Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Tano |
Umeme wa Mashariki | Sura ya 35
Kama alivyosema Mungu, “Kila mtu ana tabia nzuri, na hakuna anayethubutu kupinga. Wote wako chini ya uongozi Wangu, wakifanya kazi zao Nilizowapa.” Kwa dhahiri, hakuna binadamu hata mmoja hupokea kuadibu kwa radhi, na zaidi ya hayo, hili hutoka kwa Mungu, kwa sababu binadamu wote hutaka kuishi katika raha badala ya ghasia na vurugu. Mungu alisema, “Ni nani asiye na hofu ya kifo? Je, watu wako tayari kweli kujitoa mhanga?” Hii ni kweli kabisa; kila mtu huogopa kufa isipokuwa, bila shaka, wakati ambapo ameliwa na hasira au kukata tamaa. Hii ni dutu ya binadamu, na ndiyo ngumu zaidi kuihepa. Leo Mungu amekuja hasa kusuluhisha mashaka haya. Binadamu wote ni wadhaifu, kwa hiyo Mungu amefanya kila juhudi kuja miongoni mwao kuanzisha hospitali ya kitaalam ili kuwatibu aina hii ya ugonjwa. Watu hawawezi kujinasua wenyewe kwa ugonjwa huu wa kutatiza, ndiyo kwa sababu wote hupata wasiwasi sana mpaka wakawa na uvimbeuchungu wa mdomo, na tumbo zao kupanuka. Baada ya muda wingi wa gesi waliyonayo hukua, na kusababisha ongezeko la shinikizo. Hatimaye, tumbo zao hupasuka na wote hufa. Kwa hivyo, wakati huo, Mungu ametibu haya maradhi mabaya ya binadamu, kwa sababu kila mtu amekufa. Je, huku si kutibu hali ya binadamu? Mungu kwa makusudi amekuja kuifanya kazi hii. Kwa sababu watu huogopa kifo kupita kiasi, Mungu Mwenyewe amekuja kushiriki kazi sawa na binadamu; kwa sababu wana ujasiri kidogo sana, Ameanza kwa kutoa maonyesho ya watu kutazama. Ni baada tu ya kuona kitangulizi hiki ndipo mtu yeyote huwa radhi kutii. Kwa sababu hii, Mungu alisema, “Kwa kuwa hakuna mtu ambaye angeifanya kazi Yangu, Nimeingia vitani binafsi kukumbana na mapambano ya kufa na kupona dhidi ya Shetani.” Hivi ni vita vya kuamua mshindi na mshinde, kwa hiyo ama samaki wafe au wavu ukatike[c]. Hili ni hakika. Kwa kuwa roho itashinda mwishowe, mwili lazima uwe shabaha ya kifo. Je, mnaelewa athari za hili? Hata hivyo, msiwe wepesi kuathirika kupita kiasi. Labda sentensi hii ni rahisi, au labda ni changamano. Hata hivyo, binadamu bado hawawezi kuielewa. Hili ni hakika. Binadamu wanaweza, kutokana na kuteseka kwao, kukubali usafishaji wa neno la Mungu; kisha mtu angeweza kusema kwamba hii ni bahati yao nzuri. Hata hivyo, ingeweza pia kusemekana kuwa ya bahati mbaya kwao. Ningependa bado kumkumbusha kila mtu, hata hivyo, kwamba kusudi la Mungu ni sahihi, hata hivyo—tofauti na makusudi ya binadamu, ambayo kila mara ni kuhusu kujifanyia wenyewe mipango na matayarisho. Mnapaswa kuelewa hili, na kutozama katika tafakari zisizoisha. Je, huu sio udhaifu wa binadamu kabisa? Wote wako hivi; badala ya kumpenda Mungu kwa kiwango fulani, wao hujipenda wenyewe kwa kiwango fulani. Kwa kuwa Yeye ni Mungu ambaye ni mwenye wivu kwa binadamu, Yeye kila mara huwawekea matakwa. Kadri ambavyo watu hujipenda wenyewe, ndivyo Mungu huwahitaji zaidi wampende Yeye, na ndivyo matakwa Yake kwao huwa makali. Ni kana kwamba Mungu anawachokoza watu kwa kudhamiria. Kama watu wanampenda Yeye kweli, basi inaonekana Yeye hajali kuhusu hilo. Kwa sababu ya hili, watu wote wanakwaruza vichwa vyao na kubinya masikio yao wanapozama katika tafakari. Hii ni hadithi ya tabia ya Mungu, kutaja kwa ufupi tu kwa jambo moja au mawili. Haya ni mapenzi ya Mungu. Ni kile ambacho Mungu huwataka watu kujua; ni muhimu. Ni kazi mpya inayohitaji ninyi watu kuweza kufanya bidii kupenya na kufanya maendeleo mengine mapya. Je, unaelewa hili? Unataka Nisema mengi zaidi kuhusu mada hii?
Kuhusu enzi za awali, Mungu alisema, “hakuna mtu hata mmoja aliyechaguliwa na Mimi; kila mmoja alikataliwa na kimya Changu. Hii ni kwa sababu watu hao wa kale hawakunitumikia kwa kujitolea kwa roho moja; hivyo basi Nami wala sikuwapenda kipekee. Walikuwa wamechukua ‘vipawa’ vya Shetani na kisha wakageuka na kunitolea Mimi; kwa kufanya hivyo, je, huu haukuwa udanganyifu Kwangu?” Maneno haya yanawezaje kuelezwa? Ni kama alivyosema Mungu: “Vipaji vyote hutoka kwa Shetani.” Vizazi vya zamani vya mitume na manabii walitegemea kabisa vipaji vyao walipofanya kazi yao, na kotekote katika enzi, Mungu ametumia vipaji vyao kuendesha kazi Yake. Hii ndiyo maana inasemekana kwamba huduma ya watu wote wenye vipaji hutoka kwa Shetani. Hata hivyo, kama asemavyo Mungu[d], “Natumia ujanja wa Shetani kama foili[e]” kwa ajili ya hekima Yake. Hivyo, Mungu ametaja huduma ya watu wenye vipaji kama zawadi kutoka kwa Shetani. Kwa sababu wao ni wa Shetani, Mungu huwaita waliojaa kashfa. Hii si shutuma isiyo na msingi dhidi ya binadamu; ni ufafanuzi wenye msingi mzuri na wa kufaa. Kwa sababu hii, Alisema, “Sikufichua ghadhabu Yangu; badala yake, Nilijaribu kubadili mpango wao kwa matumizi Yangu mwenyewe kwa kuongezea ‘vipawa’ hivi kwa vifaa vinavyotumika katika usimamizi Wangu. Baadaye, mara tu vilipokuwa vimesindikwa na mtambo, Ningechoma masalio yote ya takataka.” Hiki ndicho cha ajabu sana kuhusu kazi ya Mungu. Wazo hili ni la chini mno kukubaliana na fikira za binadamu, kwa sababu hakuna ambaye angefikiri kwamba wale wanaotawala kama wafalme si watu wenye vipaji, ni watu wasio na vipaji ambao Mungu huwapenda. Kama inavyoweza kuonekana, mawazo au matumaini ya Witness Lee na Watchman Nee yote yamegeuka kuwa jivu—na watu wenye vipaji katika siku za sasa sio jambo la pekee. Sasa Mungu ameanza kazi hii, na Anachukua polepole kazi yote ya Roho Mtakatifu ndani ya binadamu ambao huhudumu kama foili kwa kazi Yake. Kazi ya Mungu itakapomalizika kabisa, watu hawa wote watarudi mahali pao pa asili. Hata hivyo, Nawasihi binadamu wasitende kwa kutojali kutokana na kile ambacho Nimesema. Lazima mfuate mkondo, kuzifuata hatua za kazi ya Mungu ili kuepuka kuikatiza. Je, mnaelewa hoja hii? Kwa sababu hii ni hatua na mbinu ya kazi ya Mungu. Wakati ambapo Mungu “atatengeneza” “zawadi” hizi ziwe “bidhaa zilizokamilishwa,” makusudi Yake yote yatakuwa wazi, na zawadi zinazomfanyia Yeye huduma zitaondoshwa zote; hata hivyo, Mungu atakuwa na bidhaa zilizokamilishwa kufurahia. Je, mnaelewa hili? Kile ambacho Mungu hutaka ni bidhaa zilizokamilishwa, sio zawadi za fahari ambazo hutolewa na binadamu. Ni wakati ambapo tu kila mtu amechukua pahali pake pa kufaa, kumaanisha wakati ambapo Mungu amerudi katika nafasi Yake ya asili na shetani, pia, ameketi katika kiti chake, na vilevile malaika, bila kinzano—wakati huo tu ndipo tabasamu ya kupendezwa itaonekana katika uso wa Mungu, kwa sababu makusudi Yake yatakuwa yameridhishwa, lengo Lake limetimizwa. Mungu hatatafuta tena “usaidizi” kutoka kwa “shetani,” kwa sababu makusudi ya Mungu yatakuwa yamefichuliwa kwa dhahiri kwa binadamu, na binadamu kamwe hawatalazimika kuyawasilisha. Wakati huu, miili yao ya tamaa za mwili itakuwa kitu kimoja na roho zao. Hili ndilo Mungu huwafichulia binadamu; ni makusudio ya mwisho ya roho, nafsi, na mwili. Ni muhtasari wa wazo la asili la “ubinadamu.” Hili halihitaji kuchunguzwa kwa utondoti; inatosha kujua jambo moja au mawili kulihusu. Je, mnaelewa?
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili yanasoma “Je, hiki si kile ambacho Mungu hutimiza na binadamu leo?”
b. Maandishi ya asili yanaacha “wakifikiria.”
c. Ama samaki wafe au wavu ukatike: nahau ya Uchina, yenye maana “mapambano ya kufa na kupona.”
d. Maandishi ya asili yanaacha “kama asemavyo Mungu.”
e. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni