9.21.2018

Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Maneno Husika ya Mungu:

Mungu na mwanadamu hawawezi kuzungumziwa kama wa kulingana. Dutu ya Mungu na kazi Yake ni vitu visivyoeleweka na kufahamika kwa mwanadamu. Ikiwa Mungu hawezi kufanya kazi Yake binafsi na kuzungumza maneno Yake katika ulimwengu wa mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kuelewa mapenzi ya Mungu, na kwa hivyo, hata wale waliotoa maisha yao yote kwa ajili ya Mungu hawataweza kupata idhini ya Mungu. Bila kazi ya Mungu, haijalishi jinsi gani mwanadamu anatenda mema, haitahesabika kama chochote, kwa maana fikira za Mungu daima zitakuwa juu ya fikira za mwanadamu, na hekima ya Mungu haieleweki kwa mwanadamu. Na kwa hivyo Nasema kwamba wale ambao “wanaona kwa wazi” Mungu na kazi Yake ni wasioweza kufanikisha chochote, wao wote ni wenye kiburi na wapumbavu. Mwanadamu hafai kufafanua kazi ya Mungu; zaidi ya hayo, mwanadamu hawezi kufafanua kazi ya Mungu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu ni mdogo kushinda mchwa, kwa hivyo mwanadamu atawezaje kuelewa kazi ya Mungu? Wale wasemao daima, “Mungu hafanyi kazi kwa njia hii ama ile” au “Mungu yuko hivi ama vile”—je hawa wote si wenye kiburi? Tunafaa sote kujua kwamba watu, ambao ni wa mwili, wote wamepotoshwa na Shetani. Ni katika hali yao asili kumuasi Mungu, na hawako katika usawa na Mungu, sembuse kuweza kutoa mawaidha kwa kazi ya Mungu. Jinsi Mungu anavyomwelekeza mwanadamu ni kazi ya Mungu mwenyewe. Mwanadamu anafaa kunyenyekea, na hafai kuwa na wazo hili ama lile, kwani mwanadamu ni mchanga tu. Kwa sababu tunajaribu kumtafuta Mungu, hatufai kuwekelea dhana zetu katika kazi ya Mungu ili Mungu Aziwaze, na zaidi hatufai kutumia tabia zetu potovu kwa kupinga kazi ya Mungu kwa makusudi. Je hili halitatufanya wapinga Kristo? Je, watu kama hawa watawezaje kusema kuwa wanamwamini Mungu? Kwa maana tunaamini kuwa kuna Mungu, na kwa maana tunatamani kumtosheleza na kumwona, tunapaswa kutafuta njia ya ukweli, na tunapaswa kutafuta njia ya kulingana na Mungu. Hatupaswi kuwa katika upinzani sugu kwa Mungu; Matendo kama haya yatakuwa na matokeo gani mazuri?
Leo hii, Mungu Anayo kazi mpya. Unaweza kuyakataa maneno haya, yanaweza kuhisi yasiyo ya kawaida kwako, lakini Nakushauri usifichue asili yako halisi, kwa maana wale tu walio na njaa ya kweli na kiu cha haki mbele za Mungu ndio wanaweza kupata ukweli, na wale wanaomcha Mungu kwa ukweli tu ndio wanaweza kupata nuru na kuongozwa na Mungu. Hakuna litakalotoka kwa kutafuta ukweli kupitia ugomvi. Ni kwa kutafuta kwa utulivu ndio tunaweza kupata matokeo. Ninaposema kwamba “Leo, Mungu Anayo kazi mpya,” Ninaashiria Mungu kurudi katika mwili. Pengine huyajali maneno haya, pengine unayachukia, au pengine una haja kubwa sana nayo. Haijalishi ni hali gani, Natumai kuwa wote walio na tamaa ya kweli ya kuonekana kwa Mungu wataweza kuukabili ukweli huu na kutafakari juu yake kwa makini. Ni vyema usiamue jambo upesi bila kuzingatia suala zima. Hivi ndivyo watu wenye hekima wanapaswa kutenda.
kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili
Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe kawaida na wenye kutojali katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?
kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Mlipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa “Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.” Kwa hivyo, watu wengi wanapoupokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani! Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulinganishwa na fikira za mwanadamu, sembuse Mungu kuonekana kwa amri ya mwanadamu. Mungu hufanya uamuzi Wake mwenyewe na huwa na mipango Yake Afanyapo kazi; aidha, Ana malengo Yake, na mbinu Zake. Si lazima Ajadiliane kazi Azifanyazo na mwanadamu au Atafute ushauri wa mwanadamu, sembuse kumfahamisha kila mtu kuhusu kazi Yake. Hii ndiyo tabia ya Mungu na, zaidi ya hayo, inafaa kutambuliwa na kila mmoja. Kama mnatamani kushuhudia kuonekana kwa Mungu, kama mnatamani kufuata nyayo za Mungu, basi kwanza ni sharti mzishinde dhana zenu. Ni sharti muache kudai kuwa Mungu afanye hiki au kile sembuse kumweka Yeye ndani ya mipaka yenu wenyewe na kumwekea upeo kwa dhana zenu. Badala yake, mnafaa kujua ni vipi mtazitafuta nyayo za Mungu, na vipi mnapaswa kukubali kuonekana kwa Mungu na ni vipi mnapaswa kutii kazi mpya ya Mungu; hiki ndicho kinapaswa kufanywa na mwanadamu. Kwa kuwa mwanadamu si ukweli, na hamiliki ukweli, mwanadamu anafaa kutafuta, kukubali na kutii.
Bila kujali kama wewe ni Mmarekani, Mwingereza, au mtu wa taifa jingine, ni lazima utoke nje ya mipaka yako, ni lazima ujipite, na ni sharti uione kazi ya Mungu kama kiumbe wa Mungu. Kwa njia hii, hutaweka vikwazo katika nyayo za Mungu. Kwa sababu, leo, watu hufikiri kuwa haiwezekani Mungu kudhihirika katika nchi au taifa fulani. Umuhimu wa kazi ya Mungu una undani kiasi gani, na kuonekana kwa Mungu kuna maana ilioje! Vinawezaje kupimwa kwa dhana na fikira za mwanadamu? Na ndiyo maana Ninasema kuwa unafaa kujiondoa katika dhana za uraia wako au kabila lako unapokutafuta kuonekana kwa Mungu. Kwa njia hii, hutafungwa na dhana zako mwenyewe; kwa njia hii, utahitimu kukaribisha kuonekana kwa Mungu. Vinginevyo, daima utakuwa gizani na hutapata kibali cha Mungu.
kutoka katika “Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu ni Mungu wa wanadamu wote. Hawi mali binafsi ya nchi au taifa lolote na hufanya kazi ya mpango Wake bila kuzuiwa na mfumo wowote, nchi au taifa. Labda hujawahi kuwazia mfumo huu, au labda wewe hukana kuwepo kwake, au labda nchi au taifa ambapo Mungu huonekana limebaguliwa na lina maendeleo duni sana duniani. Na bado Mungu ana busara Yake. Na uwezo Wake kupitia ukweli na tabia Zake kwa hakika Amepata kundi la watu wenye mawazo sawa na Yeye. Na Amepata kundi la watu ambao alitaka kutengeneza: kundi lililoshindwa Naye, watu ambao wameyavumilia majaribu machungu na aina zote za mateso na wanaweza kumfuata mpaka mwisho. Malengo ya kuonekana kwa Mungu, bila vizuizi vya nchi yoyote, ni kumruhusu Akamilishe kazi ya mpango Wake. Kwa mfano, Mungu alipopata mwili kule Uyahudi, lengo Lake lilikuwa kutimiza kazi ya msalaba na kuwakomboa wanadamu wote. Na bado Wayahudi waliamini kuwa Mungu asingeweza kulifanya hili, na wakafikiri kuwa Mungu asingeweza kuwa mwili na kuchukua umbo la Bwana Yesu. “Kutowezekana” kwao kukawa msingi wa kumshutumu na kumpinga Mungu na hatimaye ikawa kuangamizwa kwa Israeli. Leo hii, watu wengi wamefanya kosa lile lile. Wanatangaza kuonekana kwa Mungu ambako kumekaribia, na vilevile kukushutumu kuonekana huku; “kutowezekana” kwao kwa mara nyingine kunabana kuonekana kwa Mungu katika mipaka ya dhana zao. Na kwa hivyo Nimeona watu wengi wakicheka na kuanguka baada ya kuyasikia maneno ya Mungu. Kicheko hiki kinatofautianaje na shutuma na kukufuru kwa Wayahudi? Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli, sembuse kutamani ukweli. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama huwezi kuyang’amua matamshi ya Mungu, umehitimu vipi kushuhudia kuonekana kwa Mungu? Mahali ambapo Mungu anajitokeza, kuna maonyesho ya kweli, na kuna sauti ya Mungu. Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Weka dhana zako kando. Tafakari na kusoma maneno haya kwa makini. Ukitamani ukweli, Mungu atakupa nuru ya kuyafahamu mapenzi Yake na maneno Yake. Wekeni kando mitazamo yenu ya “haiwezekani”! Kadiri watu wanavyozidi kuamini kuwa jambo fulani haliwezekani, ndivyo uwezekano wa utukiaji wake unavyoendelea kujiri, kwani ufahamu wa Mungu hupaa juu kuliko mbingu, mawazo ya Mungu yako juu ya yale ya mwanadamu, na kazi ya Mungu inapita mipaka ya fikira za mwanadamu. Kadiri kitu kinavyokuwa hakiwezekani, ndivyo kunavyokuwepo na ukweli wa kutafutwa; kadiri kitu kilivyo nje ya mipaka ya dhana na fikira za mwanaadamu, ndivyo kinavyozidi kuwa na mapenzi ya Mungu. Kwani bila kujali Mungu anajidhihirishia wapi, Mungu bado ni Mungu, na kiini chake hakitawahi kubadilika kwa sababu ya mahali ama namna ya kuonekana Kwake. Tabia ya Mungu hubaki kuwa vilevile bila kujali nyayo Zake ziko wapi. Bila kujali nyayo za Mungu zilipo, Yeye ndiye Mungu wa wanadamu wote. Kwa mfano, Bwana Yesu si Mungu tu wa Waisraeli, lakini vilevile ni Mungu wa watu wote wa Asia, Ulaya, na Marekani, na hata zaidi, ndiye Mungu pekee wa ulimwengu mzima. Hivyo basi, tuyatafute mapenzi ya Mungu na tugundue kuonekana Kwake kutoka kwa matamshi Yake na tufuate nyayo Zake. Mungu ndiye ukweli, njia na uzima. Maneno Yake na kuonekana Kwake yanakuwepo sawia, na tabia na nyayo Zake daima zitapatikana na wanadamu. Ndugu wapendwa, natumaini kwamba mnaweza kuona kuonekana kwa Mungu katika maneno haya, na kwamba mtaanza kuzifuata nyayo Zake kuelekea enzi mpya, na hadi katika mbingu mpya yenye kupendeza na dunia mpya iliyoandaliwa kwa wale wanaosubiri kuonekana kwa Mungu.
kutoka katika “Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya” katika Neno Laonekana katika Mwili

   Tazama zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni