fulani, hali fulani nzuri ziliibuka, hali fulani mbaya pia ziliibuka, na mipaka ya juu ya hali hii ya ubaya ikafikia kiwango fulani. Mungu alifanya kazi Yake kutokana na mambo haya yote, na hivyo basi Alichukua haya yote ili kuweza kutimiza athari bora zaidi kwa ajili ya kazi Yake. Anatekeleza tu kazi Yake ya kuruzuku miongoni mwa watu kulingana na hali zao za sasa. Yeye Hutekeleza kila hatua ya kazi Yake kulingana na hali halisi za watu. Uumbaji wote umo mikononi Mwake; Angekosa kuujua? Kwa mujibu wa hali za watu, Kazi hii haikupangwa maelfu ya miaka kabla; hii ni dhana ya kibinadamu tu! Yeye hufanya kazi kwa kadri Anavyoangalia athari ya kazi Yake, na kazi Yake inaendelea kuwa ya kina na kukuzwa; kwa kadri Anavyoendelea kuangalia matokeo ya kazi Yake, ndipo Anapotekeleza hatua inayofuata ya kazi Yake. Yeye hutumia mambo mengi ili kuingia kwenye mpito hatua kwa hatua na kufanya kazi Yake mpya kuonekana na watu baada ya muda. Aina hii ya kazi inaweza kuruzuku mahitaji ya watu, kwani Mungu anawajua watu vizuri mno. Hivi ndivyo Anavyotekeleza kazi Yake kutoka mbinguni. Vilevile, Mungu mwenye mwili anafanya kazi Yake kwa njia iyo hiyo, Akipangilia kulingana na uhalisia na utendakazi miongoni mwa binadamu. Hakuna yoyote kati ya kazi Zake iliyopangwa kabla ya ulimwengu kuumbwa, wala kupangwa kwa umakinifu kabla ya wakati. Miaka 2,000 baada ya ulimwengu kuumbwa, Yehova aliona binadamu walikuwa wamepotoka sana kiasi cha kwamba Alikitumia kinywa cha nabii Isaya kutabiri kwamba baada ya Enzi ya Sheria kukamilika, Angetekeleza kazi Yake ya kukomboa binadamu katika Enzi ya Neema. Huu ulikuwa mpango wa Yehova, bila shaka, lakini mpango huu uliweza pia kufanywa kulingana na hali ambazo Aliangalia wakati huo; bila shaka Yeye hakuufikiria mara moja baada ya kumwumba Mwanadamu. Isaya alitabiri tu, lakini Yehova hakuandaa matayarisho mara moja wakati wa Enzi ya Sheria; badala yake, Alianza kazi hii katika mwanzo wa Enzi ya Neema, wakati mjumbe alipojitokeza katika ndoto ya Yusufu na kumpa yeye nuru, wakimwambia kwamba Mungu angekuwa mwili, na hivyo kazi Yake ya kupata mwili ikaanza. Kama watu wanavyofikiria Mungu hakujitayarishia kazi Yake ya kuwa mwili baada ya kuumba ulimwengu; jambo hili liliamuliwa tu kulingana na kiwango cha maendeleo ya binadamu na hadhi ya vita Vyake na Shetani.
Wakati Mungu anapokuwa mwili, Roho Wake anamwingia binadamu; kwa maneno mengine, Roho wa Mungu anauvaa mwili. Anafanya kazi Yake nchini, na badala ya kuleta naye hatua mbalimbali zilizozuiliwa kazi hii haina mipaka kamwe. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya katika mwili bado inaamuliwa na athari ya kazi Yake, na Yeye hutumia mambo haya kuamua urefu wa muda ambao Atafanya kazi akiwa mwili. Roho Mtakatifu hufichua moja kwa moja kila hatua ya kazi Yake; Yeye huchunguza kazi Yake anapozidi kuendelea; si jambo ambalo linazidi maumbile kiasi cha kupanua ile mipaka ya kufikiriwa na binadamu. Hii ni kama kazi ya Yehova katika kuumba mbingu na nchi na vitu vyote; Aliweza kupanga na kufanya kazi wakati huo huo Alitenga nuru kutoka kwenye giza, na asubuhi pamoja na jioni vyote vikawa—hii ilichukua siku moja. Siku ya pili Aliumba mbingu, ambayo pia ilichukua siku moja na kisha Akaiumba nchi, bahari na viumbe vilivyojaa ndani, pia ikichukua siku nyingine moja. Hali hii iliendelea hivyo hadi siku ya sita, wakati Mungu alipomwumba binadamu na kumwacha asimamie viumbe hivi vyote juu ya nchi, mpaka siku ya saba, Alipokuwa amemaliza kuumba viumbe vyote, na akapumzika. Mungu Alibariki siku ya saba na kuitenga kuwa siku takatifu. Aliiamulia siku hii takatifu baada ya kuviumba viumbe vyote, na wala si kabla ya kuviumba. Kazi hii iliweza pia kutekeleza kwa hiari; kabla ya kuviumba viumbe vyote, Hakuamua kuumba ulimwengu kwa siku sita na kuamua kupumzika siku ya saba; hoja hizi haziko hivi kamwe. Hakusema hivyo, wala Hakupanga hivi. Kwa vyovyote vile Hakusema kwamba uumbaji wa viumbe vyote ungekamilishwa katika siku ya sita na kwamba Angepumzika siku ya saba; badala yake, Aliumba kulingana na kile kilichokuwa kikionekana kizuri Kwake. Punde Alipomaliza kuumba kila kitu, tayari ilikuwa ni siku ya sita. Kama ingekuwa ni siku ya tano alipomaliza kuumba kila kitu, Angepangilia basi siku ya sita kuwa siku takatifu; hata hivyo, Alimaliza kuumba kila kitu katika siku ya sita, na hivyo basi siku ya saba ikawa siku takatifu, ambayo imepangiwa kuwa hivyo hadi siku ya leo. Hivyo basi, kazi Yake ya sasa inatekelezwa kwa njia sawa na hiyo. Yeye huongea na kuwaruzuku kulingana na hali zenu. Yaani, Roho huongea na kufanya kazi kulingana na hali za watu; Roho huangalia kila kitu na kufanya kazi wakati wowote na mahali popote. Kile Ninachofanya, kwa mfano, kuwawekea na kuwapatia bila kiwazo ni kile mnachohitaji. Ndiyo maana Nasema kwamba hakuna kazi Yangu iliyo tofauti na uhalisia; yote ni halisi, kwani nyinyi nyote mnajua ya kwamba “Roho wa Mungu hulinda vyote.” Kama haya yote yalikuwa yameamuliwa kabla ya wakati, huoni kwamba mambo yangekuwa yamekwisha amuliwa? Unafikiri kwamba Mungu alifanya kazi kwa milenia nzima sita na kisha kuamulia kabla binadamu kama waasi, wapingaji, waongo na wasio aminifu, kama kuwa na mwili, tabia za kishetani zilizopotoka, ashiki za macho na kujihusisha kwao kwa mambo yasiyofaa. Haya yote hayakupangwa awali, lakini yalitokana na upotovu wa kishetani. Baadhi watasema, “Shetani naye hakuwa ndani ya mashiko ya Mungu? Mungu naye alikuwa amepanga awali kwamba Shetani angepotosha binadamu kwa njia hii, na baada ya hapo akatekeleza kazi Yake miongoni mwa binadamu.” Je, Mungu angepanga awali Shetani hasa ili kuwapotosha binadamu? Anayo hamu mno ya kuwaruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida na kibinadamu; Angenyanyasa maisha ya binadamu? Basi kumshinda Shetani na kuokoa binadamu si kungekuwa jitihada za bure bilashi? Je, uasi wa binadamu ungeamuliwa vipi kabla? Ulitokana na kunyanyaswa na Shetani kwa hali halisi; ungepangwa vipi awali na Mungu? Shetani aliye ndani ya mashiko ya Mungu ambaye mnamwelewa na Shetani ndani ya mashiko ya Mungu ambaye Ninamzungumzia ni tofauti sana. Kulingana na kauli zenu kwamba “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake,” Shetani asingemsaliti Yeye. Je, wewe hujasema kwamba Mungu ni mwenyezi? Maarifa yenu ni ya kidhahania mno na hayaambatani na uhalisia; hayaeleweki wala hayana urazini na hayafanyi kazi! Mungu ni mwenyezi; huu si uwongo kamwe. Malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa sababu Mungu alimpa sehemu ya mamlaka awali. Bila shaka, tukio hili halikutarajiwa, kama vile Hawa kukabiliwa na jaribio la nyoka. Hata hivyo, bila kujali ni vipi ambavyo Shetani hutekeleza usaliti wake, tofauti na Mungu, yeye si mwenyezi. Kama vile mlivyosema, Shetani ni mwenye nguvu; haijalishi ni nini atafanya, mamlaka ya Mungu humshinda siku zote. Hii ndiyo maana ya kweli katika ule msemo “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake.” Hivyo basi, vita Vyake na Shetani lazima vitekelezwe hatua moja baada ya nyingine; aidha, Yeye hupanga kazi Yake katika kuitikia ujanja wa Shetani. Hivi ni kusema, kulingana na enzi, Anawaokoa watu na kufichua hekima na uweza Wake. Vilevile, kazi katika siku za mwisho haikuamuliwa awali kabla ya enzi ya Neema; haikuamuliwa awali katika mpangilio unaofuatana kama huu: Kwanza, fanya tabia ya nje ya binadamu kubadilika; pili, fanya binadamu kupokea kuadibu na majaribio yake; tatu, fanya binadamu kupitia kifo; nne, fanya binadamu kupitia zile nyakati za kumpenda Mungu na kuelezea uamuzi wa kiumbe kilichoumbwa; tano, fanya binadamu kuyaona mapenzi ya Mungu na kujua Mungu kabisa, kisha kumkamilisha binadamu. Hakupanga mambo haya wakati wa Enzi ya Neema; badala yake, Alianza kupanga mambo haya katika enzi ya sasa. Shetani yumo kazini, kama vile alivyo Mungu. Shetani huonyesha tabia yake potovu, huku naye Mungu huongea moja kwa moja na kufichua baadhi ya mambo muhimu. Hii ndiyo kazi inayofanywa leo, na hii ndiyo kanuni sawa inayofanya kazi na iliyotumika kwenye siku za kale baada ya ulimwengu kuumbwa.


Soma zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni