12.14.2018

nyimbo za dini | Katika Enzi ya Ufalme, Neno Linatimiza Kila Kitu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,nyimbo za injili,Nyimbo
I
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anaikaribisha enzi mpya na neno.
Anabadilisha mbinu ya kazi Yake, anafanya kazi ya enzi nzima na neno.
Hii ni kanuni ambayo Mungu anafanya kazi nayo katika Enzi ya Neno.
Alikuwa mwili ili kunena kutoka sehemu tofauti,
hivyo mwanadamu kweli anamwona Mungu, Neno likionekana katika mwili,
anaona ajabu Yake, na anaona hekima Yake. 
Kazi hii ni ili kufikia vizuri malengo
ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu, na kumtia mwanadamu nuru.
Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno
kufanya kazi katika Enzi ya Neno, katika Enzi ya Neno.
II
Kupitia neno, mwanadamu anakuja kujua kazi ya Mungu na tabia Yake.
Kupitia neno, mwanadamu anajua kiini chake,
na anajua kile anachofaa kuingia katika.
Kazi yote ya Mungu katika Enzi ya Neno inatimizwa kupitia neno.
Na mwanadamu anafichuliwa, kuangamizwa, na kujaribiwa kupitia neno.
Mwanadamu anaona neno, anasikia neno, na anajua uwepo wa neno.
Hivyo anaamini katika uwepo wa Mungu, ukuu na hekima,
anaamini katika upendo wa moyo wa Mungu kwa mwanadamu na hamu Yake kumwokoa mwanadamu.
Ingawa "neno" ni la kawaida na rahisi,
neno kutoka kwa mdomo wa Mungu katika mwili linatetemesha dunia na mbingu,
linabadilisha moyo wa mwanadamu, dhana na tabia ya zamani.
III
Katika enzi zote, ni Mungu wa wa leo pekee
Anayefanya kazi, Ananena na kumwokoa mwanadamu kwa njia hii.
Kisha, mwanadamu anaishi chini ya uongozi wa neno, 
kuchungwa na kurutubishwa na neno.
Watu wote wanaishi katika dunia ya neno,
katika laana na baraka za neno la Mungu.
Wengi wanahukumiwa na kuadibiwa na neno.
Maneno na kazi ni ya kumwokoa mwanadamu,
ya kufanikisha mapenzi ya Mungu
na kubadilisha dunia nzee iliyoumbwa.
Mungu aliiumba dunia, Anawaongoza wanadamu katika ulimwengu mzima,
Anawashinda na kuwaokoa na neno.
Na wakati ukiwadia,
Ataitamatisha dunia yote nzee hadi tamati na neno.
Baada ya kufikia haya,
Mpango Wake wa usimamizi unakamilika kabisa, unakamilika kabisa.
kutoka kwa "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

       Tazama zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni