8.29.2018

Upendo wa Mungu ni wa Kweli Kabisa

Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu, wokovu

Upendo wa Mungu ni wa Kweli Kabisa

Wenzhong , Beijing
Agosti 11, mwaka wa 2012
Usiku wa Julai 21, mwaka wa 2012, tulikuwa na mafuriko makubwa hapa, ambayo hutokea kwa nadra. Ningependa kumwambia kila mtu aliye na kiu ya Mungu kile nilichokipitia kwa kweli na kukiona wakati huo.
Siku hiyo mume wangu nami tuliutunza uga wa chakula kikavu cha mifugo wa dada yangu. Wakati wa usiku mvua nzito iliendelea kunyesha, na tulienda kulala mapema sana. Saa nne kasorobo usiku ndugu mkwe wangu wa kiume aliita akisema: “Wanaelekea kufungua hodhi! Kila kitu kitafurikiwa! Tunapaswa kuamka haraka!” Baada ya kusikia hayo nilishtuka, na yote niliyoyajua kumlilia Mungu ndani ya moyo wangu yalikuwa maneno, “Ee Mungu! Ee Mungu!” Nilijua tu kuwa nilipaswa kuilinda skuta ya umeme, na kicheza muziki cha MP5 na kadi ya TF inayotumika kwa kusikiliza nyimbo na mahubiri. Kwa wasiwasi mkubwa nilikwenda kwa bohari ili kuitoa skuta ya umeme, na nikaiendesha nikitaka kwenda nyumbani ili niviangalie vitabu vyangu vya maneno ya Mungu na pia kwa kuwa nilikuwa na wasiwasi kuwahusu mama mkwe wangu na watoto wangu. Niliiendesha skuta hadi barabara kuu, lakini kwa sababu sikuweza kuona vizuri kwa sababu ya mvua nzito niligonga kipande cha lami kilichokuwa kimezolewa ndani ya mvo, na skuta na mimi tukabiringika ndani ya maji. Katika moyo wangu nilikuwa nikisali, “Ee Mungu, ni haki Yako, kama nitasombwa na maji leo. Nijalie, nami nitafanya wajibu wangu kwa bidii tangu sasa!” Wakati huu kiatu kimoja changu kilikuwa kimezolewa na maji, kwa hiyo niliamua kuchukua barabara kuu. Lakini nilipoendelea mbele na kuangalia, nilishangaa; ilielekea kwamba upande huo wa barabara ulikuwa umetengwa kwa ua, na sikuweza kupita. Nilijikwaa ndani ya maji tena na kile kiatu changu kingine kilizolewa na maji. Maji sasa yalikuwa yamepanda hadi kwa mapaja yangu, na sikuwa na chaguo bali kurudi kwa mara ya tatu, wakati wote nikiomba moyoni mwangu. Wakati huu familia ya watu watatu ikaibuka kutoka kwa moja ya mashamba mengine ya nguruwe, na nikamshukuru Mungu kutoka moyoni mwangu. Nilijiunga nao na nilikuwa najiandaa kuingia barabara kuu tena, wakati mume wangu alikuja. Alitumia mpini wa kekee kufungulia shimo katika wavu wa waya na nilikuwa wa kwanza kupitia hapo kwa kuruka bila viatu na kuinuka na kwenda kwa barabara kuu. Kwa upande wa kusini kulikuwa mzingo katika mto unaotiririka kwelekea kaskazini, na kwa upande wa kaskazini barabara kuu ilikuwa ikimiminiwa na maji yakielekea upande wa kusini, kwa hiyo tulipatwa katikati na uchaguzi wetu wa pekee ukiwa ni kuchukua barabara kuu.
Nilipoingia barabara kuu na kuangalia chini, miguu yangu ikawa dhaifu. Karibu na mahali tunapokaa kuna kiwanda cha chuma; kijia cha takriban mita mbili au zaidi kwa upana hutenganisha kwetu na ukuta unaozunguka kiwanda. Maji yaliyokuwa ndani ya ukuta yalikuwa zaidi ya mita moja kwa kina, na hata nyumba zilizokuwa na vigae vya chuma vyenye rangi katika kiwanda zilikuwa zinaelea. Sasa niliomba tena: “Ee Mungu, nakushukuru Wewe kwa kuniokoa. Ni kwa sababu ya tamaa yangu ya utajiri ndio kwamba siyasikilizi maneno ya Mungu, na hutenda kwa kiburi. Nimekosea!” Kama maji yangekuwa yamepasuka kwa upande wa kaskazini, yangetusomba wakati fulani baada ya saa nane usiku. Yalikuwa, hata hivyo, yamepasukia kitakoni mwa ukuta wa upande wa kusini, na kuzamisha mashamba ya nguruwe bondeni. Wakati huu kwa kweli nilikuwa nimeuona uweza wa Mungu; kwa wale wanaomwamini Yeye hata maafa yataondoka.
Tulikaa katika shimo la magari kwa barabara kuu kwa karibu saa tatu kabla ya kulitoka na kwenda nyumbani. Nilipofika nyumbani na kufungua mkoba wangu wa chakula, kwa muujiza si kicheza muziki cha MP5 wala kadi ya TF iliyokuwa imelowa. Wakati skuta yangu ya umeme ilianguka ndani ya maji vitu hivi viwili viliingia pia; kifaa cha kuchaji skuta kilikuwa kimeloweshwa, na vitu vingine pia. Ni kicheza muziki changu cha MP5 na kadi ya TF pekee ambazo hazikuharibika. Nilikuwa nimeshuhudia matendo ya kustaajabisha ya Mungu.
Niliporudi kwa uga wa chakula kikavu cha mifugo, kile nilichokiona kilinishangaza. Kiwanja cha uga wa chakula kikavu cha mifugo kilijaa tu na mvua iliyokuwa imenyesha usiku kucha; si maji mengi yaliyokuwa yameingia ndani. Maji yalikuwa katika shamba ndogo la nafaka mbele ya nyumba, na yalikuwa yenye uketo katika shamba ndogo huko nyuma, lakini hapakuwa na maji mengi kwa sehemu ya uga wa chakula kikavu cha mifugo: Mungu alikuwa ameihifadhi.
Kwa njia ya mafuriko haya, moyo wangu umekuwa mtulivu zaidi, na sasa najua ni nini muhimu zaidi. Watu mara nyingi husema kwamba fedha ni kila kitu, lakini wakati maafa yanaposhambulia, fedha hazitaniokoa; Mungu ndiye Bwana wangu halisi. Sitafuatilia tena fedha, na nitaachana na uga wa chakula kikavu cha mifugo na kujitosa katika kazi ya kiinjili. Niliondoka siku hiyo kuhubiri injili kwa shangazi yangu, mama mkwe wangu na dada mkwe wangu. Walisikiliza uzoefu wangu na kuukubali. Katika siku za nyuma mama na dada mkwe wangu walikuwa wamenisumbua kwa kumwamini Mungu; nilikuwa nimewahubiria kwa miaka minne, lakini hawangeamini. Wakati huu niliona kwa dhahiri zaidi uweza wa Mungu. Mume wangu alinisumbua kabla, lakini sasa ameacha, na ninamhubiria injili. Katika siku za nyuma sikuweza kufungua kinywa changu kuhubiri, sikuthubutu kuzungumza. Kwa njia ya uzoefu huu mimi sitarudi nyuma tena; niko tayari kuweka jitihada zote kuchukua uzoefu wangu na kushuhudia. Kwa kuwa niliona na kupata uzoefu wa wokovu wa Mungu na upendo Wake wa kweli na halisi zaidi katika jaribio la maafa, ninawezaje kukosa kuwa na ushuhuda Kwake?

kutoka kwa Vita Baina ya Haki na Uovu

       Tazama zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni