Tamko la Arubaini na Moja
Mwenyezi Mungu alisema, Wakati mmoja Nilianza shughuli kubwa miongoni mwa wanadamu, lakini hawakutambua, kwa hivyo ilinibidi Nitumie neno Langu ili kuwafichulia. Na hata hivyo, mwanadamu bado hangeweza kuyaelewa maneno Yangu, na akasalia kutojua malengo ya mpango Wangu.
Na hivyo kwa sababu ya kasoro na dosari za mwanadamu, alifanya mambo ili kukatiza mpango Wangu wa usimamizi, na pepo wachafu wakachukua nafasi ya kujidhihirisha, wakawafanya wanadamu kafara wao, mpaka wakateswa na pepo hao wachafu na wakachafuliwa kila mahali. Ulikuwa wakati huu ambapo Niliona nia ya mwanadamu na kusudi lake. Nilishusha pumzi kutokana na kushindwa kuelewa: Ni kwa nini sikuzote lazima mwanadamuatende kwa ajili ya maslahi yake? Je, kuadibu Kwangu hakukusudii kumkamilisha? Je, Najaribu kumvunja moyo? Lugha ya mwanadamu ni nzuri sana, na nyororo, lakini matendo ya wanadamu ni mabaya mno. Kwa nini matakwa Yangu kwa mwanadamu kila mara huambulia patupu? Ni kana kwamba Nilikuwa Namtaka mbwa apande mti? Je, Najaribu kuleta taabu bila sababu? Ninapotekeleza mpango Wangu wote wa usimamizi, Nimeumba "viwanja mbalimbali vya majaribio," hata hivyo kwa ajili ya mandhari mabaya, na kwa ajili ya miaka mingi sana ya kutokuwa na mwanga wa jua, mandhari yanabadilika siku zote, yakisababisha kubomoka kwayo, na kwa hivyo katika kumbukumbu Yangu, Nimetupa viwanja vingi vya aina hii. Na bado sasa, sehemu kubwa ya mandhari inaendelea kubadilika. Kama siku moja dunia itabadilika kwa kweli kuwa aina nyingine, Nitaiweka kando bila kusita—je, hiyo si hatua ambayo Niko ndani sasa katika kazi Yangu? Lakini mwanadamu hana hisia hata kidogo kuhusu jambo hili. Anaadibiwa tu chini ya uongozi Wangu. Ya nini kujisumbua? Je, Mimi ni Mungu aliyekuja ili kumwadibu mwanadamu? Katika mbingu, wakati mmoja Nilipanga kwamba mara tu Ningekuwa miongoni mwa wanadamu, Ningejiunganisha nao, ili wale wote Niwapendao wangeweza kuwa karibu nami bila chochote kutugawanya. Hata hivyo, wakati huu, katika hali za leo, hatuwasiliani tu, zaidi ya hayo, wao hukaa mbali nami kwa sababu ya kuadibu Kwangu, Silii kwa ajili ya kutokuwapo kwao. Ni nini chaweza kufanywa? Wanadamu wote ni wachezaji wanaokubaliana na kundi. Ningewaacha wanadamu waponyoke kutoka kwa fumbato Langu, na hata zaidi Nitaweza kuwaacha warudi katika kiwanda Changu kutoka nchi za kigeni. Wakati huu, wangeweza kuwa na malalamiko gani? Mwanadamu anaweza kunifanya nini? Je, si wanadamu hushawishiwa kwa urahisi? Na hata hivyo, Simdhuru mwanadamu kwa kosa hili, bali badala yake Nampa lishe Yangu. Nani aliwalazimisha watende kidhaifu? Nani aliwafanya wakose lishe? Naisisimua mioyo baridi ya wanadamu kwa kumbatio Langu kunjufu, nani mwingine anaweza kufanya jambo kama hilo? Kwa nini Nimeipanua kazi hii miongoni mwa wanadamu? Je, mwanadamu anaweza kuufahamu moyo Wangu kweli?
Miongoni mwa watu wote ambao Nimechagua, Nimeshiriki katika shughuli, na kwa hiyo kila mara watu wengi huja na kutoka nyumbani Kwangu kwa mtiririko usiokoma. Wote hushiriki katika kanuni mbalimbali Kwangu, kana kwamba wanajadiliana na Mimi biashara, kiasi kwamba kazi Yangu ina shughuli nyingi sana hivi kwamba wakati mwingine Sina nafasi ya kushughulikia mizozo yote ya wanadamu. Nawasihi wanadamu wasiwe kero Kwangu, na waendeshe shughuli zao wenyewe badala ya kunitegemea siku zote. Wasitende kila mara kama watoto ndani ya nyumba Yangu; hiyo ni faida gani? Kazi Yangu ni biashara kubwa. Si duka fulani la mtaani, au kijiduka. Kila mara wanadamu hukosa kufahamu hali ya akili Yangu, inavyoonekana wanafanya mzaha kwa makusudi. Ingeonekana mwanadamu anapenda kuzurura kila mahali kama mtoto, hazingatii biashara ya maana kamwe, na kwa hivyo wengi hushindwa kutimiza "zoezi la kufanyia nyumbani" Ninalowapangia. Na kwa hiyo wanadamu hawa wanathubutu vipi kwenda mbele ya "mwalimu"? Kwa nini huwa hawafanyi wajibu wao asilani? Moyo wa mwanadamu ni kitu cha aina gani? Hata sasa Sielewi. Kwa nini mioyo ya wanadamu huwa inabadilika kila mara? Kama vile siku katika mwezi wa Juni, mara kwa mara jua lenye joto kali huwa katili, nyakati zingine mawingu huwa meusi na mazito, na nyakati zingine upepo mkali huvuma. Hivyo kwa nini wanadamu hawawezi kujifunza kutokana na uzoefu wao? Labda huku ni kutia chumvi. Wanadamu hawajui kubeba mwavuli wakati wa msimu wa mvua, hivyo kwa sababu ya kutojua kwao wamelowa mara nyingi kwa kuonekana ghafula kwa mvua kutoka mbinguni, kana kwamba Nilikuwa Nawachokoza kwa makusudi na walikuwa wanavamiwa kila mara na mvua ya mbinguni. Au labda ni kwamba Mimi ni "katili" sana, Nikimfanya kila mtu kuwa msahaulifu na hivyo asiye makini, asijue la kufanya siku zote. Hakuna mwanadamu ambaye amewahi kuelewa kusudi au umuhimu wa kazi Yangu. Kwa hiyo wote hufanya kazi ya kujiletea taabu, na kujiadibu. Yawezekana kwamba Nawaadibu kwa makusudi? Kwa nini wanadamu hujiletea taabu? Kwa nini kila mara wao huingia mtegoni moja kwa moja? Mbona wasijadiliane na Mimi, lakini badala yake wao hujitafutia kazi? Yawezekana kwamba Nawapa wanadamu kidogo sana?
Nilichapisha kazi Yangu ya kwanza miongoni mwa wanadamu wote, na kazi Yangu ilipowafanya watu waipende sana, wote walikuwa makini kuisoma, na kupitia kwa masomo yao ya uzingatiaji walikuwa walipata mengi. Inaonekana kazi Yangu ni kama riwaya iliyo ngumu kueleweka, ya kustaajabisha, kama shairi la nathari lenye kusisitiza hisia, kama mazungumzo ya programu ya siasa, kama mchanganyiko wenye utata wa maarifa ya kawaida ya kiuchumi. Kwa kuwa kazi Yangu ya fahari sana, kuna maoni mengi yanayotofautiana kuihusu, na hakuna anayeweza kutoa muhtasari wa dibaji ya kazi Yangu. Ingawa mwanadamu ana ufahamu na kipaji "vilivyojipambanua", kazi hii Yangu tu inatosha kuwakanganya mashujaa wote. Wakati wanadamu wanasema "damu yaweza kutiririka, machozi yaweza kutoka, lakini mtu hapaswi kuinamisha kichwa chake kwa aibu," wao wanainamisha vichwa vyao kwa aibu bila kujua, kwa kuonyesha kujisalimisha kwao kwa kazi Yangu. Mwanadamu amefanya muhtasari wa kile alichojifunza kupitia kwa uzoefu wake, akisema kwamba[a] ni kana kwamba kazi Yangu ni kitabu cha mbinguni ambacho kimeanguka kutoka angani, lakini Namsihi sana mwanadamu asiwe mwepesi zaidi kuhisi. Kwa maoni Yangu, yote ambayo Nimesema ni ya kawaida sana; hata hivyo, Natumai kwamba kutoka kwa Ensaiklopidia ya Maisha katika kazi Yangu, watu wanaweza kupata njia ya riziki, na kutoka kwa Hatima ya Mwanadamu, waweze kupata maana ya uzima, na kutoka kwa Siri za Mbinguni, waweze kupata mapenzi Yangu, na kutoka kwa Njia ya Wanadamu, wanaweza kugundua ustadi wa kuishi. Je, hili halingekuwa hata bora zaidi? Simlazimishi mwanadamu; kwa wale ambao hawana haja na kazi Yangu, "Nitawalipa" kwa ajili ya kitabu Changu, pamoja na "gharama ya huduma." Simfanyi mwanadamu atende kwa kusita. Kama mwandishi wa kitabu hiki, tumaini Langu tu ni kwamba wasomaji wataipenda kazi Yangu, lakini kile ambacho watu hufurahi huwa tofauti kila mara. Kwa hiyo Nawasihi sana wanadamu wasitie matatani matarajio yao ya siku za baadaye kwa ajili ya kujiepusha na aibu. Kama huo ungekuwa ukweli, Ningewezaje, jinsi Nilivyo mwenye huruma, kustahamili aibu kama hiyo? Kama mnapenda kazi Yangu, Natumai kwamba mtanipa mapendekezo yenu wenyewe ya thamani, ili Niweze kuendeleza uandishi Wangu, na hivyo kupitia kwa makosa ya mwanadamu Niendeleze maudhui ya uandishi Wangu. Hili linamfaidi mwandishi na msomaji, au sio? Sijui kama hili linaweza kufikiriwa kuwa sahihi. Labda kwa njia hii Naweza kuzidisha ubora wa uwezo Wangu wa kuandika, na kuimarisha urafiki wetu. Kwa jumla, Natumai kwamba wote wanaweza kushirikiana na kazi Yangu, bila pingamizi, ili maneno Yangu yaweze kuenezwa kwa kila familia na nyumba, na ili watu wote duniani waweze kuishi kati ya neno Langu. Hili ndilo lengo Langu. Natumai kwamba kupitia kwa Sura inayohusu Uzima katika maneno Yangu watu wote wanaweza kupata kitu, kama vile kanuni za maisha, au ufahamu wa[b] makosa miongoni mwa wanadamu, au ni nini Ninachohitaji kutoka kwa mwanadamu, au “siri” za watu wa ufalme wa leo. Hata hivyo, Nawasihi sana wanadamu waangalie Kashfa za Mwanadamu Leo; haya yanaweza kuwa ya manufaa kwa wote. Unaweza pia kusoma Siri ya Karibuni Zaidi, ambayo yanaweza kuwa hata ya manufaa zaidi kwa maisha ya watu. Pia kuna Mada Motomoto—Je, haya si ya manufaa hata zaidi kwa maisha ya watu? Hakuna madhara katika kutumia ushauri Wangu, na kuona kama una athari yoyote, na kunielezea vile mnahisi baada ya kuyasoma, ili Niweze kuandika maagizo ya matumizi ya dawa sahihi, ambayo mwishowe inaweza kukomesha kabisa magonjwa ya wanadamu. Sijui vile mapendekezo Yangu yatafanya kazi, lakini Natumai kwamba mnaweza kuyatumia kama marejeleo. Mnafikiriaje?
Mei 12, 1992
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili yanaacha “akisema kwamba.”
b. Maandishi ya asili yanaacha “ufahamu wa.”
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni