Sura ya 35. Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro
Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo.
Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi zaidi na muhimu zaidi ya utendaji. Hili ndilo alilofanya Petro baada ya kumwona Yesu, na ni kwa kutenda kwa njia hii tu ndio mtu hupata matokeo bora zaidi. Kujitolea kwa moyo wote kwa maneno ya Mungu hasa kunamaanisha kutafuta ukweli, kutafuta nia ya Mungu ndani ya maneno Yake, kuzingatia kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na kuelewa na kupata ukweli zaidi kutoka kwa maneno ya Mungu. Wakati wa kusoma maneno Yake, Petro hakuwa anazingatia kuelewa mafundisho ya dini na hata alikuwa anazingatia kwa kiasi kidogo kupata maarifa ya teolojia; badala yake, alikuwa anazingatia kuelewa ukweli na kufahamu mapenzi ya Mungu, na kutimiza ufahamu wa tabia yake na uzuri wake. Pia alijaribu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na kuelewa asili potovu ya mwanadamu na dosari halisi za mwanadamu, akitimiza kila hali yote ya madai anayotaka Mungu kutoka kwa mwanadamu ili kumridhisha Yeye. Alikuwa na utendaji mwingi sahihi ndani ya maneno ya Mungu; hili linalingana sana na mapenzi ya Mungu, na ni ushirikiano bora zaidi wa mwanadamu katika uzoefu wake wa kazi ya Mungu. Wakati ambapo alipitia mamia ya majaribio kutoka kwa Mungu, alijichunguza kabisa dhidi ya kila neno la hukumu ya Mungu kwa mwanadamu, kila neno la ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, na kila neno la madai Yake kwa mwanadamu, na akajaribu kufikia maana ya maneno ya Mungu. Alijaribu kwa bidii kutafakari na kukariri kila neno ambalo Yesu alimwambia, na alitimiza matokeo mazuri sana. Kupitia njia hii ya utendaji aliweza kutimiza kujifahamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na hakuja tu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu, lakini pia alikuja kuelewa kiini cha mwanadamu, asili ya mwanadamu, na aina mbalimbali za dosari ambazo mwanadamu anazo—huku ni kujifahamu kwa kweli. Kutoka kwa maneno ya Mungu, hakutimiza tu kujifahamu kwa kweli, lakini kutokana na mambo yaliyoonyeshwa katika neno la Mungu—tabia ya Mungu yenye haki, kile Anacho na alicho, mapenzi ya Mungu kwa kazi Yake, mahitaji Yake kwa wanadamu—kutoka kwa maneno haya alikuja kumjua Mungu kabisa. Alikuja kujua tabia ya Mungu, na asili yake; alikuja kujua na kuelewa kile Mungu anacho na Alicho, uzuri wa Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu. Hata ingawa wakati huo Mungu hakuzungumza sana kama Anavyofanya leo, matunda yalipatikana ndani ya Petro katika hali hizi. Hili lilikuwa jambo adimu na la thamani. Petro alipitia mamia ya majaribio lakini hakuteseka bure. Hakuja kujielewa tu kutokana na maneno na kazi ya Mungu, lakini pia alikuja kumjua Mungu. Pia alizingatia hasa matakwa ya Mungu kwa wanadamu ndani ya maneno Yake, na ni katika hali gani mwanadamu anapaswa kumridhisha Mungu ili kukubaliana na mapenzi ya Mungu. Alifanya juhudi kubwa katika hali hii na akatimiza uwazi kamili; hili lilikuwa la manufaa sana kwa kuingia kwake mwenyewe. Haijalishi kile ambacho Mungu alizungumzia, maadamu maneno hayo yangeweza kuwa maisha yake na yalikuwa ya ukweli, aliweza kufanikiwa kuyaweka ndani ya moyo wake kuyatafakari mara nyingi na kuyaelewa. Baada ya kuyasikia maneno ya Yesu aliweza kuathiriwa nayo, ambalo linaonyesha kuwa alikuwa akizingatia hasa maneno ya Mungu, na alitimiza matokeo mwishowe kwa kweli. Yaani, aliweza kuyatia maneno ya Mungu katika vitendo kwa uhuru, kutenda kwa usahihi ukweli na kukubaliana na mapenzi ya Mungu, kutenda kikamilifu kwa mujibu wa nia ya Mungu, na kuacha maoni na mawazo yake mwenyewe. Kwa njia hii aliingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Huduma ya Petro ilikubaliana na mapenzi ya Mungu hasa kwa sababu alifanya hili.
Ikiwa mtu anaweza kweli kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu kutokana na mambo na maneno yanayohitajika na Yeye, basi atakuwa mtu aliyekamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yanafaa kabisa kwa mtu huyu, kwamba maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake, anapata ukweli, na anaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili asili ya mwili wake, yaani, msingi wa kuwepo kwake kwa asili, utatikisika na kuanguka. Baada ya mtu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yake anakuwa mtu mpya. Maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake; maono ya kazi ya Mungu, matakwa yake kwa mwanadamu, ufunuo wake kwa mwanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anahitaji mwanadamu kutimiza vinakuwa maisha yake—anaishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, na mtu huyu anageuka kukamilishwa na maneno ya Mungu. Anapitia kuzaliwa upya na anakuwa mtu mpya kupitia maneno Yake. Hii ni njia ambayo Petro aliitumia kuufuatilia ukweli; Ilikuwa njia ya kukamilishwa, kukamilishwa na maneno ya Mungu, na kupata uzima kutoka kwa maneno ya Mungu. Ukweli ulioonyeshwa na maneno ya Mungu ulikuwa maisha yake, na wakati huo tu ndipo alikuwa mtu aliyepata ukweli. Sote tunajua kwamba karibu wakati wa kupaa kwa Yesu, Petro alikuwa na fikira nyingi, kutotii, na udhaifu. Kwa nini yalibadilika kabisa baada ya hilo? Hili lina uhusiano wa moja kwa moja na ufuatiliaji wake wa ukweli. Kuelewa tu mafundisho ya dini hakuna maana; hakuwezi kuleta mabadiliko katika maisha. Kuelewa tu maana halisi ya neno la Mungu si sawa na kuelewa ukweli; yale mambo muhimu ambayo yanaelezwa kwa mifano katika maneno ya Mungu ndiyo ukweli. Kila sentensi ya maneno ya Mungu ina ukweli, lakini watu huenda wasiuelewe. Kwa mfano, neno la Mungu linasema, "Lazima muwe watu waaminifu": Kuna ukweli katika kauli hii. "Lazima muwe watu wanaomtii Mungu, wanaompenda Mungu, na wanaomwabudu Mungu." "Lazima mfanye wajibu wenu vizuri kama wanadamu." Kauli hizi zina ukweli hata zaidi. Kila sentensi ya maneno ya Mungu ina ukweli mwingi, na maneno mengi yanahitajika ili kufafanua kiini cha kila kauli ya ukweli; wakati kiwango hiki kinafikiwa tu ndipo kitafikiriwa kuwa ufahamu wa ukweli. Ikiwa unaelewa tu maana halisi na kuelezea maneno ya Mungu kulingana na maana halisi ya maneno hayo, huu sio ufahamu wa ukweli—huku ni kucheza tu na mafundisho ya dini.
Zamani, wakati maneno ya Mungu hayakuwa maisha ya watu, ilikuwa ni asili ya Shetani iliyotwaa madaraka na kutawala ndani yao. Ni mambo gani maalum yalikuwa ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini lazima ulinde nafasi yako mwenyewe? Kwa nini hisia zako ni kali sana? Kwa nini unapenda mambo hayo dhalimu, na kwa nini unapenda maovu hayo? Asili ya mambo haya ni nini? Yanatoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kuyakubali mambo haya? Hivi sasa nyote mmeelewa kuwa hili hasa ni kwa sababu ya sumu ya Shetani iliyo ndani ya mambo haya. Kile sumu ya Shetani kilicho kinaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu: Kwa nini unafanya hilo?" Watasema: “Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine.” Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida: Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu, na haijalishi wanachofanya, kama ni kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, wanajifanyia tu. Watu wote hudhani kwamba "Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine," kwamba hivi ndivyo ilivyo tu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuishi kwa ajili yake tu. "Kuhifadhi nafasi kwa ajili ya raha ya kiumbe" ni maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili ya mwanadamu. "Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine," kauli hii ya Shetani ni sumu yake hasa, na inapowekwa moyoni na mwanadamu inakua asili ya mwanadamu. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia kwa kauli hii; inamwakilisha kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya mwanadamu na inakuwa msingi wa kuwepo kwake; wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na hii kwa maelfu ya miaka. Kila kitu ambacho Shetani hufanya ni kwa ajili yake. Anataka kumpita Mungu, kujiondoa kwa Mungu na kushika mamlaka mwenyewe, na kumiliki vitu vyote ambavyo Mungu ameumba; Kwa hivyo, asili ya mwanadamu ni asili ya Shetani. Kwa kweli, wito wa watu wengi unaweza kuwakilisha na kuakisi asili yao. Haijalishi jinsi mwanadamu anavyoificha, katika kila kitu afanyacho na kila kitu asemacho, hawezi kuificha asili yake. Kuna baadhi ya watu ambao huwa hawasemi ukweli kamwe na wanajua sana kujifanya, lakini baada ya wengine kuingiliana nao kwa muda, asili yao ya udanganyifu na wao kutokuwa waaminifu kabisa kutagunduliwa. Muda utafichua yote. Baada ya kuwajua kwa muda, asili yao itagunduliwa. Mwishowe hitimisho litafanywa: Yeye kamwe huwa hasemi neno lolote la ukweli, na yeye ni mdanganyifu. Kauli hii ni ukweli wa asili yake; ni ushahidi na kielezo chake. Kwa hivyo, falsafa yake ya maisha ni kutomwambia yeyote ukweli, na pia kutomwamini mtu yeyote. Je, hili haliwakilishi asili yake? Asili ya mwanadamu ya kishetani ina kiwango kikubwa cha falsafa ndani yake. Wakati mwingine wewe mwenyewe huelewi vizuri, lakini unaishi kwa kutegemea hilo kila wakati. Unafikiri kuwa ni sahihi sana, yenye mantiki sana, na isiyo kosea. Falsafa ya Shetani inageuka kuwa ukweli wa mwanadamu, na watu wanaishi kwa mujibu wa falsafa yake kabisa bila ukinzani hata kidogo. Kwa hivyo, mwanadamu daima na kila mahali hufichua asili ya Shetani katika maisha, na daima huishi kwa falsafa ya shetani. Asili ya Shetani ni maisha ya mwanadamu. Kuhusu asili ni nini, hili linaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa kuifupisha kwa maneno. Katika asili ya mwanadamu kuna kiburi na ufuatiliaji wa kuwa bora zaidi na wa kipekee; kuna pia tamaa ya kutaka faida tu bila kuyajali maisha; kuna hila, uhalifu, na kuwadanganya watu kila upande; na kuna uovu na uchafu visivyovumilika. Huu ni muhtasari wa asili ya mwanadamu. Kwa hivyo, ikiwa unaweza kuja kujua mambo mengi katika asili ya mwanadamu, basi una ufahamu wa asili yako mwenyewe. Ikiwa hujagundua kitu chochote katika asili yako mwenyewe, basi huna ufahamu wowote wa hilo. Petro alitafuta ndani ya usafishaji wa maneno ya Mungu na ndani ya majaribio mbalimbali ambayo Mungu alimtolea ili aje kujijua, kuona kile alichofichua. Mwishowe alipokuja kujifahamu kweli, aligundua mwanadamu ni mpotovu sana, na hana thamani na hastahili kumtumikia Mungu, na kwamba mwanadamu hastahili kuishi mbele za Mungu. Alianguka chini mbele za Mungu. Mwishowe alihisi: "Kumjua Mungu ni jambo la thamani zaidi! Kama singeweza kumjua Mungu, kifo changu kingekuwa cha aibu mno. Nahisi kwamba kumjua Mungu ndilo jambo muhimu sana, la maana sana. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu basi hastahili kuishi—basi hakuna uzima." Wakati uzoefu wa Petro ulikuwa umefikia kiwango hiki, alikuwa na ufahamu kiasi wa asili yake mwenyewe. Aliielewa vizuri kiasi, na ingawa hangeweza kutumia lugha kuielezea vizuri kabisa kulingana na fikira za wanadamu za sasa, alifikia eneo hili. Kwa hivyo, ufuatiliaji wa njia ya uzima ili kukamilishwa na Mungu ni kuelewa zaidi asili ya mtu mwenyewe ndani ya maneno ya Mungu na kuelewa mambo yaliyo ndani ya asili ya mtu. Kuufupisha kwa maneno, kuelewa kabisa maisha ya mtu ya kale—maisha ya asili ya kale ya shetani—huku ni kuweza kutimiza matokeo yaliyohitajika na Mungu. Ikiwa ufahamu wako haujafikia kiwango hiki lakini unasema unajielewa na kwamba umepata uzima, je, huku sio kujisifu tu? Hujijui, na hujui ulicho mbele za Mungu, kama umepata kiwango cha mwanadamu kweli, au ni vitu vingapi vya Shetani ambavyo bado unavyo. Huelewi vizuri wewe ni wa nani na hata hujifahamu—basi unawezaje kuwa na sababu mbele za Mungu? Wakati Petro alikuwa akiufuatilia uzima, katikati ya majaribio yake alizingatia kujielewa na kubadilisha tabia yake. Alijitahidi kumwelewa Mungu, na mwishowe akahisi: "Mwanadamu lazima afuatilie kumfahamu Mungu maishani; kumfahamu Mungu ndilo jambo muhimu sana; ikiwa simjui Mungu basi siwezi kupumzika kwa amani nitakapokufa. Mungu anaponifanya nife baada ya kumjua, nitahisi kwamba ni jambo la kupendeza zaidi, sitalalamika hata kidogo, na maisha yangu yote yatatimizwa."Petro hakuweza kupata ufahamu huu na kufikia kiwango hiki punde baada ya kuanza kumwamini Mungu—alipaswa kupitia majaribio mengi kwanza. Uzoefu wake ulipaswa kufikia kiwango fulani na alipaswa kujifahamu kabisa kabla ya kuweza kuhisi thamani ya kumjua Mungu. Kwa hivyo, njia aliyoishika ilikuwa njia ya uzima na ya kukamilishwa; utendaji wake maalum ulizingatia hali hii hasa.
Je, nyote mnaishika njia gani sasa? Ikiwa hamjafikia ufuatiliaji wa maisha, wa kujifahamu, au kumfahamu Mungu kama Petro, basi hiyo bado si njia ya Petro. Hivi sasa watu wengi wako katika aina hii ya hali: "Ili kupata baraka ni lazima nijitumie kwa ajili ya Mungu na kulipa gharama kwa ajili Yake. Ili kupata baraka ni lazima niache kila kitu kwa ajili ya Mungu; lazima nikamilishe kile ambacho ameniaminia na kutekeleza wajibu wangu vizuri." Hili linatawaliwa na nia ya kubarikiwa; ni kutumika kwa kusudi la kupata thawabu za Mungu, kwa ajili ya kupata taji. mtu wa aina hii hana ukweli ndani ya moyo wake, na hakika anaelewa tu maneno fulani ya mafundisho ya dini ambayo anaringia kila mahali. Njia yake ni njia ya Paulo. Kumwamini Mungu kwa mtu wa aina hii ni kitendo cha kazi ya siku zote, na katika akili yake anahisi kuwa kadri anavyofanya, ndivyo itakavyothibitisha zaidi kuwa ni mwaminifu kwa Mungu, kwamba kadri anavyofanya ndivyo Mungu ataridhika zaidi, na kwamba kadri anavyofanya ndivyo anavyopaswa zaidi kupata taji mbele za Mungu, na hakika atapata baraka kubwa zaidi katika nyumba ya Mungu. Anahisi kwamba kama anaweza kuvumilia mateso, kuhubiri, na kufa kwa ajili ya Kristo, kama anaweza kuyadharau maisha yake mwenyewe, na kama anaweza kukamilisha wajibu wote ambao Mungu alimwaminia nao, basi atakuwa mtu mwenye kubarikiwa zaidi na Mungu, yule anayepata baraka nyingi zaidi, na hakika atapokea taji. Hili ndilo hasa alilowaza Paulo alilofikiri na kile alichofuatilia; hii ndiyo hasa njia ambayo Paulo alitembea, na ilikuwa chini ya uongozi wa mawazo haya ndio Paulo alifanya kazi kumhudumia Mungu. Je, mawazo na madhumuni kama hayo hayatoki kwa asili ya Shetani? Kama tu watu wa dunia, hapa duniani lazima nifuatilie maarifa, na baada ya kupata maarifa tu ndio ninaweza kufanikiwa, kuwa afisa, na kuwa na cheo. Mara baada ya kupata cheo ninaweza kufikia lengo langu na kuifikisha nyumba yangu na biashara kwa viwango fulani. Je, wasioamini wote huwa hawaifuati njia hii? Wale ambao wanatawaliwa na asili hii ya shetani wanaweza tu kuwa kama Paulo baada ya kumwamini Mungu: "Ni lazima niache kila kitu ili nijitumie kwa ajili ya Mungu, lazima niwe mwaminifu mbele za Mungu, na mwishowe nitapokea taji kubwa zaidi na baraka kubwa zaidi." Hii ni sawa na watu wa dunia wanaofuatilia vitu vya dunia, hakuna tofauti kabisa, na wanapaswa kutii asili hiyo. Watu wana asili ya shetani, kwa hiyo ulimwenguni watafuatilia maarifa, hadhi, kujifunza, na mafanikio ya dunia; nyumbani mwa Mungu, watatafuta kujitumia kwa ajili ya Mungu, kuwa waaminifu, na hatimaye watapokea taji na baraka nyingi. Kama watu hawana ukweli baada ya kumwamini Mungu na hawajakuwa na mabadiliko katika tabia yao, basi bila shaka watakuwa kwenye njia hii—huu ni ukweli ambao hakuna mtu anayeweza kuupinga, na ni wenye kupinga kabisa njia ya Petro. Nyote mnaishika njia gani sasa? Ingawa huwezi kupanga kuishika njia ya Paulo, asili yako inakutawala kwa njia hii, na unaelekea upande huo bila kupenda. Ingawa unataka kuishika njia ya Petro, ikiwa hufahamu vizuri jinsi ya kulifanya hilo, basi bado utaishika njia ya Paulo bila kupenda—huu ni ukweli wa hali hiyo.
Kwa hiyo mnawezaje hasa kuishika njia ya Petro? Kama huwezi kubainisha kati ya njia ya Petro na njia ya Paulo, au huzijui kabisa, basi hata ukisema unapaswa kuishika njia ya Petro hayo yatakuwa maneno matupu. Unahitaji kwanza kufahamu katika mawazo yako njia ya Petro ni gani na njia ya Paulo ni gani. Kama kweli unaelewa kwamba njia ya Petro ni njia ya uzima na njia pekee ya kukamilishwa, wakati huo tu ndipo utaweza kujua na kufahamu ukweli na njia maalum za kuishika njia yake. Ikiwa huifahamu njia ya Petro, basi njia unayoishika bila shaka itakuwa ya Paulo kwa sababu hakutakuwa na njia nyingine—hutakuwa na budi. Kama huna ukweli na huna hamu za kupata kitu basi ni vigumu kuishika njia ya Petro. Inaweza kusemekana kwamba Mungu amewafichulia sasa njia ya kuokolewa naye na ya kukamilishwa. Hii ni neema ya Mungu na kutia moyo na ni Yeye anayewaongoza kwenye njia ya Petro. Bila uongozi na kupata nuru kutoka kwa Mungu hakuna ambaye angeweza kuishika njia ya Petro; chaguo la pekee lingekuwa kuelekea kwa njia ya Paulo, kuzifuata nyayo za Paulo kuelekea kwa uharibifu. Wakati huo, Paulo hakuhisi kwamba haikuwa sahihi kutembea kwenye njia hiyo. Aliamini kwa ukamilifu kwamba ilikuwa sahihi, lakini hakuwa na ukweli na hasa hakuwa na mabadiliko katika tabia. Alijiamini kupita kiasi na akahisi kwamba hakukuwa na ubaya wowote kuishika njia hiyo. Aliendelea akiwa amejaa imani na kwa kujihakikishia kabisa. Kufikia mwisho, hakupata fahamu, bado alifikiria kwamba kwake kuishi ilikuwa ni Kristo. Aliendelea kuishika njia hiyo hadi mwisho, na alipoadhibiwa mwishowe, yote ilikuwa imekwisha. Njia ya Paulo haikuhusisha kujijua au ufuatiliaji wa mabadiliko katika tabia. Hakuchangua kamwe asili yake mwenyewe na hakuwa na ufahamu wa kile alichokuwa; alijua tu kwamba alikuwa mkosaji mkuu katika kumtesa Yesu. Hakuwa amepata ufahamu hata kidogo wa asili yake mwenyewe, na baada ya kumaliza kazi yake alihisi kwamba alikuwa Kristo na anapaswa kupewa thawabu. Kazi ambayo Paulo alifanya ilikuwa tu kutoa huduma kwa Mungu. Kwake mwenyewe, ingawa alipokea ufunuo kiasi kutoka kwa Roho Mtakatifu, hakuwa na ukweli au uzima hata hivyo. Hakuokolewa na Mungu—aliadhibiwa. Kwa nini inasemekana kwamba njia ya Petro ni njia ya kukamilishwa? Kwa sababu katika utendaji wake alizingatia hasa uzima, alifuatilia ufahamu wa Mungu, na akazingatia kujifahamu. Kupitia uzoefu wake wa kazi ya Mungu alikuja kujijua, alipata ufahamu wa hali potovu za mwanadamu, alijua kasoro zake, na ni jambo gani lilikuwa muhimu sana kwa mwanadamu kulifuatilia. Aliweza kumpenda Mungu kwa dhati, alijua jinsi ya kumlipa Mungu, alipata ukweli kiasi, na alikuwa na ukweli ambao Mungu huhitaji. Kutoka kwa vitu vyote alivyosema wakati wa majaribio yake, inaweza kuonekana kwamba Petro alikuwa kweli mwenye ufahamu zaidi wa Mungu. Kwa sababu alielewa ukweli mwingi sana kutoka kwa maneno ya Mungu, njia yake ikawa yenye kung'aa zaidi na zaidi na kuzidi kufungamana na mapenzi ya Mungu. Kama hangekuwa amepata ukweli huu, basi hangeweza kuendelea kuishika njia sahihi kama hiyo.
Hivi sasa bado kuna swali hili: Kama unajua njia ya Petro ilikuwa gani, je, unaweza kuishika? Hili ni swali halisi. Lazima uweze kubainisha wazi ni mtu wa aina gani anaweza kuishika njia ya Petro na mtu wa aina gani hawezi. Wakati watu ni wakosefu hawawezi kukamilishwa na Mungu. Wale ambao wanashika njia ya Petro lazima wawe bila kosa; kama wewe ni mtu asiye na kosa tu ndipo unaweza kukamilishwa. Wale walio kama Paulo hawawezi kuishika njia ya Petro. Aina fulani ya mtu ataishika aina fulani ya njia; hii linaamuliwa kabisa na asili yake. Haijalishi jinsi unavyomwelezea Shetani kwa dhahiri njia ya Petro, hawezi kuitembea. Hata kama angetaka, hangeweza kuishika. Asili yake imeamua kwamba hawezi kuishika njia hiyo. Ni wale tu wanaopenda ukweli ndio wanaweza kuishika njia ya Petro. Mito na milima inaweza kubadilishwa lakini ni vigumu kubadilisha asili ya mwanadamu; kama hakuna dalili za kuupenda ukweli ndani ya asili yako, basi hustahili kwenda kwenye njia ya Petro. Kama wewe ni mtu anayependa ukweli, kama unaweza kukubali ukweli licha ya tabia yako potovu, unaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu na unaweza kuelewa mapenzi ya Mungu, kwa njia hii utaweza kuunyima mwili na kutii mpango wa Mungu. Wakati una mabadiliko katika tabia yako baada ya kupitia majaribio kiasi, hili linamaanisha kuwa polepole unakanyaga kwenye njia ya Petro ya kukamilishwa.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni