5.26.2018

"Siri ya Utauwa: Mfuatano" (4) - Kwa Nini Mungu Anakuwa Mwili Mara Mbili ili Kuwaokoa Wanadamu

"Siri ya Utauwa: Mfuatano" (4) - Kwa Nini Mungu
Anakuwa Mwili Mara Mbili ili Kuwaokoa Wanadamu

    Katika Enzi ya Neema, Mungu mwenye mwili alipigiliwa misumari msalabani, Akazichukua dhambi za mwanadamu na kukamilisha kazi ya kuwakomboa wanadamu. Katika siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Amepata mwili kuonyesha ukweli na kumtakasa na kumwokoa mwanadamu kabisa. Hivyo kwa nini Mungu anahitaji kupata mwili mara mbili ili kufanya kazi ya wokovu wa mwanadamu?  Mwenyezi Munguasema, "Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. ... Kupatikana kwa mwili mara ya pili kunatosha kumaliza dhambi za mwanadamu na kumtakasa mwanadamu. Hivyo, kupatikana kwa mwili mara ya pili kutafikisha tamati kazi yote ya Mungu mwenye mwili na kukamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili" (Neno Laonekana Katika Mwili).

    Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni