Tamko la Arubaini na Nne
Watu huichukulia kazi Yangu kama kijalizo, hawaachilii chakula au usingizi kwa ajili yake, na kwa hiyo Sina budi ila kufanya madai yafaayo kwa mwanadamu kama inavyostahili mtazamo wake Kwangu. Nakumbuka kuwa wakati mmoja Nilimpa mwanadamu neema nyingi sana na baraka nyingi, lakini baada ya kunyakua vitu hivi aliondoka mara moja.
Ilikuwa ni kama kwamba Nilikuwa Nampa bila kufahamu. Na kwa hiyo, mwanadamu amenipenda Mimi daima kati ya dhana zake mwenyewe. Nataka mwanadamu anipende kweli, lakini leo, watu bado wanasitasita, wasiweze kunipa upendo wao wa kweli. Katika mawazo yao, wao huamini kwamba iwapo watanipa upendo wao wa kweli, wataachwa bila chochote. Ninapopinga, miili yao yote hutetemeka—lakini wao hubaki kutotaka kutoa upendo wao wa kweli Kwangu. Ni kama kwamba wanasubiri kitu fulani, na hivyo wanatazama mbele, wasiniambie kamwe ni nini kinachoendelea. Ni kama kwamba kibandiko kimebandikwa juu ya vinywa vyao, kwa hiyo kamwe hawazungumzi waziwazi. Mbele ya mwanadamu, inaonekana, Nimekuwa bepari wa kikatili. Watu daima huniogopa: Wanaponiona, wao hupotea mara moja wasionekane tena, wakihofu juu ya kile Nitawauliza kuhusu hali zao. Sijui sababu ya watu kuweza kuwa na upendo wa kweli kwa "wanakijiji wenzao," lakini hawawezi kunipenda, ambaye ni mwadilifu katika roho. Kwa sababu ya hili Nashusha pumzi: Kwa nini watu daima huachia huru upendo wao katika ulimwengu wa mwanadamu? Kwa nini Siwezi kuonja upendo wa mwanadamu? Je, ni kwa sababu Mimi si mmoja wa wanadamu? Watu daima hunitendea Mimi kama nduli katika milima. Ni kama kwamba Nakosa kile kinachomkamilisha mtu wa kawaida, na kwa hiyo mbele Yangu watu daima hujisingizia toni ya maadili ya juu. Mara nyingi hunikokota mbele yao kunikemea, wakinikaripia kama wanavyomfanyia mtoto wa umri wa kwenda shule ya chekechea; kwa sababu, katika kumbukumbu za watu, Mimi ni mtu asiye na mantiki na asiye na elimu, wao daima huchukua jukumu la mwalimu mbele Yangu. Siwaadibu watu kwa kasoro zao, bali Nawapa msaada ufaao, kuwaruhusu kupokea "msaada wa kiuchumi" wa mara kwa mara. Kwa kuwa mwanadamu daima ameishi katikati ya janga na huona vigumu kutoroka, na katikati ya msiba huu daima ameniita, Mimi huwasilisha "riziki ya nafaka" bila kuchelewa katika mikono yake, kuwaruhusu watu wote kuishi katika jamii kubwa ya enzi mpya, na kupitia wema wa jamii kubwa. Ninapochunguza kwa makini kazi miongoni mwa wanadamu, Natambua kasoro nyingi za mwanadamu, na kutokana na hilo Nampa mwanadamu msaada. Hata wakati huu, bado kuna umasikini wa kipekee miongoni mwa wanadamu, na hivyo Nimetoa huduma ifaayo kwa "maeneo masikini," kuyainua kutoka kwa umasikini. Hii ni njia ambayo Mimi hufanyia kazi, kuruhusu watu wote kufurahia neema Yangu kadri wanavyoweza.
Watu hapa duniani hupitia kuadibu bila kufahamu, na kwa hiyo Nafungua mkono Wangu mkubwa na kuwavuta upande Wangu, kuwaruhusu bahati nzuri ya kufurahia neema Yangu duniani. Duniani, ni kitu gani kisicho tupu na bila thamani? Natembea miongoni mwa sehemu zote katika ulimwengu wa mwanadamu, na ingawa kuna majengo mengi maarufu na mazingira asili ya kupendeza, kila mahali Niendapo kwa muda mrefu pameondolewa uhai. Wakati huo tu ndipo Ninahisi huzuni na ukiwa duniani: Duniani, maisha yamepotea kitambo, kuna harufu ya kifo tu, na hivyo Nimewahi kumwomba mwanadamu kuharakisha na kuiacha nchi hii ya mateso. Yote Nionayo ni yenye kunukia utupu. Mimi Huchukua nafasi ya kuvurumisha maisha yaliyo mkononi Mwangu kwa wale ambao Nimewachagua; ghafla, kuna kiwanja cha kijani juu ya nchi. Watu wako radhi kufurahia vitu vya uhai juu ya dunia, lakini Sipati furaha kwa jambo hili; watu daima hutunza mambo yaliyo duniani, na kamwe hawaoni utupu wao, kiasi kuwa, baada ya kufikia kiwango hiki leo, bado hawaelewi kwa nini hakuna uhai uliopo duniani. Leo, wakati Ninapotembea katikati ya ulimwengu, watu wanaweza kufurahia neema ya mahali Nilipo, na wao huchukulia hili kama rasilimali, wasifuatilie kamwe chanzo cha uzima. Wote hutumia kile Ninachowapa kama rasilimali, lakini hakuna hata mmoja wao anayejaribu kutekeleza kazi ya asili ya uhai. Hawajui jinsi ya kutumia au kukuza maliasili, na hivyo wanabaki masikini. Ninakaa miongo ni mwa wanadamu, Naishi miongoni mwa wanadamu, lakini leo bado mwanadamu hanijui. Ingawa watu wamenipa msaada mwingi sana kutokana na Mimi kuwa mbali sana na nyumbani, ni kama kwamba bado Sijaanzisha urafiki wa kweli na mwanadamu, na hivyo Mimi bado Nahisi ukosefu wa haki wa ulimwengu wa mwanadamu; machoni Pangu, mwanadamu, hata hivyo, ni mtupu, na hakuna hazina ya thamani yoyote kati ya mwanadamu. Sijui watu wana mtazamo gani kuhusu maisha ya binadamu, lakini kwa jumla, Wangu mwenyewe hautenganishwi na neno "tupu." Natumai watu hawanifikirii vibaya kwa sababu ya hili—hivyo ndivyo Nilivyo tu, Mimi ni mkweli, Sijaribu kuwa wa adabu. Hata hivyo, Ningewashauri watu kuzingatia kwa makini kile Ninachofikiria, kwani maneno Yangu, hata hivyo, ni ya msaada kwao. Sijui ni ufahamu gani walionao watu kuhusu "utupu." Tumaini langu ni kwamba watatumia juhudi kidogo kwa kazi hii. Wangefanya bora kupitia kwa kweli maisha ya binadamu, na kuona kama wanaweza kupata "madini" yoyote ya thamani ndani yake. Sijaribu kufifiza matumaini ya watu, Nataka tu wapate maarifa fulani katika maneno Yangu. Mimi daima Hukimbia huku na huko kwa ajili ya mambo ya binadamu, lakini hata baada ya kufikia kiwango hiki leo, bado watu hawajazungumza neno la shukrani, kana kwamba wana shughuli nyingi sana, na wamesahau hili. Hata leo, Mimi bado Sijui ni matokeo gani yamepatikana kwa mwanadamu kukimbia huku na huko siku nzima. Hadi leo bado Sina nafasi katika mioyo ya watu, na kwa hiyo mara nyingine tena Nazama katika mawazo. Nimeanza kuingia katika kazi ya kuchunguza "kwa nini watu hawana moyo ambao unanipenda kweli": Nitamwinua mwanadamu kwenye "meza ya upasuaji," Nitaukata moyo wake vipande vipande, na kuangalia kile kinachozuia njia ndani ya moyo wake na kumzuia kunipenda kweli. Chini ya athari ya "kisu," watu hukaza macho yao na kuyafumba, wakinisubiri Nianze, kwani wakati huu, wamesalimu amri kabisa; katika mioyo yao Napata ughushi mwingine mwingi. Katika mioyo yao, kubwa kati ya haya ni mambo ya watu wenyewe. Ingawa wanaweza kuwa na mambo machache tu nje ya miili yao, yale yaliyo ndani ya miili yao hayahesabiki. Ni kama kwamba moyo wa mwanadamu ni sanduku kubwa la hifadhi, lililojaa utajiri, kila kitu ambacho watu wangewahi kuhitaji. Wakati huo tu ndio Naelewa kwa nini watu huwa hawanijali kamwe: Ni kwa sababu wana kujitosheleza kwingi—wana haja gani ya msaada Wangu? Kwa hiyo Naondoka kwa mwanadamu, kwani watu hawana haja ya msaada Wangu; kwa nini Niwe na ujasiri wa kukabiliana na jambo na kuwafanya wanichukie?
Nani anajua kwa nini, lakini kila mara Nimekuwa radhi kuzungumza miongoni mwa wanadamu—ni kama kwamba Siwezi kujisaidia. Na hivyo, watu wananiangalia kama Nisiye na thamani, daima wao hunitendea kama kitu kisicho na thamani, hawanitendei kama kitu cha kuheshimiwa. Hawanitunzi, na hunikokota nyumbani wakati wowote na tena kunitupa nje, "wakinifunua" mbele ya umma. Nina chukizo kubwa sana kwa tabia ya mwanadamu ya aibu, na hivyo Nasema waziwazi kuwa mwanadamu hana dhamiri. Lakini watu ni wenye msimamo usiobadilika, wanachukua "panga na mikuki" yao na kupigana na Mimi, wakisema kuwa maneno Yangu ni tofauti na hali halisi, wakisema kuwa Nawasingizia—lakini Siwalipizi adhabu kutokana na tabia yao ya vurugu. Mimi hutumia tu ukweli Wangu kuwavutia watu, kuwafanya wasikie aibu wenyewe, baada ya hapo wanarudi nyuma kimyakimya. Sishindani na mwanadamu, kwani hakuna faida katika hilo. Nitashikilia wajibu Wangu, na Natumai kwamba mwanadamu anaweza pia kushikilia wajibu wake, na si kutenda dhidi Yangu. Je, isingekuwa bora kupatana kwa amani hivi? Kwa nini tuumize uhusiano wetu? Tumepatana miaka hii yote—kuna haja gani kuleta taabu kwa sisi wawili? Je, hilo halitakosa manufaa kwa mojawapo ya sifa zetu? Wetu ni "urafiki wa kale" wa miaka mingi, "kufahamiana kwa zamani"—kuna haja gani kuachana kwa hali ya ukali? Je, kuna manufaa kwa hili? Natumai watu wanazingatia athari, kwamba wanajua ni nini kizuri kwao. Mtazamo wangu kwa mwanadamu leo ni wa kutosha majadiliano ya maisha na mwanadamu—kwa nini watu daima hushindwa kutambua wema Wangu? Ni kwa sababu hawana uwezo wa kujieleza? Je, wanakosa msamiati wa kutosha? Kwa nini wao daima hukosa maneno? Ni nani asiyejua jinsi Nitendavyo? Watu wanafahamu vizuri kabisa matendo Yangu. Ni vile tu wao hupenda kutumia wengine kwa manufaa yao, kwa hivyo huwa hawako radhi kamwe kuweka kando mambo wayapendayo; ikiwa neno moja linagusa mambo wayapendayo, wanakataa kuachilia mpaka wawe wamepata udhibiti—na kuna haja gani katika hilo? Badala ya kushindana juu ya kiasi gani wanachoweza kutoa, watu hushindana juu ya kiasi gani wanaweza kupata. Ingawa hakuna furaha katika cheo chao, wanakitunza sana, na hata kukiona kama hazina ya thamani kubwa sana—na hivyo heri wavumilie kuadibu Kwangu kuliko kuacha baraka za cheo. Watu hujiona sana, na hivyo huwa kamwe hawako radhi kujiweka kando. Pengine kuna upungufu fulani mdogo katika tathmini Yangu ya mwanadamu, au labda inafaa sawa tu—lakini kwa jumla, matumaini Yangu ni kwamba watu walichukue hili kama onyo.
Mei 21, 1992
Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni